Ijumaa, 29 Juni 2018

Yule Anayeshikilia Ukuu // Juu ya Kila Kitu | Ahadi ya Mungu kwa Waisraeli

Ahadi ya Mungu kwa Waisraeli

Katika mwaka wa Bwana wetu, mtoto wa kiume alizaliwa katika hori kwa nyumba ya wageni katika Bethlehemu ya Uyahudi. Wanaume watatu wenye busara kutoka mashariki, wakiongozwa na nyota ambayo haikuwahi kuonekana kabla, walifika mahali pa kuzaliwa kwa mtoto.Wakamsujudia kwa ibada. Mtoto huyu Ndiye aliyeahidiwa na Mungu, ambaye angewaongoza na kuwakomboa Waisraeli kutoka kwa sheria.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wokovu,
Mungu Kuja Duniani na Kuwa Sadaka ya Dhambi
Kuja kwa Bwana Yesu hakumalizi tu enzi nzee iliyofungwa na sheria, na kuwaleta wanadamu kwa enzi mpya, lakini pia kunaboresha uhusiano kati ya mwanadamu na Mungu, na kunaashiria mwanzo mpya, hatua mpya ya kuanzia, kwa kazi ya Mungu ya usimamizi miongoni mwa wanadamu.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Bwana Yesu,
📚Mwenyezi Mungu alisema, Katika kazi ya Enzi ya Neema, Yesu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu. Alichokuwa nacho na Aliyekuwa ni neema, upendo, huruma, uvumilivu, subira, unyenyekevu, huduma, na stahamala, na nyingi ya kazi ambayo Alifanya ilikuwa kumwokoa mwanadamu. Na kuhusu tabia Yake, ilikuwa tabia ya huruma na upendo, na kwa sababu Yeye Alikuwa na huruma na upendo, ilikuwa sharti asulubishwe msalabani kwa ajili ya mwanadamu, ili kuonyesha kwamba Mungu Alimpenda mwanadamu jinsi anavyojipenda, kwa kiasi kwamba Yeye mwenyewe Alijitoa kama kafara na kwa ukamilifu Wake. Shetani akasema, "Kwa kuwa Unampenda mwanadamu, Lazima Umpende kwakwa kiwango cha juu zaidi: Lazima Upigiliwe misumari msalabani, kumwokoa mwanadamu kutoka msalabani, kutoka kwa dhambi, na Wewe utajitolea Mwenyewe badala ya wanadamu wote." Shetani akatoa dau ifuatayo: "Kwa kuwa Wewe ni Mungu Mwenye upendo na Mwenye huruma, lazima Umpende mwanadamu kwa kiwango cha juu zaidi: Lazima Ujitoe Mwenyewe msalabani." Yesu akasema, "Maadamu ni kwa ajili ya wanadamu, basi Niko tayari kutoa Yangu yote." Baadaye, Alikwenda msalabani bila kujifikiria hata kidogo, na kuwakomboa wanadamu wote. Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu, ambalo lina maana kuwa Mungu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu, na ya kwamba Alikuwa Mungu wa rehema na wa upendo. Mungu Alikuwa na mwanadamu. Upendo wake, huruma yake, na wokovu wake uliandamana na kila mtu. Mwanadamu angeweza tu kupata amani na furaha, kupokea baraka zake, kupokea neema yake kubwa na nyingi, na kupokea wokovu wake iwapo mwanadamu angekubali jina lake na akubali uwepo wake. Kupitia kusulubiwa kwa Yesu, wale wote ambao walimfuata Yeye walipokea wokovu na walisamehewa dhambi zao. Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu. Kwa maneno mengine, kazi ya Enzi ya Neema ilifanywa hasa katika Jina la Yesu. Wakati wa Enzi ya Neema, Mungu Aliitwa Yesu. Yeye Alifanya kazi mpya zaidi ya Agano la Kale, na kazi yake ilimalizika kwa kusulubiwa, na ya kwamba huo ulikuwa ukamilifu wa kazi yake.
kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili

Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni