Ijumaa, 13 Julai 2018

Ni tofauti gani halisi zilizopo kati ya Mungu mwenye mwili na watu wanaotumiwa na Mungu❓

📜"Mimi nawabatiza na maji ili mtubu. Lakini yule ajaye baada ya mimi ni mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye sistahili kuvichukua viatu vyake. Atawabatiza na Roho Mtakatifu, na moto" (Mathayo 3:11).
📚"Na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe. … … Yote yanayomuasi Mungu yanatoka kwa Shetani; Shetani ni chanzo cha ubaya na uovu wote. Sababu kwamba mwanadamu anayo sifa sawa na ile ya Shetani ni kwa sababu mwanadamu amelagaiwa na kufinyangwa Shetani. Kristo hajawahi kupotoshwa na Shetani, hivyo Anazo tu tabia za Mungu na hakuna hata moja ya Shetani." kutoka kwa "Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni"
"Tangu mwanzo, wanadamu ambao Mungu Ametumia wote wana mawazo ya kawaida na fikra. Wao wote wanajua jinsi ya kujiendesha na kushughulikia mambo ya maisha. Wanashikilia itikadi za kawaida za binadamu na kuwa na vitu vyote ambavyo wanadamu wa kawaida wanapaswa kuwa navyo. Wengi wao wana vipaji vya pekee na werevu wa kiasili. Kwa kufanya kazi kupitia wanadamu hawa, Roho wa Mungu Anakusanya na kutumia vipaji vyao, ambavyo ni zawadi yao Aliyowapa Mungu. Ni Roho wa Mungu Ndiye Anayeleta vipaji vyao katika kazi, na kuwasababisha kutumia uwezo wao kumhudumia Mungu. Hata hivyo, kiini cha Mungu hakina itikadi na hakina fikira. Hakiungani na mawazo ya binadamu na hata kinakosa vitu ambavyo binadamu wa kawaida huwa navyo. Yaani, Mungu hata haelewi kanuni za maadili ya binadamu. Hivi ndivyo ilivyo Mungu wa leo Anapokuja duniani. Yeye Anafanya kazi na Anaongea bila kuhusisha mawazo ya binadamu au fikra za binadamu, lakini kwa wazi Anafichua nia asili za Roho na moja kwa moja Anafanya kazi kwa niaba ya Mungu. Hii ina maana Roho huja kufanya kazi, ambayo Haweki ndani mawazo ya mwanadamu hata kidogo. Yaani, Mungu katika mwili Anajumuisha Uungu moja kwa moja, Hana mawazo ya binadamu au itikadi, na Haelewi kanuni za maadili ya binadamu. Kama kungekuwa na kazi ya Uungu tu (kumaanisha iwapo ingekuwa Mungu mwenyewe pekee ndiye Anayefanya kazi hiyo), kazi ya Mungu haingeweza kufanyika duniani. Kwa hivyo Mungu Anapokuja duniani, lazima Awe na wanadamu wachache Anaowatumia kufanya kazi katika ubinadamu pamoja na kazi Yake katika Uungu. Kwa maneno mengine, Yeye Anatumia kazi ya mwanadamu ili kusaidia kazi Yake takatifu. La sivyo, mwanadamu hangeweza kuja katika mawasiliano ya moja kwa moja na kazi ya Mungu." kutoka kwa "Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni