5. Unahitaji Kusadiki Vipi Mungu Ili Kuweza Kuokolewa na Kufanywa Kuwa Mtimilifu?
Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Ingawa watu wengi wanaamini katika Mungu, ni wachache wanaoelewa ni nini maana ya imani katika Mungu, na ni nini wanachopaswa kufanya ili waupendeze moyo wa Mungu. Hii ni kwa sababu, hata ingawa watu wengi wanalifahamu neno "Mungu" na mafungu ya maneno kama "kazi ya Mungu", hawamjui Mungu, na kwa kiwango cha chini zaidi hawaijui kazi ya Mungu. Si ajabu, basi, wale wote wasiomjua Mungu wamejawa na imani iliyovurugika. Watu hawachukulii imani kwa Mungu kwa makini kwa kuwa kuamini katika Mungu ni jambo geni, jambo lisolo la kawaida sana kwao. Kwa njia hii, hawafikii mahitaji ya Mungu.
Kwa maneno mengine, ikiwa watu hawamjui Mungu, hawajui kazi Yake, basi hawafai kwa matumizi na Mungu, na zaidi ya hayo hawawezi kutimiza hamu ya Mungu. "Imani katika Mungu" inamaanisha kuamini kuwa kuna Mungu; hii ndiyo dhana rahisi zaidi ya imani katika Mungu. Zaidi ya hayo, kuamini kuwa kuna Mungu sio sawa na kuamini katika Mungu kwa ukweli; bali, ni hali ya imani sahili ikiwa na vipengee vya uzito vya kidini. Imani ya kweli katika Mungu ina maana kupitia maneno na kazi ya Mungu kwa msingi wa imani kuwa Mungu ndiye mkuu juu ya vitu vyote. Kwa hivyo mtakuwa huru kutokana na tabia yenu ya upotovu, mtatimiza hamu ya Mungu, na mtapata kumjua Mungu. Ni kwa kupitia safari ya aina hii tu ndio mnaweza kusemekana kuwa mnaamini katika Mungu. Ilhali watu mara nyingi huona kuamini katika Mungu kama jambo rahisi sana na la kipuuzi tu. Imani ya watu wa aina hii haina maana na haitawahi kupata idhini ya Mungu, kwa sababu wanatembea katika njia mbaya. Leo, kuna wale bado wanaamini katika Mungu katika barua, katika mafundisho ya dini yaliyo tupu. Hawana habari kuwa imani yao katika Mungu haina dutu, na hawawezi kupata idhini ya Mungu, na bado wanaomba kupata amani na neema ya kutosha kutoka kwa Mungu. Tunafaa kuweka kituo na kujiuliza wenyewe: Je, kuamini kwa Mungu linaweza kuwa jambo rahisi ya yote duniani? Je, kuamini kwa Mungu hakumaanishi chochote zaidi ya kupokea neema nyingi kutoka kwa Mungu? Je, watu wanaoamini kwa Mungu na hawamjui, na wanaamini kwa Mungu ila wanamuasi; je watu kama hawa wanaweza kutimiza haja za Mungu?
kutoka kwa "Dibaji" kwa Neno Laonekana katika Mwili
Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu. Ingawa ni uamuzi wa watu kama hawa kumfuata Mungu, hawafaidi chochote. Wale wasiopata chochote kwenye mkondo huu ndio watakaotupiliwa mbali, na ni wale watu wanaofanya juhudi za chini zaidi. Haijalishi ni hatua gani ya kazi ya Mungu unayopitia, lazima uandamane na maono makuu. Bila maono kama haya, itakuwa vigumu kwako kukubali kila hatua ya kazi mpya, kwa maana mwanadamu hana uwezo wa kuwaza kuhusu kazi mpya ya Mungu, ni kuu kushinda mawazo ya mwanadamu. Kwa hivyo bila mchungaji kumlinda mwanadamu, bila mchungaji kushirikiana na mwanadamu kuhusu maono hayo, mwanadamu hana uwezo kukubali kazi hii mpya. Iwapo mwanadamu hawezi kupokea maono haya, basi hawezi kupata kazi mpya ya Mungu, na iwapo mwanadamu hawezi kutii kazi mpya ya Mungu, basi mwanadamu hana uwezo wa kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na hivyo ufahamu wake wa Mungu ni bure. Kabla mwanadamu atimilize maneno ya Mungu, lazima ayajue maneno ya Mungu, hivyo ni kusema, aelewe mapenzi ya Mungu; ni kwa njia hii tu ndiyo maneno ya Mungu yanaweza kutekelezwa kwa usahihi na kulingana na moyo wa Mungu. Hili lazima liwe na kila mmoja anayetafuta ukweli, na ndiyo njia ambayo lazima kila mmoja anayejaribu kumjua Mungu aipitie. Njia ya kuyajua maneno ya Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na pia njia ya kuijua kazi ya Mungu. Na hivyo, kujua maono hakuashirii tu kuujua ubinadamu wa Mungu mwenye mwili, lakini pia kunajumuisha kujua maneno na kazi ya Mungu. Kutokana na maneno ya Mungu wanadamu wanapata kuelewa mapenzi ya Mungu, na kutokana na maneno ya Mungu wanapata kuelewa tabia ya Mungu na pia kujua kile Mungu alicho. Imani katika Mungu ndiyo hatua ya kwanza katika kumjua Mungu. Harakati ya kusonga kutoka katika imani ya mwanzo katika Mungu mpaka imani kuu kwa Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na harakati ya kuipitia kazi ya Mungu. Iwapo unaamini kwa Mungu kwa ajili tu ya kuamini kwa Mungu, na huamini kwa Mungu kwa ajili ya kumjua Mungu, basi hakuna ukweli katika imani yako, na haiwezi kuwa safi—kuhusu hili hakuna tashwishi. Iwapo, wakati wa harakati anapopata kumuonja Mungu, mwanadamu anapata kumjua Mungu polepole, basi hatua kwa hatua tabia yake itabadilika pia, na imani yake itaongezeka kuwa ya kweli zaidi. Kwa njia hii, wakati mwanadamu anafaulu katika imani yake kwa Mungu, ataweza kumpata Mungu kwa ukamilifu. Mungu alijitoa pakubwa kuingia katika mwili mara ya pili na kufanya kazi Yake binafsi ili mwanadamu apate kumjua Yeye, na ili mwanadamu aweze kumwona. Kumjua Mungu[a] ndiyo matokeo ya mwisho yanayofikiwa katika mwisho wa kazi ya Mungu; ndilo hitaji la mwisho la Mungu kwa mwanadamu. Anafanya hili kwa ajili ya ushuhuda Wake wa mwisho, na ili kwamba mwanadamu mwishowe na kwa kikamilifu aweze kumgeukia Yeye. Mwanadamu anaweza tu kumpenda Mungu kwa kumjua Mungu, na ili ampende Mungu lazima amjue Mungu. Haijalishi vile anavyotafuta, au kile anachotafuta kupata, lazima aweze kupata ufahamu wa Mungu. Ni kwa njia hii tu ndiyo mwanadamu anaweza kumridhisha Mungu. Ni kwa kumjua Mungu tu ndio mwanadamu anaweza kumwamini Mungu kwa ukweli, na ni kwa kumjua Mungu tu ndio anaweza kumwogopa na kumheshimu Mungu kwa kweli. Wale wasiomjua Mungu hawataweza kumwogopa na kumheshimu Mungu kwa kweli. Kumjua Mungu kunahusisha kujua tabia ya Mungu, kuelewa mapenzi ya Mungu, na kujua kile Mungu alicho. Na haijalishi ni kipengee gani cha kumjua Mungu, kila mojawapo kinamhitaji mwanadamu alipe gharama, na kinahitaji nia ya kutii, ambapo bila hivi hakuna atakayeweza kufuata mpaka mwisho. Kazi ya Mungu hailingani na mawazo ya mwanadamu hata kidogo, tabia ya Mungu na kile Mungu alicho ni vitu vigumu sana kwa mwanadamu kufahamu, na yote Anayosema na kufanya Mungu ni makuu sana yasiyoeleweka na mwanadamu; iwapo mwanadamu anatamani kumfuata Mungu, na hana nia ya kumtii Mungu, basi mwanadamu hatafaidi chochote. Tangu kuumbwa kwa dunia mpaka sasa, Mungu Amefanya kazi nyingi ambayo haieleweki na mwanadamu na ambayo mwanadamu amepata ugumu kuikubali, na Mungu amesema mengi yanayofanya mawazo ya mwanadamu magumu kupona. Ilhali Hajawahi kukomesha kazi Yake kwa sababu mwanadamu ana ugumu mwingi; Ameendelea kufanya kazi na kuzungumza, na hata ingawa idadi kubwa ya "wanajeshi" wameangamia njiani, Yeye bado Anaendelea na kazi Yake, na bado anateua kundi baada ya kundi la watu walio tayari kukubali kazi Yake mpya. Yeye hawahurumii wale "mashujaa" walioangamia, na badala yake anawathamini wale wanaoikubali kazi Yake mpya na maneno. Lakini ni kwa sababu gani ndiyo Anafanya kazi kwa njia hii, hatua kwa hatua? Ni kwa nini Yeye kila mara huwaondoa na kuchagua watu wengine? Ni kwa nini Yeye hutumia mbinu za aina hii kila mara? Kusudi la kazi Yake ni ile wanadamu wapate kumjua, na ili waweze kutwaliwa na Yeye. Kanuni ya kazi Yake ni kufanya kazi kwa wale wanaoweza kutii kazi Anayofanya leo, na sio kufanya kazi kwa wale wanaotii kazi Yake ya zamani, na wanaipinga kazi Yake ya leo. Hii ndiyo sababu hasa Amewafuta na kuwaangamiza watu wengi.
kutoka kwa "Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni imani katika Mungu ili uweze kumtii Mungu, kumpenda Mungu, na kufanya majukumu ambayo kiumbe wa Mungu anapaswa kufanya. Hili ndilo lengo la kuamini katika Mungu. Lazima upate ufahamu wa upendo wa Mungu, jinsi Mungu anavyostahili heshima, jinsi, katika viumbe Vyake, Mungu anafanya kazi ya wokovu na kuwafanya wakamilifu—hicho ndicho kiasi cha chini zaidi unachopaswa kuwa nacho katika imani yako kwa Mungu. Imani kwa Mungu hasa ni mabadiliko kutoka kwa maisha katika mwili kwenda kwa maisha ya kumpenda Mungu, kutoka maisha ya kiasili kwenda kwa maisha katika nafsi ya Mungu, ni kutoka kumilikiwa na Shetani na kuishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, ni kuweza kupata kumtii Mungu na sio kuutii mwili, ni kukubali Mungu kuupata moyo wako wote, kukubali Mungu akufanye mkamilifu, na kujitoa kutoka kwa tabia potovu ya kishetani. Imani kwa Mungu kimsingi ni kwa kuwezesha nguvu na sifa za Mungu kudhihirishwa kwako, ili uweze kutekeleza mapenzi ya Mungu, na kutimiza mpango wa Mungu, na uweze kutoa ushuhuda kwa Mungu mbele ya Shetani. Imani kwa Mungu haipaswi kuwa kwa ajili ya kuona ishara na maajabu, wala haipaswi kuwa kwa ajili ya mwili wako mwenyewe. Inapaswa kuwa kwa ajili ya kutafuta kumjua Mungu, na kuweza kumtii Mungu, na kama Petro, kumtii mpaka kifo. Hili ndilo imani hiyo inapaswa kupata. Kula na kunywa neno la Mungu ni kwa ajili ya kumjua Mungu na kumtosheleza Mungu. Kula na kunywa neno la Mungu kunakupa maarifa kubwa ya Mungu, na ndipo tu utakapoweza kumtii Mungu. Unapomjua tu Mungu ndipo unapoweza kupenda Mungu, na kupatikana kwa lengo hili ndilo lengo la pekee mwanadamu anapaswa kuwa nalo katika imani yake kwa Mungu. Iwapo katika imani yako kwa Mungu, unajaribu kila wakati kuona ishara na maajabu, basi mtazamo wa imani hii kwa Mungu si sahihi. Imani kwa Mungu ni hasa kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha. Ni kuweka tu katika matendo maneno ya Mungu kutoka kwa kinywa Chake na kuyatekeleza mwenyewe ndiko kupatikana kwa lengo la Mungu. Katika kuamini Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kufanywa mkamilifu na Mungu, kuweza kujiwasilisha kwa Mungu, na kumtii Mungu kikamilifu. Iwapo unaweza kumtii Mungu bila kulalamika, kuyajali mapenzi ya Mungu, kupata kimo cha Petro, na kuwa na mtindo wa Petro ilivyozungumziwa na Mungu, basi hapo ndipo utakuwa umefanikiwa katika imani kwa Mungu, na itadhihirisha kuwa umepatwa na Mungu.
kutoka kwa "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa sababu unamsadiki Mungu, lazima ule na kunywa neno Lake, upitie neno Lake, na uishi kwa kudhihirisha neno Lake. Hivi tu ndivyo unavyomsadiki Mungu! Kama unasema umemsadiki Mungu ilhali huwezi kuongea maneno Yake yoyote au kuyatia katika matendo, huchukuliwi kuwa unamsadiki Mungu. Hivi ni "kuutafuta mkate ili kuikabili njaa." … Wanaomwamini Mungu wanafaa kumiliki tabia nzuri kwa nje, angalau, na kilicho na umuhimu mkubwa zaidi ni kuwa na neno la Mungu. Haijalishi ni nini, huwezi kuligeukia neno la Mungu. Maarifa yako katika Mungu na kukamilishwa kwa mapenzi Yake vyote vinatimizwa kupitia kwa neno Lake. Mataifa yote, imani, madhehebu, na sekta zote zitaweza kushindwa kupitia kwa neno kwenye siku za usoni. Mungu ataongea moja kwa moja, na watu wote watashikilia neno la Mungu katika mikono yao; kupitia haya watu watafanywa kuwa watimilifu. Neno la Mungu limeenea kotekote: Watu huongelea neno la Mungu na kutenda kulingana na neno la Mungu, huku likiwa limehifadhiwa ndani bado huwa ni neno la Mungu. Kwa ndani na hata kwa nje, wanarowekwa katika neno la Mungu, na hivyo basi wanafanywa kuwa watimilifu. Wale wanaokamilisha mapenzi ya Mungu na wanaweza kumshuhudia Yeye ndio wale walio na neno la Mungu kama uhalisi.
Kuingia katika Enzi ya Neno, yaani, Enzi ya Ufalme wa Milenia, ndiyo kazi ambayo inakamilishwa sasa. Kuanzia sasa, fanya mazoezi ya kushiriki kuhusu neno la Mungu. Ni kupitia tu kula na kunywa neno Lake na kulipitia ndipo unapoweza kuonyesha neno la Mungu. Ni kupitia tu maneno yako ya uzoefu ndipo wengine wanapoweza kushawishika na wewe. Kama huna neno la Mungu, hakuna atakayeshawishika! Wale wote wanaotumiwa na Mungu wanaweza kuongea neno la Mungu. Kama huwezi, hii yaonyesha kwamba Roho Mtakatifu bado hajakufanyia kazi na ungali bado hujafanywa kuwa mtimilifu. Huu ndio umuhimu wa neno la Mungu.
kutoka kwa "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mchakato ambamo watu huyapitia maneno ya Mungu ni sawa na mchakato ambamo wanafahamu kujitokeza kwa maneno ya Mungu katika mwili. Kadiri watu wanavyoyapitia maneno ya Mungu, ndivyo wanavyomjua Roho wa Mungu; kwa kuyapitia maneno ya Mungu, watu wanaelewa kanuni za kazi ya Roho na kupata kumjua Mungu wa vitendo Mwenyewe. Kwa hakika, Mungu akiwafanya watu wakamilifu na kuwachukua, Anawafanya wayajue matendo ya Mungu wa vitendo; Anatumia kazi ya Mungu wa vitendo kuwaonyesha watu umuhimu halisi wa kupata mwili, na kuwaonyesha kuwa Roho wa Mungu hakika ameonekana kwa mwanadamu. Watu wakichukuliwa na kufanywa wakamilifu na Mungu, maonyesho ya Mungu wa vitendo huwa amewashinda, maneno ya Mungu wa vitendo huwa yamewabadilisha, na kutoa uzima Wake ndani yao, kuwajaza na kile Alicho (iwe ni uwepo wake wa binadamu, au ule wa uungu), kuwajaza kwa kiini cha maneno Yake, na kuwafanya watu waishi kwa kudhihirisha maneno Yake. Mungu akiwapata watu, kimsingi Anafanya hivyo kwa kutumia maneno na matamko ya Mungu wa vitendo ili kuushughulikia upungufu wa watu, na kuhukumu na kufichua tabia zao za uasi, kuwafanya wapate wanachokihitaji, na kuwaonyesha kuwa Mungu yuko miongoni mwa wanadamu. Muhimu zaidi, kazi ifanywayo na Mungu wa vitendo ni kumwokoa kila mtu kutoka katika ushawishi wa Shetani, kuwatoa katika nchi ya uchafu, na kuziondoa tabia zao potovu. Umuhimu mkubwa zaidi wa watu kupatikana na Mungu wa vitendo ni kuwa na uwezo wa kumfanya Mungu wa vitendo kielelezo, na kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida, kuweza kutenda kulingana na maneno na mahitaji ya Mungu wa vitendo, bila upotofu au kuteleza, kutenda kama Asemavyo, na kuweza kufanikisha lolote Atakalo. Kwa njia hii, utakuwa umepatwa na Mungu.
kutoka kwa "Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kadiri ufahamu wako wa maneno ya Mungu ulivyo mkuu na kadiri unavyoyatia kwenye matendo, ndivyo unavyoweza kuingia kwenye njia ya kufanywa mtimilifu na Mungu haraka. Kupitia kuomba, unaweza kufanywa mtimilifu katikati ya maombi; kwa kula na kunywa maneno ya Mungu, kuelewa kiini cha maneno ya Mungu, na kuishi kwa kudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu, unaweza kufanywa kuwa mtimilifu. Kupitia uzoefu wa maneno ya Mungu kila siku, unapata kujua kile unachokosa ndani yako, na, zaidi ya hayo, unapata kujua udhaifu wako na upungufu, na unatoa sala kwa Mungu, ambayo kwayo utafanywa mtimilifu polepole. Njia za kufanywa mtimilifu: kuomba, kula na kunywa maneno ya Mungu, kuelewa kiini cha maneno ya Mungu, kuingia katika uzoefu wa maneno ya Mungu, kuja kujua kinachokosa ndani yako, kuitii kazi ya Mungu, kuzingatia mzigo wa Mungu na kuunyima mwili kwa kupitia moyo wako wa upendo, na kuwa na ushirika wa mara kwa mara na ndugu, ambayo yanaboresha uzoefu wako. Iwe ni maisha ya jumuiya au maisha yako binafsi, na iwe ni makusanyiko makubwa au madogo, yote yanaweza kukuwezesha kupata uzoefu na kupata mafunzo ili moyo wako uwe na utulivu mbele ya Mungu na kurudi kwa Mungu. Haya yote ni mchakato wa kufanywa mtimilifu. Kuyapitia maneno ya Mungu ambayo yamesemwa kunamaanisha kuwa na uwezo wa kwa kweli kuyaonja maneno ya Mungu na kuyaruhusu yaweze kuishi kwa kudhihirishwa ndani yako ili uwe na imani kubwa na upendo kwa Mungu. Kupitia njia hii, utaondoa tabia potovu ya kishetani polepole, utaachana na motisha isiyofaa polepole, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kawaida. Kadiri upendo kwa Mungu ndani yako unavyozidi kuwa mkuu—yaani, kadiri unavyozidi kufanywa mtimilifu na Mungu mara nyingi—ndivyo unayopotoshwa na Shetani kwa kiasi kidogo. Kupitia uzoefu wako wa vitendo, utaingia kwenye njia ya kufanywa mtimilifu polepole. Hivyo, ikiwa unataka kufanywa mtimilifu, kuzingatia mapenzi ya Mungu na kuyapitia maneno ya Mungu hasa ni muhimu sana.
kutoka kwa "Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Baada ya hapo ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa.
kutoka kwa "Je, Umekuwa Hai Tena?" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu huwakamilisha watu kupitia utii wao, kupitia kula kwao, kunywa na kufurahia maneno ya Mungu, na kupitia mateso na usafishaji maishani mwao. Ni kupitia tu imani kama hii ndipo tabia za watu zinaweza kubadilika, baada ya hapo tu ndipo wanaweza kuwa na maarifa ya kweli kuhusu Mungu. Kutoridhika na kuishi katikati ya neema za Mungu, kuwa na kiu cha ukweli, na kutafuta ukweli, na kunuia kuchumwa na Mungu—hii ndio maana ya kumtii Mungu katika hali ya utambuzi; hii ndiyo aina ya imani ambayo Mungu anataka.
kutoka kwa "Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni lazima utafute uzima. Leo, wale watakaofanywa wakamilifu ni wa aina sawa na Petro: ni wale ambao hutafuta mabadiliko katika tabia yao wenyewe, na wako tayari kuwa na ushuhuda kwa Mungu na kutekeleza wajibu wao kama kiumbe wa Mungu. Ni watu kama hawa pekee watakaofanywa wakamilifu. Kama wewe tu unatazamia tuzo, na hutafuti kubadilisha tabia ya maisha yako mwenyewe, basi juhudi zako zote zitakuwa za bure—na huu ni ukweli usiobadilika!
kutoka kwa "Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea" katika Neno Laonekana katika Mwili
Je, "kubadailishwa kwa tabia" ni nini? Lazima uwe mpenzi wa ukweli, uikubali hukumu na kuadibiwa na neno la Mungu unapopitia kazi Yake, na kupitia aina zote za mateso na kusafishwa, ambayo kwayo unatakaswa kutokana na sumu ya kishetani iliyo ndani yako. … Mabadiliko katika tabia yanamaanisha kuwa mtu, kwa sababu anapenda na anaweza kuukubali ukweli, hatimaye huja kujua asili yake ya uasi na ya kumpinga Mungu; anaelewa kuwa upotovu wa mwanadamu ni wenye kina zaidi na kuelewa upumbavu na udanganyifu wa mwanadamu. Anajua uduni wa mwanadamu na kusikitisha kwake, na hatimaye anaelewa kiini cha asili ya mwanadamu. Kwa kujua haya yote, anaweza kujikana na kujinyima kabisa, kuishi kwa neno la Mungu, na kutenda ukweli katika kila kitu. Mtu wa aina hii anamjua Mungu na tabia yake imebadilishwa.
kutoka kwa "Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Mgeuzo katika tabia hasa huhusu mgeuzo katika asili yako. Asili si kitu unachoweza kuona kutoka kwa mienendo ya nje; asili inahusisha moja kwa moja thamani na umuhimu wa kuishi kwa watu. Inahusisha moja kwa moja maadili ya maisha ya binadamu, mambo yaliyo ndani kabisa ya nafsi, na kiini cha watu. Kama watu hawangeweza kukubali ukweli, basi hawangekuwa na migeuzo katika hali hizi. Ni kama watu wamepitia kazi ya Mungu tu na wameingia kwa ukamilifu katika ukweli, wamebadilisha maadili na mitazamo yao kuhusu kuishi na maisha, wameyatazama mambo kwa njia sawa na Mungu, na wamekuwa na uwezo wa kutii na kujitoa kabisa kwa Mungu ndio tabia zao zinaweza kusemekana zimebadilika.
kutoka kwa "Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Baada ya kupitia kwa kiwango fulani, maoni ya maisha ya mtu, umuhimu wa kuwepo, na msingi wa kuwepo utabadilika kabisa. Hiyo ni kwamba mtazaliwa tena, na kuwa watu tofauti kabisa. Hili ni la kushangaza! Haya ni mabadiliko makubwa; ni mabadiliko ambayo hugeuza kila kitu pindu. Utahisi kwamba umaarufu, faida, msimamo, mali, anasa, na utukufu wa dunia havina maana na kwamba una uwezo wa kuviachilia kwa urahisi. Huyu ni mtu katika mfano wa mwanadamu. Wale ambao hatimaye wamekamilishwa watakuwa kikundi kama hiki. Wao wataishi kwa ajili ya ukweli, kwa ajili ya Mungu, na kwa ajili haki. Huu ni mfano wa mtu.
kutoka kwa "Kuelewa Visawe na Tofauti katika Asili ya Binadamu" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Ni tu pale ambapo mtu anamjua Mungu na kuwa na ukweli ndipo huishi nuruni; na ni pale tu ambapo maoni yake ya dunia na maoni yake ya maisha yanabadilika ndipo anabadilika kimsingi. Anapokuwa na lengo la maisha na kujiheshimu kulingana na ukweli; anapomtii Mungu kabisa na kuishi kwa neno la Mungu; anapohisi kuhakikishiwa na kuchangamshwa ndani ya moyo wake; moyo wake unapokuwa huru bila giza; na anapoishi kikamilifu na kwa huru na bila kuzuiwa kenye uwepo wa Mungu—hapo tu ndipo atakapoishi maisha ya mwanadamu ya kweli na kuwa mtu anayemiliki ukweli. Aidha, ukweli wote ulio nao unatoka kwa neno la Mungu na kwa Mungu Mwenyewe. Mtawala wa ulimwengu mzima na kila kitu—Mungu Mkuu Zaidi—Anakupenda wewe, kama mwadamu halisi anayeishi maisha ya kweli ya mwanadamu. Je, nini linaweza kuwa la maana zaidi kuliko hili? Mtu wa aina hii ni yule aliye na ukweli.
kutoka kwa "Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Tanbihi:
a. Nakala ya kwanza inasema "Kazi ya kumjua Mungu."
Kutoka Kwa Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu (Mambo Muhimu ya Muumini Mpya)
Tufuate: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni