Jumamosi, 8 Septemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 3 Lazima Mjue Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

3. Kujua Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu.

Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Umuhimu, kusudio, na hatua ya kazi ya Yehova nchini Israeli vyote vilikuwa vya kuanzisha kazi Yake katika ulimwengu mzima, na taratibu kuieneza kwenye nchi za Mataifa kutoka kwenye kitovu chake cha Israeli. Hii ndiyo kanuni ambayo Alitumia katika kufanya kazi kotekote ulimwenguni—kuanzisha mfano, kisha kuupanua mpaka watu wote ulimwenguni waweze kukubali injili Yake. Waisraeli wa kwanza walikuwa kizazi cha Nuhu. Watu hao walikuwa tu na pumzi za Yehova, na waliweza kujitunza wakatilia maanani mahitaji ya kimsingi ya maisha, lakini hawakujua Yehova Alikuwa Mungu aina gani, wala hawakujua mapenzi Yake kwa binadamu, na hata namna ambavyo walitakikana kumstahi Bwana wa viumbe vyote. Vizazi vya Adamu havikujua ni taratibu na sheria gani ambazo lazima wangetii, au ni kazi gani ambayo viumbe lazima wafanyie Muumba. Kile walichojua tu kilikuwa kwamba mume lazima atoke jasho na atie bidii ili kutosheleza familia yake, na kwamba mke lazima amtii mume wake na kuendeleza kizazi cha binadamu ambacho Yehova Aliumba. Kwa maneno mengine, watu hawa walikuwa tu na pumzi za Yehova na maisha Yake, lakini hawakujua namna ya kufuata sheria za Mungu au namna ya kutosheleza Bwana wa viumbe vyote. Walielewa kidogo sana. Kwa hivyo ingawaje hakukuweko na chochote kisichostahili au chenye ujanja katika mioyo yao, na ingawaje ilikuwa nadra sana kwao kuwa na wivu au hata ugomvi, hawakujua wala kuelewa Yehova, Bwana wa viumbe vyote. Vizazi hivi vya binadamu vilijua tu kula kile ambacho Yehova Alikuwa Ameunda, kufurahia kile ambacho Yehova Alikuwa ameunda, lakini hawakujua kustahi Yehova; hawakujua kile ambacho kilistahili kufanywa ili kumwabudu Yeye huku wakiwa wamepiga magoti. Wangeitwaje viumbe Wake? Kama hali ingekuwa hivyo, je, maneno "Yehova ni Bwana wa viumbe vyote" na "Alimwumba binadamu ili mwanadamu aweze kumdhihirisha, kumtukuza na kumwakilisha"—je, hayangekuwa yamesemwa bure bilashi? Watu wasiomstahi Yehova wangewezaje kuwa ushuhuda kwa utukufu Wake? Wangewezaje kuwa dhihirisho la utukufu Wake? Je, maneno ya Yehova "Nilimwumba binadamu kwa mfano Wangu" yakawa silaha kwenye mikono ya Shetani—yule mwovu? Je, haya Maneno hayangekuwa basi alama ya udhalilishaji kwa uumbaji wa binadamu na Yehova? Ili kukamilisha awamu hiyo ya kazi, Yehova, baada ya kumwumba mwanadamu, hakumwelekeza wala kumwongoza kuanzia kwa Adamu hadi Nuhu. Haukuwa mpaka wakati wa mafuriko ndipo Alianza rasmi kuwaongoza Waisraeli waliokuwa vizazi vya Adamu na Nuhu. Kazi na maneno Yake nchini Israeli vyote viliongoza watu wote wa Israeli walipokuwa wakiishi maisha yao kotekote nchini Israeli, na kwa njia hii kuonyesha binadamu kwamba Yehova hakuweza tu kutia pumzi ndani ya binadamu, ili apate maisha kutoka Kwake, na ainuke kutoka kwenye vumbi na kuwa mwanadamu aliyeumbwa, lakini pia aliweza kumteketeza mwanadamu kwa moto, na kumlaani mwanadamu kwa kutumia kiboko Chake ili kutawala mwanadamu. Kwa hivyo, wao pia, waliweza kuona kwamba Yehova angeweza kuyaongoza maisha ya binadamu ulimwenguni na kuongea na kufanya kazi miongoni mwao kulingana na saa za mchana na za usiku. Alifanya tu kazi hiyo ili viumbe Vyake viweze kujua kwamba binadamu alitoka kwenye vumbi na akachukuliwa na Yeye, kwamba binadamu aliumbwa na Yeye. Aidha, kazi Aliyoianza Israeli ilikuwepo ili watu wengine na mataifa mengine (ambao kwa hakika hawakuwa kando na wale wa Israeli, lakini walikuwa wamejitenga na wana wa Israeli, ilhali bado walikuwa kizazi cha Adamu na Hawa) waweze kupokea injili ya Yehova kutoka Israeli, ili viumbe vyote ulimwenguni vingemstahi na kumchukulia kuwa mkuu. Kama Yehova Asingekuwa Ameanza kazi yake Israeli, lakini badala yake baada ya kumwumba mwanadamu, na kumwacha kuishi vivyo hivyo tu hapa ulimwenguni, basi kwa sababu ya asili ya kimaumbile ya binadamu (asili inamaanisha kwamba binadamu hawezi kujua yale mambo ambayo hayaoni, yaani, hajui kwamba Yehova Alimwumba mwanadamu, na vilevile hata hajui kwa nini Alifanya hivyo), asingewahi kujua kwamba Yehova Alimwumba mwanadamu na kwamba ndiye Bwana wa mambo yote. Kama Yehova Angemwumba mwanadamu na kumweka ulimwenguni kwa raha Zake, kisha kuikung’uta tu mikono Yake na kuondoka badala ya kumwongoza miongoni mwa wenzake kwa kipindi cha muda, basi kizazi chote cha binadamu kingerudi katika hali ya kutokuwa na maana; hata mbingu na ardhi na vitu vyote vilivyoumbwa na Yeye, wakiwemo binadamu wote, vingerudi na kuwa katika hali isiyokuwa na maana na kutupiliwa mbali na kukanyagwa na Shetani. Na kwa hivyo, mapenzi ya Yehova kwamba "Ulimwenguni, yaani, miongoni mwa viumbe Vyake, Anafaa kuwa na mahali pa kusimama, mahali patakatifu miongoni mwa viumbe Vyake" yasingetimia. Kwa hiyo badala yake, baada ya Mungu kuumba wanadamu Aliwaongoza katika maisha yao na kuwazungumzia, wote ili waweze kutambua matamanio yake, kufikia mpango Wake. Kazi ya Mungu nchini Israeli ilinuiwa kutekeleza kazi Aliyokuwa Ameiweka wazi mbele ya viumbe Vyake vyote, na kwa hivyo Yeye kufanya kazi kwanza miongoni mwa Waisraeli na viumbe Wake kati ya vitu vyote havikuwa katika mgongano, lakini vyote hivi vilikuwa kwa minajili ya usimamizi Wake, kazi Yake na utukufu Wake, na kuzidisha maana ya kuumba Kwake wanadamu. Aliyaongoza maisha ya wanadamu ulimwenguni kwa miaka elfu mbili baada ya Nuhu ambapo Aliwafunza namna ya kustahi Yehova Bwana wa vitu vyote, Akawafunza namna ya kujiendeleza na kuisha maisha yao, na muhimu kuliko vyote, namna ya kuwa shahidi wa Yehova, kumtii Yeye na kumstahi Yeye, na kumsifu Yeye kwa muziki kama Daudi na kuhani wake walivyofanya.
Kabla ya miaka hiyo elfu mbili ambayo Yehova Alifanya kazi Yake, binadamu hakujua chochote na karibu wanadamu wote walizoroteka na kugeuka kuwa uasherati na upotovu vyote ambavyo vilitangulia mafuriko; mioyo yao haikuwa na nafasi yoyote ya Yehova, wala hata njia Yake. Hawakuwahi kuelewa kazi ambayo Yehova Alikuwa Akienda kufanya; walikosa akili, na hata maarifa, kama vile mitambo inayoishi na kupumua, kutojua binadamu, Mungu, ulimwengu, na maisha vilevile. Ulimwenguni walijihusisha na kupotoka kwingi kama alivyofanya yule nyoka, na kusema mambo mengi ambayo yalimchukiza Yehova, lakini kwa sababu hawakujua lolote, Yehova hakuwaadibu wala kuwafundisha nidhamu. Baada ya mafuriko wakati Nuhu alikuwa na umri wa miaka 601, Yehova Alijionyesha rasmi kwa Nuhu na Akamwongoza yeye na familia yake, Akamwongoza yeye, ndege, na wanyama walionusurika mafuriko na vizazi vyake mpaka mwisho wa Enzi ya Sheria, jumla ya miaka 2,500. Alikuwa rasmi kazini nchini Israeli kwa miaka 2,000, na kipindi ambacho Alikuwa kazini nchini Israeli na nje ya Israeli kilikuwa miaka 500, kwa hivyo kwa pamoja ni miaka 2,500. Kwenye kipindi hiki Aliwaagiza Waisraeli kwamba ili kuweza kumhudumia Yehova, wanafaa kujenga hekalu na kuvalia majoho ya kikuhani, kutembea bila viatu kwenye hekalu wakati wa mapambazuko, na kama wasingefanya hivyo viatu vyao vingechafua hekalu na moto ungetumwa chini kwao kutoka paa la hekalu na kuwateketeza hadi kifo. Walitekeleza wajibu wao na kutii mipango ya Yehova. Walimwomba Yehova hekaluni, na baada ya huhamasishwa na Yehova, yaani baada ya Yehova kuongea, waliwaongoza watu na kuwafunza kwamba wanafaa kumstahi Yehova—Mungu wao. Na Yehova Aliwafunza kwamba wanafaa kulijenga hekalu na madhabahu, na kwa wakati uliotengwa na Yehova, yaani, kwenye msimu wa Pasaka, wanafaa kutayarisha ndama na wanakondoo wachanga kwenye madhabahu kama dhabihu ili kuhudumia Yehova ili kuwazuia wao na kuweza kumstahi Yehova katika mioyo yao. Kama wangetii sheria hii ndicho kingekuwa kipimo cha uaminifu wao kwa Yehova. Yehova pia Aliwatengea siku ya Sabato, siku ya saba ya kuumba Kwake. Siku moja baada ya hiyo, Alifanya siku ya kwanza, siku ya wao kusifu Yehova, kumpa Yehova dhabihu na kumchezea muziki Yehova. Kwenye siku hii, Yehova Aliwaita makuhani wote kugawanya dhabihu hizo kwenye madhabahu ili watu waweze kula na kufurahia kafara zilizotolewa kwa Yehova. Naye Yehova Akasema kwamba walikuwa wamebarikiwa na walikuwa na sehemu Yake, na kwamba walikuwa ndio watu Wake waliochaguliwa (ambalo ndilo lililokuwa agano la Yehova na wana wa Israeli) Na ndiyo maana, mpaka siku hii watu wa Israeli wangali wanasema kwamba Yehova ndiye Mungu wao pekee na wala si Mungu wa watu wengine.
Kwenye Enzi ya Sheria, Yehova Aliweza kuweka wazi sheria nyingi kwa Musa kupitisha kwa wana wa Israeli waliomfuata kutoka Misri. Yehova Aliwakabidhi sheria hizi wana wa Israeli ambazo hazikuwa na uhusiano wowote na Wamisri, na zilinuiwa kuwazuia wana wa Israeli, na ndiyo yaliyokuwa mahitaji Yake kwao. Kama mtu alitii sheria ya Sabato, kama mtu aliheshimu wazazi wake, kama mtu aliabudu miungu na kadhalika, hizi ndizo zilizokuwa kanuni ambazo mtu alihukumiwa na kujulikana kama mwenye dhambi au mwenye haki. Kama mtu alichomwa na moto wa Yehova, au kupigwa na mawe hadi kufa, au kupokea baraka za Yehova, vyote hivi viliamuliwa kulingana na kama mtu alitii sheria hizi. Wale ambao hawakutilia maanani Sabato wangepigwa mawe hadi kufa. Wale makuhani ambao hawakutilia maanani Sabato wangeteketezwa na moto wa Yehova. Wale ambao hawakuheshimu wazazi wao wangepigwa mawe pia hadi kufa. Haya yote yalishauriwa na Yehova. Yehova Alianzisha sheria Zake na taratibu ili huku Akiyaongoza maisha yao, watu wangeweza kumsikiliza na kuheshimu neno Lake na wala si kuasi neno Lake. Alitumia sheria hizi kuweza kudhibiti kizazi kipya cha binadamu kilichozaliwa, kuweka msingi wa kazi Yake ambayo ingefuata. Na kwa hivyo, sababu ya kazi ambayo Yehova Alifanya, enzi ya kwanza iliitwa Enzi ya Sheria. Ingawaje Yehova Aliongea sana na Alifanya kazi nyingi, Aliwaongoza tu kwa njia nzuri huku Akiwafunza watu hawa wasiojua namna ya kuwa na wema, namna ya kuishi, namna ya kuelewa njia ya Yehova. Katika sehemu kubwa ya kazi Yake kwa hakika Alinuia kuruhusu watu Wake kufuatilia njia Yake na kufuata sheria Yake. Kazi ilifanyiwa watu ambao walikuwa wamepotoka kidogo; haikujali sana mageuzi ya tabia au ukuzi wa maisha. Alijali tu matumizi ya sheria ya kuzuia na kudhibiti watu. Kwa wana wa Israeli wakati huo, Yehova Alikuwa tu Mungu kwenye hekalu, Mungu kwenye mbingu. Alikuwa mnara wa wingu, mnara wa moto. Kile ambacho Yehova Aliwahitaji kufanya kilikuwa ni kutii kile ambacho watu wanajua leo kama sheria na mafundisho Yake—mtu angeweza hata kusema taratibu—kwa sababu kazi ya Yehova haikunuiwa kuwabadilisha, lakini kuwapatia vitu vingi ambavyo binadamu anastahili kuwa navyo, kuwaambia kutoka kwenye kinywa Chake mwenyewe, kwa sababu baada ya binadamu kuumbwa, binadamu hakujua chochote kuhusu kile alichostahili kumiliki. Na kwa hivyo Yehova Aliwapatia vitu walivyostahili kumiliki katika maisha yao hapa ulimwenguni, Akawafanya watu Aliokuwa Amewaongoza kuzidi vizazi vyao, Adamu na Hawa, kwa sababu kile Yehova Alichowapatia kilizidi kile Alichokuwa Amepatia Adamu na Hawa hapo mwanzo. Licha ya hayo yote, kazi ambayo Yehova Alifanya Israeli ilikuwa tu kuongoza binadamu na kuwafanya kutambua Mungu wao. Hakuwashinda wala kuwabadilisha, Aliwaongoza tu. Hii ndiyo jumla ya kazi ya Yehova kwenye Enzi ya Sheria. Ndiyo maelezo ya ziada, hadithi ya kweli, kiini cha kazi Yake kwenye nchi nzima ya Israeli na mwanzo wa kazi Yake ya miaka elfu sita—katika kudhibiti mwanadamu kwa mkono wa Yehova. Kutokana na haya yote kazi nyingi zaidi ilijitokeza kwenye mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita.
kutoka kwa "Kazi Katika Enzi ya Sheria" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika Enzi ya Neema mwanadamu alikuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo kazi ya ukombozi wa wanadamu wote ulihitaji wingi wa neema, ustahimili usio na mwisho na uvumilivu, na hata zaidi, sadaka ya kutosha kulipia dhambi za wanadamu, ili kufikia athari yake. Kile wanadamu waliona katika Enzi ya Neema kilikuwa tu sadaka Yangu ya dhambi ya binadamu, Yesu. Na walijua kwamba ni Mungu tu ndiye Anaweza kuwa mwenye huruma na uvumilivu, na waliona tu huruma wa Yesu na fadhili Zake. Hii ni kwa sababu wao waliishi katika Enzi ya Neema. Hivyo kabla ya kukombolewa, walilazimika kufurahia neema nyingi ambayo Yesu aliwapa; hili pekee ndilo ilikuwa ya manufaa kwao. Kwa njia hii, wangeweza kusamehewa dhambi zao kupitia kufurahia kwao neema, na wangeweza kuwa na nafasi ya kukombolewa kupitia kufurahia kwa ustahimili wa Yesu na uvumilivu. Ni kwa njia ya ustahimili wa Yesu na uvumilivu ndio walikuwa na uwezo wa kupokea msamaha na kufurahia wingi wa neema kutoka kwa Yesu-kama vile Yesu alisema, "Nimekuja si kuwakomboa watu watakatifu, ila wenye dhambi, ili dhambi zao zisamehewe." Kama Yesu angekuwa mwili na tabia ya hukumu, laana, na kutovumilia makosa ya mwanadamu, basi mwanadamu kamwe hangeweza kupata nafasi ya kukombolewa, na daima yeye angebaki mwenye dhambi; na hivyo mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita haungeendelea zaidi ya Enzi ya Sheria. Enzi ya Sheria ingeendelea kwa miaka elfu sita, dhambi za mwanadamu zingeongezeka zaidi katika idadi na ziwe mbaya zaidi, na uumbaji wa binadamu ungekuwa wa bure. Wanadamu wangeweza tu kumtumikia Yehova chini ya Sheria, bali dhambi zao zingezidi za wanadamu wa kwanza kuumbwa. Jinsi Yesu alivyompenda mwanadamu zaidi, kusamehe dhambi zao na kuwapa huruma ya kutosha na fadhili, ndivyo wanadamu walizidi kuwa na uwezo wa kuokolewa, na kuitwa wanakondoo waliopotea ambao Yesu Aliwanunua tena kwa thamani kubwa. Shetani hakuweza kuingilia katika kazi hii, kwa sababu Yesu Aliwatunza wafuasi Wake kama mama mwenye upendo anachunga watoto wachanga walio katika mikono yake. Yeye hakuwa na hasira kwao au kuwadharau, bali Alikuwa Amejaa faraja; Yeye kamwe hakuwa na hasira miongoni mwao, lakini alistahimili makosa yao na akageuza jicho la kipofu kwa upumbavu wao na kutofahamu, hata Alisema, "Uwasamehe wengine mara sabini mara saba." Kwa hiyo moyo Wake ulirekebisha mioyo ya wengine, na kwa njia hii ndiyo watu walipokea msamaha kupitia uvumilivu Wake.
kutoka kwa "Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa sababu hiyo ilikuwa enzi tofauti, mara nyingi Alitoa chakula na vinywaji kwa watu ili waweze kula wasiweze tena. Yeye Aliwatendea wafuasi Wake wote kwa ukarimu, kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kufufua wafu. Ili kwamba watu waweze kumwamini na kuona kwamba yote Aliyofanya yalifanyika kwa bidii na kwa dhati, Yeye Alifanya mpaka kiwango cha kufufua maiti iliyooza, kuwaonyesha kwamba mikononi Mwake hata wafu wanaweza kuwa hai tena. Kwa njia hii Alivumilia kwa kimya kati yao na Alifanya kazi Yake ya ukombozi. Hata kabla Asulubiwe msalabani, Yesu Alikuwa tayari Amebeba dhambi za binadamu na kuwa sadaka ya dhambi kwa wanadamu. Alikuwa tayari Amefungua njia ya msalaba ili kumkomboa mwanadamu kabla hajasulubiwa. Mwishowe Aligongwa misumari msalabani, Alijitoa sadaka yeye mwenyewe kwa ajili ya msalaba, na Aliweka huruma Yake yote, fadhili Zake, na utakatifu juu ya mwanadamu.
kutoka kwa "Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi" katika Neno Laonekana katika Mwili
Bila ukombozi wa Yesu, wanadamu wangeishi milele katika dhambi, na kuwa watoto wa dhambi, kizazi cha mapepo. Kama ingeendelea hivyo, Shetani angechukua makazi duniani, na dunia nzima ingekuwa makao yake. Lakini kazi ya ukombozi ilihitaji huruma na fadhili kwa wanadamu; kupitia kwa kazi hiyo tu ndio mwanadamu angeweza kupokea msamaha na mwishowe afuzu kufanywa kuwa mkamilifu na kupatwa kikamilifu. Bila hatua hii ya kazi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita haungeweza kuendelea mbele. Kama Yesu hangesulubiwa, kama Yeye Angewaponya tu watu na kufukuza mapepo, basi watu hawangesamehewa dhambi zao kikamilifu. Miaka mitatu na nusu ambayo Yesu Alifanya kazi Yake hapa duniani ilikamilisha tu nusu ya kazi Yake ya ukombozi; kisha kwa kupigiliwa misumari msalabani na kuwa na mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kukabidhiwa kwa mwovu, Yeye Alikamilisha kazi ya kusulubiwa na Akaanzisha hatima ya mwanadamu. Baada ya Yesu kukabidhiwa mikononi mwa Shetani tu, ndipo mwanadamu alikombolewa. Kwa miaka thelathini na mitatu na nusu Aliteseka duniani, Alidhihakiwa, Akatukanwa, na Akaachwa pweke, Aliachwa hata bila mahali pa kulaza kichwa chake, Hakuwa hata na mahali pa kupumzika; kisha Akasulubiwa, nafsi Yake yote—mwili safi na usio na hatia—kupigiliwa misumari msalabani, na kupitia kila namna ya mateso. Wale waliokuwa madarakani wakamdhihaki na kumcharaza mijeledi, na askari hata wakamtemea mate usoni; ila Alibaki kimya na kuvumilia mpaka mwisho, Akinyenyekea na kujitoa bila masharti mpaka wakati wa kifo, ambapo Yeye Alikomboa binadamu wote. Hapo tu ndipo Aliruhusiwa kupumzika.
kutoka kwa "Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika kazi ya Enzi ya Neema, Yesu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu. Alichokuwa nacho na Aliyekuwa ni neema, upendo, huruma, uvumilivu, subira, unyenyekevu, huduma, na stahamala, na nyingi ya kazi ambayo Alifanya ilikuwa kumwokoa mwanadamu. Na kuhusu tabia Yake, ilikuwa tabia ya huruma na upendo, na kwa sababu Yeye Alikuwa na huruma na upendo, ilikuwa sharti asulubishwe msalabani kwa ajili ya mwanadamu, ili kuonyesha kwamba Mungu Alimpenda mwanadamu jinsi anavyojipenda, kwa kiasi kwamba Yeye mwenyewe Alijitoa kama kafara na kwa ukamilifu Wake. Shetani akasema, "Kwa kuwa Unampenda mwanadamu, Lazima Umpende kwakwa kiwango cha juu zaidi: Lazima Upigiliwe misumari msalabani, kumwokoa mwanadamu kutoka msalabani, kutoka kwa dhambi, na Wewe utajitolea Mwenyewe badala ya wanadamu wote." Shetani akatoa dau ifuatayo: "Kwa kuwa Wewe ni Mungu Mwenye upendo na Mwenye huruma, lazima Umpende mwanadamu kwa kiwango cha juu zaidi: Lazima Ujitoe Mwenyewe msalabani." Yesu akasema, "Maadamu ni kwa ajili ya wanadamu, basi Niko tayari kutoa Yangu yote." Baadaye, Alikwenda msalabani bila kujifikiria hata kidogo, na kuwakomboa wanadamu wote. Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu, ambalo lina maana kuwa Mungu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu, na ya kwamba Alikuwa Mungu wa rehema na wa upendo. Mungu Alikuwa na mwanadamu. Upendo wake, huruma yake, na wokovu wake uliandamana na kila mtu. Mwanadamu angeweza tu kupata amani na furaha, kupokea baraka zake, kupokea neema yake kubwa na nyingi, na kupokea wokovu wake iwapo mwanadamu angekubali jina lake na akubali uwepo wake. Kupitia kusulubiwa kwa Yesu, wale wote ambao walimfuata Yeye walipokea wokovu na walisamehewa dhambi zao. Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu. Kwa maneno mengine, kazi ya Enzi ya Neema ilifanywa hasa katika Jina la Yesu. Wakati wa Enzi ya Neema, Mungu Aliitwa Yesu. Yeye Alifanya kazi mpya zaidi ya Agano la Kale, na kazi yake ilimalizika kwa kusulubiwa, na ya kwamba huo ulikuwa ukamilifu wa kazi yake.
kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa mwanadamu, Mungu kusulubiwa kulihitimisha kazi ya Mungu kupata mwili, Aliwakomboa binadamu wote , na Akamruhusu kuteka ufunguo wa Kuzimu. Kila mtu anadhani kwamba kazi ya Mungu imekamilika kikamilifu. Kwa uhalisia, kwa Mungu, ni sehemu ndogo tu ya kazi Yake ndiyo imekamilika. Amemkomboa tu binadamu; Hajamshinda mwanadamu, wala kubadilisha ubaya wa Shetani kwa binadamu. Hiyo ndio maana Mungu Anasema, "Ingawa mwili Wangu ulipitia maumivu ya kifo, hilo sio lengo lote la Mimi kupata mwili. Yesu ni Mwana Wangu mpendwa na Alisulubishwa msalabani kwa ajili Yangu, lakini hakukamilisha kikamilifu kazi Yangu. Alifanya tu sehemu." Hivyo Mungu Akaanza mpango wa mzunguko wa pili ili kuendeleza kazi ya Mungu kupata mwili. Lengo kuu la Mungu ni kumkamilisha na kumpata kila mmoja aokolewe kutoka katika mikono ya Shetani….
kutoka kwa "Kazi na Kuingia (6)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi katika siku za mwisho ni kunena maneno. Mabadiliko makuu yanaweza kusababishwa kwa watu kupitia katika maneno hayo. Mabadiliko yanayosababishwa sasa kwa watu hawa kwa sababu ya kukubali maneno haya ni makubwa kuliko yale ya watu katika Enzi ya Neema kwa kukubali ishara na maajabu hayo. Kwani, katika Enzi ya Neema, mapepo yaliondoka kutoka kwa mwanadamu kwa kuwekewa mikono na maombi, lakini tabia potovu ndani ya mwanadamu ilibaki. Mwanadamu aliponywa magonjwa na kusamehewa dhambi zake, lakini kazi ya jinsi tabia potovu za kishetani katika mwanadamu haikutupiliwa mbali na bado iko ndani yake. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kupitia mwili wa Mungu mwenye mwili, lakini haimaanishi kuwa mwanadamu hana dhambi ndani yake. Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia potovu za zamani za kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili. Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwena Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na uonekano wa kiungu; kama mwanadamu angeishi katika huo msingi, alichukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, hii ina maana kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia ya kuielekea tabia iliyobadilika; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii inamfanya mwanadamu kuwa safi kupitia neno ili kumpatia mwanadamu njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendeleaa na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupuwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia kwenye neno, binadamu anajua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha binadamu, na kile ambacho binadamu anastahili kuingia ndani chake. Kupitia neno, kazi yote ambayo Mungu hupenda kufanya katika Enzi ya Neno inatimizwa. Kupitia neno, binadamu anafichuliwa, anaondolewa, na kujaribiwa. Binadamu ameliona neno, amelisikia neno, na akapata habari ya uwepo wa neno. Kutokana na haya, binadamu anaamini katika uwepo wa Mungu; binadamu anaamini katika uwezo na hekima za Mungu, pamoja na moyo wa upendo wa Mungu kwa binadamu na tamanio Lake la kumwokoa binadamu. … Katika Enzi nzima ya Ufalme, Mungu hutumia neno kufanya kazi Yake na kutimiza matokeo ya kazi Yake; Hafanyi maajabu au kutenda miujiza; Anafanya tu kazi Yake kupitia kwa neno. Kwa sababu ya neno, binadamu anastawishwa na kuruzukiwa; kwa sababu ya neno, binadamu hupokea maarifa na kupata uzoefu wa kweli.
kutoka kwa "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu, kuweka wazi hulka ya asili ya mwanadamu na tabia ya mwanadamu iliyoharibika, uondoaji wa dhana za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishiwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu.
kutoka kwa "Kuijua Kazi ya Mungu Leo" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika kazi yake ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ile ya kuadibu na hukumu, ambayo inafichua yote ambayo si ya haki, na kuhukumu wanadamu hadharani, na kukamilisha wale ambao wanampenda kwa ukweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho. Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitabainishwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua hatima ya wanadamu na kikomo cha safari yao. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wa mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watabainishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mzuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi zote zinahitaji kuadibu kwa haki na hukumu kutimizwa. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. Kwa hivyo, tabia kama hii imejazwa umuhimu wa wakati, na ufunuo na maonyesho ya tabia yake ni kwa ajili ya kazi ya kila enzi mpya. Mungu hafichui tabia yake kiholela na bila umuhimu.
kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni