Jumanne, 2 Oktoba 2018

Sura ya 4 Lazima Mjue Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

1. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Maneno.

Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia kwenye neno, binadamu anajua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha binadamu, na kile ambacho binadamu anastahili kuingia ndani chake. Kupitia neno, kazi yote ambayo Mungu hupenda kufanya katika Enzi ya Neno inatimizwa. Kupitia neno, binadamu anafichuliwa, anaondolewa, na kujaribiwa. Binadamu ameliona neno, amelisikia neno, na akapata habari ya uwepo wa neno. Kutokana na haya, binadamu anaamini katika uwepo wa Mungu; binadamu anaamini katika uwezo na hekima za Mungu, pamoja na moyo wa upendo wa Mungu kwa binadamu na tamanio Lake la kumwokoa binadamu. Ingawa neno "neno" ni rahisi na kawaida, neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu kuwa mwili hutikisa dunia nzima; neno Lake hubadilisha moyo wa binadamu, fikira na tabia zee za binadamu, na sura nzee ya ulimwengu mzima. Kupitia enzi nyingi, Mungu pekee wa leo ndiye anayefanya kazi katika njia kama hiyo, na ni Yeye tu Anayeongea na kumwokoa binadamu hivyo. Baadaye, binadamu huishi katika mwongozo wa neno, akichungwa na kujazwa na neno; wanaishi katika ulimwengu wa neno, wanaishi katika laana na baraka za neno la Mungu, na hata zaidi kuishi chini ya na hukumu na kuadibu kwa neno. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa minajili ya wokovu wa binadamu, kutimiza mapenzi ya Mungu, kubadilisha sura asilia wa ulimwengu wa uumbaji wa kale. Mungu aliuumba ulimwengu kwa neno, huwaongoza wanadamu kote ulimwenguni kwa neno, hushinda na kuwaokoa binadamu kwa neno. Hatimaye, Yeye atatumia neno ili kuutamatisha ulimwengu mzima wa kale. Ni hapo tu ndipo mpango wa usimamizi unapokuwa mkamilifu kabisa. Katika Enzi nzima ya Ufalme, Mungu hutumia neno kufanya kazi Yake na kutimiza matokeo ya kazi Yake; Hafanyi maajabu au kutenda miujiza; Anafanya tu kazi Yake kupitia kwa neno. Kwa sababu ya neno, binadamu anastawishwa na kuruzukiwa; kwa sababu ya neno, binadamu hupokea maarifa na kupata uzoefu wa kweli. Binadamu katika Enzi ya Neno amepokea kwa kweli baraka za kipekee. Binadamu huwa hapati maumivu ya mwili na hufurahia tu mjazo mengi ya neno la Mungu; hawahitaji tena kutafuta au kushika safari, na kwa utulivu huona kuonekana kwa Mungu, wanamsikiliza Yeye akiongea binafsi, wanapokea ujazo Wake, na kumwona Yeye binafsi akifanya kazi Yake. Binadamu katika enzi zilizopita hakuweza kufurahia mambo kama haya, na hizi ndizo baraka ambazo wasingewahi kupokea.
kutoka kwa "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati wa siku za mwisho Mungu Amekuja mahususi kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake. Anazungumza kutokana na mtazamo wa Roho, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, na kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu; Anazungumza kwa namna tofauti, Akitumia njia moja kwa kipindi fulani, na Anatumia njia za kuzungumza ili kubadilisha dhana za mwanadamu na kuondoa taswira ya Mungu yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii ndiyo kazi kuu iliyofanywa na Mungu. Kwa sababu mwanadamu anaamini kwamba Mungu Amekuja kuponya wagonjwa, kutoa mapepo, kufanya miujiza, na kumpatia mwanadamu baraka za vitu, Mungu Anatekeleza hatua hii ya kazi—kazi ya kuadibu na hukumu—ili kuweza kuondoa mambo hayo kutoka katika dhana za mwanadamu, ili mwanadamu aweze kuuelewa uhalisia na ukawaida wa Mungu, na ili kwamba taswira ya Yesu iweze kuondolewa moyoni mwake na kuwekwa taswira mpya ya Mungu.
kutoka kwa "Kuijua Kazi ya Mungu Leo" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu, kuweka wazi hulka ya asili ya mwanadamu na tabia ya mwanadamu iliyoharibika, uondoaji wa dhana za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishiwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu.
kutoka kwa "Kuijua Kazi ya Mungu Leo" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika hatua hii ya mwisho ya kazi, matokeo yanapatikana kupitia kwa neno. Kupitia kwa neno, mwanadamu anaelewa mafumbo mengi na kazi ya Mungu katika vizazi vilivyopita; kupitia kwa neno, mwanadamu anapewa nuru na Roho Mtakatifu; kupitia kwa neno, mwanadamu anapata kuelewa mafumbo ambayo hayajawahi kuelezwa na vizazi vilivyopita, na pia kazi za manabii na ,mitume wa enzi zilizopita, na kanuni ambazo walitumua kufanya kazi; kupitia kwa neno, mwanadamu anatambua tabia ya Mungu Mwenyewe, na pia uasi na pingamizi ya mwanadamu, na kujua dutu yao. Kupitia kwa hatua hizi za kazi na maneno yote yaliyonenwa, mwanadamu anatambua kazi ya Roho Mtakatifu, kazi ya mwili wa Mungu, na zaidi ya hayo, tabia Yake yote. Maarifa yako ya kazi ya usimamizi wa Mungu wa kupita miaka elfu sita ulitwaliwa kupitia kwa neno. Je, maarifa yako hayakuwa ya fikira zako za awali na mafanikio kwa kuyaweka kando pia yalipatikana kupitia neno? Katika hatua ya awali, Yesu Alifanya ishara na maajabu, lakini sio hivyo katika hatua hii. Je si kuelewa kwako kwa nini Hafanyi hivyo pia kulipatikana kupitia neno? … Kwa maneno yaliyonenwa katika hatua hii, kuna unabii na ukweli, lakini hasa yanafanya kazi ya kutawaza maisha juu ya mwanadamu. Maneno ya wakati huu sio kama unabii wa manabii. Hii ni hatua ya kazi isioya unabii ila ya maisha ya mwanadamu, kubadili tabia ya maisha ya mwanadamu.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati huo, Yesu alifanya kazi kubwa ambayo haikueleweka kwa wanafunzi Wake, na kusema mengi kwamba watu hawakuelewa. Hii ni kwa sababu, wakati huo, Hakutoa maelezo. Kwa hivyo, miaka kadhaa baada ya Yeye kuondoka, Mathayo aliunda kizazi chake, na wengine pia walifanya kazi kubwa ambayo ilikuwa ya mapenzi ya mwanadamu. Yesu hakuja kumkamilisha na kumpata mwanadamu, lakini kufanya awamu moja ya kazi: kuleta injili ya ufalme wa mbinguni na kukamilisha kazi ya kusulubiwa—na punde tu Yesu Aliposulubishwa, kazi Yake ilifika mwisho kamili. Lakini kwa awamu iliyoko sasa—kazi ya ushindi—maneno mengi zaidi lazima yasemwe, kazi nyingi zaidi lazima ifanywe, na lazima kuwa na hatua nyingi. Hivyo pia ni lazima siri za kazi ya Yesu na Yehova zitafichuliwa, ili wanadamu wote waweze kuwa na ufahamu na uwazi wa imani yao, kwa kuwa hii ni kazi ya siku za mwisho, na siku za mwisho ni mwisho wa kazi ya Mungu, wakati wa kuhitimisha kazi hii. Hii awamu ya kazi itakufafanulia sheria ya Yehova na ukombozi wa Yesu, na ni hasa ili uweze kuelewa kazi nzima ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na kuelewa kusudi la kazi zote Alizozifanya Yesu na maneno Aliyoyasema, na hata upofu wako wa imani kwenye na katika ibada ya Biblia. Yote haya yatakuwezesha kujua. Wewe utakuja kufahamu kazi anayoifanya Yesu na kazi ya Mungu leo; utaelewa na kushuhudia ukweli wote, uzima, na njia. Katika awamu ya kazi Aliyoifanya Yesu, kwa nini Yesu Aliondoka bila kumaliza kazi ya Mungu? Kwa sababu awamu ya kazi ya Yesu haikuwa kazi ya kumalizia. Wakati Yeye Alisulubishwa msalabani, maneno ambayo Alikuwa Ameyasema pia yalikuwa yamefika mwisho; baada ya kusulubiwa kwake, kazi Yake kwa hivyo ilimalizika. Awamu ya sasa ni tofauti. Ni baada tu ya maneno hayo kusemwa hadi mwisho na kazi nzima ya Mungu iwe imehitimika ndipo kazi yake itakapokuwa imemalizika. Wakati wa awamu ya kazi ya Yesu, kulikuwa na maneno mengi yaliyobakia bila kusemwa, au ambayo hayakuwa yameelezwa kikamilifu kwa ufasaha. Waama, Yesu hakujali Alichosema au kile ambacho hakusema, kwa kuwa huduma yake haikuwa huduma ya maneno; na hivyo baada ya Yeye kusulubishwa msalabani Aliondoka. Awamu hiyo ilikuwa hasa kwa ajili ya kusulubiwa, na ni tofauti na awamu ya sasa. Awamu ya kazi hii ni hasa kwa ajili ya kukamilisha, kufumbua, na kuleta kazi yote kwenye hitimisho. Kama maneno hayasemwi hadi tamati yake kabisa, hakutakuwa na mbinu ya kuhitimisha kazi hii, kwa kuwa awamu hii ya kazi yote inafikishwa mwisho na kukamilika kwa kutumia maneno. Wakati huo, Yesu Alifanya kazi kubwa isiyoeleweka na mwanadamu. Akaondoka kimya kimya, na leo bado kunao wengi wasioelewa maneno Yake, ambao ufahamu wao ni potofu lakini bado unaaminika nao kwamba ni sahihi, ambao hawajui kuwa wao si sahihi. Mwishoni, awamu hii ya sasa itafikisha kazi ya Mungu mwisho ulio kamilifu, na kutoa hitimisho Lake. Wote watakuja kufahamu na kujua mpango wa usimamizi wa Mungu. Dhana zilizo ndani ya mwanadamu, nia yake, fahamu yake potofu, dhana zake kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, maoni yake kuhusu watu wa Mataifa mengine na michepuko na makosa yake yote yatarekebishwa. Na mwanadamu ataelewa njia yote ya haki ya uzima, na kazi yote anayofanya Mungu, na ukweli wote. Wakati hayo yatafanyika, awamu hii ya kazi itafikia kikomo.
kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (2)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa hivyo, katika siku za mwisho, Mungu anapokuwa mwili, kimsingi Anatumia neno kukamilisha yote na kufanya yote yawe wazi. Katika maneno Yake pekee ndipo unaweza kuona kile Alicho; ni katika maneno Yake pekee ndiyo unaweza kuona kwamba yeye ni Mungu Mwenyewe. Mungu katika mwili Anapokuja duniani, hafanyi kazi nyingine ila kuongea maneno—hivyo basi hakuna haja ya kutumia uhakika; maneno yanatosha. Hii ni kwa sababu Amekuja kimsingi kufanya kazi hii, kumruhusu mwanadamu aone nguvu Zake na ukuu ulio kwenye neno Lake, kumruhusu mwanadamu kuona kupitia kwa maneno Yake jinsi Alivyojificha kwa unyenyekevu, na kumruhusu mwanadamu kujua ukamilifu Wake kupitia kwa maneno Yake. Kila kitu Alicho nacho na kile Alicho kiko katika maneno Yake, hekima Yake na ajabu yako katika maneno Yake. Katika hii ndipo unapofanywa kuona mbinu nyingi ambazo Mungu anatumia kuongea maneno Yake. …
…Mungu amekuja duniani wakati wa siku za mwisho ili kutekeleza huduma ya neno ili mwanadamu amtambue, na ili mwanadamu aone kile Alicho, na aone hekima Yake na matendo Yake yote ya maajabu kutoka kwa neno Lake. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno kimsingi kushinda watu wote. Baadaye neno Lake litakuja katika kila dhehebu, kikundi, taifa na madhehebu; Mungu hutumia neno kushinda, kuwafanya wanadamu wote waone kuwa neno Lake lina mamlaka na nguvu—na kwa hivyo leo, unakumbana tu neno la Mungu.
kutoka kwa "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu wa siku za mwisho hasa hutumia neno kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Hatumii ishara na maajabu kumdhulumu mwanadamu, ama kumshawishi mwanadamu; hii haiweki wazi nguvu za Mungu. Iwapo Mungu angeonyesha tu ishara na maajabu, basi hakungekuwa na uwezo wa kuweka wazi ukweli wa Mungu, na hivyo haingewezekana kufmanya mwanadamu mkamilifu. Mungu hamfanyi mwanadamu mkamilifu kwa kutumia ishara na maajabu, ila Anatumia neno kunyunyizia na kumchunga mwanadamu, na baada ya haya kunapatikana utiifu kamili wa mwanadamu na ufahamu wa mwanadamu kuhusu Mungu. Hili ndilo lengo la kazi Anayofanya na maneno Anenayo. Mungu hatumii mbinu ya kuonyesha ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kamili—Anatumia maneno, na Anatumia mbinu nyingi za kazi kumfanya mwanadamu kamili. Iwe ni usafishaji, kushughulikia, upogoaji, ama kupewa maneno, Mungu hunena kutoka taswira nyingi tofauti kumfanya mwanadamu kamili, na kumpa mwanadamu maarifa kuu ya kazi, hekima na ajabu ya Mungu.
kutoka kwa "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Umuhimu mkubwa zaidi wa kazi ya maneno ni kuwaruhusu watu kuweza kutia katika matendo ukweli baada ya kuuelewa ukweli, kutimiza mabadiliko katika tabia yao, na kutimiza maarifa kuhusu wao wenyewe na kazi ya Mungu. Mbinu za kufanya kazi tu kupitia kwa kuongea ndizo zinazoweza kuleta mawasiliano kuhusu uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu, maneno tu ndiyo yanayoweza kuelezea ukweli. Kufanya kazi kwa njia hii ndiyo mbinu bora zaidi ya kumshinda mwanadamu; mbali na matamko ya maneno, hakuna mbinu nyingine inayoweza kumpatia mwanadamu uelewa wa wazi zaidi wa ukweli na kazi ya Mungu, na hivyo basi katika awamu Yake ya mwisho ya kazi, Mungu anazungumza naye mwanadamu ili kuweza kuwa wazi kwa mwanadamu kuhusu ukweli na siri zote ambazo haelewi, na hivyo basi kumruhusu kufaidi njia ya kweli na uzima kutoka kwa Mungu na kisha kutosheleza mapenzi ya Mungu. … Hatua hii ya kazi—kazi ya maneno—humwekea wazi mwanadamu njia na siri zote ambazo haelewi, ili mwanadamu aweze kuelewa mapenzi ya Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu, ili aweze kuwa katika ile hali ya kutia katika matendo maneno ya Mungu na kutimiza mabadiliko hayo katika tabia yake.
kutoka kwa "Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika enzi hii, Mungu atafanya jambo la uhalisia miongoni mwenu ili kwamba kila binadamu aweze kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, aweze kutia ukweli katika matendo, na kumpenda Mungu kwa dhati; kwamba binadamu wote waweze kutumia neno la Mungu kama msingi na uhalisia wao na kuwa na mioyo ya kumcha Mungu; na kwamba, kupitia kwa kutenda neno la Mungu, binadamu basi anaweza kutawala pamoja na Mungu. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu atatimiza. Unaweza kuendelea na maisha bila ya kusoma neno la Mungu? Kuna wengi sasa wanaohisi kwamba hawawezi kukaa hata siku moja au mbili bila ya kusoma neno la Mungu. Lazima wasome neno Lake kila siku, na kama muda hauruhusu, kusikiliza neno Lake kunatosha. Hii ndiyo hisia ambayo Roho Mtakatifu anampa binadamu na namna ambavyo Anaanza kumbadilisha binadamu. Yaani, Hutawala binadamu kupitia kwa maneno ili binadamu aweze kuingia katika uhalisia wa neno la Mungu. … Mungu hutumia neno ili kumtawala binadamu; unahisi vyema kama utakula na kunywa neno la Mungu, na kama huhisi hivyo, hutakuwa na njia yoyote ya kufuata. Neno la Mungu linakuwa chakula cha binadamu na nguvu zinazomwendesha. Biblia inasema kwamba "Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo kwa kinywa cha Mungu." Hii ndiyo kazi ambayo Mungu ataikamilisha leo. Atafanikisha ukweli huu ndani yenu. Ikoje kwamba binadamu katika siku za kale angekaa siku nyingi bila ya kusoma neno la Mungu lakini angeendelea kula na kufanya kazi? Na kwa nini hali sivyo hivi sasa? Katika enzi hii, Mungu hutumia kimsingi neno ili kutawala yote. Kupitia kwa neno la Mungu, binadamu anahukumiwa na kufanywa mtimilifu, kisha hatimaye kupelekwa katika ufalme. Ni neno la Mungu tu linaloweza kuruzuku maisha ya binadamu, na ni neno la Mungu tu ndilo linaloweza kumpa binadamu nuru na njia ya kutenda, hasa katika Enzi ya Ufalme. Mradi tu kila siku unakula na kunywa neno Lake na huachi uhalisia wa neno la Mungu, Mungu ataweza kukufanya mtimilifu.
kutoka kwa "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" katika Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Kuhusu Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni