Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote
|
Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II
(Sehemu ya Pili)
Baada ya Ukinzani wa Mara kwa Mara wa Sodoma na Ukatili Wao Dhidi Yake, Mungu Anaifuta Kabisa
Mwenyezi Mungu alisema, Mara tu tunapokuwa na ufahamu wa jumla kuhusu tabia ya haki ya Mungu, tunaweza kurejesha umakinifu wetu kwenye mji wa Sodoma—kile ambacho Mungu aliona kuwa mji wa dhambi. Kwa kuelewa hali halisi ya mji huu, tunaweza kuelewa ni kwa nini Mungu alitaka kuuangamiza na ni kwa nini Aliuangamiza kabisa. Kutokana na haya, tunaweza kujua tabia ya haki ya Mungu.
Kutoka katika mtazamo wa binadamu, Sodoma ilikuwa ni mji ulioweza kutosheleza kikamilifu matamanio ya binadamu na maovu ya binadamu. Ulivutia na uliduwaza, kwa muziki na densi usiku baada ya usiku, ufanisi wake uliwasukuma wanaume kufurahia na kuruka kichwa. Maovu yake yalidhuru mioyo ya watu na yakawaduwaza hadi kuzoroteka. Huu ulikuwa mji uliokuwa na roho chafu na roho za Shetani ziliduruduru hewani; ulijaa dhambi na mauaji na harufu ya damu iliyovunda. Ulikuwa mji ambao ulitisha watu kabisa, mji ambao mtu angejitoa kwake kwa hofu. Hakuna mtu katika mji huu—awe wa kiume au wa kike, awe mchanga au mzee—aliyetafuta njia ya kweli; hakuna aliyetamani mwangaza au kutaka kuachana na dhambi. Kila mmoja aliishi chini ya udhibiti wa Shetani, upotovu na uwongo. Kila mmoja alikuwa ameupoteza ubinadamu wake; walikuwa wamepoteza hisia zao, na walikuwa wamepoteza shabaha asilia ya kuweko kwa binadamu. Walitenda dhambi zisizohesabika za ukinzani dhidi ya Mungu; walikataa mwongozo wake na kupinga mapenzi Yake. Yalikuwa matendo yao maovu ambayo yaliwapeleka watu hawa, mji na kila kiumbe kilichokuwa ndani ya mji huu, hatua kwa hatua, kwenye njia ya maangamizo.
Ingawaje mafungu haya mawili hayarekodi maelezo yanayofafanua kiwango cha kupotoka cha watu wa Sodoma, badala yake yanarekodi mwenendo wao kwa watumishi wawili wa Mungu kufuatia kuwasili kwao mjini, ukweli mtupu unaweza kufichua kiwango ambacho watu wa Sodoma walikuwa wamepotoka, walijaa maovu na walimpinga Mungu. Kwa mujibu wa haya, ukweli wa mambo na hali halisi ya watu wa mji huu vinafichuliwa pia. Mbali na kutokubali maonyo ya Mungu, hawakuogopa pia adhabu Yake. Kinyume cha mambo ni kwamba, walifanyia mzaha ghadhabu ya Mungu. Walimpinga Mungu bila sababu. Haijalishi ni nini Alichofanya au ni vipi Alivyokifanya, asili yao ya tamaa ilizidi kuongezeka, na wakampinga Mungu mara kwa mara. Watu wa Sodoma walikuwa wakatili kwa uwepo wa Mungu, kuja Kwake, adhabu Yake, na hata zaidi, maonyo Yake. Hawakuona chochote kingine chenye thamani karibu nao. Waliwapotosha na kuwadhuru watu wote walioweza kupotoshwa na kupata madhara, na wakawatendea watumishi wa Mungu vivyo hivyo. Kuhusiana na matendo yote ya uovu yaliyotendwa na watu hawa wa Sodoma, kuwadhuru watumishi wa Mungu kulikuwa mfano tu wa tone baharini ya kile walichokuwa wakifanya, na asili yao ya uovu yaliyofichuliwa kwa kweli yalionekana tu kuwa madogo zaidi kuliko hata tone moja ndani ya bahari kubwa. Kwa hivyo, Mungu alichagua kuwaangamiza kwa moto. Mungu hakutumia gharika, wala Hakutumia zilizala, mtetemeko wa ardhi, tsunami au mbinu yoyote nyingine ya kuuangamiza mji huu. Kule kutumia moto na Mungu kuangamiza mji huu kulimaanisha nini? Kulimaanisha uangamizaji kamili wa mji huo; kulimaanisha kwamba mji huu ulitoweka kabisa kutoka ulimwenguni na kutoka katika kuwepo kwake. Hapa, “kuangamiza” hakurejelei tu kule kutoweka kwa umbo na muundo au sura ya nje ya mji huo; kunamaanisha pia kwamba nafsi za watu ndani ya mji huo zilisita kuwepo, baada ya kufutwa kabisa. Kwa ufupi, watu wote, matukio na mambo yote yaliyohusiana na mji huu yaliangamizwa. Kusingekuwa na maisha baada ya kifo au roho kuwa mwilini mwao; Mungu alikuwa amewafuta kabisa kutoka katika ubinadamu, uumbaji Wake, mara moja na tena milele. Yale “matumizi ya moto” yalimaanisha kusitisha dhambi, na yalimaanisha mwisho wa dhambi; dhambi hii ingesita kuwepo na kuenea. Yalimaanisha kwamba uovu wa Shetani ulikuwa umepoteza mahali pake pa kunawiri pamoja na eneo la kaburi ambalo liliupatia mji huo mahali pa kukaa na kuishi. Kwenye vita kati ya Mungu na Shetani, matumizi ya moto na Mungu ni alama ya ushindi Wake ambayo Shetani anatajiwa. Kuangamizwa kwa Sodoma ni hatua kubwa ya kuzuia maono ya Shetani ya kupinga Mungu kwa kupotosha na kudanganya binadamu, na vilevile ni ishara ya kudhalilishwa kwa muda kwenye maendeleo ya ubinadamu ambapo binadamu alikataa mwongozo wa Mungu na akajiachilia kutenda maovu. Aidha, ni rekodi ya ufunuo wa kweli wa tabia ya haki ya Mungu.
Wakati ule moto ambao Mungu alituma kutoka mbinguni ulikuwa umeteketeza kabisa Sodoma hata zaidi ya majivu, ilimaanisha kwamba mji huu ulioitwa “Sodoma” ungesita kuwepo, na vilevile kila kitu ndani ya mji wenyewe. Uliangamizwa kwa ghadhabu ya Mungu; ulitoweka kutokana na hasira na adhama ya Mungu. Kwa sababu ya tabia ya haki ya Mungu Sodoma ilipokea adhabu yake ya haki; kutokana na tabia ya haki ya Mungu, ilipokea mwisho wake wa haki. Mwisho wa kuwepo kwa Sodoma ulitokana na maovu yake, na ulitokana pia na tamanio la Mungu kutowahi kuutazamia mji huu tena, pamoja na watu wote walioishi ndani ya mji huo au maisha yoyote yaliyowahi kukua ndani ya mji huo. “Tamanio la kutowahi kuutazamia mji huo tena” la Mungu ni hasira Yake, pamoja na adhama Yake. Mungu aliuteketeza mji kwa sababu maovu na dhambi zake vilimsababisha Yeye kuhisi ghadhabu, maudhi na chuki katika mji huu na tamanio lake la kutowahi kuuona au watu wowote wa mji huo na viumbe vyote vilivyo hai vilivyokuwa ndani ya mji huo tena. Baada ya mji huo kuacha kuchomeka, huku ukiwa umeacha nyuma jivu pekee, ulikuwa kwa kweli umesita kuwepo mbele ya macho ya Mungu; hata kumbukumbu za Mungu kuuhusu ziliondolewa, zilifutwa. Hii inamaanisha kwamba moto ulioangushwa kutoka mbinguni haukuangamiza tu mji wote wa Sodoma kwa jumla na watu waliokuwa wamejaa dhambi ndani yake, wala kuangamiza tu vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji uliokuwa umepatwa na dosari ya dhambi; hata zaidi, moto huu uliangamiza kumbukumbu za maovu na ukinzani wa binadamu dhidi ya Mungu. Hili ndilo lilikuwa kusudio la Mungu kwa kuuchoma ule mji.
Ubinadamu ulikuwa umepotoka kupindukia. Watu hawa hawakujua Mungu alikuwa nani au kule walikokuwa wametokea. Kama ungemtaja Mungu, watu hawa wangekushambulia, kukutukana na kukufuru. Hata wakati watumishi wa Mungu walikuwa wamekuja kueneza onyo Lake, watu hawa waliopotoka hawakuweza kuonyesha ishara zozote za toba; vilevile hawakuacha mwenendo wao wa maovu. Kinyume cha mambo ni kwamba, waliweza bila ya haya, kuwadhuru watumishi wa Mungu. Kile walichoonyesha na kufichua kilikuwa asili na hali yao halisi ya uadui mkubwa kwa Mungu. Tunaweza kuona kwamba ukinzani wa watu hawa waliopotoka dhidi ya Mungu ulikuwa zaidi ya ufunuo wa tabia yao potoshi, kama vile tu ilivyokuwa zaidi ya tukio la matusi au kejeli iliyotokana na ukosefu wa ufahamu wa ukweli. Ujinga wala kutojua havikusababisha mwenendo huu wa maovu; haikuwa kwa sababu watu hawa walikuwa wamedanganywa, na bila shaka si kwa sababu walikuwa wamepotoshwa. Mwenendo wao ulikuwa umefikia kiwango cha uhasama wa wazi wa kupinga na kuasi dhidi ya Mungu. Bila shaka, aina hii ya tabia ya binadamu ingempa hasira kali Mungu, na ingeongeza hasira kali kwenye tabia Yake—tabia ambayo haifai kukosewa. Kwa hivyo, Mungu aliachilia kwa njia ya moja kwa moja na kwa uwazi hasira Yake na adhama Yake; huu ni ufunuo wa kweli wa tabia Yake ya haki. Akiwa amekabiliwa na mji uliotiririka na dhambi, Mungu alitamani kuuangamiza kwa njia ya haraka zaidi iliyowezekana; Alipenda kuwaondoa watu waliokuwa ndani yake na uzima wa dhambi zao kwa njia kamilifu zaidi, kuwafanya watu hawa wa mji kusita kuwepo na kukomesha dhambi ndani ya mahali hapa kuongezeka. Njia ya haraka zaidi na kamilifu zaidi ya kufanya hivyo ilikuwa ni kuuteketeza kwa moto. Mtazamo wa Mungu kwa watu wa Sodoma haukuwa ule wa kuwaacha au kutowajali; bali, Alitumia hasira Yake, adhama na mamlaka kuwaadhibu, kuwaweka chini na kuwaangamiza kabisa watu hawa. Mtazamo wake kwao haukuwa tu ule wa kuwaangamiza kimwili bali pia kuwaangamiza kinafsi, ukomeshaji wa milele. Hii ndiyo athari ya kweli ya tamanio la Mungu kwao “kuweza kusita kuwepo.”
Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote
Namna Mungu alivyoshughulikia ubinadamu wote wa ujinga na kutojua ulitokana kimsingi na huruma na uvumilivu. Hasira yake, kwa upande mwingine, imefichwa kwenye wingi mkubwa mno wa muda na wa mambo; haijulikani kwa binadamu. Kutokana na hayo, ni vigumu sana kwa binadamu kumwona Mungu akionyesha hasira Yake, na ni vigumu pia kuelewa hasira Yake. Kwa hivyo, binadamu huchukulia hasira ya Mungu kuwa ndogo. Wakati binadamu anapokabiliwa na kazi ya mwisho ya Mungu na hatua ya kuvumilia na kusamehe binadamu—yaani, wakati onyesho la mwisho la Mungu la huruma na onyo Lake la mwisho linapowafikia—kama bado wangali wanatumia mbinu zile kumpinga Mungu na hawafanyi jitihada zozote za kutubu, kurekebisha njia zao au kukubali huruma Yake, Mungu hataweza tena kuwapatia uvumilivu na subira yake. Kinyume cha mambo ni kwamba, ni katika wakati huu ambapo Mungu atafuta huruma Yake. Kufuatia hili, Atatuma tu hasira Yake. Anaweza kuonyesha hasira Yake kwa njia tofauti, kama vile tu Anavyoweza kutumia mbinu tofauti kuwaadhibu na kuwaangamiza watu.
Matumizi ya Mungu ya moto kuuangamiza mji wa Sodoma ndio mbinu Yake ya haraka zaidi ya kuondoa kabisa ubinadamu au kitu. Kuwachoma watu wa Sodoma kuliangamiza zaidi ya miili yao ya kimwili; kuliangamiza uzima wa roho zao, nafsi zao na miili yao, na kuhakikisha kwamba watu waliokuwa ndani ya mji wangesita kuwepo kwenye ulimwengu wa anasa na hata ulimwengu usioonekana na mwanadamu. Hii ni njia moja ambayo Mungu hufichua na kuonyesha hasira Yake. Mfano huu wa ufunuo na maonyesho ni dhana moja ya hali halisi ya hasira ya Mungu, kama vile ilivyo kwa kawaida pia ufunuo wa hali halisi ya tabia ya haki ya Mungu. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, Yeye husita kufichua huruma au upole wa upendo wowote, na wala haonyeshi tena uvumilivu au subira Yake; hakuna mtu, kitu au sababu inayoweza kumshawishi kuendelea kuwa na subira, kutoa huruma Yake tena, na kumpa binadamu uvumilivu wake kwa mara nyingine. Badala ya mambo haya, bila kusita hata kwa muda mfupi, Mungu atashusha hasira Yake na adhama, kufanya kile Anachotamani, na Atafanya mambo haya kwa haraka na kwa njia safi kulingana na matamanio Yake binafsi. Hii ndiyo njia ambayo Mungu hushusha hasira Yake na adhama, ambayo binadamu hafai kukosea, na pia ni maonyesho ya dhana moja ya tabia Yake ya haki. Wakati watu wanaposhuhudia Mungu akionyesha wasiwasi na upendo kwa binadamu, hawawezi kugundua hasira Yake, kuuona adhama Yake au kuhisi kutovumilia Kwake kwa kosa. Mambo haya siku zote yamewaongoza watu kusadiki kwamba tabia ya haki ya Mungu ni ile ya huruma, uvumilivu na upendo tu. Hata hivyo, wakati mtu anapoona Mungu akiuangamiza mji au akichukia ubinadamu, hasira Yake katika kuangamiza binadamu na adhama Yake huruhusu watu kuona picha ya upande ule mwingine wa tabia Yake ya haki. Huyu ni Mungu asiyevumilia kosa. Tabia ya Mungu isiyovumilia kosa inazidi yale mawazo ya kiumbe chochote kilichoumbwa, na miongoni mwa viumbe ambavyo havikuumbwa, hakuna kati ya hivyo kinachoweza kuhitilafiana na kingine au kuathiri kingine; lakini hata zaidi, hakiwezi kughushiwa au kuigwa. Kwa hivyo, dhana hii ya tabia ya Mungu ndiyo ambayo ubinadamu unafaa kujua zaidi. Mungu Mwenyewe Pekee ndiye aliye na aina hii ya tabia, na Mungu Mwenyewe pekee ndiye anayemiliki aina hii ya tabia. Mungu anamiliki aina hii ya tabia kwa sababu Anachukia maovu, giza, maasi na vitendo vya uovu vya Shetani—vya kupotosha na kudanganya wanadamu—kwa sababu Anachukia vitendo vyote vya dhambi vinavyompinga Yeye na kwa sababu ya hali Yake halisi takatifu na isiyo na doa. Ni kwa sababu ya haya ndiposa Hataacha viumbe vyovyote kati ya vile vilivyoumba au ambavyo havikuumbwa vimpinga waziwazi au kushindana na Yeye. Hata mtu binafsi ambaye Aliwahi kumwonyesha huruma au kuchagua anahitaji tu kuchochea tabia Yake na kukiuka kanuni Yake ya subira na uvumilivu, na Ataachilia na kufichua tabia Yake ya haki bila ya huruma hata kidogo au kusitasita kokote—tabia isiyovumilia kosa lolote.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni