Kanisa la Mwenyezi Mungu |11. Kiini cha Ulipizaji Kisasi wa Mtu Binafsi
Zhou Li Mji wa Xintai, Mkoa wa Shandong
Wakati fulani kitambo, tulihitaji kuzichora wilaya katika eneo letu, na kwa msingi wa kanuni zetu kwa ajili ya uteuzi wa viongozi, kulikuwa na ndugu mmoja wa kiume aliyekuwa mtaradhia mzuri kiasi. Nilitayarisha kumpandisha cheo hadi kuwa kiongozi wa wilaya. Siku moja nilipokuwa nikizungumza na ndugu huyu, alitaja kwamba alihisi kuwa nilikuwa mwenye nguvu sana katika kazi yangu, mkali sana, na kwamba katika mkusanyiko pamoja nami hapakuwa na furaha nyingi .... Niliposikia jambo hili, nilihisi kuwa nilikuwa nimedunishwa.
Nilihisi vibaya sana; mara moja nikakuza maoni fulani ya ndugu huyu, na sikukusudia tena kumpandisha cheo kuwa kiongozi wa wilaya. Niliporejea kwa familia wenyeji wangu, nilikuwa bado ninakerwa na singetulia. Wakati huo, niliwaza juu ya kitu fulani kutoka kwa "Viongozi Wazembe Wasiotekeleza Kazi Yao Inayofaa Wanapaswa Kuondoshwa" katika ushirika wa mwanadamu: "Jinsi viongozi wanavyowatendea ndugu wa kiume na wa kike ambao huwaona ni wenye kusumbua, ambao wanawapinga, ambao wana maoni tofauti kabisa nao–hili ni suala la maana sana na linapaswa kushughulikiwa kwa tahadhari. Wasipoingia katika ukweli, kwa hakika watabagua na kumgomea mtu huyu wakati wanapokumbwa na aina hii ya suala. Aina hii ya hatua inafichua kabisa asili ya joka kubwa jekundu linalompinga na kumdharau Mungu. Ikiwa kiongozi ni mtu ambaye hufuatilia ukweli, ambaye ana dhamiri, na hisi, atatafuta ukweli na kuushughulikia kwa usahihi. ... Kama watu, tunahitaji kuwa wa haki na wa kutopendelea. Kama viongozi, tunapaswa kushughulikia mambo kulingana na maneno ya Mungu ili kuwa mashahidi. Tukifanya mambo kulingana na mapenzi yetu wenyewe, tukiipa uhuru tabia yetu potovu, basi huo utakuwa ushinde wa kuogofya." Sikuweza kujizuia kulinganisha mitazamo yangu miwili tofauti kabisa tangu kabla na baada ya mazungumzo yangu na ndugu huyo. Kwanza nilikuwa tayari kumpandisha cheo kuwa kiongozi wa wilaya, lakini alisema mambo fulani yaliyonisababisha kupoteza heshima nilipozungumza naye, hivyo nilibadili maoni yangu juu yake mara moja na sikupanga tena kumpandisha huko cheo. Je, si huku kulikuwa kutumia nguvu yangu kulipiza kisasi cha ubinafsi? Je, kuna tofauti gani kati ya hili na joka kuu jekundu kubagua na kuchapa dhidi ya wale wanaopinga? Je, si aina hii ya kitendo ni ya kudharauliwa? Kanisa si sawa na jamii. Kanisa linahitaji kila ngazi ya viongozi wake kuwa watu wenye ubinadamu, wanaoupenda ukweli, na wanaoweza kuukubali ukweli. Halihitaji watu wanaojikomba, ambao hawatambui ukweli. Lakini kile nilichokuwa nikikifanya kilikuwa kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu. Wakati wa kuchagua mtaradhia nilifikiria tu juu ya maslahi yangu mwenyewe na mradi tu yule mtu mwingine hakuniunga mkono, aliposema kitu ambacho hakikunipendeza, nilifanya ubaguzi dhidi yake na kumchukia. Je, si kutenda kwangu jinsi hii kulifichua kabisa asili ya joka kubwa jekundu likimpinga na kumsaliti Mungu? Je, si ulikuwa mfichuo wa tabia ya Shetani kabisa, "Nitii au uangamie"? Si kutenda jinsi hii kulikuwa kuwa mtumishi wa Shetani, kuivuruga kazi ya Mungu na kuwa adui Yake? Je, si moyo wangu ni mwovu sana? Kanisa lilikuwa karibu kumchagua mtu kwa nafasi fulani, na ndugu huyo alikuwa mtaradhia mzuri kwa nafasi ya kiongozi wa wilaya. Tathmini yake kwangu ilikuwa haikubaliki kwangu; Ningepaswa kutafuta ukweli juu ya jambo hili na kuyakubali maoni yake. Ningepaswa kujichunguza mwenyewe na kujijua mwenyewe, na kufidia upungufu katika kazi yangu. Hata hivyo, sio tu kwamba sikuangalia sababu ndani yangu, lakini niliipa uhuru asili ya Shetani ndani yangu kubagua na kulipiza kisasi kwake. Mimi ni mwenye kiburi sana, nikipungukiwa sana katika ubinadamu! Tabia hii yangu ni ya kuchukiza sana kwa Mungu! Kama ningeendelea kukupa uhuru asili ya aina hii ya upotovu, hatimaye ningekuwa nimekwisha kuharibika kama mtumishi mwenye kiburi wa uovu ambaye ni kipofu kwa Mungu. Kwa hakika nilikuwa katika hatari kubwa. Wakati huo singeweza kujizuia kutetemekea mawazo na matendo yangu, kujiona nimejaa sumu ya joka kubwa jekundu, kwamba yaliyofichuliwa yote yalikuwa ni uadui dhidi ya Mungu. Mungu kwa hakika huchukia hili, na huchukizwa nalo.
Ee Mungu, asante kwa kunurisha Kwako kwa haraka, kwa kuzuia tabia yangu ya ubaguzi, kwa kuniruhusu kuona vyema zaidi asili yangu mbovu na uso wangu wa Shetani ukitenda kama adui Yako. Kuanzia siku hii kwendelea, ninapenda kufuata mabadiliko katika tabia, na wakati ninapokutana na watu au vitu ambavyo havinipendezi, nitajifunza kujiweka kando, kuunyima mwili, na katika vitu vyote kuyalinda maslahi ya kanisa, kufanya kila linalowezekana ili kutimiza majukumu yangu.
Utukufu wote Uwe kwa Mwenyezi Mungu!
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni