Matamshi ya Mwenyezi Mungu | (Sehemu ya Nne)
(II) Ubinadamu Hupata Kibali cha Huruma na Uvumilivu wa Mungu Kupitia kwa Toba ya dhati
Kinachofuata ni hadithi ya biblia ya “Wokovu wa Mungu kwa Ninawi.”
(Yona 1:1-2) Basi neno la BWANA lilimjia Yona mwana wa Amitai, likisema, Inuka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, upige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.
(Yona 3) Neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili, likisema, Inuka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, uhubiri habari Ninayokuamuru. Basi Yona akainuka, akaenda Ninawi, kulingana na amri ya BWANA. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu. Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti, akasema, Baada ya siku arobaini mji wa Ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, wakavaa nguo za magunia, kutoka Yule aliye mkubwa hadi aliye mdogo. Hivyo habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akavaa nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake, ikisema, Mwanadamu au myanma asionje kitu, wala makundi ya ng’ombe wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji: Bali mwanadamu na mnyama pia afunikwe nguo za magunia, nao wamlilie Mungu kwa nguvu: naam, na wageuke, kila mmoja aache njia yake ya uovu, na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye iwapo Mungu atageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili tusiangamizwe? Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya; Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; na hakulitenda.
(Yona 4) Lakini jambo hili lilimchukiza Yona sana, naye akakasirika sana. Akaomba kwa BWANA, akasema, Nakuomba, Ee BWANA, sivyo hivyo nilivyosema, nilipokuwa bado katika nchi yangu? Kwa hivyo nilikimbilia Tarshishi kabla: kwa maana nilijua kuwa wewe ni Mungu mwenye neema, na mwenye huruma, si mwepesi wa hasira, na mwingi wa rehema, nawe unaghairi mabaya. Basi sasa, Ee BWANA, chukua, nakuomba, uhai wangu kutoka kwangu; kwa maana ni afadhali mimi nife kuliko kuishi. Naye BWANA akasema, Je, unatenda vema kukasirika? Hivyo Yona akatoka nje ya mji, akaketi upande wa mashariki wa mji, na huko akajifanyia kibanda, akakaa chini yake kivulini, mpaka aone mji ule utakuwaje. Na BWANA Mungu akatayarisha mtango, akaufanya uje juu ya Yona, ili uwe kivuli juu ya kichwa chake, na kumwokoa kutoka katika huzuni wake. Basi Yona akaufurahia sana ule mtango. Lakini Mungu akatayarisha buu siku ya pili kulipopambazuka, nalo likautafuna ule mtango hadi ukanyauka. Na hivyo ikawa, jua lilipopanda juu, kwamba Mungu akautayarisha upepo mkali wa mashariki; na jua likampiga Yona kichwani, hata akazimia, naye akatamani afe, na akasema, Ni heri mimi nife kuliko niishi. Mungu akamwambia Yona, Je, unatenda vema kukasirika kwa ajili ya mtango? Naye akasema, Ndiyo, natenda vema kukasirika, hata mpaka kufa. Kisha Bwana akasema, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuukuza; uliomea kwa usiku mmoja, na kuangamia kwa usiku mmoja: Na mimi, je, Sipaswi kuuhurumia mji wa Ninawi, mji ule mkubwa, ambao ndani yake wamo zaidi ya watu mia na ishirini elfu ambao hawawezi kupambanua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?
Muhtasari wa Hadithi ya Ninawi
Ingawaje hadithi ya “wokovu wa Mungu wa Ninawi” ni fupi kwa urefu, inaruhusu mtu kuweza kuona kidogo tu ule upande mwingine wa tabia ya haki ya Mungu. Ili kuweza kuelewa haswa upande huo unajumuisha nini, lazima turudi kwenye Maandiko na kuangalia nyuma katika mojawapo ya matendo ya Mungu.
Hebu kwanza tuangalie mwanzo wa hadithi hii: “Basi neno la BWANA lilimjia Yona mwana wa Amitai, likisema, Inuka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, upige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu” (Yona 1:1-2). Katika fungu hili kutoka kwenye Maandiko, tunajua kwamba Yehova Mungu alimwamuru Yona kwenda katika mji wa Ninawi. Kwa nini alimwamuru Yona kwenda katika mji huo? Biblia iko wazi kabisa kuhusu suala hili: Maovu ya watu walio ndani ya mji huo yalikuwa yamefikia macho ya Yehova Mungu, na hivyo basi Alimtuma Yona ili kuwatangazia kile Alichonuia kufanya. Ingawa hakuna kitu kilichorekodiwa kinachotwambia Yona alikuwa nani, jambo hili, bila shaka, halina uhusiano wowote na kumjua Mungu. Hivyo basi, huhitaji kumwelewa mwanamume huyu. Unahitaji kujua tu kile ambacho Mungu alimwamuru Yona kufanya na kwa nini Alifanya kitu hicho.
Onyo la Yehova Mungu Lawafikia Waninawi
Hebu tuendelee hadi kwenye fungu la pili, sura ya tatu ya kitabu cha Yona: “Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti, akasema, Baada ya siku arobaini mji wa Ninawi utaangamizwa.” Haya ndiyo maneno ambayo Mungu alipitisha moja kwa moja kwake Yona ili aweze kuwaambia Waninawi. Ndiyo pia, kwa kawaida, maneno ambayo Yehova alipenda kusema kwa Waninawi. Maneno haya yanatwambia kwamba Mungu alianza kukerwa na kuchukia watu wa mji huu kwa sababu ya maovu yao yaliyokuwa yamefika machoni pa Mungu, na hivyo basi, Alipenda kuuangamiza mji huo. Hata hivyo, kabla ya Mungu kuangamiza mji, Aliwatangazia Waninawi, na hapo kwa hapo Akawapa fursa ya kutubu maovu yao na kuanza upya. Fursa hii ingedumu kwa siku arubaini. Kwa maneno mengine, kama watu waliokuwa ndani ya mji huu wasingetubu, na kukubali dhambi au maovu yao wao wenyewe mbele ya Yehova Mungu ndani ya siku arubaini, Mungu angeangamiza mji huu kama Alivyoangamiza Sodoma. Hivi ndivyo ambavyo Yehova Mungu alipenda kuwaambia watu wa Ninawi. Ni wazi kwamba, hili halikuwa tangazo rahisi. Halikuweza tu kuonyesha hasira ya Yehova Mungu, lakini pia lilionyesha mtazamo Wake kwa wale Waninawi; wakati uo huo tangazo hili rahisi lilitumika kama onyo kali kwa watu waliokuwa wakiishi ndani ya mji huo. Onyo hili liliwaambia kwamba matendo yao maovu yalikuwa yamewafanya kuchukiwa na Yehova Mungu na liliwaambia kwamba matendo yao maovu yangewaletea hivi karibuni fedheha kutokana na maangamizo yao wenyewe; kwa hivyo, maisha ya kila mmoja kule Ninawi yalikuwa karibu kuangamia.
Utofautishaji Mkavu wa Ninawi na Mwitikio wa Sodoma kwa Onyo la Yehova Mungu
Kupinduliwa kunamaanisha nini? Kwa muktadha wa mazungumzo, kunamaanisha kutoweka. Lakini kwa njia gani? Ni nani angefanya mji mzima kupinduliwa? Haiwezekani kwa binadamu kufanya kitendo kama hicho, bila shaka. Watu hawa hawakuwa wajinga; mara tu waliposikia matangazo haya, walipata wazo hilo. Walijua kwamba yalikuwa yametoka kwa Mungu; walijua kwamba Mungu angetekeleza kazi Yake; walijua kwamba maovu yao yalikuwa yamemkasirisha Yehova Mungu na kumfanya kuwa na hasira kali kwao, ili waweze kuangamizwa pamoja na mji wao. Je, watu wa mji huo walichukulia vipi suala hilo baada ya kusikiliza onyo la Yehova Mungu? Biblia inafafanua kwa maelezo fafanuzi namna ambavyo watu hawa walivyoitikia, kuanzia kwa mfalme wao hadi kwa binadamu wa kawaida. Kama ilivyorekodiwa kwenye Maandiko: “Basi watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, wakavaa nguo za magunia, kutoka Yule aliye mkubwa hadi aliye mdogo. Hivyo habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akavaa nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake, ikisema, Mwanadamu au myanma asionje kitu, wala makundi ya ng’ombe wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji: Bali mwanadamu na mnyama pia afunikwe nguo za magunia, nao wamlilie Mungu kwa nguvu: naam, na wageuke, kila mmoja aache njia yake ya uovu, na udhalimu ulio mikononi mwake. …”
Baada ya kusikia tangazo la Yehova Mungu, watu wa Ninawi walionyesha mtazamo uliokuwa kinyume kabisa na ule wa watu wa Sodoma—watu wa Sodoma walimpinga Mungu waziwazi, huku wakiendelea kutoka kwa maovu hadi maovu, lakini baada ya kusikia maneno haya, Waninawi hawakupuuza suala hilo, wala hawakuweza kulipinga; badala yake walimsadiki Mungu na kutangaza kufunga. “Walisadiki” inarejelea nini hapa? Neno lenyewe linapendekeza imani na unyenyekevu. Kama tutatumia tabia halisi ya Waninawi kuelezea neno hili, inamaanisha kwamba walisadiki Mungu anaweza na angeweza kufanya vile Alivyosema, na kwamba walikuwa radhi kutubu. Je, watu wa Ninawi walihisi woga mbele ya janga lililokuwa karibu kutokea? Imani yao ndiyo iliyotia woga katika mioyo yao. Kwa kweli, ni nini tunachoweza kutumia kuthibitisha Imani na woga wa Waninawi? Ni sawa na vile Biblia inavyosema: “Na wao[a] wakatangaza kufunga, na wakavalia nguo ya gunia, kuanzia wale walio wakubwa zaidi na hata kwa wale walio wadogo zaidi.” Hivi ni kusema kwamba Waninawi walisadiki kweli, na kwamba kutoka kwenye imani hii woga uliibuka, ambao sasa ulisababisha kufunga na kuvaliwa kwa nguo ya gunia. Hivi ndivyo walivyoonyesha mwanzo wa toba yao. Tofauti kabisa na watu wa Sodoma, Waninawi hawakumpinga Mungu tu, bali walionyesha pia waziwazi toba yao kupitia kwa tabia na matendo yao. Bila shaka, hii haikutumika tu kwa watu wa kawaida wa Ninawi; hata mfalme wao hakubakizwa.
Toba ya Mfalme wa Ninawi Inasababisha Pongezi ya Yehova Mungu
Wakati mfalme wa Ninawi alipozisikia habari hizi, aliinuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua nguo zake, akavalia nguo ya gunia na kukalia jivu. Kisha akatangaza kwamba hakuna mtu kwenye mji huo ambaye angeruhusiwa kuonja chochote, na kuwa hakuna mifugo, wanakondoo na ng'ombe ambao wangekunywa maji na kula nyasi. Binadamu na mifugo kwa pamoja walitakikana kujifunika nguo ya gunia; nao watu wangemsihi Mungu kwa uaminifu. Mfalme pia alitangaza kwamba watu wote wangetupilia mbali njia zao za maovu na kukataa udhalimu ulioko mikononi mwao. Tukifanya uamuzi kutoka kwenye misururu ya vitendo hivi, mfalme wa Ninawi alionyesha toba yake ya dhati. Misururu ya vitendo alivyofanya—kutoka kwenye kiti chake cha ufalme, kulitupa joho lake la kifalme, kuvalia nguo ya gunia na kukalia majivu—kulionyesha watu kwamba mfalme wa Ninawi aliweka kando hadhi yake ya kifalme na kuvalia nguo ya gunia pamoja na watu wa kawaida wa nchi. Hii ni kusema kwamba mfalme wa Ninawi hakuweza kushikilia wadhifa wake wa kifalme ili aendelee na njia zake za maovu au udhalimu katika mikono yake baada ya kikao cha tangazo kutoka kwa Yehova Mungu; badala yake, aliweka pembeni mamlaka aliyoyashikilia na kutubu mbele ya Yehova Mungu. Kwenye kipindi hiki cha muda, mfalme wa Ninawi hakuwa akitubu akiwa mfalme; alikuwa amekuja mbele ya Mungu kuungama na kutubu dhambi zake akiwa binadamu wa kawaida wa Mungu. Aidha, aliuambia mji mzima kuungama na kutubu dhambi zao mbele ya Yehova Mungu kwa njia sawa na yeye; vilevile, alikuwa na mpango mahususi wa namna ya kufanya hivyo kama inavyoonekana kwenye Maandiko: “Mwanadamu au mnyama asionje kitu, wala makundi ya ng’ombe wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji. … nao wamlilie Mungu kwa nguvu: naam, na wageuke, kila mmoja aache njia yake ya uovu, na udhalimu ulio mikononi mwake.” Kama kiongozi wa mji, mfalme wa Ninawi alimiliki hadhi na nguvu za kimamlaka na angefanya chochote alichopenda. Alipokabiliwa na tangazo la Yehova Mungu, angeweza kupuuza suala hilo au kutubu na kuungama tu dhambi zake pekee; kuhusiana na kama watu wa mji wangechagua kutubu au la, angepuuza suala hili kabisa. Hata hivyo, mfalme wa Ninawi hakufanya hivyo kamwe. Mbali na kuinuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, kuvalia nguo ya gunia na kujipaka jivu na kuungama na kutubu dhambi zake mbele ya Yehova Mungu, aliweza pia kuwaamuru watu na mifugo ndani ya mji huo kufanya hivyo. Aliweza hata kuamuru watu “kumlilia Mungu kwa nguvu.” Kupitia misururu hii ya vitendo, mfalme wa Ninawi aliweza kukamilisha kwa kweli kile ambacho kiongozi anafaa kufanya; misururu ya vitendo vyake ndiyo iliyokuwa migumu kwa mfalme yeyote katika historia ya binadamu kutimiza, hatua na pia hatua ambayo hakuna aliyewahi kutimiza. Matendo haya yanaweza kuitwa shughuli isiyo na kifani katika historia ya binadamu; yanastahili kukumbukwa na kuigwa na binadamu. Tangu enzi ya mwanadamu, kila mfalme alikuwa amewaongoza wafuasi wake kukinzana na kumpinga Mungu. Hakuna yule aliyewahi kuwaongoza wafuasi wake kusihi Mungu kutafuta ukombozi kwa ajili ya maovu yao, kupokea msamaha wa Yehova Mungu na kuepuka adhabu kali. Mfalme wa Ninawi, hata hivyo, aliweza kuwaongoza raia wake kumlilia Mungu, kuacha njia zao mbalimbali za maovu na kutupilia mbali udhalimu ulio mikono mwao. Aidha, aliweza pia kuweka kando kiti chake cha enzi, na badala yake, Yehova Mungu alibadilisha na kughairi na kugeuza hasira Yake, na kuruhusu watu wa mji huu kuishi na kuwalinda dhidi ya kuangamia. Matendo ya mfalme yanaweza kuitwa tu muujiza wa nadra katika historia ya binadamu; yanaweza hata kuitwa kielelezo cha ubinadamu uliopotoka unaoungama na kutubu dhambi zake mbele ya Mungu.
Mungu Aona Kutubu kwa Dhati katika Kina cha Mioyo ya Waninawi
Baada ya kusikiliza tangazo la Mungu, mfalme wa Ninawi na raia Wake walitekeleza misururu ya vitendo. Je, ni nini asili ya tabia na matendo yao? Kwa maneno mengine, ni nini kiini cha uzima wa mwenendo wao? Kwa nini walifanya kile walichofanya? Katika macho ya Mungu walikuwa wametubu kwa dhati, si tu kwa sababu walikuwa wamemsihi Mungu kwa dhati na kuungama dhambi zao mbele Yake, lakini pia kwa sababu walikuwa wameacha mwenendo wao wenye maovu. Walichukua hatua namna hii kwa sababu baada ya kusikia matamshi ya Mungu, walitishika pakubwa na kusadiki kwamba angefanya vile ambavyo alikuwa amesema. Kwa kufunga, kuvalia nguo ya gunia na kukalia jivu, walipenda kuonyesha namna walivyokuwa radhi kubadilisha njia zao na kujizuia na maovu, kumwomba Yehova Mungu kuzuia hasira Yake, kusihi Yehova Mungu kutupilia mbali uamuzi Wake, pamoja na msiba mkuu ambao ulikuwa karibu kuwasibu. Kupitia uchunguzi wa tabia yao yote, tunaona ya kwamba tayari walielewa kwamba vitendo vyao vya awali vilimchukiza Yehova Mungu na kwamba walielewa sababu iliyomfanya kutaka kuwangaamiza hivi karibuni. Kwa sababu hizi, wote walipenda kutubu kabisa, kugeuka na kuacha njia zao za maovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Kwa maneno mengine, pindi tu walipotambua tangazo la Yehova Mungu, kila mmoja wao alihisi woga katika mioyo yao; hawakuendelea tena na mwenendo wao wa maovu wala kuendelea kutenda vitendo ambavyo Yehova Mungu alichukia. Vilevile, walimsihi Yehova Mungu kusamehe dhambi zao za kale na kutowatendea kulingana na vitendo vyao vya kale. Walikuwa radhi kutowahi kujihusisha tena katika maovu na kutenda kulingana na maagizo ya Yehova Mungu, kama tu wasingewahi kumkasirisha Yehova Mungu. Toba yao ilikuwa ya dhati na ya kweli. Ilitoka kwenye kina cha mioyo yao na haikuwa ya kujidanganya, wala haikuwa ya muda.
Baada ya watu wa Ninawi, kutoka kwa mfalme mwenye mamlaka hadi kwa raia wake, kujua kwamba Yehova Mungu alikuwa amewakasirikia, kila mojawapo ya vitendo vyao, tabia yao nzima, pamoja na kila mojawapo ya uamuzi na machaguo yao vilikuwa wazi na dhahiri mbele ya Mungu. Moyo wa Mungu ulibadilika kulingana na tabia yao. Akili Zake Mungu zilikuwa zinafikiria nini wakati huo? Biblia inaweza kukujibia swali hili. Kama ilivyorekodiwa kwenye Maandiko: “Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya; Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; na hakulitenda.” Ingawaje Mungu alibadilisha fikira Yake, hakukuwa na chochote kigumu kuhusu mtazamo wa fikira Yake. Aliweza kubadilika kutoka katika kuonyesha hasira Yake hadi kutuliza hasira Yake, na kisha kuamua kutouleta msiba mkuu katika mji wa Ninawi. Sababu ya uamuzi wa Mungu wa—kuwaokoa Waninawi dhidi ya msiba wao mkuu—ilikuwa ya haraka mno, ni kwa sababu Mungu aliangalia moyo wa kila mmoja wa wale Waninawi. Aliona kwamba katika kina cha mioyo yao waliweza: kuungama na kutubu kwa dhati dhambi zao, imani yao ya dhati kwake Yeye, mtazamo wao wa kina kuhusu vile vitendo vyao vya maovu vilikuwa vimeipa tabia Yake hasira kali, na woga uliotokana na adhabu ya Yehova Mungu iliyokuwa inakaribia. Wakati uo huo, Yehova Mungu aliweza kusikia maombi kutoka kwenye kina cha mioyo yao wakimsihi kusitisha hasira Yake dhidi yao ili waweze kuepuka msiba huu mkuu. Wakati Mungu alipoangalia hoja hizi zote, kwa utaratibu hasira yake ilitoweka. Licha ya vile hasira yake ilivyokuwa kuu hapo awali, alipoona kutubu kwao kwa dhati ndani ya kina cha mioyo ya watu hawa, moyo Wake uliguswa na hili, na kwa hivyo Hakuweza kuvumilia kuwaletea msiba mkuu, na Alisitisha hasira yake kwao. Badala yake Aliendelea kuwaonyesha huruma Yake na uvumilivu kwao na akaendelea kuwaongoza na kuwakimu.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni