Alhamisi, 23 Novemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

(Sehemu ya Kwanza)
Mwenyezi Mungu alisema, Leo tunawasiliana kuhusu mada muhimu. Hii ni mada ambayo imezungumziwa tangu kuanza kwa kazi ya Mungu mpaka sasa, na inayo umuhimu mkuu kwa kila mtu. Kwa maneno mengine, hili ni suala ambalo kila mmoja atakutana nalo kwenye mchakato wote wa kusadiki kwake katika Mungu na suala ambalo lazima lizungumziwe. Ni suala muhimu, lisiloepukika ambalo mwanadamu hawezi kujitenganisha nalo. Tukizungumzia umuhimu, ni nini kitu muhimu zaidi kwa kila muumini katika Mungu?  Baadhi ya watu wanafikiri kwamba kitu muhimu zaidi ni kuyaelewa mapenzi ya Mungu; baadhi wanasadiki ni muhimu zaidi kula na kunywa maneno ya Mungu; baadhi wanahisi kitu muhimu zaidi ni kujijua wenyewe; wengine wanayo maoni kwamba kitu muhimu zaidi ni kujua namna ya kupata wokovu kupitia kwa Mungu, namna ya kumfuata Mungu, na namna ya kuyatimiza mapenzi ya Mungu. Tutayaweka masuala haya yote pembeni kwa leo. Hivyo basi ni nini tunachozungumzia? Tunazungumzia mada kuhusu Mungu. Je, hii ndiyo mada muhimu zaidi kwa kila mtu? Maudhui ya mada kuhusu Mungu ni yapi? Bila shaka, mada hii haiwezi kamwe kutenganishwa na tabia ya Mungu, kiini cha Mungu na kazi ya Mungu. Hivyo leo, hebu tuzungumzie “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe.”
Tangu wakati binadamu walipoanza kumsadiki Mungu, wamekuwa wakikutana na mada kama vile kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Inapokuja kwa kazi ya Mungu, baadhi ya watu watasema: “Sisi ndio tunaofanyiwa kazi ya Mungu; tunaipitia kila siku, na hivyo basi tumezoeana nayo.” Na kuhusiana na tabia ya Mungu, baadhi ya watu watasema: “Tabia ya Mungu ni mada tunayoisoma, kuchunguza, na kuzingatia katika maisha yetu yote, hivyo basi tunafaa kuzoeana nayo.” Na kama ni Mungu Mwenyewe, baadhi ya watu watasema: “Mungu Mwenyewe ndiye tunayemfuata, tuliye na imani Kwake, na ndiye tunayemfuata, hivyo tumejuzwa pia kuhusu Yeye.” Mungu hajawahi kukomesha kazi Yake tangu uumbaji, wakati wote huu Ameendelea kuonyesha tabia Yake na kutumia njia mbalimbali kuonyesha neno Lake. Wakati huohuo, hajawahi kusita kujionyesha Yeye Mwenyewe na kiini Chake kwa mwanadamu, akionyesha mapenzi Yake kwa binadamu na kile Anachohitaji kutoka kwa huyo binadamu. Hivyo kutoka katika mtazamo wa moja kwa moja, mada hizi hazifai kuwa za kigeni kwa yeyote yule. Kwa watu wanaomfuata Mungu leo, hata hivyo, Kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe kwa hakika ni mambo ambayo hayajulikani kwao. Kwa nini hali iko hivi? Kwa kadri binadamu anapopitia kazi ya Mungu, anawasiliana pia na Mungu, na kuwafanya kuhisi ni kana kwamba wanaelewa tabia ya Mungu au wanajua sehemu kidogo kuhusu vile inavyofanana. Hivyo basi, binadamu hafikiri kuwa yeye ni mgeni katika kazi ya Mungu au tabia ya Mungu. Badala yake, binadamu anafikiri ni mwenyeji kabisa na Mungu na anaelewa mengi kuhusu Mungu. Lakini kulingana na hali ya sasa, uelewa wa watu wengi kumhusu Mungu umezuiliwa katika kile walichosoma vitabuni, na upana mfinyu wa kile walichopitia wao binafsi, wakiwa wamezuiliwa na kufikiria kwao, na zaidi ya yote, ukiwa umewekewa mipaka ya ukweli wanaoweza kuona kwa macho yao binafsi. Haya yote yapo mbali sana na Mungu Mwenyewe wa kweli. Sasa huu umbali upo “mbali” vipi? Pengine binadamu mwenyewe hana hakika, au pengine binadamu anayo dhana, ana fununu kiasi—lakini kwake Mungu Mwenyewe, uelewa wa binadamu kumhusu Yeye u mbali sana na kiini cha Mungu Mwenyewe wa kweli. Hii ndiyo maana tunahitajika kutumia mada kama “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe” ili kuwasilisha ujumbe huu hatua kwa hatua na kwa njia mahususi.
Kwa hakika, tabia ya Mungu iko wazi kwa kila mmoja na haijafichwa, kwa sababu Mungu hajawahi kuepuka kimakusudi mtu yeyote na Hajawahi kimakusudi kujaribu kujificha Mwenyewe ili watu wasiweze kumjua Yeye au kumwelewa Yeye. Tabia ya Mungu siku zote imekuwa wazi na siku zote imekuwa ikitazama kila mtu kwa njia ya uwazi. Katika usimamizi wa Mungu, Mungu hufanya kazi Yake akitazama kila mmoja; na kazi Yake ndiyo inafanywa kwa kila mtu. Anapofanya kazi hii, Anafichua bila kusita tabia Yake, huku Akitumia bila kusita kiini Chake na kile Anacho na alicho kuongoza na kukimu kila mmoja. Katika kila enzi na kila awamu, licha ya kama hali ni nzuri au mbaya, tabia ya Mungu siku zote iko wazi kwa kila mtu binafsi, na vile vitu Anavyomiliki na uwepo Wake siku zote viko wazi kwa kila mtu binafsi, kwa njia sawa kwamba maisha Yake yanamtoshelezea mwanadamu kila wakati na bila kusita na kumsaidia mwanadamu. Licha ya haya yote, tabia ya Mungu inabakia fiche kwa baadhi ya watu. Kwa nini iko hivyo? Ni kwa sababu ingawaje watu hawa wanaishi ndani ya kazi ya Mungu na wanamfuata Mungu, hawajawahi kutafuta kuelewa Mungu au kutaka kumjua Mungu, sikwambii hata kumkaribia Mungu. Kwa watu hawa, kuelewa tabia ya Mungu kunamaanisha mwisho wao wawadia; kwa maanisha karibu wanahukumiwa na kushtakiwa na tabia ya Mungu. Hivyo basi, watu hawa hawajawahi kutamani kuelewa Mungu au tabia Yake, na hawatamani uelewa au maarifa ya kina ya mapenzi ya Mungu. Hawanuii kufahamu mapenzi ya Mungu kupitia ushirikiano wa kimakusudi—wanafurahia tu milele na hawachoki kufanya mambo wanayotaka kuyafanya; kusadiki kwa Mungu wanayetaka kusadiki kwake; kusadiki kwa Mungu anayekuwepo tu katika dhana zao, Mungu anayekuwepo tu katika fikira zao, Mungu anayekuwepo tu katika dhana zao; na kusadiki kwa Mungu asiyeweza kutenganishwa na wao katika maisha yao ya kila siku. Na kwake Mungu Mwenyewe wa kweli, wanapuuza kabisa, hawataki kusikia mambo ya Mungu na hawana tamanio la kumwelewa Yeye, kumtilia maanani Yeye, na hata hawana nia kidogo ya kuwa karibu zaidi na Yeye. Wanayatumia tu maneno ambayo Mungu anayaonyesha ili kuweza kujipamba, kujiandaa upya. Kwa wao, hilo tayari linawafanya kuwa waumini wenye mafanikio na watu walio na imani kwa Mungu ndani ya mioyo yao. Ndani ya mioyo yao, wanaongozwa na kufikiria kwao, dhana zao, na hata ufasili wao binafsi wa Mungu. Mungu Mwenyewe wa kweli, kwa mkono mwingine, hana chochote kuhusiana na wao. Kwa sababu pindi wanapomwelewa Mungu Mwenyewe wa kweli, kuelewa tabia ya Mungu ya kweli, na kuelewa kile Mungu anacho na alicho, hii inamaanisha kwamba vitendo vyao, imani yao, na yale yote wanayoyafuatilia yatashutumiwa. Na ndiyo maana hawako radhi kukielewa kiini cha Mungu, na ndiyo maana wanasitasita na hawako radhi kutafuta kwa bidii au kuomba kumwelewa zaidi Mungu, kupata kujua zaidi kuhusu mapenzi Yake Mungu, na kuelewa kwa njia bora zaidi tabia ya Mungu. Afadhali Mungu kwao awe kitu kilichotungwa, kisicho na chochote na kibaya. Afadhali kwao Mungu awe mtu ambaye yupo hasa vile ambavyo wamemfikiria Yeye, Anayeweza kunyenyekea mbele zao, Asiyeishiwa na ujazo na Anayepatikana siku zote. Wanapotaka kufurahia neema ya Mungu, wanamuomba Mungu kuwa hiyo neema. Wanapohitaji baraka za Mungu, wanamuomba Mungu kuwa baraka hizo. Wanapokabiliwa na dhiki, wanamwomba Mungu kuwatia wao moyo, na kuwa usalama wao. Maarifa ya watu hawa kumhusu Mungu imebakia palepale pa mipaka ya neema na baraka. Uelewa wao wa kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu umezuiliwa pia na kufikiria kwao na vilevile barua na mafundisho ya kidini tu. Lakini wapo baadhi ya watu walio na hamu ya kuielewa tabia ya Mungu, wanaotaka kumwona Mungu Mwenyewe kwa kweli, na kuielewa tabia ya Mungu kwa kweli na kile Anacho na alicho. Watu hawa wanautafuta uhalisia wa ukweli na wokovu wa Mungu na wanatafuta kupokea ushindi, wokovu, na utimilifu wa Mungu. Watu hawa wanaitumia mioyo yao kulisoma neno la Mungu, wanaitumia mioyo yao kuthamini hali na kila mtu, tukio, au kitu ambacho Mungu amewapangia, na kuomba na kutafuta kwa uaminifu. Kile wanachotaka zaidi ni kuyajua mapenzi ya Mungu na kuielewa tabia ya kweli na kiini cha Mungu. Hivi ndivyo ilivyo ili wasiweze tena kumkosea Mungu, na kupitia kwa mambo waliyoyapitia, waweze kuona upendo zaidi wa Mungu na upande Wake wa kweli. Iko hivyo pia ili Mungu halisi na wa kweli ataweza kuwepo ndani ya mioyo yao, na ili Mungu atakuwa na nafasi katika mioyo yao, kiasi cha kwamba hawatakuwa wakiishi tena miongoni mwa kufikiria, dhana, au hali ya kuyaepuka mambo. Kwa watu hawa, sababu inayowafanya kuwa na tamanio kuu la kuielewa tabia ya Mungu na kiini Chake ni kwa sababu tabia ya Mungu na kiini Chake ni mambo ambayo mwanadamu anaweza kuyahitaji wakati wowote katika uzoefu wao, mambo yanayojaza uhai katika maisha yao yote walioishi. Pindi wanapoielewa tabia ya Mungu, wataweza kumheshimu sana kwa njia bora zaidi, kushirikiana kwa njia bora zaidi na kazi ya Mungu, na kuyaweka zaidi katika fikira mapenzi ya Mungu na kutekeleza wajibu wao kwa njia bora zaidi wakitumia uwezo wao. Hawa ndio watu wa aina mbili inapokuja katika mielekeo yao kwa tabia ya Mungu. Watu wa aina ya kwanza hawataki kuielewa tabia ya Mungu. Ingawaje wanasema wanataka kuielewa tabia ya Mungu, kupata kumjua Mungu Mwenyewe, kuona kile Mungu anacho na alicho, na kushukuru kwa dhati mapenzi ya Mungu, ndani yao kabisa wanaona afadhali Mungu asikuwepo. Ni kwa sababu watu wa aina hii wanakosa kumtii Mungu kila wakati na wanampinga; wanapigana na Mungu kwa sababu ya vyeo vilivyo ndani ya mioyo yao na mara nyingi wanashuku na hata kukataa uwepo wa Mungu. Hawataki kuruhusu tabia ya Mungu au kuacha Mungu mwenyewe wa kweli kumiliki mioyo yao. Wanataka tu kutosheleza matamanio, kufikiria, na maono yao binafsi. Hivyo basi, watu hawa wanaweza kumsadiki Mungu, kumfuata Mungu, na hata wanaweza kutupilia mbali familia na kazi zao kwa sababu Yake Yeye, lakini hawasitishi njia zao za maovu. Baadhi yao hata huiba au kubadhiri sadaka au kumlaani Mungu kisirisiri, huku wengine wakiweza kutumia vyeo vyao kushuhudia mara kwa mara kuhusu wao wenyewe, kujiongezea zaidi umaarufu wao, na kushindana na Mungu kwa ajili ya watu na hadhi. Wanatumia mbinu na njia mbalimbali kuwafanya watu kuwaabudu, kujaribu mara kwa mara kuwa na ufuasi mkubwa wa watu na kutaka kuwadhibiti watu hao. Baadhi hata hupotosha kimakusudi watu na kuwafanya kufikiria kwamba wao ni Mungu ili waweze kuchukuliwa kama Mungu. Hawawezi katu kuwaambia watu kwamba wamepotoshwa, kwamba pia wao wamepotoka na wana kiburi, na hivyo basi hawafai kuwaabudu, na kwamba haijalishi watafanya vyema kiasi kipi, haya yote ni kutokana na utukuzaji wa Mungu na kile wanachostahili kufanya kwa kweli. Kwa nini hawasemi mambo haya? Kwa sababu wana hofu kuu ya kupoteza nafasi yao ndani ya mioyo ya watu. Hii ndiyo maana watu kama hao hawamtukuzi Mungu katu na katu hawamshuhudii Mungu, kwani hawajawahi kujaribu kumwelewa Mungu. Wanaweza kumjua Mungu kama hawamwelewi? Haiwezekani! Hivyo, ingawa maneno katika mada “kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu mwenyewe” yanaweza kuwa rahisi, maana yao ni tofauti kwa kila mmoja. Kwa mtu anayekosa kumtii Mungu mara kwa mara, na anampinga Mungu na ni mkatili kwa Mungu, yanamaanisha shutuma; huku kwa mtu anayefuatilia uhalisia wa kweli na mara nyingi anakuja mbele ya Mungu kutafuta mapenzi ya Mungu, maneno hayo bila shaka ni kama samaki na maji. Hivyo miongoni mwenu, wakati baadhi yenu mnaposikiza mazungumzo ya tabia ya Mungu na kazi ya Mungu, wanaanza kuumwa na kichwa, mioyo yao inajaa upinzani, na wanakuwa katika hali isiyo na utulivu kabisa. Lakini kuna wengine miongoni mwenu wanaofikiria: Mada hii ndiyo hasa Ninayohitaji, kwa sababu mada hii ni yenye manufaa sana kwangu. Ni sehemu ambayo haiwezi kukosekana katika uzoefu wangu wa maisha; ni swali ambalo halijapata jibu bado, msingi wa imani kwa Mungu, na jambo ambalo mwanadamu hawezi kufikiria kuliacha. Kwenu nyote, mada hii inaweza kuonekana kuwa karibu na mbali, isiyojulikana ilhali inayozoeleka. Lakini haijalishi ni nini, hii ni mada ambayo kila mmoja aliyeketi hapa lazima aisikilize, aijue, na lazima aielewe. Haijalishi ni vipi utakavyoishughulikia, haijalishi ni vipi utakavyoiangalia au utakavyoipokea, lakini umuhimu wa mada hii huwezi kupuuzwa.
Mungu amekuwa akifanya kazi Yake tangu Alipomuumba mwanadamu. Mwanzoni, kazi ilikuwa rahisi sana, lakini hata hivyo, ingali ilikuwa na maonyesho ya kiini na tabia ya Mungu. Ingawa kazi ya Mungu sasa imepandishwa daraja, na Yeye akitia kiwango kikubwa mno cha kazi thabiti kwa kila mmoja anayemfuata Yeye, na kuonyesha kiwango kikubwa cha neno Lake, kuanzia mwanzo hadi sasa, nafsi ya Mungu imekuwa ikifichwa kutoka kwa mwanadamu. Ingawaje amekuwa mwili mara mbili, kuanzia wakati wa simulizi za biblia hadi kwa siku za kisasa, nani amewahi kuona nafsi halisi ya Mungu? Kutokana na uelewa wenu, yupo mtu amewahi kuona nafsi halisi ya Mungu? La. Hakuna aliyewahi kuona nafsi halisi ya Mungu, kumaanisha hakuna aliyewahi kuona nafsi ya kweli ya Mungu. Hili ni jambo ambalo kila mmoja anakubaliana nalo. Hivi ni kusema, nafsi halisi ya Mungu, au Roho wa Mungu, amefichwa kutoka kwa binadamu wote, wakiwemo Adamu na hawa, ambao Aliwaumba, na akiwemo Ayubu mwenye haki, ambaye alikuwa Amemkubali. Hata wao hawakuona nafsi halisi ya Mungu. Lakini kwa nini Mungu anaficha kimakusudi nafsi Yake halisi? Baadhi ya watu husema: “Mungu anaogopa kuwaogofya watu.” Wengine husema: “Mungu huficha nafsi Yake halisi kwa sababu binadamu ni mdogo sana na Mungu ni mkubwa sana; wanadamu hawaruhusiwi kumwona Yeye, la sivyo watakufa.” Wapo pia wale wanaosema: “Mungu ameshughulika sana akisimamia kazi Yake kila siku, huenda Asiwe na muda wa kuonekana na kuruhusu watu kumwona Yeye.” Haijalishi ni nini mnachosadiki, Ninayo hitimisho hapa. Hitimisho hilo ni nini? Ni kwamba Mungu hataki hata watu kuona nafsi Yake halisi. Akiwa amefichwa kutoka kwa binadamu ni kitu ambacho Mungu anafanya kimakusudi. Kwa maneno mengine, ni nia ya Mungu kwa watu kutoona nafsi Yake halisi. Hili linafaa kuwa wazi kwa wote sasa. Kama Mungu hajawahi kuonyesha nafsi Yake kwa yeyote, basi mnafikiria nafsi ya Mungu ipo? (Ipo.) Bila shaka ipo. Uwepo wa nafsi ya Mungu haupingiki. Lakini kuhusu nafsi ya Mungu ni kubwa vipi au inafanana vipi, haya ni maswali ambayo mwanadamu anafaa kuchunguza? La. Jibu ni la. Kama nafsi ya Mungu si mada ambayo tunafaa kuchunguza, basi ni swali lipi ambalo tunafaa kuchunguza? (Tabia ya Mungu.) (Kazi ya Mungu.) Kabla hatujaanza kuwasiliana mada hii rasmi, hata hivyo, hebu turudi katika kile tulichokuwa tukikizungumzia muda mfupi uliopita: Kwa nini Mungu hajawahi kuonyesha nafsi Yake kwa mwanadamu? Kwa nini Mungu anaficha kimakusudi nafsi Yake kutoka kwa mwanadamu? Kunayo sababu moja tu, nayo ni: Ingawaje binadamu aliyeumbwa amepitia miaka elfu na elfu ya kazi ya Mungu, hakuna hata mtu mmoja anayejua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na kiini cha Mungu. Watu kama hao, mbele ya macho ya Mungu, ni upinzani kwake Yeye, na Mungu hatajionyesha kwa watu walio wakatili kwake Yeye. Hii ndiyo sababu ya pekee mbona Mungu hajawahi kumwonyesha binadamu nafsi Yake na ndiyo sababu anaikinga yeye kimakusudi nafsi Yake dhidi yao. Sasa mnaelewa kuhusu umuhimu wa kujua tabia ya Mungu?

kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni