Jumapili, 3 Juni 2018

Yule Anayeshikilia Ukuu // Juu ya Kila Kitu | Mungu Akitoa Sheria

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yehova,

Yule Anayeshikilia Ukuu // Juu ya Kila Kitu | Mungu Akitoa Sheria
Amri na sheria ambazo Yehova Mungu aliwapa Waisraeli hazijakuwa na athari kubwa sana kwa sheria ya binadamu tu, lakini pia zimetekeleza jukumu muhimu katika kuanzishwa na utengenezwaji wa ustaarabu wa kimaadili na taasisi za kidemokrasia katika jamii za binadamu.

"Kwenye Enzi ya Sheria, Yehova Aliweza kuweka wazi sheria nyingi kwa Musa kupitisha kwa wana wa Israeli waliomfuata kutoka Misri. Yehova Aliwakabidhi sheria hizi wana wa Israeli ambazo hazikuwa na uhusiano wowote na Wamisri, na zilinuiwa kuwazuia wana wa Israeli, na ndiyo yaliyokuwa mahitaji Yake kwao. Kama mtu alitii sheria ya Sabato, kama mtu aliheshimu wazazi wake, kama mtu aliabudu miungu na kadhalika, hizi ndizo zilizokuwa kanuni ambazo mtu alihukumiwa na kujulikana kama mwenye dhambi au mwenye haki. Kama mtu alichomwa na moto wa Yehova, au kupigwa na mawe hadi kufa, au kupokea baraka za Yehova, vyote hivi viliamuliwa kulingana na kama mtu alitii sheria hizi. Wale ambao hawakutilia maanani Sabato wangepigwa mawe hadi kufa. Wale makuhani ambao hawakutilia maanani Sabato wangeteketezwa na moto wa Yehova. Wale ambao hawakuheshimu wazazi wao wangepigwa mawe pia hadi kufa. Haya yote yalishauriwa na Yehova. Yehova Alianzisha sheria Zake na taratibu ili huku Akiyaongoza maisha yao, watu wangeweza kumsikiliza na kuheshimu neno Lake na wala si kuasi neno Lake. Alitumia sheria hizi kuweza kudhibiti kizazi kipya cha binadamu kilichozaliwa, kuweka msingi wa kazi Yake ambayo ingefuata. Na kwa hivyo, sababu ya kazi ambayo Yehova Alifanya, enzi ya kwanza iliitwa Enzi ya Sheria." kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili


"Umuhimu, kusudio, na hatua ya kazi ya Yehova nchini Israeli vyote vilikuwa vya kuanzisha kazi Yake katika ulimwengu mzima, na taratibu kuieneza kwenye nchi za Mataifa kutoka kwenye kitovu chake cha Israeli. Hii ndiyo kanuni ambayo Alitumia katika kufanya kazi kotekote ulimwenguni—kuanzisha mfano, kisha kuupanua mpaka watu wote ulimwenguni waweze kukubali injili Yake." 
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili


Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni