13. Bwana Yesu Ala Mkate na Kuonyesha Maandiko Baada ya Kufufuka Kwake
Luka 24:30-32 Na ikatimia, alipokuwa akikaa na wao ili wale, aliuchukua mkate, na kuubariki, na akaupasua, na kuwapa. Na macho yao yakafunguka, na wakamjua, na akatoweka wasimwone. Na wakaambiana, je, Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu sisi, wakati alipokuwa akituzungumzia njiani, na wakati alipotufungulia maandiko?
14. Wanafunzi Wampa Bwana Yesu Kipande cha Samaki wa Kuokwa Ale
Luka 24:36-43 Na wakati walipokuwa wakinena hayo, Yesu mwenyewe alisimama katikati yao, na akasema kwao, Amani iwe kwenu ninyi. Lakini walikuwa na woga na hofu sana, na wakafikiri kwamba walikuwa wameona roho. Naye akawaambia, Mbona mnasumbuka? na mbona mashaka yanaibuka mioyoni mwenu? Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe: Niguseni, na kuona; kwa sababu roho haina mwili na mifupa, jinsi mnavyoniona mimi nikiwa nayo. Na baada ya yeye kunena hayo, akawaonyesha mikono yake na miguu yake. Na wakati walikuwa bado hawajaamini kwa furaha, na wakishangaa, akawaambia, Mnacho chakula chochote huku? Na wakampa kipande cha samaki wa kuokwa kwa asali. Na akakichukua, na kukila mbele yao.
Mwenyezi Mungu anasema, Halafu tutaangalia dondoo zilizo hapo juu. Dondoo ya kwanza inamulika upya ulaji wa mkate na Bwana Yesu na unaeleza maandiko baada ya kufufuka Kwake na dondoo ya pili inaonyesha upya Bwana Yesu akila kipande cha samaki aliyekaushwa. Ni aina gani ya msaada ambao dondoo hii mara mbili inatupa kwa kuijua tabia ya Mungu? Unaweza kuwaza ni picha ya aina gani unayopata kutoka katika ufafanuzi huu wa Bwana Yesu akila mkate na kisha kipande cha samaki aliyekaushwa? Unaweza kufikiria, kama Bwana Yesu alikuwa Amesimama mbele yako wewe ukila mkate, unaweza kuhisi vipi? Au kama Angekuwa Akila pamoja nawe kwenye meza moja, huku Akila samaki kwa mkate na watu, ni hisia aina gani ambayo ungekuwa nayo wakati huo? Kama unahisi ungekuwa karibu sana na Bwana, kwamba yuko karibu sana na wewe, basi hisia yako i sahihi. Hivi ndivyo hasa tunda ambalo Bwana Yesu alitaka lizaliwe kutokana na kula Kwa mkate na samaki mbele ya umati wa watu baada ya kusulubishwa Kwake. Kama Bwana Yesu angekuwa ameongea tu na watu baada ya kufufuka Kwake, kama wasingeweza kuhisi mwili na mifupa Yake, lakini walihisi Alikuwa roho isiyoweza kufikika, wangehisi vipi? Hawangesikitishwa? Wakati watu wangesikitishwa, hawangehisi kwamba wameachwa? Hawangehisi ule umbali wa Bwana Yesu Kristo? Ni athari hasi ya aina gani ambayo umbali huu ungeweza kujenga katika uhusiano wa watu na Mungu? Watu wangehisi woga bila shaka, kwamba wasingethubutu kusonga karibu na Yeye, na wangekuwa na mwelekeo wa kumweka kwa mbali kiasi. Kuanzia hapo mpaka leo, wangekatiza uhusiano wao wa karibu na Bwana Yesu Kristo, na kurudi katika uhusiano kati ya wanadamu na Mungu aliye juu mbinguni, kama ilivyokuwa kabla ya Enzi ya Neema. Mwili wa kiroho ambao watu wasingeweza kuugusa au kuuhisi ungesababisha ukomeshaji wa ukaribu wao na Mungu, na ungefanya ule uhusiano wa karibu—ulioanzishwa wakati Bwana Yesu Kristo akiwa mwili bila ya umbali wowote kati Yake yeye na binadamu—ukose kuwepo. Hisia za watu kwa mwili wa kiroho ni za woga tu, kuepuka, na mtazamo usioeleweka. Hawathubutu kukaribia zaidi au kuwa na mazungumzo na Yeye, sikuambii hata kufuata, kuwa na imani, au kuwa na matumaini Kwake. Mungu hakupenda kuiona hisia ya aina hii ambayo wanadamu walikuwa nayo kwake Yeye. Hakutaka kuwaona watu wakimwepuka Yeye au wakijiondoa Kwake yeye; Aliwataka tu watu kumwelewa Yeye, kumkaribia na kuwa familia Yake. Kama familia yako binafsi, watoto wako wangekuona lakini wasingekutambua wewe, na hawakuthubutu kukukaribia lakini siku zote walikuepuka wewe, kama usingeweza kupata ufahamu wao kwa kila kitu ulichokuwa umewafanyia, ungehisi vipi? Halingekuwa jambo la uchungu? Je, hungevunjika moyo? Hivyo hasa ndivyo Mungu anavyohisi wakati watu wanamwepuka. Hivyo basi, baada ya kufufuka Kwake, Bwana Yesu bado alijitokeza kwa watu katika umbo Lake la mwili na damu, na kula na kunywa pamoja nao. Mungu huwaona watu kama familia na pia anataka wanadamu kumwona Yeye kwa njia hiyo; ni kwa njia hii tu ndivyo Mungu anavyoweza kuwapata watu kwa kweli, na ndio watu wanavyoweza kumpenda na kumwabudu Mungu kwa kweli. Sasa mnaweza kuelewa nia Yangu katika kudondoa dondoo hizi mbili kutoka katika maandiko pale ambapo Bwana Yesu anaula mkate na kuonyesha maandiko, na wanafunzi wanampa kipande cha samaki aliyechomwa ale baada ya kufufuka Kwake?
Inaweza kusemekana kwamba misururu ya mambo ambayo Bwana Yesu alisema na kufanya baada ya kufufuka Kwake yalikuwa ya fikira njema, na kufanywa kwa nia njema. Ilijaa huruma na huba ambayo Mungu anashikilia kwa binadamu, na akiwa amejaa shukrani na utunzaji wa makini Aliokuwa nao kwa minajili ya uhusiano wa karibu aliokuwa Ameanzisha na wanadamu wakati Akiwa katika mwili. Hata zaidi walijaa kumbukumbu za kitambo na tumaini Alilokuwa nalo kutokana na maisha ya kula na kuishi pamoja na wafuasi Wake wakati akiwa katika mwili. Hivyo basi, Mungu hakuwataka watu kuhisi umbali kati ya Mungu na binadamu, wala Hakutaka wanadamu kuwa mbali na Mungu. Hata zaidi, Hakutaka wanadamu wahisi kwamba Bwana Yesu baada ya kufufuka Kwake hakuwa tena Bwana ambaye alikuwa wa karibu na watu, kwamba Hakuwa pamoja tena na wanadamu kwa sababu Alirudi katika ulimwengu wa kiroho, alirudi kwa Baba ambaye watu wengi wasingeweza kumwona wala kumsikia. Hakutaka watu kuhisi kwamba kulikuwa na tofauti yoyote katika cheo kati Yake na wanadamu. Mungu anapowaona watu wanaotaka kumfuata lakini wanamweka katika umbali fulani, moyo Wake unapata maumivu kwa sababu hiyo inamaanisha kwamba mioyo yao iko mbali sana na Yeye, inamaanisha kwamba itakuwa vigumu sana Kwake yeye kuweza kuipata mioyo yao. Hivyo basi kama angekuwa amejitokeza kwa watu kupitia kwa mwili wa kiroho ambao wasingeweza kuuona ama kuugusa, hali hii kwa mara nyingine tena ingeweza kumweka binadamu mbali na Mungu, na ingewasababisha wanadamu kumwona Kristo kimakosa baada ya kufufuka Kwake kuonekana kuwa Amegeuka kuwa na majivuno, wa aina tofauti na wanadamu, na mtu ambaye asingeweza tena kushiriki meza na kula pamoja na binadamu kwa sababu wanadamu ni wenye dhambi, wananuka, na hawawezi kumkaribia Mungu hata kidogo. Ili kuondoa kutoelewana huku kwa wanadamu, Bwana Yesu alifanya mambo kadha wa kadha ambayo mara kwa mara Alifanya katika mwili, kama ilivyorekodiwa katika Biblia, “aliuchukua mkate, na kuubariki, na akaupasua, na kuwapa.” Pia Aliwachambulia maandiko, kama Alivyokuwa amezoea kufanya. Yote haya ambayo Bwana Yesu alifanya yalimfanya kila mmoja aliyemwona Yeye kuhisi kwamba Bwana hakuwa amebadililika, kwamba alikuwa bado Bwana Yesu. Hata ingawa Alikuwa amesulubishwa msalabani na kupitia kifo, Alikuwa amefufuliwa, na hakuwa amemwacha binadamu. Alikuwa amerudi kuwa miongoni mwa wanadamu, na kila kitu Chake hakikuwa kimebadilika. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele ya watu alikuwa bado Bwana Yesu. Mwenendo Wake na mazungumzo Yake na watu yalikuwa ya kawaida sana. Alikuwa angali bado na huruma na upendo, neema, na uvumilivu—Alikuwa bado Bwana Yesu aliyewapenda wengine kama Alivyojipenda Mwenyewe, ambaye angeweza kuwasamehe wanadamu mara sabini mara saba. Kama kawaida, Alikula na watu, kuzungumza maandiko na wao, na hata muhimu zaidi, sawa tu na kama alivyofanya awali, Alifanywa kuwa mwili na damu na aliweza kuguswa na kuonekana. Mwana wa Adamu katika njia hii aliwaruhusu watu kuhisi upendo huo, kuhisi kuwa watulivu, na kuhisi furaha ya kupata tena kitu ambacho kilikuwa kimepotea, na wao pia walihisi watulivu kwa njia tosha ya kuanza kumtegemea na kumtumainia Mwana huyu wa Adamu kwa ujasiri na kwa imani ambaye angeweza kuwasamehe wanadamu dhambi zao. Walianza pia kuomba kwa jina la Bwana Yesu bila ya kusita, kuomba ili kupokea neema Yake, baraka Zake, na kupokea amani na furaha kutoka Kwake, kupata utunzaji na ulinzi kutoka Kwake na kuanza kutenda uponyaji na kupunga mapepo kwa jina la Bwana Yesu.
Katika muda huu ambao Bwana Yesu alifanya kazi katika mwili, wengi wa wafuasi Wake wasingeweza kuthibitisha kikamilifu utambulisho Wake na mambo Aliyoyasema. Wakati aliposulubishwa msalabani, mwelekeo wa wafuasi Wake ulikuwa ule wa matarajio; aliposulubiwa msalabani na kupitishiwa yale yote aliyopitishiwa hadi alipowekwa katika kaburi, mwelekeo wa watu Kwake yeye ulikuwa wa kutoridhika. Wakati huu, watu walikuwa tayari wameanza kusonga katika mioyo yao kutoka katika kushuku hadi kukataa mambo ambayo Bwana Yesu alikuwa amesema wakati Akiwa mwili. Na Alipotembea nje ya kaburi na kujitokeza kwa watu mmoja baada ya mwengine, wengi wa watu ambao walikuwa wamemwona Yeye kwa macho yao au kusikia habari za kufufuka Kwake, walibadilika kwa utaratibu kutoka katika hali ya kumkataa hadi ile ya nadharia ya kushuku. Kufikia muda ule ambao Bwana Yesu alimfanya Tomaso kuuweka mkono wake katika upande Wake, kufikia wakati ambao Bwana Yesu aliuvunja mkate na kuula mbele ya umati wa watu baada ya kufufuka Kwake na baada yake kula kipade cha samaki aliyechemshwa mbele yao, hapo tu ndipo walipokubali kwa kweli Bwana Yesu ni Kristo katika mwili. Mnaweza kusema kwamba ni kana kwamba mwili huu wa kiroho ulio na nyama na damu uliosimama mbele ya hao watu ulikuwa ukizindua kila mmoja wao kutoka katika ndoto. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele yao Ndiye aliyekuwepo tangu miaka hiyo ya nyuma. Alikuwa na umbo, na mwili, na mifupa, na Alikuwa tayari ameishi na kula na wanadamu kwa muda mrefu…. Wakati huu, watu walihisi kwamba uwepo Wake ulikuwa halisi, wa ajabu sana; wote walichangamka na kufurahi mno, na wakati uo huo walijawa na hisia. Na kuonekana Kwake tena kuliwaruhusu watu waweze kuona kwa kweli unyenyekevu Wake, kuhisi ukaribu Wake na tamanio Lake, uhusiano Wake wa karibu na wanadamu. Kupatana huku kwa kufupi kuliwafanya watu waliomwona Bwana Yesu kuhisi kana kwamba muda mrefu umepita. Mioyo yao iliyopotea, kuchanganyikiwa, yenye woga, yenye wasiwasi, inayotarajia na isiyosikia hisia zozote vyote vilipata utulivu. Hawakuwa na shaka tena au kutoridhika tena kwa sababu walihisi kwamba sasa kulikuwa na tumaini na kitu cha kutegemea. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele yao Angekuwa nao milele, Angekuwa mnara wao dhabiti, kimbilio lao la kila wakati.
Ingawa Bwana Yesu alifufuliwa, moyo Wake na kazi Yake vyote havikuwa vimeondoka kwa wanadamu. Aliwaambia watu Alipoonekana ya kwamba haijalishi ni umbo gani Alilokuwemo ndani, Angeandamana na watu, kutembea na wao, na kuwa na wao siku zote na katika sehemu zote. Na nyakati zote na mahali popote, Angewatosheleza wanadamu na kuwachunga, kuwaruhusu kumgusa na kumwona Yeye, na kuhakikisha kwamba hawatawahi kuhisi tena kama wasio na msaada. Bwana Yesu alitaka pia watu wajue yafuatayo: Maisha yao ulimwenguni hawapo pekee. Mwanadamu ana utunzaji wa Mungu, Mungu yuko pamoja nao; watu siku zote wanaweza kumwegemea Mungu; Yeye ndiye familia ya kila mmoja wa wafuasi Wake. Akiwa na Mungu wa kumwegemea, mwanadamu hatawahi tena kuwa mpweke au bila usaidizi, na wale wanaomkubali kama sadaka yao ya dhambi hawataishia katika dhambi tena. Katika macho ya binadamu, sehemu hizi za kazi Zake ambazo Bwana Yesu alitekeleza baada ya kufufuka Kwake zilikuwa chache mno lakini Ninavyoona Mimi, kila kitu kilikuwa na maana yenye thamani sana na zote zilikuwa zenye umuhimu na uzito.
Ingawa muda wa Bwana Yesu kufanya kazi katika mwili ulijaa ugumu na mateso, kupitia katika kuonekana Kwake katika mwili Wake wa kiroho wa mwili na damu, Alikamilisha vyema na kwa njia timilifu kazi Yake ya wakati huo akiwa kwa mwili ili kuwakomboa wanadamu. Aliianza huduma Yake kwa kugeuka mwili na Alihitimisha huduma Yake kwa kujitokeza kwa wanadamu Akiwa katika umbo Lake la mwili. Alikuwa mjumbe wa Enzi ya Neema, Aliianzisha Enzi ya Neema kupitia kwa utambulisho Wake kama Kristo. Kupitia utambulisho Wake kama Kristo, Alitekeleza kazi katika Enzi ya Neema na Akaipatia nguvu na kuwaongoza wafuasi katika Enzi ya Neema. Inaweza kusemwa kuhusu kazi ya Mungu kwamba kwa kweli Yeye humaliza kazi Anayoianza. Kunazo hatua na mpango, na umejaa hekima ya Mungu, kudura Yake, na matendo Yake ya ajabu. Umejaa pia upendo na rehema za Mungu. Bila shaka, uzi mkuu unaotiririka katika kazi yote ya Mungu ni utunzaji Wake kwa binadamu; umejawa na hisia Zake za kujali ambazo Hawezi kuweka pembeni. Katika aya hizi za Biblia, katika kila kitu ambacho Bwana Yesu alifanya baada ya kufufuka Kwake, kile kilichofichuliwa kilikuwa ni matumaini yasiyobadilika ya Mungu na kujali Kwake kwa wanadamu, pamoja na utunzaji wa Mungu wenye umakinifu na kuwathamini wanadamu. Mpaka sasa hakuna chochote kati ya hivi vyote ambacho kimebadilika—unaweza kukiona? Unapoviona hivi, moyo wako haugeuki bila kusukumwa na kuwa karibu na Mungu? Kama uliishi katika enzi hiyo na Bwana Yesu Akakuonekania baada ya kufufuka Kwake, kwa njia ya kushikika ili wewe uweze kuona, na kama Aliketi mbele yako, Akala mkate na samaki na kukuchambulia wewe maandiko, Akaongea na wewe, basi ungehisi vipi? Ungehisi furaha? Je, ungehisi kuwa mwenye hatia? Kutoelewana kwa awali na kuepuka Mungu kwa awali, migogoro na shaka dhidi ya Mungu—hivi vyote havingetoweka tu? Je, unadhani kwamba uhusiano kati ya binadamu na Mungu ungekuwa bora zaidi?
Kupitia kwa ufasiri wa sura hizi finyu za Biblia, uligundua makosa yoyote katika tabia ya Mungu? Uligundua uchafuzi wowote katika upendo wa Mungu? Uliuona udanganyifu au uovu wowote katika kudura ya Mungu au hekima? Bila shaka la! Sasa unaweza kusema kwa uhakika kwamba Mungu ni mtakatifu? Unaweza kusema kwa uhakika kwamba hisia za Mungu zinafichua kiini Chake na tabia kwa ujumla? Natumai kwamba baada ya kuyasoma maneno haya, kile ambacho umeelewa kutoka katika maneno haya kitakusaidia na kukufaidi katika ufuatiliaji wako wa mabadiliko katika tabia na hali ya kumcha Mungu. Natumai pia kwamba maneno haya yataweza kukuzalia matunda ambayo yatakua kila siku, hivyo basi katika mchakato wa ufuatiliaji huu kukuleta karibu na Mungu zaidi na zaidi, wa kukuleta karibu na karibu zaidi na kiwango ambacho Mungu anahitaji, ili usichoke tena na ufuatiliaji wa ukweli na usihisi tena kwamba ufuataji wa ukweli na ule wa mabadiliko katika tabia ni usumbufu au jambo duni. Ni, kwa kweli, udhihirisho wa tabia ya kweli ya Mungu na kiini kitakatifu cha Mungu ambayo yanakupa motisha kutamani mwangaza, kutamani haki, na kuazimia kufuatilia ukweli, kufuatilia ridhaa ya mapenzi ya Mungu, na kuwa binadamu anayepatwa na Mungu, na kuwa mtu halisi.
Leo tumezungumzia baadhi ya mambo ambayo Mungu alifanya katika Enzi ya Neema wakati ambapo Alikuwa mwili kwa mara ya kwanza. Kutoka kwa mambo haya, tumeona tabia ambayo Alionyesha na kuifichua katika mwili, pamoja na kila kipengele cha kile Alicho nacho na kile Alicho. Vipengele hivi vyote vya kile Alicho nacho na kile Alicho vinaonekana kuhisishwa mno, lakini uhalisi ni kwamba kiini cha kila Alichofichua na kuonyesha hakiwezi kutenganishwa na tabia Yake mwenyewe. Kila mbinu na kila dhana ya Mungu mwenye mwili inaonyesha tabia Yake katika ubinadamu na imeunganishwa bila kutenganishwa katika kiini Chake Mwenyewe. Hivyo, ni muhimu sana kwamba Mungu alikuja kwa wanadamu kwa njia ya kuwa mwili na kazi aliyofanya katika mwili ni muhimu sana pia. Na, tabia Aliyoifichua na mapenzi Alionyesha ni muhimu hata sana kwa kila mtu anayeishi katika mwili, kwa kila mtu anayeishi katika upotovu. Je, hili ni jambo ambalo unaweza kuelewa? Baada ya kuelewa tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho, umefanya hitimisho lolote kuhusiana na namna unavyofaa kumtunza Mungu? Katika kulijibu swali hili, kwa hitimisho Ningependa kukupa onyo tatu: Kwanza, usimjaribu Mungu. Haijalishi ni kiasi kipi unachoelewa kuhusu Mungu, haijalishi ni kiwango kipi unachojua kuhusu tabia Yake, kwa vyovyote vile usimjaribu Yeye. Pili, usishindane na Mungu kuhusiana na hadhi. Haijalishi ni aina gani ya hadhi ambayo Mungu anakupa au ni kazi ya aina gani Anayokuaminia kuifanya, haijalishi ni wajibu wa aina gani ambao Atakuinua ili utende, na haijalishi ni kiasi kipi ambacho umegharimika au kujitolea kwa ajili Mungu, kwa vyovyote vile usishindane na Mungu kwa hadhi. Tatu, usishindane na Mungu. Haijalishi kama unaelewa au kama unaweza kutii kile ambacho Mungu anafanya na wewe, kile Anachopanga na wewe, na mambo Anayokuletea wewe, kwa vyovyote vile usishindane na Mungu. Kama unaweza kutekeleza onyo hizi tatu, basi utakuwa salama kwa kiasi fulani, na hutamghadhabisha Mungu kwa urahisi. Hayo ndiyo yote ya kushiriki kwa siku ya leo.
November 23, 2013
Tanbihi:
a. Maandishi ya asili yanaacha “udhihirisho huu wa.”
b. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki, Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni