Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo hukumu-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo hukumu-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 26 Agosti 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu

Unampenda Mungu kiasi gani hasa leo? Na unajua kiasi gani hasa kuhusu yote ambayo Mungu amefanya ndani yako? Haya ni mambo unayopaswa kujifunza. Mungu anapowasili duniani, yote ambayo Amefanya ndani ya mwanadamu na kumkubalia mwanadamu kuona ni ili mwanadamu atampenda na kumjua Yeye kweli. Kwamba mwanadamu anaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu na ameweza kufikia umbali huu ni, kuhusiana na jambo moja, kwa sababu ya upendo wa Mungu, na kuhusiana na jambo lingine, ni kwa sababu ya wokovu wa Mungu; zaidi ya hayo, ni kwa sababu ya kazi ya hukumu na kuadibu ambayo Mungu ametekeleza ndani ya mwanadamu.

Jumatano, 6 Februari 2019

Swahili Christian Music Video | "Ni Watu Waaminifu Pekee Walio na Mfano wa Binadamu" | God Led Me Onto the Right Path of Life

I
Kwa ajili ya faida niliacha viwango vyote vya mwenendo,
na bila haya nikatumia udanganyifu kutafuta riziki yangu.
Sikujali chochote kuhusu dhamiri au maadili, chochote kuhusu uadilifu au heshima.
Niliishi tu kuridhisha tamaa na uroho wangu vilivyozidi kukua.
Kwa moyo usio na amani, nilitembea katika matope ya dhambi,
bila njia yoyote ya kuepuka giza hii isiyo na mipaka.

Alhamisi, 31 Januari 2019

8. Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

8. Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. Hivyo ndivyo alivyokuwa mwanzoni na Mungu" (YN. 1:1-2).
"Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli" (YN. 1:14).
"Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu" (YN. 14:6).
"Maneno ninayoongea kwenu ni roho, na ni uhai" (YN. 6:63).
Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hauwezi kufikiwa na mwanadamu.

Jumanne, 10 Oktoba 2017

Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kiambatisho: Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kama mamia ya mamilioni ya wafuasi wengine wa Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana.