Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima
Tamko la Ishirini
Mwenyezi Mungu alisema, Utajiri wa jumba Langu ni bila idadi na usioeleweka, lakini mwanadamu hajawahi kuja Kwangu kuufurahia. Hana uwezo wa kuufurahia mwenyewe, wala wa kujilinda mwenyewe kwa kutumia juhudi zake mwenyewe; badala yake, yeye daima huweka imani yake kwa wengine. Kati ya wale wote Ninaowatazamia, hakuna mtu aliyewahi kunitafuta kwa makusudi na moja kwa moja.
Wao wote huja mbele Zangu kwa kushawishiwa na wengine, wakiwafuata watu wengi, na hawana nia ya kulipa gharama au kutumia muda kustawisha maisha yao. Kwa hivyo, miongoni mwa watu hakuna mtu aliyewahi kuishi katika hali halisi, na watu wote huishi maisha yasiyo na maana. Kwa sababu ya njia na desturi za mwanadamu zilizoanzishwa kitambo, miili ya watu wote imejawa na harufu ya udongo wa ardhini. Kwa sababu hii, binadamu amekuwa sugu; hana hisia zozote kwa ukiwa wa ulimwengu, na yeye badala yake hujishughulisha na kazi ya kujifurahisha katika dunia hii iliyoganda. Maisha ya mwanadamu hayana joto hata kidogo, na hayana ubinadamu wala mwanga wowote—lakini hajawahi kujizoeza nayo, akivumilia maisha yasiyo ya thamani ambayo yeye huenda hapa na pale akiharakisha kufanya mambo bila kufikia kitu chochote. Kwa haraka sana, siku ya kufa inakaribia, na mtu anakufa kifo cha uchungu. Katika dunia hii, yeye hajawahi fanikisha kitu chochote, au kufaidi na kitu chochote—yeye hufika tu kwa haraka, na kwa haraka anaondoka. Hakuna yeyote miongoni mwa wale walio machoni Mwangu amewahi kuleta chochote wala kuchukua chochote, kwa hivyo mwanadamu anahisi kwamba dunia haina haki. Lakini hakuna anayenuia kuondoka kwa haraka. Wanangoja kwa hamu siku ambayo ahadi Yangu kutoka mbinguni itatimizika ghafla miongoni mwa watu, ikiwaruhusu, wakati ambapo wamepotea, kwa mara nyingine tena kutazama njia ya uzima wa milele. Kwa hivyo, binadamu hutazama kwa makini kila tendo Langu na hatua ili kuona kama Mimi kweli nimetimiza ahadi Yangu kwake. Wakati yeye yuko katika mateso, au katika maumivu makali, au amekumbwa na majaribio na anakaribia kuanguka, binadamu hulaani siku ya kuzaliwa kwake akikusudia kuondokewa na taabu zake na aelekee mahali palipo pema. Lakini wakati majaribio yanapopita, binadamu hujawa na furaha. Anaadhimisha siku ya kuzaliwa kwake duniani na ananiomba Niibariki siku yake ya kuzaliwa; wakati huu, binadamu huwa hataji tena viapo vya zamani, anahofu sana kwamba kifo kitamjia mara ya pili. Mikono Yangu inapoinua dunia, watu hucheza kwa furaha, hawaoni tena huzuni, na wao wote wananitegemea Mimi. Ninapoufunika uso Wangu kwa mikono Yangu, na kuwasukuma watu chini ya ardhi, mara moja wao hupungukiwa na pumzi, na ni vigumu waweze kuishi. Wao wote hunililia, wakiwa wenye hofu kwamba Nitawaangamiza, kwa maana wote wanatamani kutazama siku ambayo Nitatukuzwa. Mwanadamu huchukua siku Yangu kama kanuni ya uwepo wake, na ni kwa sababu tu ya matarajio ya watu ya wakati utukufu Wangu utafika kwamba mwanadamu anaishi mpaka leo. Baraka iliyotoka kwa kinywa changu ni kwamba wale waliozaliwa katika siku za mwisho ni wenye bahati ya kutosha kuona utukufu Wangu wote.
Katika enzi zote, wengi wametoweka duniani kwa taabu, na kusita, na wengi wamekuja duniani kwa matumaini na imani. Nimeandaa kuja kwa wengi, na pia Nimewaondoa wengi. Watu wengi wamepitia mikono Yangu. Roho nyingi zimetupwa Kuzimu, wengi wameishi katika mwili, na wengi wamekufa na wamezaliwa upya duniani. Hata hivyo kamwe hakuna yeyote kati yao aliyepata nafasi ya kufurahia baraka za ufalme leo. Mimi nimewapa wanadamu mengi sana, lakini wamepata kidogo, lakini kwa sababu mashambulizi ya jeshi la Shetani imewafanya wasiweze kufurahia utajiri Wangu wote. Amekuwa tu na bahati nzuri ya kuangalia juu, lakini hajawahi kuwa na uwezo wa kujifurahisha kikamilifu. Mwanadamu hajawahi gundua nyumba ya hazina mwilini mwake ili kupokea utajiri wa mbinguni, kwa hivyo amepoteza baraka ambazo Nimempa. Je, si roho ya mwanadamu ndio haswa uwezo wa kumuunganisha na Roho Wangu? Mbona mwanadamu hajawahi Kunihusisha na roho yake? Mbona ananikaribia kimwili na asiweze kunikaribia kiroho? Je, sura Yangu ya kweli ni ya kimwili? Mbona mwanadamu hatambui kiini Changu? Kuna uwezekano kuwa hakujawahi kuonekana ishara yoyote Yangu ndani ya roho ya mwanadamu? Je, Nimetoweka kabisa katika roho ya mwanadamu? Ikiwa mwanadamu hataingia katika ulimwengu wa kiroho, atawezaje kufahamu nia Zangu? Je, kuna chochote machoni mwa mwanadamu ambacho kinaweza penyeza moja kwa moja mpaka ulimwengu wa kiroho? Ni mara nyingi Nimemwita mwanadamu kwa Roho Wangu, lakini matendo yake huwa ni kama amechomwa kisu na Mimi, anahusiana nami kwa umbali, katika hofu kubwa kuwa Nitamwongoza kwenda ulimwengu mwingine. Kwa mara nyingi Nimepeleleza ndani ya moyo wa mwanadamu, lakini anabaki bila ufahamu kabisa, akiwa na hofu kubwa kabisa kuwa Nitaingia nyumbani mwake na kuchukua fursa hiyo kumnyang’anya mali yake yote. Kwa hivyo, ananifungia nje, kuniacha bila chochote ila mlango uliofungwa na kukazwa na kuniacha nje kwenye baridi. Ni mara nyingi mwanadamu ameanguka na Nimemwokoa, lakini baada ya kuamka ananiacha mara moja, bila kuguswa na upendo Wangu, mwanadamu kunipiga macho ya hadhari; Sijawahi pasha joto moyo wa mwanadamu. Mwanadamu ni kiumbe kikatili kisichokuwa na hisia. Hata kama amepashwa joto na kumbatio Langu, kamwe hajawahi guswa na jambo hili. Mwanadamu ni kama kiumbe katili cha mlimani. Hajawahi thamini upendo Wangu wa binadamu. Hana nia ya kunikaribia, akipendelea kukaa katika milima, ambapo anavumilia tishio la wanyama pori—lakini bado hana nia ya kuchukua makao ndani Yangu. Simshawishi mwanadamu yeyote: Ninafanya tu kazi Yangu. Siku itawadia ambapo mwanadamu ataogelea kuja upande Wangu kutoka katikati ya bahari kuu, ili aweze kufurahia mali yote ya dunia na kuacha hatari ya kumezwa na bahari.
Kwa kuwa maneno Yangu yametimilika, ufalme utaumbwa duniani hatua kwa hatua na mwanadamu atarudishwa kwa ukawaida hatua kwa hatua, na hivyo basi kutaanzishwa duniani ufalme ndani ya moyo Wangu. Katika ufalme, watu wote wa Mungu hupata maisha ya mwanadamu wa kawaida. Msimu wa barafu yenye baridi kali umeenda, umebadilishwa na dunia ya miji ya majira ya chipuko, ambapo majira ya chipuko yanashuhudiwa mwaka mzima. Kamwe, watu hawakumbwi tena na ulimwengu wa mwanadamu wenye huzuni na wenye taabu, na hawavumilii kuishi kwenye baridi kali ya dunia ya mwanadamu. Watu hawapigani na wenzao, mataifa hayaendi vitani dhidi ya wenzao, hakuna tena uharibifu na damu imwagikayo kutokana na uharibifu huo; maeneo yote yamejawa na furaha, na kila mahali pote panafurikwa na joto baina ya wanadamu. Naenda Nikipitia dunia nzima, Nafurahia kutoka juu ya kiti Changu cha enzi, Naishi miongoni mwa nyota. Na malaika wananipa nyimbo mpya na dansi mpya. Udhaifu wao hausababishi machozi kutiririka nyusoni mwao tena. Sisikii tena, mbele Yangu, sauti za malaika wakilia, na hakuna tena anayeninung’unikia kuwa ana shida. Leo hii, nyote mko hai mbele Yangu; kesho nyote mtakua hai ndani ya ufalme Wangu. Je, si hii ndiyo baraka kubwa zaidi ambayo Nimempa mwanadamu? Kwa sababu ya gharama ambayo mnalipa leo, mtarithi baraka za wakati ujao na mtaishi ndani ya utukufu Wangu. Je, si bado mnataka kujihusisha na kiini cha Roho Wangu? Je, bado mnataka kujiua wenyewe? Watu wako tayari kufuata ahadi ambazo wanaweza kuziona, hata kama ni za muda mfupi, lakini hakuna aliye tayari kukubali ahadi za kesho, hata kama ni za milele. Vitu vinavyoonekana kwa mwanadamu ni vitu ambavyo Nitaangamiza, na vitu visivyoweza kushikika na mwanadamu ndivyo Nitakavyotimiza. Hii ndiyo tofauti ya Mungu na mwanadamu.
Mwanadamu amehesabu siku Yangu, lakini hakuna yeyote amewahi jua siku kamili, na hivyo mtu anaweza kuishi tu katikati ya mzubao. Kwa sababu matamanio ya mwanadamu huvuma katika anga isiyo na kikomo, halafu inapotea, mwanadamu amepoteza tumaini mara kwa mara tena, hadi ameshuka kwa hali yake ya sasa. Lengo la matamko Yangu si kumfanya mwanadamu kufuata tarehe, wala si kumsukuma aangamie kwa sababu ya kukata tamaa. Natamani kumfanya mwanadamu akubali ahadi Yangu, na Ninatamani watu duniani kote kuwa na mgawo wa ahadi Yangu. Kile Ninachotaka ni viumbe walio hai ambao wamejawa na uzima, si maiti ambazo zimegubika katika kifo. Kwa kuwa Ninaketi mezani pa ufalme, Nitatoa amri kwa watu wote duniani ili wapate ukaguzi Wangu. Siruhusu uwepo wa kitu chochote kisicho safi mbele Yangu. Sivumilii uwezekano wa mtu yeyote kuingilia kazi Yangu; wale wote ambao huingilia kati kazi Yangu wanatupwa katika gereza la chini ya ardhi, na baada ya kuachiliwa huru bado watakabiliwa na janga, watapokea miale ya moto ya kuunguza dunia. Wakati Mimi Niko katika hali yangu ya kimwili, yeyote anayepinga Kazi Yangu na mwili Wangu atanichukiza. Ni mara nyingi Nimewakumbusha wanadamu wote kwamba Mimi sina jamaa duniani, na yeyote aonaye kuwa Mimi ni sawa na yeye, na ananivuta kuja kwake ili aweze kupata kumbukumbu za nyakati za zamani na Mimi, ataangamia. Hii ndiyo amri Yangu. Katika masuala hayo Sina huruma kwa mwanadamu. Wale wote ambao huingilia kazi Yangu na hutoa ushauri Kwangu wanaadibiwa na Mimi, na kamwe Sitawasamehe. Kama Sizungumzi waziwazi, mwanadamu kamwe hataacha kufanya upumbavu kamwe, na ataanguka katika kuadibu Kwangu bila kujua—kwa kuwa mwanadamu hanijui katika nafsi ya mwili Wangu.
Machi 20, 1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni