Lee Chungmin alikuwa mzee wa kanisa fulani huko Seoul, Korea ya Kusini. Kwa zaidi ya miaka ishirini, alimtumikia Bwana kwa shauku kubwa, akamakinika kikamilifu juu ya kusoma Biblia. Akifuatia mfano wa viongozi wake wa kidini, alidhani kuwa kumwamini Bwana kulimaanisha kuiamini Biblia, na kwamba kuwa na imani katika Biblia kulikuwa sawa kabisa na kuwa na imani katika Bwana. Aliamini kwamba almuradi angeshika Biblia, angenyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni. Dhana hizi zilimbana kama jozi ya pingu, zikimzuia kufuata nyayo za Mungu na kumwamini Mungu. Matokeo yake, Lee Chungmin kamwe hakufikiria kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho …
Siku moja, kwa bahati kabisa, alitazama video za nyimbo katika tovuti ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Maneno yake ya kusisimua ya nyimbo na lahani sanifu zilimgusa kwa uzito, zikimtia msukumo kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Baada ya kupitia mijadala michache kuhusu ukweli, alikuja kuelewa maelezo ya ndani ya Biblia kupitia maneno ya Mwenyezi Mungu. Alikuja kuuelewa ukweli halisi wa hali kwa dhahiri: Mafarisayo wa ulimwengu wa kidini hupinga na kushutumu kuonekana kwa Mungu kwa kisingizio cha kuiinua Biblia. Hatimaye, aliachana na udhibiti na vizuizi vya Mafarisayo wa kidini na kufikia nyayo za Mungu …
Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni