Ijumaa, 4 Agosti 2017

Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela “Yasifu Maisha Mapya”


Kanisa la Mwenyezi MunguYasifu Maisha Mapya


Haleluya! Twakushukuru na kukusifu Wewe!
Haleluya! Twakushukuru na kukusifu Wewe, Mwenyezi Mungu!

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu.
Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.
Ni neno la Mungu ambalo limenibadilisha,
kwa hivyo nina maisha mapya ya kumsifu Mungu. (Halleluya!)
Maumivu na mkanganyo vimetoweka; Nimefunguliwa katika roho na ninaimba wimbo. (Halleluya!)
Ni vizuri kweli kuelewa ukweli. Nimeupita mwili, mimi ni huru sana! (Msifu Mungu!)
Dhana zote na kutokuelewana kumeondolewa mbali, tabia yangu asi imebadilishwa.
Mimi hutembea katika njia ng'avu ya maisha ya binadamu; upendo wa Mungu ni wa thamani na halisi sana! (Msifu Mungu!)
Ni furaha ya Mungu kuufurahia upendo wa Mungu.
Nimeuonja upendo wa Mungu na siwezi kumwacha Mungu tena.

Jumanne, 1 Agosti 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,  

Kanisa la Mwenyezi Mungu  | Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kunayo siri kubwa moyoni mwako. Huifahamu kamwe kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu usio na mwanga unaoangaza. Moyo wako na roho yako vimechukuliwa mateka na yule mwovu. Macho yako yamefunikwa na giza; huwezi kuliona jua angani, wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yatiririkayo kutoka katika kiti cha enzi.