Kanisa la Mwenyezi Mungu
Uhusiano Kati ya Uwakilishi wa Mungu ya Ayubu na Shetani na Malengo ya Kazi ya Mungu
Ingawaje watu wengi sasa wanatambua kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, utambuzi huu hauwapi uelewa mkubwa zaidi wa nia ya Mungu. Wakati huohuo wakionea wivu ubinadamu na ushughulikaji wa Ayubu, wanamuuliza Mungu swali lifuatalo: Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu sana, watu walimpenda sana, kwa hivyo kwa nini Mungu akamkabidhi kwa Shetani na kumpitishia maumivu haya makali? Maswali kama hayo yanatarajiwa kuwepo katika mioyo ya watu wengi—au, kushuku huku ndiko hasa swali katika mioyo ya watu wengi. Kwa sababu kushuku huku kumeshangaza watu wengi sana, lazima tuliwasilishe swali hili waziwazi na kulielezea kikamilifu.
Mwenyezi Mungu alisema, Kila kitu ambacho Mungu anafanya kinahitajika, na kina umuhimu usio wa kawaida, kwani kila kitu anachofanya ndani ya binadamu kinahusu usimamizi wake na wokovu wa mwanadamu. Kiasili kazi ambayo Mungu alimfanyia Ayubu si tofauti, ingawaje Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu mbele ya macho ya Mungu kwa maneno mengine, licha ya kile ambacho Mungu anafanya au mbinu ambazo Anatumia kufanya, licha ya gharama, au lengo Lake, kusudio la hatua Zake halibadiliki. Kusudio Lake ni kuweza kumshughulikia binadamu ili maneno ya Mungu yaingie ndani yake, mahitaji ya Mungu, na mapenzi ya Mungu kwa binadamu; kwa maneno mengine, ni kufanyia kazi huyu binadamu ili vyote ambavyo Mungu Anasadiki kuwa vizuri kulingana na hatua Zake, kumwezesha binadamu kuuelewa moyo wa Mungu na kufahamu kiini cha Mungu, na kumruhusu yeye kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, na hivyo basi kumruhusu binadamu kuweza kufikia kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—yote ambayo ni kipengele kimoja ya kusudio la Mungu katika kila kitu Anachofanya. Kipengele kingine ni kwamba, kwa sababu Shetani ndiye foili[e] na chombo cha huduma katika kazi ya Mungu, mara nyingi binadamu hukabidhiwa Shetani; hizi ndizo mbinu ambazo Mungu hutumia ili kuwaruhusu watu kuweza kuona maovu, ubaya, kudharaulika kwa Shetani katikati ya majaribio na mashambulizi ya Shetani na hivyo basi kuwasababisha watu kumchukia Shetani na kuweza kutambua kile ambacho ni kibaya. Mchakato huu unawaruhusu kwa utaratibu kuanza kuwa huru dhidi ya udhibiti wa Shetani, na dhidi ya mashtaka, uingiliaji kati, na mashambulizi ya Shetani—mpaka, kwa sababu ya maneno ya Mungu, maarifa yao na utiifu wao kwa Mungu, na imani yao kwa Mungu na kuweza kwao kumcha Mungu, wanashinda dhidi ya mashambulizi ya Shetani na kushinda dhidi ya mashtaka ya Shetani; hapo tu ndipo watakapokuwa wamekombolewa kabisa dhidi ya utawala wa Shetani. Ukombozi wa watu unamaanisha kwamba Shetani ameshindwa, unamaanisha kwamba wao si tena chakula kwenye kinywa cha Shetani— kwamba badala ya kuwameza wao, shetani amewaachilia. Hii ni kwa sababu watu kama hao ni wanyofu, kwa sababu wanayo imani, utiifu na wanamcha Mungu, na kwa sababu wako huru kabisa dhidi ya Shetani. Wamemleta Shetani aibu, wamemfanya kuonekana mjinga, na wamemshinda kabisa Shetani. Imani yao katika kumfuata Mungu, na utiifu na kumcha Mungu kunamshinda Shetani, na kumfanya Shetani kukata tamaa kabisa na wao. Watu kama hawa ndio ambao Mungu amewapata kwa kweli, na hili ndilo lengo kuu la Mungu katika kumwokoa binadamu. Kama wangependa kuokolewa, na wangependa Mungu awapate kabisa, basi wote wanaomfuata Mungu lazima wakabiliane na majaribio na mashambulizi yakiwa makubwa na hata madogo kutoka kwa Shetani. Wale wanaoibuka katika majaribio na mashambulizi haya na wanaweza kumshinda Shetani ni wale waliookolewa na Mungu. Hivi ni kusema kwamba wale waliookolewa na Mungu ni wale ambao wamepitia majaribio ya Mungu, na ambao wamejaribiwa na kushambuliwa na Shetani mara nyingi. Wale waliookolewa na Mungu wanayaelewa mapenzi na mahitaji ya Mungu, na wanaweza kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu na hawaachi njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu katikati ya majaribio ya Shetani. Wale waliookolewa na Mungu wanamiliki uaminifu, wao ni wakarimu, na wanaweza kutofautisha upendo na chuki, wanayo hisia ya haki na urazini, na wanaweza kumtunza Mungu na kuthamini sana kila kitu ambacho ni cha Mungu. Watu kama hao hawatekwi bakunja, kufanyiwa upelelezi, kushtakiwa au kudhulumiwa na Shetani, wako huru kabisa, wamekombolewa na kuachiliwa kabisa. Ayubu alikuwa mtu kama huyo mwenye uhuru na huu ndio umuhimu hasa wa kwa nini Mungu alimkabidhi kwa Shetani.
Ayubu alidhulumiwa na Shetani, lakini pia aliweza kupata uhuru na ukombozi wa milele, na kupata haki ya kutowahi kukabidhiwa tena kwa upotovu, unyanyasaji, na mashtaka ya Shetani, na badala yake kuishi katika nuru ya udhibiti wa Mungu usio na pingamizi na kuishi katikati ya baraka kutoka kwa Mungu. Hakuna ambaye angechukua au kuangamiza, au kupata haki hii. Ilipewa kwa Ayubu kutokana na imani, bidii, na utiifu wake kwa na kumcha Mungu; Ayubu alilipia gharama ya maisha yake ili kuweza kupata shangwe na furaha duniani, ili kufanikiwa kupata haki na kuweza kustahili, kama ilivyoamriwa mbinguni na kutambuliwa na dunia, ili kumwabudu Muumba bila ya uingiliaji kati kama kiumbe wa kweli wa Mungu duniani. Hivyo pia ndivyo yalivyokuwa matokeo makubwa zaidi ya majaribio yaliyovumiliwa na Ayubu.
Wakati watu bado hawajaokolewa, maisha yao mara nyingi yanaingiliwa kati na hata kudhibitiwa na, Shetani. Kwa maneno mengine, watu ambao hawajaokolewa ni wafungwa wa Shetani, hawana uhuru, hawajaachiliwa na Shetani, hawajafuzu wala kustahili kumwabudu Mungu, na wanafuatiliwa kwa karibu na kushambuliwa kwa ukali na Shetani. Watu kama hawa hawana furaha ya kuzungumzia, hawana haki ya uwepo wa kawaida wa kuzungumzia, na zaidi hawana heshima ya kuzungumzia. Ni pale tu unaposimama imara na kupigana na Shetani, kwa kutumia imani yako katika Mungu na utiifu kwake, pamoja na kumcha Mungu kama silaha ambazo utatumia kupigana vita vya maisha na mauti dhidi ya Shetani, kiasi cha kwamba utamshinda kabisa Shetani na kumsababisha kukata tamaa na kuwa mwoga kila anapokuona wewe, ili aache kabisa mashambulizi na mashtaka yake dhidi yako—hapo tu ndipo utakapookolewa na kuwa huru. Kama umeamua kutengana kabisa na Shetani lakini huna silaha zitakazokusaidia kupigana na Shetani, basi bado utakuwa katika hatari; kwa kadri muda unaposonga, baada ya wewe kuteswa na Shetani kiasi cha kwamba huna hata usuli wa nguvu uliobakia ndani mwako, lakini bado hujaweza kuwa na ushuhuda, bado hujajifungua kabisa kuwa huru dhidi ya mashtaka na mashambulizi ya Shetani dhidi yako, basi utakuwa na tumaini dogo la wokovu. Mwishowe, wakati hitimisho la kazi ya Mungu itakapotangazwa, bado utakuwa katika mashiko ya Shetani, usiweze kujiachilia kuwa huru, na hivyo hutawahi kuwa na fursa au tumaini. Matokeo yake, hivyo basi, ni kwamba watu kama hao watakuwa mateka kabisa wa Shetani.
Kubali Mitihani ya Mungu, Shinda Majaribio ya Shetani, na Ruhusu Mungu Kupata Nafsi Yako Nzima
Wakati wa kazi wa utoaji Wake wa kudumu na msaada kwa binadamu, Mungu anaambia binadamu kuhusu wa mapenzi Yake na mahitaji Yake yote, na anaonyesha vitendo Vyake, tabia, na kile Anacho na alicho kwa binadamu. Lengo ni kuweza kumtayarisha binadamu ili awe na kimo, na kumruhusu binadamu kupata ukweli mbalimbali kutoka kwa Mungu wakati anaendelea kumfuata Yeye— ukweli ambao ni silaha alizopewa binadamu na Mungu ambazo atatumia kupigana na Shetani. Hivyo akiwa na silaha hizo, binadamu lazima akabiliane na mitihani ya Mungu. Mungu anazo mbinu na njia nyingi za kumjaribu binadamu, lakini kila mojawapo inahitaji “ushirikiano” wa adui wa Mungu: Shetani. Hivi ni kusema, baada ya kumpa binadamu silaha ambazo atatumia kupigana na shetani, Mungu anamkabidhi binadamu kwa Shetani na kuruhusu Shetani “kujaribu” kimo cha binadamu. kama binadamu anaweza kufanikiwa dhidi ya uundaji wa vita vya Shetani, kama anaweza kutoroka mizunguko ya Shetani na bado akaishi, basi mwanadamu atakuwa ameupita mtihani. Lakini kama binadamu atashindwa kuondoka kwenye uundaji wa vita vya Shetani, na kujinyenyekeza kwa Shetani, basi hatakuwa ameupita mtihani. Haijalishi ni kipengele kipi cha binadamu ambacho mungu anachunguza, kigezo ni kama binadamu atasimama imara katika ushuhuda wake atakaposhambuliwa na Shetani au la, kujua kama amemuacha Mungu au la na akajisalimisha na akajinyenyekeza kwa Shetani baada ya kunaswa na Shetani. Inaweza kusemekana kwamba, iwapo binadamu anaweza kuokolewa au la yote haya yanategemea kama anaweza kumzidi na kumshinda Shetani, na kama ataweza kupata uhuru au la yanategemea kama anaweza kuinua, yeye binafsi, silaha alizopewa na Mungu ili kushinda utumwa wa Shetani, na kumfanya Shetani kuwacha kabisa tumaini na kumwacha pekee. Kama Shetani ataliacha tumaini na kumwachilia mtu, hii inamaanisha kwamba Shetani hatawahi tena kujaribu kuchukua mtu huyu kutoka kwa Mungu hatawahi tena kumshtaki na kuingilia kati mtu huyu, hatawahi tena kutaka kumtesa au kumshambulia; mtu kama huyu tu ndiye atakuwa kwa kweli amepatwa na Mungu. Huu ndio mchakato mzima ambao Mungu anapata watu.
Onyo na Upataji Nuru Ulilotolewa kwa Vizazi vya Baadaye Na Ushuhuda wa Ayubu
Huku wakielewa mchakato ambao Mungu anampata kabisa mtu, watu wataweza pia kuelewa nia na umuhimu wa Mungu kumpeleka Ayubu kwa Shetani. Watu hawasumbuliwi tena na maumivu makali ya Ayubu, na wanatambua upya umuhimu wake. Hawawi na wasiwasi tena kuhusu kama wao wenyewe watapitia majaribio sawa na yale ya Ayubu, na hawapingi tena au kukataa tena ujio wa majaribio ya Mungu. Imani, utiifu, na ushuhuda wake Ayubu wa kushinda Shetani, vyote hivi vimekuwa ni chanzo cha msaada mkubwa na himizo kwa watu. Kwa Ayubu, wanaona tumaini la wokovu wao binafsi, na wanaona kwamba kupitia kwa imani na utiifu kwa na kumcha Mungu, inawezekana kabisa kushinda Shetani, na kumshinda Shetani. Wanaona kwamba mradi tu waukubali ukuu na mipangilio ya Mungu, na kumiliki uamuzi na imani ya kutomwacha Mungu baada ya kupoteza kila kitu, basi wanaweza kumletea Shetani aibu na hali ya kushindwa, na kwamba wanahitaji tu kumiliki uamuzi na ustahimilivu wa kusimama imara katika ushuhuda wao—hata kama itamaanisha kupoteza maisha yao—ili Shetani aweze kuaibika na kurejea nyuma haraka. Ushuhuda wa Ayubu ni onyo kwa vizazi vya baadaye, na onyo hili linawaambia kwamba kama hawatamshinda Shetani, basi hawatawahi kuweza kujiondolea mashtaka na uingiliaji kati wa Shetani, na wala hawatawahi kuweza kutoroka dhulma na mashambulizi ya Shetani. Ushuhuda wa Ayubu ulipatia nuru vizazi vya baadaye. Upatiaji Nuru huu unafunza watu kwamba ni pale tu wanapokuwa watimilifu na wanyofu ndipo watakapoweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu; unawafunza kwamba ni pale tu wanapomcha Mungu na kujiepusha na maovu ndipo watapoweza kuwa na ushuhuda wenye udhabiti na wa kipekee kwa Mungu; pale tu watakapokuwa na ushuhuda dhabiti na wakipekee wa Mungu ndipo hawatawahi kudhibitiwa na Shetani, na kuishi katika mwongozo na ulinzi wa Mungu—na hapo tu ndipo watakapokuwa wameokolewa kwa kweli. Hulka ya Ayubu na ufuatiliaji wake wa maisha unafaa kuigwa na kila mmoja anayefuata wokovu. Kile alichoishi kwa kudhihirisha katika maisha yake yote na mwenendo wake wakati wa majaribio yake ni hazina yenye thamani kwa watu wote wanaotaka kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.
Ushuhuda wa Ayubu Waleta Tulizo kwa Mungu
Nikikwambia sasa kwamba Ayubu ni mtu mzuri, huenda usiweze kutambua maana yaliyomo kwenye maneno haya, na huenda usiweze kung’amua mawazo yaliyopo katika yale maneno Niliyoyaongea kwa ujumla; lakini subiri mpaka siku ile utakapokuwa umepitia majaribio sawa na au yale yanayofanana na yale ambayo Ayubu alipitia, wakati utakapokuwa umepitia magumu, wakati utakapokuwa umepitia majaribio wewe binafsi yaliyopangiliwa kwa ajili yako na Mungu, wakati utakapojitolea kila kitu ulichonacho, na kuvumilia udhalilishaji na ugumu, ili kuweza kushinda Shetani na kuwa na ushuhuda kwa Mungu katikati ya majaribio hayo yote—basi utaweza kutambua maana ya maneno haya Ninayoyaongea. Wakati huo, utahisi kwamba wewe ni duni kuliko Ayubu, utahisi namna Ayubu alivyo mzuri, na kwamba anastahili kuigwa; wakati huo utakapowadia, utatambua namna ambavyo maneno yale ya kimapokeo yaliyozungumzwa na Ayubu yalivyo muhimu kwa yule aliyepotoka na anayeishi kwenye nyakati hizi, na utatambua namna ambavyo ilivyo vigumu kwa watu wa leo kuweza kutimiza kile Ayubu alitimiza. Unapohisi kuwa ni vigumu, utatambua na kuona namna ambavyo moyo wa Mungu ulivyo na dukuduku na wasiwasi, utatambua namna bei aliyolipa Mungu kuwapata watu kama hao ilivyo ya juu kupata watu kama hao, na jinsi lilivyo tukio la thamani kufanywa na kutekelezwa na Mungu kwa wanadamu. Kwa sababu sasa umeyasikia maneno haya, unao uelewa sahihi na ukadiriaji wa kweli kuhusu Ayubu? Katika macho yako, Ayubu alikuwa kweli mtu mtimilifu na mnyofu aliyejiepusha na maovu? Nasadiki kwamba watu wengi bila shaka watasema, ndio. Kwani ukweli kuhusu zile hatua ambazo Ayubu alichukua na kufichua haziwezi kupingwa na binadamu au Shetani yeyote. Hizo ndizo ithibati zenye nguvu zaidi kuhusu ushindi wa Ayubu dhidi ya Shetani. Ithibati hii ilitolewa kwa Ayubu, na ndio ushuhuda wa kwanza uliopokelewa na Mungu. Hivyo, wakati Ayubu aliposhinda majaribio ya Shetani na kuwa na ushuhuda kwa Mungu, Mungu aliona tumaini kwake Ayubu, na moyo wake ulitulizwa na Ayubu. Tangu uumbaji mpaka wakati wa Ayubu, huu ndio ulikuwa wakati wa kwanza ambao Mungu kwa kweli alipitia na kujua tulizo lilikuwa nini, na nini iliyokuwa maana ya kutulizwa na binadamu, na ndio uliokuwa wakati wa kwanza ambao Alikuwa ameona, na kupata, ushuhuda wa kweli uliotokana na Yeye.
Ninaamini kwamba, baada ya kuusikia ushuhuda wa Ayubu na simulizi za vipengele mbalimbali vya Ayubu, wengi wa watu watakuwa na mipango ya njia iliyo mbele yao. Hivyo, pia, Ninaamini kwamba watu wengi zaidi walio na wasiwasi na woga wataanza kwa utaratibu kuwa watulivu katika mwili na akili zao, na wataanza kuhisi tulizo, hatua kwa hatua. …
Vifungu vilivyo hapa chini ni simulizi pia kumhusu Ayubu. Wacha tuendelee kusoma.
4. Ayubu Amesikia Kuhusu Mungu kwa Kusikiliza juu ya Sikio
(Ayubu 9:11) “Tazama, anapita karibu nami, na mimi simwoni: Tena anapita kwenda mbele, lakini mimi simtambui.”
(Ayubu 23:8-9) “Tazama, naenda mbele, lakini hayuko huko; narudi nyuma, lakini siwezi kumwona; Katika mkono wa kushoto, anapofanya kazi, lakini siwezi kumwona: anajificha katika upande wa mkono wa kuume, hata siwezi kumwona.”
(Ayubu 42:2-6) “Najua ya kwamba unaweza kufanya mambo yote, na ya kuwa hakuna kusudi lako linaloweza kuzuilika. Ni nani yeye anayeficha ushauri bila maarifa? Hivyo, nimesema maneno nisiyoyafahamu; mambo ya ajabu kwangu nisiyoyajua. Sikiliza, nakusihi, nami nitazungumza: Nitauliza kutoka kwako, nawe ujiweke wazi kwangu. Nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio: Lakini sasa jicho langu linakuona. Ndiyo sababu najichukia nafsi yangu, na kutubu kwenye vumbi na jivu.”
Ingawaje Mungu Hajajifichua kwa Ayubu, Ayubu Anasadiki Mamlaka Ya Mungu
Ni nini Nguvu za maneno haya? Je, Yupo yeyote aliyetambua kwamba kunayo ukweli hapa? Kwanza, ni vipi ambavyo Ayubu alijua kwamba Mungu yupo? Na ni vipi alivyojua kwamba mbingu na ardhi na mambo yote yanatawaliwa na Mungu? Kunayo kifungu kinachojibu maswali haya mawili: Nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio: Lakini sasa jicho langu linakuona. Ndiyo sababu najichukia nafsi yangu, na kutubu kwenye vumbi na jivu (Ayubu 42:5-6). Kutokana na maneno haya tunajifunza kwamba, badala ya kuwa kwamba alimwona Mungu kwa macho yake mwenyewe, Ayubu alikuwa amejifunza kuhusu Mungu kutoka kwa hekaya. Ni katika hali hizi ndipo alipoanza kutembea njia ya kumfuata Mungu, na baadaye akathibitisha uwepo wa Mungu katika Maisha yake, na miongoni mwa mambo yote. Kunayo ukweli usiopingika hapa—nayo ni gani? Licha ya kuweza kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu. Katika haya, hakuwa sawa na watu wa leo? Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu, matokeo yake ni kwamba ingawaje alikuwa amewahi kumsikia Mungu, hakujua ni wapi Mungu alikuwa, au ni vipi Mungu alifanana, au ni nini Mungu alikuwa akifanya, mambo ambayo ni ya kibinafsi; tukiongea bila mapendeleo, ingawaje alimfuata Mungu, Mungu alikuwa hajawahi kumwonekania yeye au kumzungumzia yeye. Je, huu si ukweli? Ingawaje Mungu alikuwa hajaongea na Ayubu au kumpa amri zozote, Ayubu alikuwa ameuona uwepo wa Mungu, na kutazama ukuu Wake miongoni mwa mambo yote na katika hekaya ambazo Ayubu alikuwa amesikia kumhusu Mungu kwa kusikia kwa sikio, na baadaye alianza maisha ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hizi ndizo zilizokuwa asili na mchakato ambao Ayubu alimfuata Mungu. Lakini haikujalisha ni vipi alivyomcha Mungu na kujiepusha na maovu, ni vipi ambavyo alishikilia uadilifu wake, bado Mungu alikuwa hajawahi kujitokeza kwake. Hebu tuisome kifungu hiki. Alisema, “Tazama, anapita karibu nami, na mimi simwoni: Tena anapita kwenda mbele, lakini mimi simtambui.” (Ayubu 9:11). Yale ambayo maneno haya yanasema ni kwamba Ayubu huenda alihisi Mungu karibu naye au pengine hakuhisi— lakini alikuwa hajawahi kuweza kumwona Mungu. Kunazo nyakati ambapo alifikiria Mungu akipita mbele yake au akitenda, au akimwongoza binadamu, lakini alikuwa hajawahi kujua. Mungu humjia binadamu wakati hatarajii; binadamu hajui ni lini Mungu atamjia, au ni wapi anapomjia yeye, kwa sababu binadamu hawezi kumwona Mungu, kwa hivyo, kwa binadamu Mungu amefichwa kutoka kwake.
Imani ya Ayubu Katika Mungu Haitikisiki kwa Sababu Mungu Amefichwa Kutoka Kwake
Katika kifungu kifuatacho ya maandiko, Ayubu anasema, “Tazama, naenda mbele, lakini hayuko huko; narudi nyuma, lakini siwezi kumwona; Katika mkono wa kushoto, anapofanya kazi, lakini siwezi kumwona: anajificha katika upande wa mkono wa kuume, hata siwezi” (Ayubu 23:8-9). Katika simulizi hii, tunajifunza kwamba katika hali alizopitia Ayubu, Mungu alikuwa amefichwa kutoka kwake wakati wote huo; Mungu alikuwa hajajitokeza waziwazi kwake yeye, na alikuwa hajamzungumzia waziwazi maneno yoyote kwake yeye, lakini katika moyo wake Ayubu alikuwa na ujasiri wa uwepo wa Mungu. Alikuwa siku zote amesadiki kwamba Mungu huenda anatembea na yeye au huenda Anatenda akiwa kando yake, na kwamba ingawaje hakuweza kumwona Mungu, Mungu alikuwa kando yake yeye akitawala mambo yake yote. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu, lakini aliweza kuwa mkweli katika imani yake, jambo ambalo hakuna mtu yeyote aliwahi kuweza kufanya. Na kwa nini watu hawakuweza kufanya hivyo? Kwa sababu Mungu hakuongea na Ayubu, au kujitokeza kwake yeye, na kama asingekuwa amesadiki kwa kweli, asingeweza kuendelea, wala asingeweza kushikilia njia hiyo ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Je, huu si ukweli? Unahisi vipi unaposoma kumhusu Ayubu akisema maneno haya? Unahisi kwamba utimilifu na unyofu wa Ayubu, na haki yake mbele ya Mungu, ni kweli, na wala si kupiga chuku kwa upande wa Mungu? Ingawaje Mungu alimshughulikia Ayubu kwa njia sawa na watu wengine, na hakujitokeza wala kuongea na yeye, Ayubu bado alishikilia ubinadamu wake, bado alisadiki ukuu wa Mungu, na, isitoshe, mara kwa mara alitoa sadaka za kuteketezwa na kuomba mbele ya Mungu kutokana na hofu yake ya kumkosea Mungu. Katika uwezo wa Ayubu wa kumcha Mungu bila ya kuwahi kumwona Mungu, tunaona ni kiasi kipi alichopenda mambo mazuri na ni vipi imani yake ilivyokuwa thabiti na ya kweli. Hakukataa uwepo wa Mungu kwa sababu Mungu alikuwa amefichwa kutoka kwake, wala hakupoteza imani yake na kumkataa Mungu kwa sababu hakuwahi kumwona Yeye. Badala yake, katikati ya kazi fiche ya Mungu ya kutawala mambo yote, alikuwa ametambua uwepo wa Mungu na akahisi ukuu wa Mungu na Nguvu za Mungu. Hakukata tamaa katika kuwa mnyofu kwa sababu Mungu alikuwa amefichwa, wala hakuiacha njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwa sababu Mungu alikuwa hajawahi kujitokeza kwake yeye. Ayubu alikuwa hajawahi kuuliza kwamba Mungu aonekane waziwazi kwake ili kuthibitisha uwepo Wake, kwani alikuwa tayari ametangaza ukuu wa Mungu miongoni mwa mambo yote na alisadiki kwamba alikuwa amepata baraka na neema ambazo wengine hawakuwa wamepata. Ingawaje Mungu alibakia fiche kwake yeye, imani ya Ayubu kwa Mungu haikuwahi kutikisika. Hivyo, alivuna kile ambacho hakuna yeyote aliwahi kuvuna. Idhini ya Mungu na baraka za Mungu.
Ayubu Abariki Jina la Mungu na Wala Hafikirii Baraka au Janga
Kunayo ukweli ambao haurejelewi katu kwenye hadithi za maandiko kuhusu Ayubu, ambayo ndio itakayokuwa zingatio letu leo. Ingawaje Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu kwa masikio yake mwenyewe, Mungu alikuwa na nafasi katika moyo wa Ayubu. Na mwelekeo wa Ayubu kwa Mungu ulikuwa upi? Ulikuwa, kama ulivyorejelewa awali, “libarikiwe jina la Bwana.” Baraka yake kwa jina la Mungu haikuwa ya masharti, wala isiyofuzu, na bila ya sababu. Tunaona kwamba Ayubu alikuwa ameukabidhi moyo wake kwa Mungu, na kuuruhusu kudhibitiwa na Mungu; kila kitu alichofikiria, kila kitu alichoamua, na kila kitu alichopangilia katika moyo wake kilikuwa wazi kwa Mungu na wala moyo wake haukuwa umefungwa kuzuia Mungu. Moyo wake haukumpinga Mungu, na hakuwahi kuuliza Mungu kumfanyia chochote au kumpa chochote yeye, na wala hakuwa na matamanio yasiyo ya kawaida ambayo angepata chochote kutoka kwa kumwabudu Mungu. Ayubu hakuzungumzia biashara na Mungu, na wala hakutoa ombi lolote au madai yoyote kwa Mungu. Hali yake ya kusifia jina la Mungu ilikuwa kwa sababu ya nguvu kuu na mamlaka ya Mungu katika kutawala mambo yote, na haikutegemea kama alipata baraka au alipigwa na janga. Aliamini kwamba haijalishi kama Mungu anawabariki watu au analeta janga kwao, mamlaka na nguvu vyote havitabadilika, na hivyo, haikujalisha hali za mtu, jina la Mungu linafaa kusifiwa. Kwamba binadamu amebarikiwa na Mungu ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu, na wakati janga lilipompata binadamu, hivyo, pia ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Nguvu na mamlaka ya Mungu vyote vinatawala na kupangilia kila kitu cha binadamu; matukio yasiyo ya kawaida kuhusu utajiri wa binadamu ni maonyesho ya nguvu na mamlaka ya Mungu, na licha ya maoni yake mtu, jina la Mungu linafaa kusifiwa. Haya ndiyo ambayo Ayubu alipitia na kuishia kujua katika miaka ya maisha yake. Fikira na matendo yote ya Ayubu vyote vilifikia masikio ya Mungu na vikawasili mbele ya Mungu, na vikaonekana kuwa muhimu na Mungu. Mungu aliyapenda sana maarifa haya ya Ayubu na akathamini sana Ayubu kwa kuwa na moyo kama huo. Moyo huu ulisubiria amri ya Mungu siku zote, na pahali pote, na haijalishi ni muda au mahali gani ulikaribisha chochote kile kilichomsibu. Ayubu hakutoa mahitaji yoyote kwa Mungu. Kile alichohitaji kutoka kwake kilikuwa kusubiria, kukubali, kukabiliana na kutii mipangilio yote iliyotoka kwa Mungu; Ayubu alisadiki hili kuwa wajibu wake, na ndio hasa kile ambacho Mungu Alitaka. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu wala kumsikiliza Akiongea mambo yoyote, akitoa amri zozote, akiyatoa mafundisho yoyote, au kuelekeza yeye kuhusu chochote. Kwa maneno ya leo, kwake yeye kuweza kumiliki mwelekeo kama huo kwa Mungu, wakati Mungu alikuwa hajampa nuru, mwongozo, au toleo kuhusiana na ukweli—hili lilikuwa lenye thamani sana, na kwake yeye kuonyesha mambo kama hayo kulitosha kwa Mungu, na ushuhuda wake ulipongezwa na Mungu, na kutunzwa na Mungu. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu au kumsikia Mungu binafsi akitamka mafundisho yoyote kwake yeye, lakini kwa Mungu moyo wake na yeye mwenyewe vyote vilikuwa vyenye thamani zaidi kuliko wale watu ambao, mbele ya Mungu waliweza tu kuongea kuhusu nadharia kuu, ambao waliweza tu kujigamba na kuongea kuhusu kutoa sadaka lakini walikuwa hawajawahi kuwa na maarifa ya kweli ya Mungu na walikuwa hawajawahi kumcha Mungu kwa kweli. Kwani moyo wa Ayubu ulikuwa safi, na haukufichwa kuonekana na Mungu, na ubinadamu wake ulikuwa wenye uaminifu na ukarimu, na alipenda haki na kile kilichokuwa kizuri. Binadamu kama huyu pekee aliyemiliki moyo kama huo na ubinadamu ndiye aliyeweza kufuata njia ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Binadamu kama huyo angeona ukuu wa Mungu, angeona mamlaka na nguvu Yake, na angeweza kutimiza utiifu kwa ukuu Wake na mipangilio. Binadamu tu kama huyo ndiye angeweza kusifu jina la Mungu kwa kweli. Hii ni kwa sababu hakuangalia kama Mungu angembariki yeye au Angemletea janga, kwa sababu alijua kwamba kila kitu kinadhibitiwa na mkono wa Mungu, na kwamba binadamu kuwa na wasiwasi ni ishara ya ujinga, kutojua, na kutoweza kufikiria vyema, kuwa na shaka katika ukweli wa ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, na ya kutomcha Mungu. Maarifa ya Ayubu hasa ndiyo ambayo Mungu alitaka. Hivyo basi, Ayubu alikuwa na maarifa makubwa ya kinadharia kumhusu Mungu kuliko wewe? Kwa sababu kazi na matamko ya Mungu wakati huo yalikuwa machache, halikuwa jambo rahisi kutimiza maarifa ya Mungu. Mafanikio kama hayo ya Ayubu hayakukuwa jambo dogo. Alikuwa hajapitia kazi ya Mungu wala hakuwahi kusikia Mungu akiongea, au kuuona uso wa Mungu. Kwamba aliweza kuwa na mwelekeo kama huo kwa Mungu yalikuwa ni hasa matokeo yaliyoonyesha ubinadamu wake na ufuatiliaji wake wa kibinafsi, ubinadamu na ufuatiliaji ambao haujamilikiwa na watu leo. Hivyo, katika enzi hiyo, Mungu alisema, “hakuna kama yeye duniani, mtu mkamilifu na aliye mnyoofu mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu.” Katika enzi hiyo, Mungu alikuwa tayari amefanya ukadiriaji wake Ayubu, na alikuwa amefikia hitimisho fulani. Ungekuwa ukweli zaidi kwa kiasi kipi hii leo?
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Tufuate: Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni