Jumamosi, 3 Machi 2018

Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III (Sehemu ya Tatu)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa,
(Sehemu ya Tatu)
Uhuru: Awamu ya Tatu
Mwenyezi Mungu alisema, Baada ya mtu kupita utoto na wakati wake wa kubaleghe na kwa utaratibu bila kuzuilika kufikia ukomavu, hatua inayofuata ni kwake yeye kuuaga kabisa ule ujana wake, kuwaaga wazazi wake, na kukabiliana na barabara iliyo mbele yake akiwa mtu mzima huru. Wakati huo[c]lazima wakabiliane na watu, matukio na mambo yote ambayo mtu mzima lazima apitie, na kukabiliana na viungo mbalimbali katika msururu wa hatima yake. Hii ndiyo awamu ya tatu ambayo lazima mtu apitie.
1. Baada ya Kuwa Huru, Mtu Huanza Kupitia Ukuu wa Muumba
Kama kuzaliwa kwa mtu na kulelewa kwake ni “kipindi cha matayarisho” katika safari ya mtu maishani, kuweka lile jiwe la msingi katika hatima ya mtu, basi uhuru wa mtu ndio mazungumzo nafsi ya kufungua hatima ya maisha ya mtu. Kama kuzaliwa na kukua kwa mtu ni utajiri ambao wameweza kulimbikiza kwa minajili ya hatima yao maishani, basi uhuru wa mtu huyo unaanza wakati ule wanaanza kutumia au kuongeza utajiri huo. Wakati mtu anawaacha wazazi na kuwa huru, masharti ya kijamii ambayo anakabiliana nayo, na aina ya kazi na ajira inayopatikana kwa mtu, vyote vinaamriwa na hatima na havina uhusiano wowote na wazazi wa mtu. Baadhi ya watu huchagua kozi nzuri katika chuo na huishia kupata kazi ya kutosheleza baada ya kuhitimu, na hivyo basi kupiga hatua ya kwanza ya mafanikio katika safari yao ya maisha. Baadhi ya watu hujifunza na kumiliki mbinu nyingi tofauti na ilhali hawapati kazi katu ambayo inawafaa au hawapati cheo chao, bila kutaja kwamba hawana ajira yoyote; wakati wa safari ya maisha yao wanajipata wakiwa wamekwazwa katika kila kona, wameandamwa na matatizo, matumaini yao madogo na maisha yao hayana uhakika. Baadhi ya watu wanatia bidii katika masomo yao, ilhali wanakosa kwa karibu sana fursa zao zote za kupokea elimu ya juu zaidi, na wanaonekana kuwa na hatima ya kutotimiza fanisi, matamanio yao ya kwanza kabisa katika safari yao ya maisha yanatowekea tu hewani. Bila kujua[d]kama barabara iliyo mbele ni laini au yenye miamba, wanahisi kwa mara ya kwanza namna ambavyo hatima ya binadamu imejaa vitu vya kubadilikabadilika, na wanachukulia maisha kwa tumaini na hofu. Baadhi ya watu, licha ya kutokuwa na elimu nzuri sana, huandika vitabu na kutimiza kiwango cha umaarufu; baadhi, ingawaje hawajui kusoma na kuandika sana, huunda pesa katika biashara na hivyo basi wanaweza kujikidhi…. Kazi anayochagua mtu, namna mtu anavyozumbua riziki: je, watu wanao udhibiti wowote kuhusu, kama wanaweza kufanya uchaguzi mzuri au uchaguzi mbaya? Je, yanapatana na matamanio na uamuzi wao? Watu wengi zaidi hutamani wangeweza kufanya kazi kidogo na kupata mapato mengi zaidi, wasitie bidii sana katika jua na mvua, wavalie vyema, wametemete na kung’aa wakiwa kila pahali, kuwapita sana wengine kwa uwezo, na kuleta heshima kwa mababu wao. Matamanio ya watu ni timilifu kweli, lakini watu wanapochukua hatua zao za kwanza katika safari ya maisha yao, wanaanza kwa utaratibu kutambua namna ambavyo hatima ya binadamu ilivyo na hali ya kutokuwa timilifu, na kwa mara ya kwanza wanang’amua kwa kweli hoja hii kwamba, ingawaje mtu anaweza kufanya mipango thabiti kwa minajili ya mustakabali wake, ingawaje mtu anaweza kuhodhi mawazoni ndoto shupavu, hakuna yule aliye na uwezo au nguvu za kutambua ndoto zake mwenyewe, hakuna yule aliye katika hali ya kudhibiti mustakabali wake. Siku zote kutakuwepo na kitalifa fulani kati ya ndoto za mtu na uhalisia ambao lazima mtu akabiliane nao; mambo siku zote hayawi vile ambavyo mtu angetaka yawe, na watu wanapokumbwa na uhalisi kama huu hawawezi kutimiza hali ya kutosheka au kuridhika. Baadhi ya watu wataenda hadi kiwango chochote cha kufikirika, wataweza kutia bidii za kipekee na kujitolea pakubwa kwa minajili ya riziki na mustakabali wao, katika kujaribu kubadilisha hatima yao wenyewe. Lakini hatimaye, hata kama wataweza kutambua ndoto na matamanio yao kupitia kwa njia ya bidii yao wenyewe, hawawezi kubadilisha hatima zao, na haijalishi watajaribu vipi kwa njia ya ukaidi hawatawahi kuzidi kile ambacho hatima yao imewapangia. Licha ya tofauti katika uwezo, kiwango cha akili, na hiari ya kutenda, watu wote ni sawa mbele ya hatima, jambo ambalo halileti utofauti kati ya wakubwa na wadogo, wale wa kiwango kile cha juu na cha chini, wanaotukuzwa na wakatili. Ile kazi ambayo mtu anafuatilia, kile anachofanya mtu ili kuzumbua riziki, na kiwango kipi cha utajiri ambacho mtu amelimbikiza katika maisha yake vyote haviamuliwi na wazazi wa mtu, vipaji vya mtu, jitihada za mtu au malengo ya mtu, vyote vinaamuliwa kabla na Muumba.
2. Kuwaacha Wazazi wa Mtu na Kuanza kwa Bidii Kuendeleza Wajibu Wako Kwenye Ukumbi wa Sanaa wa Maisha
Wakati mtu anapofikia ukomavu, mtu anaweza kuacha wazazi wake na kulikanyaga guu lake nje kivyake, na ni katika wakati huu ambapo mtu huanza kwa kweli kuonyesha wajibu wake binafsi, kwamba kazi maalum ya mtu maishani husita kutoeleweka na polepole kuanza kuwa wazi. Kimsingi mtu huyo bado huonyesha uhusiano wa karibu na wazazi wake, lakini kwa sababu kazi yake maalum na wajibu anaoendeleza katika maisha huwa hauna uhusiano wowote na mama na baba wa mtu huyo, kwa hakika uhusiano huu wa karibu huvunjika polepole kwa kadiri ambavyo mtu anazidi kuendelea kuwa huru. Kutoka katika mtazamo wa kibiolojia, watu bado hawana budi kutegemea wazazi katika njia za kufichika akilini, lakini kama tutaongea kwa malengo, mara baada ya kukua huwa na maisha tofauti kabisa na yale ya wazazi wao, na wataweza kutekeleza wajibu watakaoamua kufanya kwa uhuru wao. Mbali na kuzaliwa na kulea watoto, jukumu la kila mzazi katika maisha ya mtoto ni kuweza kuwapatia tu mazingira rasmi ya kukulia ndani, bila malipo yoyote isipokuwa kule kuamuliwa kabla kwa Muumba ambako kunachukua mwelekeo katika hatima ya mtu huyu husika. Hakuna anayeweza kudhibiti ni mustakabali gani ambao mtu atakuwa nao; huwa umeamuliwa kabla na mapema sana, na hata wazazi wa mtu hawawezi kubadilisha hatima yake. Kulingana na mambo ya hatima, kila mtu yuko huru na kila mtu anayo hatima yake. Kwa hivyo hakuna wazazi wa mtu yeyote wanaweza kuiondoa hatima ya mtu katika maisha au kusisitizia ushawishi wowote ule mdogo katika wajibu ambao mtu huendeleza maishani. Inaweza kusemekana kwamba, familia ambayo mtu ameamuliwa kuzaliwa ndani, na mazingira ambayo mtu atakulia ndani, ni yale masharti ya awali ya kutimiza kazi maalum ya mtu maishani. Yote haya hayaamui kwa vyovyote vile hatima ya mtu katika maisha au aina ya hatima ambayo mtu huyo atatimiza katika kazi yake maalum. Na kwa hivyo hakuna wazazi wa mtu yeyote yule wanaweza kusaidia katika kutimiza kazi hii maalum katika maisha, hakuna watu wowote wa ukoo wanaweza kusaidia mtu kuchukua wajibu huu katika maisha. Vile ambavyo mtu hutimiza kazi yake maalum na katika aina gani ya mazingira ya kuishi ambayo mtu hutekeleza wajibu wake, vyote vinaamuliwa na hatima ya mtu maishani. Kwa maneno mengine, hakuna masharti yoyote mengine yenye malengo yanaweza kuathiri kazi maalum ya mtu, ambayo imeamuliwa kabla na Muumba. Watu wote hukomaa katika mazingira yao binafsi ya kukulia, na kisha kwa taratibu, hatua kwa hatua, huanza safari katika barabara zao binafsi za maisha, hutimiza hatima walizopangiwa na Muumba, kwa kawaida, bila hiari wao huingia katika bahari kuu ya ubinadamu na kuchukua nafasi zao binafsi katika maisha, pale ambapo wao huanza kutimiza majukumu yao kama viumbe vilivyoumbwa kwa minajili ya kuamuliwa kabla kwa Muumba, kwa minajili ya ukuu Wake.

Ndoa: Awamu ya Nne
Wakati mtu anavyokua mzee na kukomaa, mtu huanza kukua na kuwa mbali na wazazi wake na mazingira ambayo amezaliwa na kulelewa, na badala yake mtu huanza kutafuta mwelekeo wa maisha yake na kufuatilia shabaha binafsi kwa njia ya maisha iliyo tofauti na ile ya wazazi. Kwenye kipindi hiki cha muda mtu hahitaji tena wazazi wake, bali mwandani ambaye anaweza kuishi maisha yake na mtu huyo: mwenza, mtu ambaye hatima yake imejipinda kwake ndani kwa ndani. Kwa njia hii, tukio kuu ambalo mtu hukabiliana nalo kufuatia uhuru wake ni ndoa, awamu ya nne ambayo lazima mtu apitie.
1. Mtu Hana Chaguo Kuhusu Ndoa
Ndoa ni tukio muhimu katika maisha ya mtu yeyote; ni wakati ule ambao mtu huanza kwa kweli kuendeleza aina mbalimbali za majukumu, huanza kwa utaratibu kutimiza aina mbalimbali za kazi maalum. Watu huwa na picha nyingi kuhusu ndoa kabla ya kuipitia wao wenyewe, na picha hizi zote ni nzuri. Wanawake hufikiria kwamba waume wao watakuwa Kaka Mwenye Mvuto na Haiba, nao wanaume hufikiria kwamba wataweza kuoa Binti wa Kifalme Anayependeza. Kubuni huku kwa mawazo kunaonyesha kwamba kila mtu anayo mahitaji fulani ya ndoa, orodha fulani ya kile anachohitaji na viwango anavyopenda. Ingawaje katika enzi hii ya maovu watu wanaambiwa kila mara kuhusu ujumbe uliopotoka juu ya ndoa, hali ambayo husababisha hata mahitaji mengi zaidi, pamoja na kupatia watu aina zote za mizigo na mitazamo isiyo ya kawaida, mtu yeyote aliyepitia ndoa anajua kwamba haijalishi ni kiasi kipi ambacho mtu ataielewa, haijalishi pia mtu anao mtazamo gani katika ndoa hiyo, ndoa si suala la chaguo la mtu binafsi.
Mtu hukumbana na watu wengi katika maisha yake, lakini hakuna anayejua ni nani atakayekuwa mwandani wake katika ndoa. Ingawaje kila mtu anazo fikira zake binafsi na mtazamo wake wa kibinafsi kuhusu suala la ndoa, hakuna anayeweza kuona mbele na kujua ni nani atakayekuwa mwandani wake wa kweli hatimaye, na fikira za mtu huwa zinachangia kidogo sana. Baada ya kukutana na mtu unayempenda, unaweza kumfuatilia mtu huyo; kama mtu huyo amevutiwa na wewe au la, kama mtu huyo anaweza kuwa mwandani wako au la, si wewe kuamua. Kiini cha mahaba yenu si haswa mtu ambaye mtaweza kuishi naye katika maisha yako; na huku haya yakiendelea mtu ambaye hukuwahi kutarajia anaingia katika maisha yako na kuwa mwandani wako, anakuwa msingi muhimu sana katika hatima yako, nusu yako ile nyingine, ambaye hatima yako imefungamanishwa naye ajabu. Na kwa hiyo, ingawaje kunazo ndoa milioni kwa milioni ulimwenguni, kila ndoa ni tofauti: Ni ndoa ngapi ambazo hazitoshelezi, ni ngapi zinayo furaha; ni ngapi zinazopatikana Mashariki na Magharibi, ni ngapi Kaskazini na Kusini; ni ngapi ambazo wanandoa wanafaa na wamelingana, na ni ngapi zenye kiwango sawa; ni ngapi zenye furaha na utulivu, ni ngapi zenye maumivu na huzuni; ni ngapi zinaonewa wivu na wengine, na ni ngapi hazieleweki na hazipendelewi kabisa; ni ngapi zimejaa furaha, na ni ngapi zimejaa machozi na zinakatisha tamaa.…. Kwenye ndoa hizi zote, binadamu wanafichua utiifu na kujitolea kwa maisha katika ndoa hizo, au pendo, au mtagusano, na hali ya kutotenganishwa, au kukata tamaa na kutoeleweka, au usaliti, au hata chuki. Haijalishi kama ndoa inaleta furaha au maumivu, kazi maalum ya kila mmoja katika ndoa iliamuliwa kabla na Muumba na haitabadilika; kila mmoja lazima aitimize. Na hatima ya kibinafsi inayokuwa katika kila ndoa haibadiliki; iliamuliwa kitambo naye Muumba.
2. Ndoa Inazaliwa Kutokana na Hatima ya Wandani Wawili
Ndoa ni awamu muhimu katika maisha ya mtu. Ni zao la hatima ya mtu, kiungo muhimu katika hatima ya mtu; haiundwi kwa misingi ya uamuzi wa mtu yeyote binafsi au mapendeleo yake, na haiathiriwi na mambo yoyote ya nje, lakini inaamuliwa kabisa na hatima za wandani wawili, kupitia kwa maandalizi na kuamuliwa kabla kwa Muumba kuhusiana na hatima za wanandoa hao. Ukiangalia juujuu, kusudi la ndoa ni kuendeleza kizazi cha binadamu, lakini kwa kweli ndoa si chochote ila ni kawaida ya dini ambayo mtu anapitia katika mchakato wa kutimiza kazi yake maalum. Wajibu mbalimbali ambao watu huendeleza katika ndoa si ule tu wa kuleta kizazi kinachofuata; kunao wajibu mbalimbali ambao mtu huwa nao na kazi maalum ambazo mtu lazima atimize kwenye mkondo wa kuendeleza ndoa. Kwa sababu kuzaliwa kwa mtu huathiri mabadiliko ya watu, matukio, na mambo yanayomzunguka, ndoa ya mtu itaweza pia kuathiri bila shaka watu hao, na zaidi itawabadilisha kwa njia tofauti.
Wakati mtu anapokuwa huru, mtu huanza safari yake binafsi ya maisha, inayoongoza mtu hatua kwa hatua kuelekea kwa watu, na kwa matukio, na kwa vitu vinavyohusiana na ndoa ya mtu; na wakati uo huo, yule mtu mwengine atakayeunda ile ndoa anakaribia, hatua kwa hatua, kuelekea watu ao hao, matukio na hata mambo. Kwenye ukuu wa Muumba, watu wawili wasiohusiana walio na hatima inayohusiana wanaingia kwa utaratibu kwenye ndoa na kuwa, kimiujiza, familia, “nzige wawili wanaoshikilia kamba moja.” Kwa hivyo mtu anapoingia kwenye ndoa, safari ya mtu katika maisha itaathiri na kumgusa yule mwenzake, na vilevile safari ya mwandani katika maisha itashawishi na kugusa hatima ya yule mwenzake katika maisha. Kwa maneno mengine, hatima za mwanadamu zimeingiliana na hakuna yule anayeweza kutimiza kazi yake maalum maishani au kutekeleza wajibu wake kabisa akiwa huru mbali na wengine. Kuzaliwa kwa mtu kunao mwelekeo kwa msururu mkubwa wa mahusiano; kukua pia kunahusisha msururu mkubwa wa mahusiano; na vilevile, ndoa inakuwepo bila shaka na kuendelezwa katika mtandao mpana na mgumu wa miunganisho ya binadamu, ikihusisha kila mwanachama na kuathiri hatima ya kila mmoja ambaye ni sehemu yake. Ndoa si mazao ya familia za wanachama wale wawili, hali ambazo wao walilelewa, maumbo yao, umri wao, ubora wao, vipaji vyao, au mambo mengine yoyote; badala yake, inatokana na kazi maalum ya pamoja na hatima inayohusiana. Hii ndiyo asili ya ndoa, zao la hatima ya binadamu lililopangwa na lililopangiliwa na Muumba.
Uzao: Awamu ya Tano
Baada ya kuoa, mtu anaanza kulea kizazi kijacho. Mtu hana uwezo wa kujua atakuwa na watoto wangapi na watoto hawa watakuwa aina gani; hili pia linaamuliwa na hatima ya mtu, iliyoamuliwa kabla na Muumba. Hii ndiyo awamu ya tano ambayo lazima mtu apitie.
Kama mtu amezaliwa ili kutimiza jukumu la mtoto wa mwengine, basi mtu analea kizazi kijacho ili kutimiza jukumu la mzazi wa mwengine. Mabadiliko haya ya majukumu yanamfanya mtu kupitia awamu tofauti za maisha kutoka mitazamo tofauti. Yanampa pia mtu mseto tofauti wa mambo mbalimbali ya maisha kupitia, ambapo mtu anajua ukuu ule wa Muumba, pamoja na hoja kwamba hakuna mtu anayeweza kuzidi au kubadilisha kile ambacho Muumba aliamua kabla.
1. Mtu Hana Udhibiti wa Hatima ya Uzao Wake
Kuzaliwa, kukua, na kuoa ni awamu ambazo zinaleta aina tofauti na viwango tofauti vya masikitiko. Baadhi ya watu hawatosheki na familia zao au maumbo yao ya kimwili; baadhi hawapendi wazazi wao; baadhi wanachukia au wanalalamikia mazingira ambayo walikulia ndani. Na kwa baadhi ya watu wengi, miongoni mwa masikitiko haya yote, ndoa ndiyo ambayo haitoshelezi zaidi. Licha ya vile ambavyo unayo masikitiko kwa kuzaliwa kwako, au kukua kwako, au ndoa yako, kila mmoja ambaye amepitia awamu hizi amejua kwamba hawezi kuchagua ni wapi au ni lini alizaliwa, ni vipi anavyofanana, wazazi wake ni nani, na mume au mke wake ni nani, lakini wanaweza kukubali tu mapenzi ya Mbinguni. Lakini wakati wa watu kulea kizazi kijacho unapowadia, wataweza kuweka matamanio yao yote ambayo hayajatimizwa katika nusu ya kwanza ya maisha yao kwenye vizazi vyao, wakitumai kwamba, uzao wao utajaliza sehemu ile ambayo wao wamepitia masikitiko, kwenye nusu ile ya kwanza ya maisha yao. Kwa hivyo watu hujihusisha katika aina zote za fantasia kuhusu watoto wao: kwamba binti zao watakua na kuwa warembo ajabu, watoto wao wa kiume watakuwa wanaume wa kipekee; kwamba binti zao watakuwa na maadili na wenye vipaji nao watoto wao wa kiume watakuwa wanafunzi werevu, na wanariadha sifika; na kwamba binti zao watakuwa watulivu na waadilifu, wenye akili razini, kwamba watoto wao wa kiume watakuwa wenye akili, wenye uwezo na wanaojali. Wanatumai kwamba wawe watoto wa kike au wa kiume wataheshimu wazee wao, watajali wazazi wao, watapendwa na kusifiwa na kila mmoja. … Kufikia hapa matumaini ya maisha yanajitokeza upya, na matamanio mapya yanapata nguvu katika mioyo ya watu. Watu wanajua kwamba hawana nguvu na tumaini katika maisha haya, kwamba hawatakuwa na fursa nyingine, tumaini jingine, la kujitokeza mbele ya watu, na kwamba hawana chaguo lolote ila kukubali hatima zao. Na kwa hivyo wanatazamia matumaini yao yote, matamanio na maadili yao ambayo hayajatimizwa, hadi kwenye kizazi kijacho, wakitumai uzao wao unaweza kuwasaidia kutimiza ndoto zao na kutambua matamanio yao; na kwamba binti zao na watoto wao wa kiume wataleta utukufu katika jina la familia, kuwa muhimu, kuwa matajiri au maarufu; kwa ufupi, wanataka kuuona utajiri wa watoto wao ukizidi na kuzidi. Mipango na fantasia za watu ni timilifu; kwani hawajui kwamba idadi ya watoto walio nayo, umbo, uwezo na kadhalika wa watoto wao, si juu yao kuamua, kwamba hatima za watoto wao hazimo kamwe katika viganja vya mikono yao? Binadamu si waendeshaji wa hatima yao binafsi, ilhali wanatumai kubadilisha hatima ya kizazi kichanga zaidi; hawana nguvu za kutoroka hatima zao wenyewe, ilhali, wanajaribu kudhibiti zile za watoto wao wa kiume na kike. Je, hawazidishi ukadiriaji wao? Je, huu si ujinga na hali ya kutojua kwa upande wa binadamu? Watu huenda kwa mapana yoyote kwa minajili ya uzao wao, lakini hatimaye, idadi ya watoto aliyonayo mtu, na vile ambavyo watoto wake walivyo, si jibu la mipango na matamanio yao. Baadhi ya watu hawana hela lakini wanazaa watoto wengi; baadhi ya watu ni tajiri ilhali hawana mtoto. Baadhi wanataka binti lakini wananyimwa tamanio hilo; baadhi wanataka mtoto wa kiume lakini wanashindwa kuzaa mtoto wa kiume. Kwa baadhi, watoto ni baraka; kwa wengine, mtoto ni laana. Baadhi ya wanandoa ni werevu, ilhali wanawazaa watoto wanaoelewa polepole; baadhi ya wazazi ni wenye bidii na waaminifu, ilhali watoto wanaowalea ni wavivu. Baadhi ya wazazi ni wapole na wanyofu lakini wana watoto wanaogeuka na kuwa wajanja na wenye inda. Baadhi ya wazazi wana akili na mwili timamu lakini wanajifungua watoto walemavu. Baadhi ya wazazi ni wa kawaida na hawajafanikiwa ilhali watoto wao wanafanikiwa pakubwa. Baadhi ya wazazi ni wa hadhi ya chini ilhali watoto wanaowalea ni wenye taadhima. …
2. Baada ya Kulea Kizazi Kijacho, Watu Hufaidi Ufahamu Mpya wa Hatima Yao
Watu wengi wanaooa hufanya hivyo karibu kwenye umri wa miaka thelathini, na kwa wakati huu wa maisha, mtu hana ufahamu wowote wa hatima ya binadamu. Lakini wakati watu wanapoanza kulea watoto, kwa kadri uzao wao unapokua, wanatazama kizazi kipya kikirudia maisha na hali zote walizopitia katika kizazi cha awali, na wanaona maisha yao ya kale yakijionyesha kwao na wanatambua kwamba barabara inayotumiwa na kizazi kile kichanga zaidi, kama tu yao, haiwezi kupangwa wala kuchaguliwa. Wakiwa wamekabiliwa na hoja hii, hawana chaguo lolote bali kukubali kwamba hatima ya kila mtu iliamuliwa kabla; na bila ya hata kutambua wanaanza kwa utaratibu kuweka pembeni matamanio yao binafsi, na hisia kali katika mioyo yao inapungua na kuwatoka…. Kwenye kipindi hiki cha muda, mtu ameweza kupita sehemu nyingi zaidi na muhimu katika mafanikio ya maisha yake na ametimiza ufahamu mpya wa maisha, na kuchukua mtazamo mpya. Je, mtu wa umri huu anaweza kutarajia kwa siku za usoni kiasi kipi cha mambo na matarajio yake ni yapi? Ni mwanamke yupi mwenye umri wa miaka hamsini na mmoja angali anaota kuhusu Kaka Mwenye Mvuto na Haiba? Ni mwanamume yupi wa miaka hamsini na mmoja angali anatafuta Binti wa Kifalme Anayependeza? Ni mwanamke yupi wa umri wa kati atakuwa anatumai kugeuka kutoka kwa mtoto wa bata mwenye sura mbaya hadi batamaji? Je, wanaume wazee zaidi wangali wana msukumo sawa wa ajira na wanaume wachanga? Kwa ujumla, haijalishi kama mtu ni mwanamume au mwanamke, yeyote anayeishi na kuufikia umri huu anao uwezekano wa kuwa na mtazamo wa kueleweka na kutumika kiasi fulani katika ndoa, familia, na watoto. Mtu kama huyo, kimsingi hana machaguo yoyote yaliyobakia, hana msukumo wowote wa kukabiliana na hatima yake. Kwa mujibu wa kile ambacho binadamu amepitia, punde tu mtu anapofikia umri huu mtu huanza kwa kawaida kuwa na mtazamo kwamba “lazima mtu akubali hatima yake; watoto wake wanao utajiri wao binafsi; hatima ya binadamu inaamriwa Mbinguni.” Watu wengi ambao hawaelewi ukweli, baada ya kupitia mabadiliko, mahangaiko, na ugumu wote wa ulimwengu huu, watatoa muhtasari wa utambuzi wao wa maisha ya binadamu kwa maneno matatu: “Hiyo ndiyo hatima!” Ingawaje kauli hii inatoa muhtasari wa hitimisho ya watu wa ulimwengu na utambuzi kuhusu hatima ya binadamu, ingawaje inaelezea kutoweza kusaidika kwa ubinadamu na inaweza kusemekana kwamba inapenyeza na ni sahihi, ni kilio cha mbali kutoka kwa ufahamu wa ukuu wa Muumba, na si kibadala cha maarifa ya mamlaka ya Muumba.
3. Kusadiki Katika Hatima si Kibadala cha Maarifa ya Ukuu wa Muumba
Baada ya kuwa mfuasi wa Mungu kwa miaka mingi, je, kunayo tofauti kubwa katika maarifa yako ya hatima na yale ya watu wa ulimwengu? Je, umeelewa kwa kweli kule kuamuliwa kabla kwa Muumba, na unaweza kujua kwa kweli ukuu wa Muumba? Baadhi ya watu wanao ufahamu mkuu, wa kina wa kauli hii “hiyo ndiyo hatima,” ilhali hawasadiki hata kidogo katika ukuu wa Mungu, hawasadiki kwamba hatima ya binadamu hupangiliwa na kupangwa na Mungu, na hawako radhi kunyenyekea mbele ya ukuu wa Mungu. Watu kama hao ni kana kwamba wanaelea baharini, wanatoswatoswa na mawimbi, huku wakielea na kufuata mkondo wa maji, wasiwe na chaguo ila kusubiri kimyakimya na kuachia maisha yao hatima. Ilhali hawatambui hatima ya binadamu inategemea ukuu wa Mungu; hawawezi kujua ukuu wa Mungu wao binafsi, na hivyo basi kutimiza utambulisho wa mamlaka ya Mungu, kunyenyekea katika mipango na mipangilio ya Mungu, kuacha kukinzana na hatima na kuishi katika utunzwaji, ulinzi na mwongozo wa Mungu. Kwa maneno mengine, kukubali hatima si jambo sawa na kunyenyekea kwa ukuu wa Muumba; kusadiki hatima hakumaanishi kwamba mtu akubali, atambue, na ajue ukuu wa Muumba; kusadiki katika hatima ni ule utambulisho wa hoja hii na suala hili la nje, ambalo ni tofauti na kujua namna Muumba Anavyotawala hatima ya ubinadamu, kuanzia katika kutambua kwamba Muumba ndiye chanzo cha kutawala juu ya hatima za mambo yote na hata zaidi kunyenyekea kwa mipangona mipangilio ya Muumba kwa ajili ya hatima ya binadamu. Kama mtu anasadiki tu katika hatima—hata anahisi kwa kina kuihusu—lakini papo hapo hawezi kujua, kutambua, kunyenyekea, na kukubali ukuu wa Muumba kuhusu ile hatima ya ubinadamu basi maisha yake yatakuwa kwa kweli msiba mkuu, maisha yaliyopita kwa masikitiko, utupu; yeye atakuwa hawezi kutii utawala wa Muumba, kuwa binadamu aliyeumbwa katika hali ya kweli zaidi ya kauli hiyo, na kufurahia idhini ya Muumba. Mtu anayejua na kupitia kwa kweli ukuu wa Muumba anafaa kuwa katika hali amilifu, isiyo baridi au ya kutoweza kusaidika. Huku wakati uo huo akikubali kwamba mambo yote yanategemea hatima ya maisha, yeye anafaa kumiliki ufafanuzi sahihi wa maisha na hatima: kwamba kila maisha yanategemea ukuu wa Muumba. Wakati mtu anapoangalia nyuma kwenye barabara aliyotembelea, wakati mtu anapokusanya tena kila awamu ya safari ya maisha yake, mtu anaona kila hatua, haijalishi kama barabara ya mtu inakuwa mbaya au nzuri, Mungu alikuwa akiongoza njia ya mtu, akipanga kila kitu. Ilikuwa ni mipangilio ya umakinifu ya Mungu, upangiliaji Wake makinifu ulioongoza mtu, bila kujua, hadi kufikia leo. Ili kuweza kukubali ukuu wa Muumba, ili kupokea wokovu Wake—utajiri mwingi ulioje! Kama mtazamo wa mtu katika hatima ni wa baridi, inathibitisha kwamba yeye anakinzana na kila kitu ambacho Mungu amempangilia, kwamba yeye hana mtazamo wa kunyenyekea. Kama mtazamo wa mtu katika ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu ni amilifu, basi mtu anapotazama nyuma katika safari yake, wakati mtu anapong'amua kwa kweli ukuu wa Mungu, mtu huyo ataweza kutamani kwa dhati kunyenyekea kila kitu ambacho Mungu amepangilia, atakuwa na jitihada zaidi na ujasiri wa kumwacha Mungu kuunda hatima yake, ili kuacha kuasi dhidi ya Mungu. Kwani mtu anaona kwamba akikosa kuelewa hatima, wakati mtu haelewi ukuu wa Mungu, wakati mtu anapotutusa mbele kwa hiari yake, akichechemea na kupenyeza kwenye ukungu, safari inakuwa ngumu sana, ya kuvunja moyo. Kwa hivyo wakati watu wanapotambua ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu, wale walio werevu wanachagua kuijua na kuikubali, kuaga kwaheri siku zenye maumivu ambapo walijaribu kuwa na maisha mazuri kwa nguvu za mikono yao miwili, badala ya kuendelea kung’ang’ana dhidi ya hatima na kuzitafuta zile shabaha maarufu za maisha kwa njia yao wenyewe. Wakati mtu hana Mungu, wakati mtu hawezi kumwona Mungu, wakati hawezi kutambua waziwazi ukuu wa Mungu, kila siku inakosa maana, inakosa thamani, na kuwa yenye taabu. Popote pale mtu yupo, kazi yoyote ile anayofanya, mbinu za mtu za kuzumbua riziki na kutafuta shabaha zake huweza kumletea kitu kimoja ambacho ni kuvunjika moyo kusikoisha na mateso yasiyopona, kiasi cha kwamba mtu hawezi kuvumilia kuangalia nyuma. Ni pale tu mtu anapokubali ukuu wa Muumba, ananyenyekea katika mipangona mipangilio Yake, na kutafuta maisha ya kweli ya binadamu, ndipo mtu atakapokuwa huru kwa utaratibu dhidi ya kuvunjika moyo na kuteseka, kutupilia mbali utupu wote wa maisha.
4. Wale tu Wanaonyenyekea Ukuu wa Muumba Ndio Wanaweza Kupata Uhuru wa Kweli
Kwa sababu watu hawatambui mipango ya Mungu, na ukuu wa Mungu, siku zote wanakabiliana na hatima hiyo kwa kuasi, kwa mtazamo wa kuasi, na siku zote wanataka kutupilia mbali mamlaka na ukuu wa Mungu, na mambo yale ambayo hatima imewahifadhia, wakitumai kwamba watabadilisha hali zao za sasa na kubadilisha hatima yao. Lakini hawawezi kufaulu; wanazuiliwa kwa kila sehemu ya mabadiliko katika maisha. Mvutano huu, unaoendelea ndani ya nafsi ya mtu, ni wa maumivu; maumivu haya hayasahauliki; na wakati wote huu mtu anapoteza maisha yake mwenyewe. Sababu ya maumivu haya ni nini? Je, ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu au kwa sababu ya mtu kuzaliwa bila bahati? Bila shaka kati ya sababu hizi hakuna iliyo kweli. Kimsingi, ni kwa sababu ya njia ambazo watu huchukua, njia ambazo watu huchagua kuishi katika maisha yao. Baadhi ya watu huenda wasitambue mambo haya. Lakini unapojua kwa kweli, unapotambua kwa kweli kwamba Mungu anao ukuu juu ya hatima ya binadamu, unapoelewa kwa kweli kwamba kila kitu ambacho Mungu amekupangilia na kukuamulia ni chenye manufaa makubwa, na ni ulinzi mkubwa, basi unahisi maumivu yako yakipungua kwa utaratibu, na uzima wako wote unaanza kutulia, kuwa huru na kukombolewa. Tukiamua kutokana na hali za wingi wa watu, ingawaje kwa kiwango cha kibinafsi hawataki kuendelea kuishi kama walivyokuwa wakiishi awali, ingawaje wanataka tulizo katika maumivu yao, kimsingi hawawezi kung’amua kwa kweli thamani na maana halisi ya ukuu wa Muumba ya hatima ya binadamu; hawawezi kutambua kwa kweli na kunyenyekea kwa ukuu wa Muumba, isitoshe kujua namna ya kutafuta na kukubali mipango na mipangilio ya Muumba. Kwa hivyo kama watu hawawezi kutambua hoja kwamba Muumba anao ukuu juu ya hatima ya binadamu na juu ya mambo yote ya binadamu, kama hawawezi kunyenyekea kwa kweli chini ya utawala wa Muumba, basi itakuwa vigumu sana kwao kutoendeshwa na kutiwa pingu za miguu na, fikira hii kwamba “hatima ya mtu imo kwenye mikono ya mtu,” itakuwa vigumu kwao kutupilia mbali maumivu ya kung’ang’ana kwao kwingi dhidi ya hatima na mamlaka ya Muumba, ni wazi kwamba hali hii pia itakuwa ngumu kwao katika kuweza kukombolewa kwa kweli na kuwa huru, kuwa watu wanaoabudu Mungu. Kunayo njia rahisi zaidi ile ya kujifanya kuwa huru kutoka katika hali hii: kuaga kwaheri njia yako ya awali ya kuishi, kuaga kwaheri shabaha zako za maisha za awali, kuhitimisha na kuchambua hali ya maisha ya awali, filosofia, mambo uliyofuatilia, matamanio, na maadili, na kisha kuyalinganisha yote haya na mapenzi ya Mungu na mahitaji ya binadamu, na kuona kama yoyote kati ya haya yanakubaliana na mapenzi na mahitaji ya Mungu, kujua kama yoyote kati ya haya yanakuletea maadili sahihi ya maisha, yanakuongoza katika ufahamu mwingi zaidi wa ukweli, na kuruhusu mtu kuishi kwa ubinadamu na mfano wa binadamu. Unapochunguza mara kwa mara na kuchambua kwa makini shabaha mbalimbali za maisha ambazo watu hufuatilia na njia zao tofauti za kuishi, utapata kwamba hata hakuna moja kati ya hizo zote ambayo inaingiliana na nia ya Muumba wakati Alipoumba binadamu. Zote hizi zinawavuta watu mbali na ukuu na utunzwaji wa Muumba; zote ni mitego ambayo binadamu hujipata amenaswa nayo, na ambayo inawaelekeza jehanamu. Baada ya kutambua haya, kazi yako ni kuweka pembeni mtazamo wako wa maisha ya awali, kuwa mbali na mitego mbalimbali, kumwachia Mungu kuchukua usukani wa maisha yako na kukufanyia mipangilio, jaribu tu kunyenyekea katika mipango na mwongozo wa Mungu, kutokuwa na chaguo, na kuwa mtu anayemwabudu Mungu. Haya yote yanaonekana kuwa rahisi, lakini ni jambo gumu kufanya. Baadhi ya watu wanaweza kuvumilia maumivu yake, wengine hawawezi. Baadhi wako radhi kutii, wengine hawako radhi. Wale wasiokuwa radhi wanakosa tamanio na uamuzi wa kufanya hivyo; wanayo habari kamili kuhusu ukuu wa Mungu, wanajua vyema kabisa kwamba ni Mungu anayepangilia na kupanga hatima ya binadamu, na ilhali wangali wanang'ang'ana tu, bado hawajaridhiana na nafsi zao kuhusiana na kuziacha hatima zao kwenye kiganja cha mkono wa Mungu na kunyenyekea katika ukuu wa Mungu, na zaidi, wanachukia mipango na mipangilio ya Mungu. Kwa hivyo, siku zote kutakuwa na baadhi ya watu wanaotaka kujionea wenyewe kile wanachoweza kufanya; wanataka kubadilisha hatima zao wenyewe kwa mikono yao miwili, au kutimiza furaha kwa kutumia nguvu zao wenyewe, kuona kama wanaweza kukiuka mipaka ya mamlaka ya Mungu na kuinuka juu ya ukuu wa Mungu. Huzuni ya binadamu, si kwamba binadamu anatafuta maisha mazuri, si kwamba anatafuta umaarufu na utajiri au anang'ang'ana dhidi ya hatima yake mwenyewe kupitia kwenye ukungu, lakini kwamba baada ya yeye kuona uwepo wa Muumba, baada ya yeye kujifunza hoja kwamba Muumba anao ukuu juu ya hatima ya binadamu, bado hawezi kurekebisha njia zake, hawezi kuvuta miguu yake kutoka kwenye mtego, lakini anaufanya moyo wake kuwa mgumu na anasisitizia makosa yake. Afadhali aendelee kutapatapa kwenye matope, akiapa kwa ukaidi dhidi ya ukuu wa Muumba, akiupinga mpaka mwisho wake mchungu, bila ya hata chembechembe kidogo ya majuto, na mpaka pale anapolazwa akiwa amevunjika na anavuja damu ndipo anapoamua hatimaye kusalimu amri na kugeuka na kubadilisha mwenendo. Kwa kweli huu ni huzuni kwa binadamu. Kwa hivyo Ninasema, wale wanaochagua kunyenyekea ni werevu na wale waliochagua kutoroka ni vichwa vigumu.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni