Jumapili, 17 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II | (Sehemu ya Nane)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia,

Ingawaje Mungu Amefichwa Kutoka kwa Binadamu, Matendo Yake Miongoni mwa Mambo Yote Yanatosha Binadamu Kumjua Yeye

Mwenyezi Mungu alisema, Ayubu alikuwa hajauona uso wa Mungu, wala kusikia matamshi yaliyoongelewa na Mungu, isitoshe yeye mwenyewe binafsi alikuwa hajapitia kazi ya Mungu, lakini kumcha kwake Mungu na ushuhuda aliyokuwa nao wakati wa majaribio kunashuhudiwa na kila mmoja, na kunapendwa, kunafurahiwa, na kupongezwa na Mungu na watu wakayaonea wivu na kuvutiwa nayo, na vilevile, wakaimba nyimbo zao za sifa. Hakukuwepo chochote kikubwa au kisicho cha kawaida kuhusu maisha yake: Kama vile tu mtu yeyote wa kawaida, aliishi maisha yasiyo ya kina, akienda kufanya kazi wakati wa macheo na akirudi nyumbani kupumzika wakati wa magharibi. Tofauti ni kwamba wakati wa miongo hii mbalimbali isiyo ya kina, alipata maono kuhusu njia ya Mungu, na akatambua na kuelewa nguvu kubwa na ukuu wa Mungu, kuliko mtu yeyote mwingine.. Hakuwa mwerevu zaidi kuliko mtu yeyote wa kawaida, maisha yake hayakukuwa sanasana yenye ushupavu, wala, zaidi, yeye hakuwa na mbinu maalum zisizoonekana. Kile alichomiliki, hata hivyo, kilikuwa ni hulka iliyokuwa na uaminifu, upole, unyofu, na hulka iliyopenda kutopendelea na haki, na iliyopenda mambo mazuri—hakuna kati ya haya aliyomiliki yalimilikiwa na watu wa kawaida wengi. Alitofautisha kati ya upendo na chuki, alikuwa na hisia ya haki, hakukubali kushindwa na alikuwa hakati tamaa, na alikuwa mwenye bidii katika fikira zake, na hivyo basi wakati wake usio wa kina duniani aliyaona mambo yote yasiyo ya kawaida ambayo Mungu alikuwa amefanya, na akauona ukubwa, utakatifu, na uhaki wa Mungu, aliona kujali kwa Mungu, neema yake, na ulinzi wake wa binadamu, na kuona utukufu na mamlaka ya Mungu mwenye mamlaka zaidi. Sababu ya kwanza iliyomfanya Ayubu kuweza kupata mambo haya yaliyokuwa zaidi ya mtu yeyote wa kawaida ilikuwa ni kwa sababu alikuwa na moyo safi, na moyo wake ulimilikiwa na Mungu na kuongozwa na Muumba. Sababu ya pili ilikuwa ni ufuatiliaji wake: ufuatiliaji wake wa kuwa maasumu, na mtimilifu, na mtu aliyekubaliana na mapenzi ya Mbinguni, aliyependwa na Mungu, na kujiepusha na uovu. Ayubu alimiliki na kufuata mambo haya huku akiwa hawezi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu; ingawaje alikuwa hajawahi kumwona Mungu, alikuwa amejua mbinu ambazo Mungu alitawala mambo yote, na kuelewa hekima ambayo Mungu anatumia ili kufanya hivyo. Ingawaje alikuwa hajawahi kusikia maneno ambayo yalikuwa yametamkwa na Mungu, Ayubu alijua kwamba matendo ya kutuna binadamu na kuchukua kutoka kwa binadamu yote yalitoka kwa Mungu. Ingawaje miaka ya maisha yake haikuwa tofauti na ile ya mtu wa kawaida, hakuruhusu ukosefu wa kina hiki cha maisha yake kuathiri maarifa yake ya ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, au kuathiri kufuata kwake kwa njia za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Katika macho yake, sheria za mambo yote zilijaa matendo ya Mungu na ukuu wa Mungu ungeweza kuonekana katika sehemu yoyote ya maisha ya mtu. Alikuwa hajamwona Mungu lakini aliweza kutambua kwamba Matendo ya Mungu yako kila pahali, na katika wakati wake usiokuwa wa kina duniani, katika kila kona ya maisha yake aliweza kuona na kutambua matendo ya kipekee na ya maajabu ya Mungu, na aliweza kuona mipangilio ya ajabu ya Mungu. Ufiche na kimya cha Mungu hakikuzuia utambuzi wa Ayubu wa matendo ya Mungu, wala hakikuathiri maarifa yake kuhusu ukuu wa Mungu juu ya mambo yote. Maisha yake yalikuwa utambuzi wa ukuu na mipangilio ya mungu, ambaye amefichwa miongoni mwa mambo yote, katika maisha yake ya kila siku. Katika maisha yake ya kila siku alisikia pia na kuelewa sauti na maneno ya moyoni, ambayo Mungu, akiwa kimya miongoni mwa mambo yote, alionyesha kupitia kwa kutawala Kwake kwa sheria ya mambo yote. Unaona, basi, kwamba kama watu wanao ubinadamu sawa na ufuatiliaji kama Ayubu, basi wanaweza kupata utambuzi na maarifa sawa kama Ayubu, na kupata ule uelewa na maarifa sawa ya ukuu wa Mungu juu ya mambo yote kama Ayubu. Mungu alikuwa hajajionyesha kwa Ayubu au kuongea na yeye, lakini Ayubu aliweza kuwa mtimilifu na mnyofu, na pia aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa maneno mengine, bila ya Mungu kuweza kujitokeza kwa au kuongea na binadamu, matendo ya Mungu miongoni mwa mambo yote na ukuu Wake juu ya mambo yote ni tosha kwa binadamu ili kuweza kuwa na ufahamu wa uwepo wa Mungu, nguvu na mamlaka ya Mungu ni tosha kumfanya binadamu huyu kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa sababu binadamu wa kawaida kama vile Ayubu aliweza kutimiza hali ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, basi kila mtu wa kawaida anayemfuata Mungu anafaa pia kuweza kufanya hivyo. Ingawaje maneno haya yanaweza kusikika ni kana kwamba ni hitimisho ya kimantiki. Hii haikiuki sheria ya mambo. Bado ukweli haujalingana na matarajio: Kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, kunaweza kuonekana, ni hifadhi ya Ayubu na Ayubu pekee. Kwa kutaja “kumcha Mungu na kujiepusha na maovu,” watu hufikiria kwamba hii inafaa tu kufanywa na Ayubu, ni kana kwamba njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ilikuwa imebandikwa jina la Ayubu na haikuhusika na watu wengine. Sababu ya hii ni wazi: Kwa sababu Ayubu tu ndiye aliyemiliki hulka iliyokuwa na uaminifu, ukarimu, na nyofu, na iliyopenda kutopendelea na haki na mambo yaliyokuwa mazuri, hivyo ni Ayubu tu ambaye angeweza kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Lazima nyinyi wote mkuwe mmeelewa matokeo hapa—ambayo ni kwamba kwa sababu hakuna yule anayemiliki ubinadamu ulio na uaminifu, ukarimu, na unyofu, na ule ambao unapenda kutopendelea na haki na ule ambao ni mzuri, hakuna mtu anayeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na hivyo hawezi kupata furaha ya Mungu au kusimama imara katikati ya majaribio. Ambayo pia inamaanisha kwamba, bila kujumuisha Ayubu, watu wote wangali wamefungwa na kunaswa na Shetani, wote wanashtakiwa, wanashambuliwa, na kudhulumiwa na Shetani, na wale ambao Shetani anajaribu kumeza, na wote hawana uhuru, ni wafungwa ambao wametekwa nyara na Shetani.

Kama Moyo wa Binadamu Unao Uadui na Mungu, Anawezaje Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu

Kwa sababu watu wa leo hawamiliki ubinadamu sawa na Ayubu, na je kiini cha asili yao, na mwelekeo wao kwa Mungu? Wanamcha Mungu? Wanajiepusha na maovu? Wale wasiomcha Mungu na kujiepusha na maovu wanaweza kujumuishwa tu kwa maneno manne: Ni adui za Mungu. Mara nyingi mnasema maneno haya, lakini hamjawahi kujua maana yake halisi. Maneno “ni adui za Mungu” yanayo kiini ndani yake: Hayasemi kwamba Mungu anamuona binadamu kama adui, lakini kwamba binadamu anamuona Mungu kama adui. Kwanza, wakati watu wanapoanza kusadiki Mungu, ni nani asiyekuwa na nia, motisha na maono yake binafsi? Ingawaje sehemu moja yao inasadiki uwepo wa Mungu, na imeona uwepo wa Mungu, imani yao katika Mungu bado inayo hiyo motisha, na nia yao kuu ya kusadiki Mungu ni kupokea baraka Zake na mambo wanayotaka. Katika uzoefu wa watu katika maisha yao, mara nyingi wanafikiria ndani yao, nimetoa familia yangu na ajira yangu kwa Mungu, na Amenipatia nini? Lazima niongezee na kuthibitisha haya—je, nimepokea baraka zozote hivi majuzi? Nimetoa mengi sana wakati huu, nimekimbia na kukimbia na kuteswa sana—je Mungu amenipa ahadi zozote baada ya haya? Je Amekumbuka matendo yangu mazuri? Mwisho wangu utakuwa vipi? Ninaweza kuzipokea baraka za Mungu? … Kila mtu kila wakati, na mara nyingi hufanya hesabu kama hizi ndani ya mioyo yao, na wao wanatoa madai yao kwa Mungu yanayoonyesha motisha yao na malengo na mipango. Hivi ni kusema, ndani ya moyo wake binadamu siku zote anamweka Mungu majaribuni, siku zote anaunda njama kumhusu Mungu, na kila wakati anabishana na Mungu kuhusu kesi yake na kujaribu kumfanya Mungu kutoa kauli, ili aweze kuona kama Mungu anaweza kumpa kile anachotaka au hawezi. Wakati huohuo akimfuata Mungu, binadamu hamchukulii mungu kama Mungu. Siku zote amejaribu kufanya mipango na Mungu, akitoa madai bila kusita kwake Yeye na hata akimsukuma Yeye kwa kila hatua, akijaribu kupiga hatua ya maili licha ya kupewa inchi moja. Wakati huohuo akijaribu kuunda mipango na Mungu, binadamu pia anabishana na Yeye, na wapo hata watu ambao, wakati majaribio yanapowapata au wanapojipata katika hali ya kuteketea, mara nyingi wanakuwa wanyonge, wananyamaza na kuzembea katika kazi yao, na wanajaa malalamiko kuhusu Mungu. Tangu wakati ule alipoanza kusadiki Mungu, binadamu amemchukulia Mungu kama alama ya pembe inayoonyesha wingi wa neema, kisu cha Kijeshi cha Uswisi, na amejichukulia yeye mwenyewe kuwa mdaiwa mkubwa zaidi wa Mungu, ni kana kwamba kujaribu kupata baraka na ahadi kutoka kwa Mungu ni haki yake ya asili na jukumu, huku jukumu la Mungu likiwa ni kulinda na kutunza binadamu na kumtoshelezea. Huu ndio uelewa wa kimsingi wa “imani katika Mungu” wa wale wote wanaosadiki Mungu, na uelewa wao wa kina zaidi wa dhana ya imani katika Mungu. Kutoka kwenye kiini cha asili ya binadamu hadi katika ufuatiliaji wake wa kibinafsi, hakuna kitu chochote kinachohusiana na kumcha Mungu. Nia ya binadamu kwa kusadiki Mungu huenda isiwe na uhusiano na kuabudu Mungu. Hivi ni kusema kwamba, binadamu hajawahi kufikiria wala kuelewa kwamba imani katika Mungu inahitaji kumcha Mungu, na kumwabudu Mungu. Kwa mujibu wa haya yote, kiini cha binadamu ni wazi. Na kiini hicho ni nini? Ni kwamba moyo wa binadamu una kijicho, unabeba udanganyifu na ujanja, haupendi mambo ya kutopendelea na haki, au kile kilicho kizuri, nao ni wenye kuleta dharau na ulafi. Moyo wa binadamu usingeweza kumzuia Mungu zaidi, hajaupatia Mungu kamwe. Mungu hajawahi kuona moyo wa kweli wa binadamu, wala hajawahi kuabudiwa na binadamu. Haijalishi ni gharama gani ambayo Mungu amelipia, au ni kiasi kipi cha kazi Anachofanya, au ni kiwango kipi Anachompa binadamu, binadamu anabakia yule asiyeona hayo yote, na hajali. Binadamu hajawahi kumpa Mungu moyo wake, anataka tu kujali moyo wake wenyewe, kufanya uamuzi wake mwenyewe—mada madogo ambayo ni kwamba binadamu hataki kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, au kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, wala hataki kumwabudu Mungu kama Mungu. Hivyo ndivyo mwanadamu anavyozungukwa na hali mbalimbali leo. Sasa hebu tumwangalie tena Ayubu. Kwanza kabisa, aliweza kufanya mpango na Mungu? Alikuwa na nia zozote fiche katika kushikilia njia ile ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu? Wakati huo, je, Mungu alikuwa ameongea na yeyote kuhusu mwisho ujao? Wakati huo, Mungu alikuwa hajatoa ahadi zozote kwa yeyote kuhusu mwisho, na ilikuwa katika hali hii ndipo Ayubu aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Je, watu wa leo wanaweza kulinganishwa na Ayubu? Kunazo tofauti nyingi, wanapatikana katika nyanja tofauti. Ingawaje Ayubu hakuwa na maarifa mengi ya Mungu, alikuwa ameutoa moyo wake kwa Mungu na ulimilikiwa na Mungu. Hakuwahi kupanga chochote na Mungu, na hakuwa na matamanio yoyote ya zaidi au madai kwa Mungu; badala yake, alisadiki kwamba “Bwana alitoa na Bwana atatwaa.” Hii ndiyo alikuwa ameona na kupata kutokana na kushikilia ukweli njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu wakati wa miaka yake mingi ya maisha. Vilevile, alikuwa amepata matokeo ya “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” Sentensi hizi mbili ndizo ambazo alikuwa ameona na akaja kujua kutokana na mwelekeo wake wa utiifu kwa Mungu katika uzoefu wa maisha yake, na ndizo pia zilikuwa silaha zake zenye nguvu zaidi ambazo alitumia akashinda majaribio ya Shetani, na msingi wa yeye kusimama imara katika ushuhuda kwa Mungu. Wakati huu, bado unamwona Ayubu kama mtu mzuri? Je unatumaini kuwa mtu kama huyo? Unaogopa kupitia majaribio ya Shetani? Unaamua kumwomba Mungu ili aweze kukupitisha kwenye majaribio kama haya ya Ayubu? Bila shaka watu wengi wasingethubutu kuombea mambo kama hayo. Ni wazi, basi, kwamba imani yako ni ndogo ya kusikitiwa; ikilinganishwa na ile ya Ayubu, imani yako haistahili kutajwa. Nyinyi ndio adui za Mungu, hamchi Mungu, hamwezi kusimama imara katika ushuhuda kwa Mungu, na hamwezi kushangilia dhidi ya mashambulio, mashtaka, na majaribio ya Shetani. Ni nini kinachowafanya kufuzu ili kupokea ahadi za Mungu? Baada ya kusikia hadithi ya Ayubu na kuelewa nia ya Mungu katika kuokoa binadamu, na maana ya wokovu wa binadamu, je mnayo sasa imani ya kukubali majaribio sawa na ya Ayubu? Hamfai kuwa na kusudio kidogo, ili mjiruhusu kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu?

Msiwe na Wasiwasi Wowote Kuhusu Majaribio ya Mungu

Baada ya kuupokea ushuhuda kutoka kwa Ayubu kufuatia mwisho wa majaribio yake, Mungu aliamua kwamba angepata kundi au zaidi ya kundi—la watu kama Ayubu, ilhali aliamua kutowahi tena kumruhusu Shetani kushambulia au kunyanyasa mtu yeyote mwingine kwa kutumia mbinu ambazo alikuwa amemjaribu, akamshambulia na kumnyanyasa Ayubu, kwa kucheza karata na Mungu; Mungu hakumruhusu Shetani tena kufanya mambo kama hayo kwa binadamu ambaye ni mnyonge, mjinga, na asiyejua—ilikuwa tosha kwamba Shetani alikuwa amemjaribu Ayubu! Kutomruhusu Shetani kuwanyanyasa watu vyovyote anavyotaka ndiyo rehema ya Mungu. Kwa Mungu, ilitosha kwamba Ayubu alikuwa ameteseka majaribio na minyanyaso ya Shetani. Mungu hakumruhusu Shetani tena kufanya mambo kama hayo, kwani maisha na kila kitu cha watu wanaomfuata Mungu yanatawaliwa na kupangiliwa na Mungu, na Shetani hastahili kutawala waliochaguliwa na Mungu apendavyo—unafaa kuwa wazi kuhusu hoja hii! Mungu anajali kuhusu unyonge wa binadamu, na kuelewa ujinga na kutojua kwake. Ingawaje, ili binadamu aweze kuokolewa kabisa, lazima Mungu amkabidhi kwa Shetani, Mungu hayuko radhi kumwona tena binadamu akichezewa tena kama kikaragosi na Shetani na kunyanyaswa na Shetani na hataki kumwona binadamu siku zote akiteseka. Binadamu aliumbwa na Mungu, na inaeleweka kikamilifu kwamba Mungu anatawala na anapangilia kila kitu cha binadamu; hili ni jukumu la Mungu na mamlaka ambayo Mungu anatawala mambo yote! Mungu hamruhusu Shetani kunyanyasa na kutumia vibaya binadamu apendavyo, Hamruhusu Shetani kutumia mbinu mbalimbali za kumpotosha binadamu, na vilevile, Hamruhusu Shetani kuingilia kati ukuu wa Mungu wa binadamu, wala Hamruhusu Shetani kukanyaga na kuangamiza Sheria ambazo Mungu anatawalia mambo yote, kutosema chochote kuhusu kazi kuu ya Mungu ya kusimamia na kuwaokoa wanadamu! Wale ambao Mungu anataka kuokoa na wale ambao wanaweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, ndio msingi na hali halisi ya kazi ya Mungu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita, pamoja na bei ya jitihada zake katika kazi yake ya miaka elfu sita. Mungu anawezaje kuwakabidhi watu hawa kwa Shetani hivihivi.
Watu mara nyingi wanakuwa na wasiwasi kuhusu na wana uoga ya majaribio ya Mungu, ilhali siku zote wanaishi katika mtego wa Shetani na kuishi katika maeneo hatari ambapo wanashambuliwa na kunyanyaswa na Shetani—lakini hawaogopi na hawashangazwi. Nini kinaendelea? Imani ya binadamu katika Mungu ni finyu mno kwa mambo anayoweza kuona. Hana shukrani hata chembe kuhusu upendo na kujali kwa Mungu kwa binadamu, au wema Wake na utiliaji maanani kwa binadamu. Lakini kwa hofu na wasiwasi kidogo kuhusu majaribio, hukumu na kuadibu kwa Mungu na adhama na hasira Yake, binadamu hana hata chembe cha uelewa wa nia nzuri za Mungu. Kwa kutajwa kwa majaribio, watu wanahisi ni kana kwamba Mungu anazo nia nyingine zisizo wazi na hata baadhi wanasadiki kwamba Mungu ana mipango ya maovu, wasijue hata kile ambacho Mungu atawafanyia; hivyo, wakati huohuo kutaka kuwa watiifu kabisa kwa ukuu na mipangilio ya Mungu, wanafanya kila wawezalo kuzuia na kupinga ukuu wa Mungu juu ya binadamu na mipangilio kwa binadamu, kwani wanasadiki kwamba kama hawatakuwa makini watapotoshwa na Mungu, na kama hawatakuwa na mshikilio thabiti ya hatima yao binafsi, basi kila kitu walichonacho kinaweza kuchukuliwa na Mungu, na maisha yao huenda hata yakaisha. Binadamu yumo kwenye kambi la Shetani, lakini hawi na wasiwasi kamwe kuhusu kunyanyaswa na Shetani, na ananyanyaswa na Shetani lakini haogopi kamwe kutekwa nyara na Shetani. Siku zote anasema kwamba anaukubali wokovu wa Mungu, ilhali hajawahi kumwamini Mungu au kusadiki kwamba Mungu atamwokoa kwa kweli binadamu kutoka kwenye makucha ya Shetani. Kama, sawa na Ayubu, binadamu anaweza kunyenyekea kwa mipango na mipangilio ya Mungu na anaweza kuitoa nafsi nzima kwa mikono ya Mungu, basi hatima ya binadamu haitakuwa sawa na ile ya Ayubu—kupokea baraka za Mungu? Kama binadamu anaweza kukubali na kunyenyekea Sheria ya Mungu, nini kipo cha kupoteza? Na hivyo Napendekeza kwamba uwe makinifu kwa vitendo vyako, utahadhari na kila kitu ambacho kiko karibu kukufanyikia wewe. Usiwe wa pupa au msukumo na umshughulikie Mungu na watu, masuala, vitu alivyokupangilia kwa namna mshawasha unavyokupeleka, au kulingana na nafsi yako ya kiasili au kufikiria na dhana zako; lazima uwe mmakinifu katika vitendo vyako na lazima uombe na utafute zaidi, kuepuka kuchochea hasira ya Mungu. Kumbuka hili!
Kisha, tutaangalia vile Ayubu alikuwa baada ya majaribio yake.
5. Ayubu Baada ya Majaribio yake
(Ayubu 42:7-9) Basi ikawa, baada ya BWANA kumwambia Ayubu maneno hayo, BWANA akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira yangu inawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili: kwa kuwa nyinyi hamjanena yaliyo sawa kunihusu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu. Basi sasa, jichukulieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, muende kwa mtumishi wangu Ayubu, na mjitolee sadaka ya kuteketezwa; na mtumishi wangu Ayubu atawaombea: kwa kuwa yeye Nitamkubali: nisije Nikawatendea kulingana na makosa yenu, hivi kwamba nyinyi hamkunena maneno yaliyo sawa kunihusu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu. Hivyo Elifazi, Mtemani, na Bildadi, Mshuhi, na Sofari, Mnaamathi, wakaenda, wakafanya vile BWANA alivyowaamuru: BWANA pia akamkubali Ayubu.
(Ayubu 42:10) Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, alipowaombea rafiki zake: BWANA pia akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kabla.
(Ayubu 42:12) Basi hivyo BWANA akaubariki mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake: kwani alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng’ombe elfu moja, na punda wa kike elfu moja.
(Ayubu 42:17) Basi Ayubu akafa, akiwa mzee sana na mwenye kujawa na siku.

Wale Wanaomcha Mungu na Kujiepusha Na Maovu Wanatazamiwa kwa Utunzwaji na Mungu, Huku Wale Walio Wajinga Wanaonekana kuwa Wanyenyekevu

Katika Ayubu 42:7-9, Mungu Anasema kwamba Ayubu ni mtumishi Wake. Matumizi Yake ya neno “mtumishi” kumrejelea Ayubu yanaonyesha umuhimu wa Ayubu katika moyo Wake; ingawaje Mungu hakumwita Ayubu kitu chenye heshima zaidi, jina hili halikuwa na uamuzi wowote katika umuhimu wa Mungu ndani ya moyo wa Ayubu. “Mtumishi” hapa ni jina la lakabu la Mungu kwa Ayubu. Marejeleo mbali mbali ya Mungu kwa “mtumishi wangu Ayubu” yanaonyeshwa ni vipi ambavyo Alipendezwa na Ayubu, ingawaje Mungu hakuongea kuhusu maana ya nyuma ya neno “Mtumishi,” ufafanuzi wa Mungu wa neno “mtumishi” unaweza kuonekana kupitia kwa maneno Yake katika kifungu hiki ya maandiko. Kwanza Mungu alimwambia Elifazi Mtemani: “Hasira yangu inawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili: kwa kuwa nyinyi hamjanena yaliyo sawa kunihusu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.” Maneno haya ndiyo ya mara ya kwanza kwa Mungu kuambia watu waziwazi kwamba alikuwa amekubali yale yote yaliyokuwa yamesemwa na kufanywa na Ayubu baada ya majaribio ya Mungu kwake yeye, na ndiyo mara ya kwanza Alikuwa amedhibitisha waziwazi ukweli na usahihi wa yale yote Ayubu alikuwa amefanya na kusema. Mungu alikuwa na ghadhabu kwake Elifazi na wengine kwa sababu ya mazungumzo yao yasiyokuwa sahihi na mabovu, kwa sababu, kama Ayubu wasingeweza kuona mwonekano wa Mungu au kusikia maneno aliyoongea katika maisha yao ilhali Ayubu alikuwa na maarifa sahihi Kumhusu Mungu, huku nao waliweza tu kukisia bila mpango kuhusu Mungu, kukiuka mapenzi ya Mungu na kujaribu uvumilivu wake kwa yote waliyoyafanya Kwa hivyo, wakati sawa na kukubali yote yalikuwa yamefanywa na kusemwa na Ayubu, Mungu alizidi kuongeza hasira zake kwa wale wengine, kwani ndani yao Hakuweza tu kuuona uhalisia wowote wa kumcha Mungu, lakini pia Hakusikia chochote cha kumcha Mungu kwa yale waliyoyasema. Na hivyo Mungu kwa kilichofuata Alisema madai yafuatayo kuwahusu. “Basi sasa, jichukulieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, muende kwa mtumishi wangu Ayubu, na mjitolee sadaka ya kuteketezwa; na mtumishi wangu Ayubu atawaombea: kwa kuwa yeye Nitamkubali: Nisije Nikawatendea kulingana na makosa yenu.” Katika kifungu hiki Mungu anamwambia Elifazi na wengine kufanya jambo ambalo litakomboa dhambi zao, kwani upumbavu wao ulikuwa ni dhambi dhidi ya Yehova Mungu, na hivyo wangelazimika kutoa sadaka zilizoteketezwa ili kusuluhisha makosa yao. Sadaka zilizoteketezwa mara nyingi zinatolewa kwa Mungu, lakini kile kisicho cha kawaida kuhusu sadaka hizi zilizoteketezwa ni kwamba zilitolewa kwa Ayubu. Ayubu alikubaliwa na Mungu kwa sababu alikuwa nao ushuhuda kwa Mungu wakati wa majaribio yake. Rafiki hawa wa Ayubu, nao walifichuliwa katika kipindi kile cha majaribio yake, kwa sababu ya upumbavu wao, walishutumiwa na Mungu na wakachochea hasira ya Mungu, na wanafaa kuadhibiwa na Mungu—kuadhibiwa kwa kutoa sadaka zilizoteketezwa mbele ya Ayubu—na baadaye Ayubu aliwaombea wao ili kuiondoa ile adhabu na hasira ya Mungu kwao. Nia ya Mungu ilikuwa ni kuwaaibisha wao, kwani hawakuwa watu waliomcha Mungu na wa kujiepusha na maovu, na walikuwa wameshutumu uadilifu wa Ayubu. Kwa upande mmoja, Mungu alikuwa akiwaambia kwamba Hakukubali vitendo vyao lakini Alikubali pakubwa na Alifurahishwa na Ayubu; kwa upande mwingine, Mungu alikuwa akiwaambia kwamba kukubaliwa na Mungu kunampandisha daraja binadamu mbele ya Mungu, kwamba binadamu anachukiwa na Mungu kwa sababu ya upumbavu wake, na anamkosea Mungu kwa sababu ya hali hii, na anakuwa mdogo na mbaya mbele ya macho ya Mungu. Huu ndio ufafanuzi uliotolewa na Mungu kuhusu watu wa aina mbili, ni mielekeo ya Mungu kwa watu hawa wa aina mbili na ni ufafanuzi wa Mungu kuhusu thamani na hadhi ya watu wa aina hizi mbili. Ingawaje Mungu alimwita Ayubu mtumishi Wake, ndani ya macho ya Mungu huyu “mtumishi” alikuwa mpendwa Wake, na alipewa mamlaka ya kuwaombea wengine na kuwasamehe makosa yao. “Mtumishi huyu” aliweza kuongea moja kwa moja na Mungu na kuwa na mgusano wa moja kwa moja na Mungu, hadhi yake ilikuwa ya juu zaidi na ya heshima zaidi kuliko ya wale wengine. Haya ndiyo maana halisi ya neno “mtumishi” kama Mungu alivyoongea. Ayubu alipewa heshima hii maalum kwa sababu ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na sababu iliyofanya wengine kutoitwa watumishi na Mungu ni kwa sababu hawakumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mielekeo hii miwili tofauti na maalum ya Mungu ndiyo mielekeo yake kwa watu wa aina mbili: Wale wanaomcha Mungu na kujiepusha na maovu wanakubaliwa na Mungu, na wanaonekana wenye thamani mbele ya macho Yake, huku wale walio wapumbavu hawajamcha Mungu na hawawezi kujiepusha na maovu, na hawawezi kupokea kibali cha Mungu, mara nyingi wanachukiwa na kushutumiwa na Mungu, na ni wadogo mbele ya macho ya Mungu.

Mungu Anamtawaza Mamlaka Ayubu

Ayubu aliwaombea rafiki zake, na baadaye, kwa sababu ya maombi ya Ayubu, Mungu hakushughulika nao kama walivyostahili juu ya upumbavu wao —Hakuwaadhibu au kuchukua adhabu yoyote dhidi yao. Na sababu ilikuwa nini? Kwa sababu kulingana na wao maombi yanayohusu mtumishi wa Mungu, Ayubu, yalikuwa yamefikia masikio Yake; Mungu naye aliwasamehe kwa sababu Aliyakubali maombi ya Ayubu. Na tunaona nini katika haya? Wakati Mungu anapombariki mtu, Anampa tuzo nyingi, na si tu zile za kidunia, pia: Mungu anawapa pia mamlaka, na Kuwaambia kuwa wanastahili kuwaombea wengine, naye Mungu husahau na kusamehe makosa ya hao watu kwa sababu Anayasikia maombi haya. Haya ndiyo mamlaka yenyewe ambayo Mungu alimpa Ayubu. Kupitia kwa maombi ya Ayubu kusitisha kushutumiwa kwao, Yehova Mungu aliwaletea aibu wale watu wapumbavu— ambayo, bila shaka, ndiyo iliyokuwa adhabu Yake maalum kwa Elifazi na wale wengine.

Ayubu Anabarikiwa kwa Mara Nyingine Tena na Mungu, na Hashtakiwi Tena na Shetani

Miongoni mwa matamko ya Yehova Mungu ni maneno kwamba “hivi kwamba nyinyi hamkunena maneno yaliyo sawa kunihusu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.” Ni nini kile ambacho Ayubu alikuwa amesema? Ni kile tulichozungumzia awali, pamoja na kile ambacho kurasa nyingi za maneno kwenye kitabu cha Ayubu ambacho Ayubu amerekodiwa kuwa alisema. Katika kurasa hizi nyingi za maneno, Ayubu hajawahi hata mara moja kuwa na malalamiko au mashaka yoyote kumhusu Mungu. Yeye anasubiria tu matokeo. Ni kusubiri huku ambako ndiko mwelekeo wake wa uaminifu, matokeo yake yakiwa, na kutokana na maneno aliyomwambia Mungu, Ayubu alikubaliwa na Mungu. Alipovumilia majaribio na kupata mateso ya Ugumu, Mungu alikuwa upande wake na ingawaje ugumu wake hukupunguzwa na uwepo wa Mungu, Mungu aliona kile Alichotaka kuona na kusikia kile Alichotaka kusikia. Kila mojawapo ya vitendo na maneno ya Ayubu kiliweza kufikia macho na masikio ya Mungu; Mungu alisikia na Akaona—na hii ni ukweli. Maarifa ya Ayubu kumhusu Mungu na fikira zake kumhusu Mungu katika moyo wake wakati huo, katika kipindi hicho, hazikuwa kwa hakika kama zile za watu wa leo, lakini katika muktadha wa wakati huo, Mungu aliweza kutambua bado kila kitu alichokuwa amesema, kwa sababu tabia yake na fikira zake ndani ya moyo wake, na kile alichokuwa ameelezea na kufichua, kilikuwa tosha kwa mahitaji Yake. Katika kipindi hiki cha wakati ambao Ayubu alipitia majaribio, yale ambayo alifikiria katika moyo wake na kuamua kufanya yaliweza kumwonyesha Mungu matokeo, yale ambayo yalimtosheleza Mungu, na baadaye Mungu akayaondoa majaribio ya Ayubu, Ayubu akaibuka kutoka kwenye matatizo yake, na majaribio yake yakawa yameondoka yasiwahi kumpata tena yeye. Kwa sababu Ayubu alikuwa tayari amepitia majaribio, na akawa amesimama imara katika majaribio haya, na akamshinda kabisa Shetani, Mungu alimpatia baraka ambazo kwa kweli alistahili. Kama ilivyorekodiwa katika Ayubu 42:10, 12, Ayubu alibarikiwa kwa mara nyingine tena, na akabarikiwa zaidi ya hata mara ya kwanza. Wakati huu Shetani alikuwa amejiondoa, na hakusema tena au kufanya chochote, na kutoka hapo kuenda mbele Ayubu hakuhitilafiana tena na Shetani au kushambulia Shetani, na Shetani hakutoa mashtaka tena dhidi ya baraka za Mungu kwa Ayubu.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni