Kanisa la Mwenyezi Mungu | 4. Unawezaje Kutambua Tofauti Kati ya Njia za Kweli na za Uongo, na Makanisa ya Kweli na ya Uongo?
Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Kanuni ya msingi kabisa katika kuutafuta ukweli ni nini? Unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu au la, iwapo maneno haya ni udhihirishaji wa ukweli, yanamshuhudia nani, na ni kitu gani yanaweza kukupatia. Kutofautisha kati ya njia ya kweli na hizi njia za uongo kunahitaji njia kadhaa za maarifa ya msingi, ya msingi kabisa kati ya zote ni kusema iwapo kuna Kazi ya Roho Mtakatifu au la. Maana kiini cha imani ya mwanadamu kwa Mungu ni imani katika Roho Mtakatifu.
Hata imani yake kwa Mungu mwenye mwili ni kwa sababu mwili huu ni mfano halisi wa Roho wa Mungu, ikiwa na maana kwamba imani hiyo bado ni imani katika Roho. Kuna tofauti kati ya Roho na mwili, lakini kwa kuwa mwili unatokana na Roho, na ndio Neno linakuwa mwili, hivyo kile ambacho mwanadamu anaamini katika ni uungu halisi wa Mungu. Na hivyo, katika kutofautisha kama ni njia sahihi au la, zaidi ya yote unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu, na baada ya hapo unapaswa kuangalia kama kuna ukweli katika njia hii. Ukweli huu ni silika ya maisha ya mwanadamu wa kawaida, ni sawa na kusema, kile ambacho Mungu alikitaka kwa mwanadamu alipomuumba hapo mwanzo, yaani, ubinadamu wote wa kawaida (ikiwa ni pamoja na hisia za kibinadamu, umaizi, hekima, na maarifa ya msingi ya kuwa mwanadamu). Yaani, unapaswa kuangalia iwapo njia hii inampeleka mwanadamu katika maisha ya mwanadamu wa kawaida au la, iwapo ukweli uliozungumzwa unahitajika kulingana na uhalisia wa ubinadamu wa kawaida au la, iwapo ukweli huu ni wa kiutendaji au hali, na iwapo ni wa wakati muafaka au la. Ikiwa kuna ukweli, basi unaweza kumpeleka mwanadamu katika uzoefu wa kawaida na halisi; aidha, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, hisia za kawaida za kibinadamu zinakuwa kamili zaidi, maisha ya mwanadamu katika mwili na maisha ya kiroho yanakuwa katika mpangilio mzuri zaidi, na mihemko ya mwanadamu inakuwa ya kawaida kabisa. Hii ni kanuni ya pili. Kuna kanuni nyingine moja zaidi, ambayo ni kama mwanadamu ana maarifa mengi juu ya Mungu, kama unapitia uzoefu wa kazi hiyo na ukweli unaweza kuchochea upendo wa Mungu ndani yake au la, na kumsogeza karibu zaidi na Mungu. Katika hili inaweza kupimwa kama ni njia sahihi au la. Kanuni ya msingi ni iwapo njia hii ni ya uhalisia badala ya kuwa ya kimiujiza, na iwapo inaweza kutoa maisha ya mwanadamu. Kama hukubaliana na kanuni hizi, hitimisho linaweza kuwekwa kwamba njia hii ni njia ya kweli. … Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida kabisa, na ubinadamu wake unakuwa wa kawaida kabisa. Mwanadamu ana maarifa mengi ya tabia yake, ambayo yameharibiwa na Shetani, na asili ya mwanadamu, na ana shauku kubwa ya kuuelewa ukweli. Ni sawa na, kusema, maisha ya mwanadamu yanakuwa na kukua, na Atabia ya upotovu ya mwanadamu inakuwa na uwezo wa mabadiliko zaidi na zaidi—yote hiyo ni maana ya Mungu kuwa maishi ya mwanadamu. Kama njia haiwezi kufunua vitu hivyo ambavyo ni asili ya mwanadamu, haiwezi kubadilisha atabia ya mwanadamu, na, zaidi ya hayo, hauwezi kumleta mbele ya Mungu au kumpa uelewa wa kweli juu ya Mungu, na hata kufanya ubinadamu wake kuwa duni zaidi na hisia zake kuwa si za kawaida zaidi, basi njia hii itakuwa si njia ya kweli, na inaweza kuwa ni kazi ya roho mchafu, au njia ya zamani. Kwa ufupi, haiwezi kuwa kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu. Umeamini katika Mungu kwa miaka yote hii, halafu bado huna uwezo wa kutofautisha kati ya njia ya kweli na njia ya uongo au kuweza kuitafuta njia ya kweli. Watu wengi hawapendi hata kusikia masuala haya; wanakwenda tu kule ambapo wengi wanakwenda, na wanarudia kile ambacho watu wengi wanasema. Ni kwa njia gani mtu huyu ni mtu anayetafuta njia ya kweli? Na ni kwa njia gani watu kama hao wanaweza kuipata njia ya kweli? Ikiwa utaelewa kanuni hizi muhimu, basi chochote kitakachotokea hutaweza kudanganywa.
kutoka kwa "Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale wote walio kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu wanamilikishwa na uwepo na adabu ya Roho Mtakatifu na wasiokuwemo kwenye mkondo huu wako chini ya utawala wa Shetani na hawana kazi yoyote ya Roho Mtakatifu. Walio kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale walioikubali kazi mpya ya Mungu, wanaoshiriki katika kazi mpya ya Mungu. Iwapo walio ndani ya mkondo huu hawana uwezo wa kushirikiana, na hawawezi kuweka ukweli unaotakiwa na Mungu katika vitendo wakati huu, basi watafundishwa nidhamu, na vibaya zaidi kuachwa na Roho Mtakatifu. Wale ambao wanakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wataishi kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu, wapokee huduma na ulinzi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao wako tayari kuweka ukweli katika vitendo wanapewa nuru na Roho Mtakatifu na wale wasiotaka kuweka ukweli katika vitendo wanadhibitiwa na Roho Mtakatifu na huenda wakaadhibiwa. Bila kujali ni aina gani ya watu, ili mradi tu wamo kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu, Mungu atawawajibikia wote wanaoikubali kazi Yake mpya kwa minajili ya jina Lake. Wale wanaolitukuza jina Lake na wako radhi kuweka maneno Yake katika vitendo watapokea Baraka Zake; wale wasiomtii na kuyaweka maneno Yake katika vitendo watapokea adhabu Yake. … Sio hivyo na watu wasioikubali kazi mpya: Wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na adhabu na lawama ya Roho Mtakatifu haitumiki kwao. Kila siku hawa watu wanaishi katika mwili, wanaishi katika mitazamo yao, na yote wayafanyayo ni kulingana na mafundisho ya kidini yaliyozalishwa na uchanganuzi pamoja na utafiti wa bongo zao. Si matakwa ya kazi mpya ya Roho Mtakatifu wala sio ushirika na Mungu. Wale wasioikubali kazi mpya ya Mungu wanajinyima uwepo wa Mungu na zaidi wanakosa baraka na ulinzi wa Mungu. Mengi ya maneno na matendo yao yanashikilia matakwa ya zamani ya kazi ya Roho Mtakatifu; ni mafundisho ya kidini tu na wala si ukweli. Mafundisho na taratibu kama hizo ni thibitisho la kutosha kuwa kitu cha pekee kinachowaleta pamoja ni dini; si watu walioteuliwa au vyombo vya kazi ya Mungu. Mikutano ya wote walio miongoni mwao haiwezi kuitwa kanisa bali mkutano mkubwa wa watu wa dini. Huu ni ukweli usioweza kubadilishwa.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa nini inasemekana kwamba vitendo vya walio katika makanisa ya kidini vimepitwa na wakati? Ni kwa kuwa wanayoyaweka katika vitendo ni tofauti na kazi ya leo. Katika Enzi ya Neema, walichotenda kilikuwa sahihi, ila kwa kuwa enzi yenyewe imepita na kazi ya Mungu kubadilika, vitendo vyao hatua kwa hatua vimepitwa na wakati. Vimeachwa nyuma na kazi mpya na mwangaza mpya. Ikiwa imesimama juu ya msingi wake asili, kazi ya Roho Mtakatifu imepiga hatua kadhaa kwa kina. Na bado watu hao wamebaki katika hatua ya asili ya kazi ya Mungu na bado wanapenyeza katikati ya vitendo na mwangaza wa zamani. Kazi ya Mungu yaweza kubadilika pakubwa kwa miaka mitatu au mitano, hivyo si mabadiliko hata makubwa zaidi yaweza kuja kwa kipindi cha miaka zaidi ya 2000? Ikiwa mwanadamu hana vitendo vipya ama mwangaza mpya, inamaanisha hajaenda sawia na kazi ya Roho Mtakatifu. Hili ni anguko la mwanadamu; uwepo wa kazi mpya ya Mungu hauwezi kukanwa kwa sababu, leo hii, wale walio na kazi asili ya Roho Mtakatifu bado wanashikilia vitendo vilivyopitwa na wakati. Kazi ya Roho Mtakatifu daima inasonga mbele, na wote walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu wanafaa waendelee mbele na kubadilika, hatua kwa hatua. Hawapaswi kukwama katika hatua moja. Ni wale tu wasioifahamu kazi ya Roho Mtakatifu ndio wanaweza kubaki katika hatua ya kazi ya Mungu ya awali na wasikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu. Ni wale tu walio waasi ndio watakosa uwezo wa kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ikiwa vitendo vya mwanadamu haviendani na mwendo wa kazi mpya ya Roho Mtakatifu, basi vitendo vya mwanadamu hakika vimetengana na kazi ya leo na kwa hakika havilingani na kazi ya leo. Watu waliopitwa na wakati kama hawa hawawezi kutimiza mapenzi ya Mungu, na zaidi hawawezi kuwa wale watu wa mwisho ambao watamshuhudia Mungu. Aidha, kazi nzima ya usimamizi haiwezi kutimilika miongoni mwa kundi la watu kama hao. Kwa wale walioshikilia sheria za Yehova kipindi fulani, na wale walioumia wakati fulani chini ya msalaba, ikiwa hawawezi kukubali hatua ya kazi ya siku za mwisho, basi yale yote waliyofanya ni bure na yasiyofaa. … Ikiwa mwanadamu atasalia amekwama katika hatua moja tu, basi hili linaonyesha kuwa haendi sawia na kazi ya Mungu na mwangaza mpya; haimaanishi kuwa mpango wa usimamizi wa Mungu haujabadilika. Walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu daima hudhani wako sahihi, lakini kwa hakika, kazi ya Mungu ndani yao ilisita zamani na kazi ya Roho Mtakatifu haimo ndani yao. Kazi ya Mungu imeshahamishiwa kwa kundi jingine la watu, kundi ambalo kwalo Anapania kukamilishia kazi Yake mpya. Kwani walio kwenye dini hawawezi kuikubali kazi mpya ya Mungu, na kushikilia tu kazi kongwe za zamani, hivyo Mungu amewaacha watu hawa na anafanya kazi Yake mpya kwa watu wanaoikubali kazi hii mpya. Hawa ni watu wanaoshiriki katika kazi Yake mpya, na usimamizi Wake utatimilika kwa njia hii tu. Usimamizi wa Mungu daima unasonga mbele na vitendo vya mwanadamu daima vinapanda juu. Mungu daima anafanya kazi na mwanadamu mara zote ni mhitaji ili kwamba wote wanafikia upeo wao, Mungu na mwanadamu wamo katika muungano kikamilifu. Haya ni maonyesho ya kutimilika kwa kazi ya Mungu, na ndiyo matokeo ya mwisho ya kazi nzima ya usimamizi.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ushirika wa Mtu:
Njia ya kweli ni njia ambayo inaweza kuwaokoa watu, kuwabadilisha watu, na kuwawezesha kufanikisha kukubaliwa na Mungu na kuingia katika hatima ya kweli. Hii tu ndiyo njia ya kweli. Iwapo watu wanadhani kuwa wao wanaamini katika njia ya kweli, lakini malengo haya na matokeo haya hayajapatikana, basi inaweza kusemwa kwamba yao ni njia ya uongo, kwamba si njia ya kweli. Watu wengine husema: "Je, nitawezaje kutambua tofauti kati ya mazuri na mabaya?" Hili linakamilishwa kulingana na maneno ya Mungu. Yote yanayokubaliwa na Mungu, yote Anayomhitaji mwanadamu kumiliki, na kila ambacho Mungu Anapenda mwanadamu afanye ni kizuri; yote ambayo Mungu Anataka wanadamu wayakatae na kuyaacha, na yote yanayoshutumiwa na Mungu, ni mabaya. Kutathmini mazuri na mabaya huamuliwa hivyo, kulingana na maneno ya Mungu; Maneno ya Mungu ni kipimo ambacho huthibitisha iwapo kitu chochote ni cha kweli au cha uongo, na ndicho kiwango pekee cha kupima iwapo kitu chochote ni kweli au uongo. Unatathmini vipi njia gani ni ya kweli, na gani ni ya uongo? Njia inayoweza kukuletea maisha ya kweli, inayoweza kukufanya uone mwanga, inayoweza kukuruhusu ujiondolee upotovu na ushawishi wa Shetani, na kukuwezesha kupata kibali na baraka ya Mungu—hii ndiyo njia ya kweli. Je, huo si ukweli? Je, hukumu na kuadibu kwa Mungu kumetuletea nini? Kumetuletea ukweli wote ambao watu wapotovu lazima wamiliki ili kupata wokovu, kumeleta njia ya kweli ya maisha, kumeturuhusu kuuona mwanga wa maisha, kumetupa wokovu mkuu zaidi, na wokovu wa kweli, ambao ulipangiwa awali na Mungu katika uumbaji wa dunia, na kumetubadilisha sisi kutoka kwa watu ambao walipotoshwa na Shetani, na kumilikiwa na Shetani, na kuwa watu halisi ambao kwa hakika wametakaswa na Mungu na wamejawa na ukweli na ubinadamu. Haya yote ndiyo matokeo yaliyofanikishwa na hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Bila hukumu na kuadibu kwa Mungu, hatungeweza kupata ukweli, upotovu wetu ungebaki bila kutatuliwa, kamwe hatungeweza kuona mwanga wa maisha, na kamwe hatungepata kibali cha Mungu. Hivyo, baraka zote ambazo tumepokea leo zinatokana na kupitia na kutii hukumu na kuadibu kwa Mungu.
…………
Baadhi ya watu husema: "Hebu, iwapo hii ni njia ya kweli, kwa nini watu wachache tu ndio waliojiunga nayo? Kwa kuwa ni njia ya kweli, si inapaswa kuwa na waumini wengi? Si binadamu wote wanapaswa kuamini kwayo?" Watu wanaosema mambo kama hayo hawaelewi ukweli, wao ni wapumbavu. Upotovu wa binadamu wote umefikia hatua fulani; watu wachache zaidi na zaidi ndio wanapenda ukweli, watu wengi zaidi na zaidi wanafuatilia maslahi yao wenyewe, na bila kujali ni imani gani watakubali, wao kwanza huangalia kama ni ya faida kwao—ambayo ina maana kwamba wale ambao wanaamini katika njia ya kweli kwa hakika ni wachache, na wale ambao wanaamini katika njia za uongo, na njia ambazo zinatoa neema na faida, kwa hakika ni wengi. Baada ya kusikia maelezo yangu, utaweza kuona ndani kwenye kiini cha suala. Njia tunayoamini kwayo haiponyi watu, wala kujaza matumbo yao kwa mkate, au kuwapa neema, au kupunga pepo waovu kutoka kwao. Lakini tukiongeza kitu kimoja zaidi kwa njia tunayoamini kwayo—kwamba waumini hawatakufa wakati maafa yoyote yatawasibu—basi watu wote wa dunia wataamini ndani yake. Leo, hili halijahusishwa katika njia yetu. Mungu hajasema, "Naahidi kwamba wote ambao wanaamini katika jina la Mwenyezi Mungu hawatakufa." Hivyo, unapoeneza injili una tahadhari. Watu huuliza, "Kwa hivyo sitakufa nikiamini katika Mwenyezi Mungu?" "Mimi sijui." "Kama Hawezi kunizuia kufa, basi hakuna haja ya kuamini katika Yeye." Watu pia watauliza, "Nitafaidi nini kutoka kwa kuamini katika Mwenyezi Mungu?" "Unaweza kupata ukweli." "Kupata ukweli kutanipatia nini?" "Utanusurika" "Ni nani amewahi kuona hili?" "Nani anayeweza kulithibitisha? Kupata ukweli kunamaanisha nini?" "Mimi Sijui." "Hakuna jinsi ninavyoweza kuamini." Hivyo, ni vigumu kwetu kumshuhudia Mwenyezi Mungu na kueneza injili, kwa kuwa wale wanaopenda ukweli ni wachache sana. Huu ni ukweli. Ilhali baada ya kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu, jinsi tunavyoamini zaidi, ndivyo tunavyohisi kuwa ni halisi zaidi, na ndivyo imani yetu inavyokuwa na nguvu zaidi. Ni kwa nini vile? Haya ni matokeo ya kuuelewa ukweli. Zaidi mtu anavyoelewa ukweli, ndivyo wanavyohisi zaidi kuwa ni njia ya kweli, na kazi ya Mungu. Zaidi wanavyoulewa ukweli, zaidi wanavyojiambia wenyewe, "Ah, wokovu wa Mungu wa binadamu kwa njia hii ni halisi sana, kuelewa ukweli hakika kunaweza kuniokoa, kusababisha mabadiliko katika tabia yangu, kunifanya mimi kuwa binadamu wa kweli, na kuniruhusu niishi maisha halisi ya ubinadamu wa kawaida—na kwa hivyo njia hii ina maana." Wanahisi kwamba kuupata ukweli kuna maana zaidi, kunastahili, na kwenye thamani zaidi ya faida yoyote, au uponyaji wa wagonjwa, au kujaza matumbo ya watu na chakula. Kwa sababu hiyo, wale ambao wameamini katika Mwenyezi Mungu kwa miaka kadhaa huhisi kwamba hakuna kitu cha thamani kuhusu neema yoyote wanayoweza kupewa, kwamba kupata ukweli tu ni kwa thamani—na katika hili, wameona njia ya kweli. Tazama, kuna wowote wa wale wanaoamini katika Mwenyezi Mungu wametoroka? Ingawa baadhi ya watu hawautafuti ukweli, mradi wao wamesikiliza mahubiri kwa miaka michache, je watataka kuondoka? Hakuna hata mmoja angetaka. Na kwa nini wasitake? Wanachojua ni kwamba "Hii ndiyo njia ya kweli. Bora tu nifanye kazi kwa bidii, na kufanya wajibu wangu vizuri, basi kuna uwezekano mkubwa kwamba nitaishi, kwamba mwisho wangu hautakuwa kifo. Kutokufa ni kwa thamani mno." Leo, watu hawajui ni nini kinahitajika ili kuepuka kifo. Punde tu wangejua, basi kila mtu angekuwa muumini, na imani yao ingekuwa imara.
kutoka kwa "Mafunzo Manne muhimu Ambayo Lazima Yaingiwe ili Kuitii Kazi ya Mungu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (VI)
Iwapo jamii ya kidini nzima haingekuwa na uhasama na kuipinga, basi hii haingekuwa njia ya kweli. Kumbuka: Njia ya kweli lazima ipingwe na watu wengi, hata na duniani. Wakati Bwana Yesu Alikuja mara ya kwanza kufanya kazi na kuhubiri, je, Uyahudi mzima haukumpinga Yeye? Kila wakati Mungu anapoanza kazi mpya, ubinadamu mpotovu unapata ugumu mkubwa katika kuikubali, kwa kuwa kazi ya Mungu inakinzana na na inakanusha dhana za watu; watu hawana uwezo wa kuelewa, na hawana uwezo wa kuupenya ulimwengu wa kiroho, na kama sio kazi ya Roho Mtakatifu, hawangeweza kukubali njia ya kweli. Ikiaminiwa kuwa ni kazi ya Mungu, lakini haipingwi na jamii za kidini, na inakosa upinzani na uhasama wa dunia, basi hii inathibitisha kwamba kazi hii ya Mungu ni ya uongo. Kwa nini wanadamu hawawezi kuukubali ukweli? Kwanza, mwanadamu ni wa mwili, yeye ni wa dutu ya kimwili. Mambo ya kimwili hayawezi kupenya ulimwengu wa kiroho. Inamaanisha nini kwamba "hayawezi kupenya ulimwengu wa kiroho"? Hii ina maana ya kushindwa kuona roho, shughuli za roho na ulimwengu wa kiroho, kuwa asiyeona Anayofanya na kusema Mungu. Watu wangekuwa vipofu katika ulimwengu wa kiroho. Ukifunga macho yako katika ulimwengu wa kimwili, huoni chochote. Ukiyafungua, unaweza kuona nini? Dunia ya asili. Je, unaweza kuona ni roho yupi anafanya kazi gani ndani ya watu? Je, unaweza kuona kile ambacho Roho wa Mungu amekuja kufanya na kusema? Huwezi. Wakati mwingine unaweza kusikia sauti Yake, na kusoma maneno ya Mungu yaliyoandikwa kwenye kitabu, lakini bado hujui ni vipi au lini Mungu Alinena maneno haya. Unaweza kusikia sauti Yake, lakini hujui inakotoka; unayaona maneno ya Mungu yamechapishwa kwenye ukurasa, lakini hujui ni nini maana yake. Watu hawawezi kupenya ulimwengu wa kiroho, au kushika chanzo cha maneno ya Mungu, na hivyo wanahitaji kupata nuru na kuangaziwa kwa Roho Mtakatifu, na kazi ya Roho Mtakatifu, ili kupata matokeo. Pili, ubinadamu umekuwa mpotovu kwa undani sana, na ndani yake imejazwa na sumu nyingi ya Shetani na ufahamu mwingi; akitathmini kila kitu kwa kutumia falsafa mbalimbali za kishetani na maarifa, basi kamwe hataweza kusadikisha ukweli ni upi. Bila kupata nuru na kuangaziwa kwa Roho Mtakatifu, mwanadamu hangekuwa na uwezo wa kuelewa ukweli. Binadamu mpotovu kwa silika hawezi kupenya ulimwengu wa kiroho. Amejazwa na falsafa za kishetani na maarifa, na hawezi kuutambua ukweli. Na hivyo njia ya kweli bila kuepukika inakabiliwa na mateso na kukataliwa kwa mwanadamu. Kwa nini ni rahisi kwa watu kukubali maarifa na falsafa za Shetani? Kwanza, iko sambamba na dhana zao na maslahi ya miili yao, na ni ya manufaa kwa miili yao. Wanajiambia wenyewe, "Kukubali maarifa kama haya yananisaidia: Yatanipa kuongezwa cheo, yatanifanya niwe mwenye mafanikio, na kuniruhusu kufanikisha mambo. Na maarifa kama haya watu wataniheshimu." Tazama jinsi vinavyowafaa watu viko sambamba na dhana zao. ... Kuwa wapotovu kwa kiasi hiki, na kushindwa kupenya ulimwengu wa kiroho, watu wanaweza tu kumpinga Mungu, na hivyo kuwasili kwa kazi ya Mungu kumekutana na kukataliwa na mwanadamu, upinzani, na hukumu. Je, si hili linatarajiwa? Kama kuwasili kwa kazi ya Mungu hakungekutana na hukumu na upinzani wa dunia na wanadamu, basi hili lingethibitisha kuwa sio ukweli. Iwapo yote yaliyosemwa na Mungu yangekuwa sambamba na dhana ya watu, je, wangeyashutumu? Je, wangeyapinga? Bila shaka hawangefanya hivyo.
kutoka kwa "Ushirika na Mahubiri ya wa Juu Kuhusu Kueneza Injili"
Ni kanisa tu ambalo liko na kazi ya Roho Mtakatifu ndilo kanisa la Mungu, na kama tu lina watu ambao hakika wanafuatilia ukweli na kutii kazi ya Mungu ndipo kanisa linaweza kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu; Mungu anatambua makanisa ambayo yako na kazi ya Roho Mtakatifu, na hayatambui makanisa yasiyo na kazi ya Roho Mtakatifu. Hili linapaswa kueleweka kwa wateule wa Mungu.
…………
Kanisa halisi linajumuisha wale ambao hakika wanaamini katika Mungu na wanapenda ukweli, na ni mkusanyiko wa wote wanaomcha Mungu. Hapo tu ndipo linaweza kuitwa kanisa. ... Ni tu mkusanyiko wa wale ambao wameamuliwa kabla na waliochaguliwa na Mungu na wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu ndio kanisa.
kutoka kwa "Jinsi ya Kukabili na Kutatua Vurugu Kati ya Makanisa ya Mitaani" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirika na Mipangilio ya Kazi ya Kanisa (II)
Kanisa linajumuisha wale ambao hakika wameamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mungu—linajumuisha wale wanaopenda ukweli, wanaotafuta ukweli, na wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu. Ni wakati tu watu hawa wanakusanyika ili kula na kunywa neno la Mungu, kuishi maisha ya kanisa, kupitia kazi ya Mungu, na kufanya wajibu wao kama viumbe wa Mungu ndio linaweza kuwa kanisa. Umati wenye zogo ukisema kwa kweli unaamini katika Mungu, lakini haupendi au kuutafuta ukweli, na hauna kazi ya Roho Mtakatifu, na unafanya sherehe za kidini, na kuomba, na kusoma maneno ya Mungu, basi hili sio kanisa. Kwa usahihi, makanisa yasiyo na kazi ya Roho Mtakatifu si makanisa; hayo ni kumbi za kidini na watu ambao hufanya sherehe za kidini tu. Wao si watu ambao kwa kweli wanamtii Mungu na kupitia kazi ya Mungu.
…………
Kanisa ni mkusanyiko wa watu ambao wanaamini katika Mungu kwa kweli na kufuatilia ukweli, na halishirikishi waovu kabisa—wao si wa kanisa. Iwapo kundi la watu ambao hawakutafuta ukweli na wala kufanya kitu chochote kuuweka ukweli katika vitendo wangekusanyika pamoja, je, hili lingekuwa kanisa? Je, mkusanyiko huu ungekuwa nini? Ungekuwa ukumbi wa kidini, au umati wenye zogo. Kanisa lazima liundwe na watu ambao kwa kweli wanaamini katika Mungu na kuufuatilia ukweli, wanaokula na kunywa maneno ya Mungu, na kumwabudu Mungu, kufanya wajibu wao, na kupitia kazi ya Mungu na wamepata kazi ya Roho Mtakatifu. Hili tu ndilo kanisa. Hivyo, unapotathmini kanisa, lazima kwanza uangalie ni aina gani ya watu linao. Pili, lazima uangalie iwapo wana kazi ya Roho Mtakatifu au la; kama mkutano wao hauna kazi ya Roho Mtakatifu, hilo si kanisa, na kama si mkusanyiko wa wale wanaofuatilia ukweli, basi sio kanisa. Iwapo kanisa halina mtu yeyote anayefuatilia ukweli, na liko bila kazi ya Roho Mtakatifu kabisa, basi kama kuna mtu ndani lake aliye na nia ya kuufuatilia ukweli, na wanabakia katika kanisa kama lile, je, mtu huyo anaweza kuokolewa? Hawezi, na anapaswa kuuacha umati huo wenye zogo na kutafuta kanisa haraka awezavyo. Iwapo, ndani ya kanisa, kuna watu watatu au watano ambao huufuatilia ukweli, na watu 30 au 50 ambao ni umati wenye zogo, basi wale watu watatu au watano ambao wanaamini katika Mungu kwa kweli na kuufuatilia ukweli lazima waje pamoja; wakija pamoja mkutano wao bado ni kanisa, kanisa la wanachama wachache zaidi, lakini lililo safi.
kutoka kwa "Kuelewa Maana ya Kweli ya Kanisa na Kufanya Kazi kulingana na Kanuni Tano za Kazi ya Kanisa Kuna Umuhimu MkubwaSana Wakati wa Mwisho" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (VII)
Watu wengi wanaamini katika Mungu lakini wanaabudu makanisa makuu ya dayosisi na kusadiki kipofu katika wachungaji—na matokeo kwamba, baada ya kuamini katika Mungu kwa miaka mingi, bado hawajaelewa ukweli au kuingia katika hali halisi, wamepata tu baadhi ya mafundisho ya dini na sherehe za kidini na mazoea, na hawamjui Mungu kwa kweli. Katika matokeo, hakuna mabadiliko hata kidogo katika tabia ya maisha yao. Si ajabu, basi, kwamba viongozi hao wa dini na wachungaji hutumia maisha yao yote kwa kuamini katika Mungu na kuhubiri, ilhali hakuna hata mmoja wao anayemjua Mungu kwa kweli, au hata kuwa na moyo unaomcha Mungu; wao hubaki kama Mafarisayo kutoka nyakati za kale, kufanya wawezayo kumpinga Kristo, kuhukumu njia ya kweli, na kuwatega na kuwadhibiti watu wa Mungu waliochaguliwa kwa ajili ya hali zao wenyewe na kuendesha maisha yao. Sababu yao kutoa mfano wa kupenda na kuthamini kundi la wanakondoo wa Mungu kimsingi ni kwa sababu ya kulinda maisha yao wenyewe, kama vile wafanyabiashara wanavyowatendea wateja wao kama miungu ili wapate pesa na kupata utajiri. Kila kitu ambacho jamii ya kidini inafanya ni udhihirisho wa upinzani wake kwa Mungu; si chochote ila sherehe za kidini, na haina uhalisi wa ukweli hata kidogo, na zaidi hakuna dalili yoyote ya kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa dhahiri, jamii ya kidini haimwabudu Mungu wa kweli, ila Mungu asiye dhahiri na Mungu wa kubuniwa tu. Inahubiri mafundisho ya kidini, na elimu halisi ya Biblia, na haina kabisa kupata nuru na mwanga wa Roho Mtakatifu. Hivyo, jamii ya kidini kimsingi haiwezi kuwaleta watu mbele ya Mungu, haiwezi kuwaongoza kwenye njia sahihi ya kuamini katika Mungu, na, zaidi ya hayo, haiwezi kuchukua watu hadi katika hali halisi ya ukweli, au kuwasaidia waokolewe. Hiyo ni kwa sababu viongozi wake na wachungaji hawajafanywa wakamilifu na kujengwa na Roho Mtakatifu wanapopitia kazi ya Mungu, lakini badala yake wamekuwa viongozi na wachungaji katika jamii ya kidini baada ya kufuzu kutoka katika seminari na kupewa cheti cha diploma. Hawana kazi na uthibitisho wa Roho Mtakatifu, hawana ufahamu wa kweli wa Mungu hata kidogo, na midomo yao haiwezi kuzungumza kuhusu kitu kingine ila maarifa ya kitheolojia na nadharia. Wao kwa kweli hawana uzoefu wa kitu chochote. Watu kama hao hawajafuzu kabisa kutumiwa na Mungu; watawezaje kumwongoza mwanadamu kwenda mbele za Mungu? Kwa kiburi hushikilia kuhitimu kutoka chuo seminari kama ushahidi wa haki yao wenyewe, wanafanya kila wawezalo ili kuonyesha kwa majivuno maarifa yao ya Biblia, ni wenye kiburi kisichostahimilika—na kwa sababu hii, wanahukumiwa na Mungu, na kuchukiwa na Mungu, na wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Kuhusu hili hakuna shaka. Kwa nini jamii ya kidini imekuwa adui mkubwa wa Kristo ni swali la kuchochea fikira nyingi sana. Inaonyesha nini kuwa, katika Enzi ya Neema, Uyahudi ulimpiga Yesu Kristo msalabani? Katika Enzi ya Ufalme wa siku za mwisho, jamii za kidini zimeungana na kuweka juhudi zake zote katika kupinga na kuhukumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho, zinamkana na kumkataa Kristo mwenye mwili wa siku za mwisho, zimeunda uvumi mbalimbali kuhusu, na kushambulia, kusingizia na kukufuru dhidi ya Mungu mwenye mwili na kanisa la Mungu, na kwa muda mrefu sasa zimempiga misumari Yesu Aliyerudi, Kristo wa siku za mwisho, msalabani. Hii inathibitisha kuwa jamii za kidini kwa muda mrefu sasa zimepotoka na kuwa majeshi ya Shetani yanayopinga na kuasi dhidi ya Mungu. Jamii ya kidini haitawaliwi na Mungu, wala kutawaliwa na ukweli kweli; inatawaliwa kikamilifu na binadamu wapotovu, na zaidi ya hayo, na wapinga Kristo.
Watu wanapoamini katika Mungu kwenye ukumbi wa dini kama huu—ambao ni mali ya Shetani na unatawaliwa na kudhibitiwa na mapepo na wapinga Kristo—wanaweza tu kuelewa mafundisho ya dini, wanaweza tu kufuata sherehe za kidini na kanuni, na kamwe hawatawahi kuuelewa ukweli, kamwe hawatawahi kuipitia kazi ya Mungu, na kwa kikamilifu hawawezi kuokolewa. Hii ni bila shaka. Kwa kuwa hakuna jambo lolote la kazi ya Roho Mtakatifu katika kumbi za kidini, na ni maeneo ambayo yanamkera Mungu, ambayo yanachukiwa na Mungu, na yanashutumiwa na kulaaniwa na Yeye. Mungu hajawahi kuitambua dini, wala hajawahi kuisifu, na kutoka wakati wa Yesu jamii ya kidini imekuwa ikishutumiwa na Mungu. Hivyo, unapoamini katika Mungu lazima upate mahali palipo na kazi ya Roho Mtakatifu; haya tu ndiyo makanisa ya kweli, na ni katika makanisa ya kweli pekee ndiyo utaweza kusikia sauti ya Mungu, na kugundua nyayo za kazi ya Mungu. Hivyo ndivyo ilivyo njia ambayo Mungu Anatafutwa.
kutoka kwa "Athari za Kuelewa Ukweli kwa Uhalisi" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirika na Mipangilio ya Kazi ya Kanisa (I)
Chanzo: Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu (Mambo Muhimu ya Muumini Mpya)
Soma Zaidi: Maswali na Majibu ya Injili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni