Sura ya 46. Ni Kwa Kuujua Uweza wa Mungu Pekee Ndipo Unaweza Kuwa na Imani ya Kweli
Wengi wa watu hawaelewi kazi ya Mungu na si rahisi kuelewa kipengele hiki. Kitu cha kwanza ambacho lazima ujue ni kwamba kunawakati ulioteuliwa wa kazi yote ya Mungu na bila shaka si kama ilivyodhaniwa na watu. Mwanadamu hawezi kamwe kuelewa kazi ambayo Mungu ataifanya ama wakati Ataifanya.
Anafanya sasa kile kinachostahili kufanywa sasa na hiki ni kitu ambacho hakuna anayeweza kukiharibu; Anafanya baadaye kile kinachostahili kufanywa baadaye, na hachelewi hata kwa sekunde moja, na hakuna anayeweza kuharibu jambo hilo pia. Kanuni ya kazi Yake ni kwamba inafanywa kulingana na mipango Yake, wakati huo pia ikifanywa kulingana na mapenzi Yake. Hili ni jambo ambalo hakuna anayeweza kulibadilisha, na utaiona tabia ya Mungu atika jambo hilo. Iwapo unafikiri hujafikia kiwango hicho bado, na kwamba Mungu anapaswa kuendelea kukusubiri, basi hilo haliwezekani. Kazi ambayo lazima ifanywe wakati fulani lazima ifanywe wakati huo. Mnaweza kuona kwamba kazi imefanywa kwa njia hii kwa miaka hii mingi. Maneno gani yanapaswa kuzungumzwa, jinsi mwanadamu anapaswa kupewa, ni kazi ipi inapaswa kufanywa wakati upi—ni nani awezaye kuharibu lolote la haya? Wakati kuenezwa kwa injili kulianza na vitabu vilikuwa vikipitishwa kila mahali, kunao wale ambao wangechoma vitabu hivi, wale ambao wangewakomesha watu wasivisome, wale ambao wangekashifu, wale ambao wangewasaka waumini na kutoa ripoti kwa maadui na kulikuwa na wale ambao wangewatafuta na kuwakandamiza. Kila mahali kulikuwa na upinzani mkali lakini, mwishowe, tukio la kuvutia la kazi ya injili bado halikuonekana? Bado hakukuwa na watu wengi waliopatwa kila mahali? Ni nani labda angeweza kuuharibu mpango wa Mungu? Wale ambao wanapaswa kupatwa bila shaka lazima wapatwe, na wale ambao hawapaswi kupatwa lakini wameingia ndani lazima wafukuzwe. Huu ni ukweli usioweza kuharibika. Kama tu inavyosemwa, “Moyo wa mfalme uko katika mikono ya BWANA, kama mito ya maji: anaigeuza mahali ataigeuza”; sembuse wasio na maana? Hatua gani ya kazi inapaswa kufanywa wakati upi yote yako katika mpango wa Mungu. Si kama wanavyodhani watu, kwamba kazi itasimamishwa wakati mazingira mabaya yataibuka, na si kama wanavyoamini, kwamba kwa kufanya hivi au vile, mwanadamu anaweza kuuharibu mpango wa Mungu wa usimamizi. Hizo ni fikira za watu tu. Hata ingawa unajaribu kwa bidii zaidi kuharibu na kubughudhi kazi ya Mungu, haina haja. Kazi ya Roho Mtakatifu inaamua kila kitu. Bila kazi ya Roho Mtakatifu, mtu hawezi kutimiza lolote. Wakati mwingine watu ni wajinga na wanaendelea kutembea mbele, lakini iwapo Roho Mtakatifu hatendi, basi bado hawatimizi lolote. Kuhusu kipengele hiki, watu wanapaswa kuwa na mantiki ya aina gani? Inapogunduliwa kwamba Roho Mtakatifu hayupo kazini, basi kazi ya sasa inapaswa kupangwa na wanapaswa kusubiri na kutafuta nia za Mungu—hili pekee ndilo chaguo la busara kufanya. Mwanadamu lazima afanye kile anachopaswa kufanya na mwanadamu lazima afanye iwezekanavyo kuutekeleza wajibu wake. Huwezi kuogopa kufanya vitu vibaya na kisha usubiri kwa kukaa tu, sembuse kusema “Mungu bado hajatenda. Mungu bado hajaniambia nifanye chochote, kwa hivyo sitafanya chochote bado.” Si jambo hili ni wewe kuupoteza wajibu wako? Hiki ni kitu ambacho lazima ukione wazi, kwani si suala la upuuzi.
Hatua zote za kazi katika mpango wa usimamizi wa Mungu zinafanywa kulingana na ratiba na kwa wakati. Bila shaka si kulingana na mawazo yako: “Aa, Hapaswi kufanya jambo hili! Hapaswi kufanya jambo hilo! Hivi si vyema!” Mungu ni mwenyezi. Hakuna kitu chochote ambacho Mungu hukiona kuwa ngumu kukifanya. Mwanadamu anaweza kufanya nini? Mwanadamu hawezi tu kutenda ukweli, lakini pia ni mwenye kiburi na wa kujiona; anafikiri kwamba anaweza kufanya lolote, na moyo wake umejawa na matamanio ya kupita kiasi. Tena kuna wale wanaoamini kwamba siku ya Mungu itakuja punde, kwamba hawahitaji kustahimili mateso tena, kwamba wanaweza kufurahia siku za furaha na kwamba matumaini yao hatimaye yatatimizwa. Nawaambieni: Watu wa aina hii wako tu, wanacheza huku na kule na wanaweza tu kuadhibiwa mwishowe, wasipate chochote. Unaweza kupata nini iwapo imani yako ni ya siku ya Mungu kuja na ya wewe kutoroka kutoka kwa maafa makuu? Wale wanaoamini zaidi kwa ajili ya siku ya Mungu kuja lazima wataangamia zaidi. Wale wanaoamini ili kutafuta ukweli, kubadili tabia yao na kuokolewa watabaki—hii ni imani ya kweli. Wale walio na imani iliyochanganyika hawatapata chochote mwishowe lakini watakuwa tu wamefanya juhudi isiyo na manufaa, na zaidi lazima wateseke adhabu kali zaidi. Watu wana umaizi hafifu. Iwapo unamwamini Mungu lakini hujishughulishi katika wajibu wako wa kufaa, lakini badala yake daima unafikiri njia mbovu zisizo aminifu, basi unajiumiza tu. Watu hao wa dunia wasiomwamini Mungu—hawako pia katika mikono ya Mungu? Ni nani awezaye kutoroka mikono ya Mungu? Hakuna yeyote! Wale wanaotoroka lazima mwishowe warudi mbele za Mungu kuteseka adhabu. Hili ni dhahiri; watu bado hawawezi kuliona?
Kuna baadhi ambao, ingawa wanamwamini Mungu Mwenyezi, hawana ufahamu hata kidogo wa uweza wa Mungu. Kila mara wamechanganyikiwa, wakifikiri: “Mungu ni mwenyezi, Anayo mamlaka na Anaweza kutawala yote, kwa hivyo mbona bado Alimuumba Shetani na kumruhusu kumpotosha mwanadamu kwa miaka elfu sita? Kwa nini kumruhusu Shetani kugeuza dunia kuwa ukungu mbaya wa vurumai na machafuko? Mbona Shetani asiangamizwe? Mwanadamu angekuwa sawa iwapo Shetani angeangamizwa?” Sasa mnaweza kuelezea swali hili? Hili linahusiana na maono. Wengi wamelifikiria swali hili, lakini sasa mmefanya matayarisho kidogo ya kazi na hivyo hakuna shaka yoyote kuhusu Mungu inaweza kuibuka ndani yenu kwa sababu ya suala hili. Lakini lazima mtatue matatizo madogo katika shida hii—hamna budi ila kufanya hivyo. Tena kuna baadhi wanaouliza: “Mbona Mungu humruhusu Shetani kuasi dhidi Yake? Kwa malaika mkuu kuwa na uwezo wa kuasi dhidi ya Mungu—je, Mungu hakujua? Je, ilikuwa kwamba Mungu alishindwa kumdhibiti ama kwamba Mungu alimruhusu, ama Mungu alikuwa na madhumuni mengine? “Ni kawaida kwa watu kuibua swali hili, na wanapaswa kujua kwamba swali hili linahusu mpango mzima wa usimamizi wa Mungu. Mungu alipanga kuwe na malaika mkuu na uasi huu wa malaika mkuu dhidi ya Mungu uliruhusiwa na Mungu na pia kupangwa na Yeye—bila shaka jambo hili liko katika wigo wa mpango wa Mungu wa usimamizi. Mungu alimruhusu malaika mkuu kuwapotosha binadamu ambao Alikuwa Amewaumba, baada ya Shetani kuasi dhidi Yake. Si kwamba Mungu alishindwa kumdhibiti Shetani, ili kwamba binadamu alishawishiwa na nyoka na kupotoshwa na Shetani, lakini kwamba ilikuwa Mungu aliyemruhusu Shetani kufanya hivi. Ni baada tu ya Yeye kutoa ruhusa Yake kwa haya kufanyika ndipo Mungu alianza mpango Wake wa usimamizi na kazi Yake. Je, mwanadamu anaweza kuelewa siri iliyo hapa? Punde tu binadamu alipokuwa amepotoshwa na Shetani, Mungu basi Alianza kazi Yake ya kuwasimamia binadamu. Kwanza, Alifanya kazi ya Enzi ya Sheria katika Israeli. Baada ya miaka elfu mbili kupita, Aliitekeleza kazi ya ukombozi wa msalaba katika Enzi ya Neema, na wanadamu wote walikombolewa. Wakati wa siku za mwisho, Anapata mwili na Ameshinda na kuokoa kundi hili la watu katika siku za mwisho. Watu ambao wamezaliwa siku za mwisho ni watu wa aina gani? Ni wale ambao wamepitia upotovu wa Shetani kwa elfu nyingi za miaka, ambao walikuwa wamepotoshwa kwa kina ambacho hawaonekani kama binadamu tena, ambao hatimaye wamepitia hukumu, kuadibiwa na kufichuliwa kwa neno la Mungu, ambao wameshindwa na ambao kisha wamepata ukweli kutoka ndani ya maneno ya Mungu; ni wale ambao wameshawishiwa kwa dhati na Mungu, ambao wamefikia uelewa wa Mungu, ambao wanaweza kutii Mungu kikamilifu na kuyakidhi mapenzi Yake. Mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi ni kupata kundi la watu kama hawa. Wewe Niambie, ni wale ambao hawajapitia upotovu wa Shetani ambao wanaweza kuyakidhi mapenzi ya Mungu? Ama ni wale ambao wataokolewa mwishowe ambao wanaweza kuyakidhi mapenzi ya Mungu? Wale miongoni mwa wanadamu ambao watapatwa kupitia mpango mzima wa usimamizi ni kundi linaloweza kuelewa mapenzi ya Mungu, wanaoupata ukweli kutoka kwa Mungu, wanaomiliki maisha na kufanana na mwanadamu ambayo Mungu anahitaji. Mwanadamu alipoumbwa kwanza, alionekana tu kama binadamu na alikuwa na uhai. Lakini hakufanana na binadamu ndani yake ambako Mungu alihitaji ama alimtumania kufikia. Kundi la watu ambao watapatwa mwishowe ni wale ambao watabaki mwishowe, na kundi hilo ni wale ambao Mungu anawahitaji pia, ambao Anawapenda na ambao Amefurahishwa nao. Katika mpango wa usimamizi wa miaka elfu kadhaa, hawa watu wamepata zaidi, ambayo yametokana na kunyunyiziwa na Mungu na yamepewa mwanadamu kwa njia ya vita Vyake na Shetani. Watu katika kundi hili ni bora kuliko wale ambao Mungu aliwaumba mwanzoni kabisa; hata ingawa wamepitia upotovu, hili haliwezi kuepukika, na ni suala ambalo liko katika wigo wa mpango wa Mungu wa usimamizi ambao unafichua uweza Wake na hekima Yake vya kutosha na zaidi, ukifichua pia kwamba yote ambayo Mungu amepanga, kunuia na kutimiza ni kubwa zaidi. Ukiulizwa tena badaye: “Iwapo Mungu ni mwenyezi, ni jinsi gani malaika mkuu angeasi dhidi Yake? Kisha Mungu akamrusha chini duniani ambapo alimpotosha binadamu. Ni nini umuhimu wa haya?” unaweza kusema hivi: “Suala hili liko katika wigo ulioamuliwa kabla na Mungu nalo ni la umuhimu mkubwa zaidi. Mwanadamu hawezi kulielewa kabisa, lakini kutoka kwa kiwango ambacho mwanadamu anaweza kuelewa na kulifikia, inaweza kuonekana kwamba Mungu anafanya kazi hadi kiwango kikubwa cha umuhimu.” Hii si kusema hasa kwamba Mungu anateleza kwa muda, ama kwamba Anapoteza udhibiti naye hana namna yoyote ya kusimamia vitu, na kisha Anazigeuza hila za Shetani dhidi yake; si kwamba Anafikiri kwamba malaika mkuu ameasi hata hivyo kwa hivyo afadhali amwache aendele, naye Anapanga kumwokoa wanadamu baada ya kumruhusu Shetani kuwapotosha wote. Hivi sivyo hata kidogo. Watu angalau wanapaswa kujua kwamba suala hili liko katika wigo wa mpango wa Mungu wa usimamizi. Mpango upi? Katika hatua ya kwanza, kulikuwa na malaika mkuu; katika hatua ya pili, malaika mkuu aliasi, katika hatua ya tatu, baada ya malaika mkuu kuasi, alikuja miongoni mwa wanadamu kuwapotosha, na kisha Mungu alianza kazi Yake ya kumsimamia mwanadamu. Wakati watu humwamini Mungu lazima waelewe maono ya mpango wa Mungu wa usimamizi. Wengine hawaelewi kipengele hiki cha ukweli, kamwe wakihisi siku zote kwamba kuna ukinzani mwingi usioweza kutatuliwa. Bila uelewa wanahisi kutokuwa na imani na, kwa sababu ya kuhisi kutokuwa na imani, hawawezi kusonga. Ni vigumu, bila shaka, kuwashughulikia watu. Kwa sababu sasa tumeshiriki, sasa unaelewa hili, sivyo? Kwanza kulikuwa na malaika mkuu, kisha Mungu alikuwa na mpango Wake, akipiga hesabu ni lini angeanza kuasi dhidi Yake na kupitia matukio yapi angeanza kuasi polepole—yote yalikuwa ni mchakato. Bila shaka haiwezi kuwa rahisi inavyoonekana kama imeandikwa kwenye ukurasa. Kama tu wakati Yuda alimsaliti Yesu, haikuwezekana yeye kufanya jambo hili ghafla. Kwa kumfuata Yesu kwa muda mrefu, bila shaka lazima alikuwa ametenda kwa njia fulani. Kisha Shetani akaanza kazi akitoa fikira zake, kisha Yuda akafanya baadhi ya mambo mengine, na akawa mbaya polepole. Kupitia mazingira yake—na muda ulipowadia—alianza kumsaliti Yesu. Mwanadamu kugeuka kuwa mbaya pia kunapitia mchakato wa kawaida na kufuata sheria ya kawaida; hakuwezi kuwa rahisi kama wanavyodhania watu. Unaweza kuelewa tu suala la mpango wa Mungu wa usimamizi hadi kiwango hiki. Baada ya wewe kupata kimo kikubwa zaidi, utakuja kutambua umuhimu wake wa kina zaidi.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni