Alhamisi, 31 Januari 2019

8. Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

8. Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. Hivyo ndivyo alivyokuwa mwanzoni na Mungu" (YN. 1:1-2).
"Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli" (YN. 1:14).
"Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu" (YN. 14:6).
"Maneno ninayoongea kwenu ni roho, na ni uhai" (YN. 6:63).
Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hauwezi kufikiwa na mwanadamu.

Jumatano, 30 Januari 2019

Worship and Praise Dance | "Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu" | The Kingdom of Christ Is Paradise for the Honest (Swahili Subtitles)

Worship and Praise Dance | "Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu" | The Kingdom of Christ Is Paradise for the Honest (Swahili Subtitles)

Safi na mwaminifu kama mtoto, asiye na hatia na mchangamfu, aliyejawa na nguvu za ujana,
wao ni kama malaika wanaokuja ulimwenguni.
Hakuna uongo, udanganyifu au hadaa, na moyo ulio wazi na mwaminifu, wanaishi na heshima.
Wanaitoa mioyo yao kwa Mungu, Mungu anawaamini, na wao ni watu waaminifu ambao Mungu anapenda.
Wale wanaopenda ukweli wote wana mioyo ya uaminifu.

Jumanne, 29 Januari 2019

Fasiri ya Mafumbo ya Maneno ya Mungu | Sura ya 13

Fasiri ya Mafumbo ya Maneno ya Mungu | Sura ya 13

Mungu anachukia urithi wote wa joka kubwa jekundu, na Hulichukia joka kubwa jekundu hata zaidi. Huu ni mzizi wa ghadhabu iliyo ndani ya moyo wa Mungu. Inaonekana kwamba Mungu anataka kutupa vitu vyote ambavyo ni mali ya joka kubwa jekundu ndani ya ziwa la moto wa jahanamu kuviteketeza kabisa. Kuna nyakati ambazo hata inaonekana kwamba Mungu anataka kuunyosha mkono Wake kuliangamiza binafsi—hilo tu ndilo lingeweza kufuta chuki iliyo ndani ya moyo Wake.

Jumatatu, 28 Januari 2019

5. Ni zipi tofauti muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na hao watu ambao hutumiwa na Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kazi ya Roho Mtakatifu

I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

5. Ni zipi tofauti muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na hao watu ambao hutumiwa na Mungu?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Mimi nawabatiza na maji ili mtubu. Lakini yule ajaye baada ya mimi ni mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye sistahili kuvichukua viatu vyake. Atawabatiza na Roho Mtakatifu, na moto" (MT 3:11).
Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe.

Jumapili, 27 Januari 2019

Have You Been Rapturned? | "Kutamani Sana" | Swahili Christian Movie

Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu aliwaahidi wafuasi Wake: "Naenda kuwatayarishia mahali. Na nikienda kuwatayarishia mahali, nitarudi tena na kuwapokea kwangu; ili mahali nipo, muweze kuwa pia" (Yohana 14:2-3). Kwa sababu ya hili, vizazi vya waumini vimeendelea kujawa na tumaini na kushikilia maombi kwa ajili ya kutimizwa kwa ahadi ya Bwana, na kutumaini na kuomba kwamba wanyakuliwe hadi kwenye mbingu ili kukutana na Bwana na kuingia katika ufalme wa mbinguni wakati Bwana atakapokuja.

Jumamosi, 26 Januari 2019

Maonyesho ya Mungu | "Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo" (sehemu ya kwanza)

Maonyesho ya Mungu | "Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo" (sehemu ya kwanza)

Mwenyezi Mungu anasema, "Ukamilifu wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii yamefanyika kulingana na hali za ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya binadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji. … Hutekeleza kazi Yake kulingana na maendeleo ya nyakati, na Anatekeleza kazi Yake nyingi zaidi halisi kulingana na mabadiliko ya mambo.

Ijumaa, 25 Januari 2019

4. Kwa nini Mungu hamtumii mwanadamu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho lakini badala yake Yeye ni lazima apate mwili na kuifanya Mwenyewe?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha
Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

4. Kwa nini Mungu hamtumii mwanadamu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho lakini badala yake Yeye ni lazima apate mwili na kuifanya Mwenyewe?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana" (YN. 5:22).
"Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu" (YN. 5:27).
Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Kazi mzima ya mpangilio wa usimamizi wa Mungu inafanywa binafsi na Mungu mwenyewe. Awamu ya kwanza—uumbaji wa ulimwengu—ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na kama haikuwa hivyo, basi hakuna yeyote ambaye angekuwa na uwezo wa kumuumba mwanadamu; awamu ya pili ilikuwa ukombozi wa wanadamu wote, na pia ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, awamu ya tatu inaenda bila kusemwa: Kuna haja kuu zaidi ya mwisho wa kazi ya Mungu kufanywa na Mungu Mwenyewe.

Alhamisi, 24 Januari 2019

Swahili Christian Video "Kutoroka Kizimba" (Crosstalk) | Christians Are Determined to Follow God

Swahili Christian Video "Kutoroka Kizimba" (Crosstalk) | Christians Are Determined to Follow God

Mazungumzo chekeshi Kutoroka Kizimbani yanaeleza hadithi ya jinsi Mkristo Xiaolan aliteswa na kufungiwa nyumbani mwao kwa mwezi mmoja na baba yake afisa wa Chama cha Kikomunisti, pale ambapo hakuweza kushiriki katika maisha ya kanisa, na uzoefu wake wa kutoroka nyumbani na kukimbia. Familia iliyokuwa na furaha ilitenganishwa, binti akamwacha mamake, na babake akawekea kisasi cha ndani dhidi yake. Ni nani aliyekuwa mbunifu mkuu? Na ni nani aliyempatia Xiaolan imani na nguvu, na kumwelekeza kutoroka kizimba na kutembea kwa njia sahihi ya maisha?

Jumatano, 23 Januari 2019

Swahili Christian Video "Macho Kila Mahali" (Mazungumzo Chekeshi) | The Means the CCP Uses to Capture Christians

Mchezo wa kuchekesha Macho Kila Mahali unaeleza jinsi Chama cha Kikomunisti cha China kinavyojaribu kuondoa dini kwa kutumia uchunguzi mkubwa kote nchini, pamoja na kuwageuza watu katika kila tabaka na kazi ya maisha kuwa macho ili kuchunguza, kusimamia, na kupeleleza Wakristo. Kupitia igizo chekeshi dhahiri, jozi hii ya mchezo wa kuigiza inatuonyesha sote mbinu zinazostahili kudharauliwa na makusudi ya kuchukiwa sana ambayo kwayo CCP kinakamata Wakristo, na wakati huohuo inatuonyesha sisi jinsi Wakristo wanavyomtegemea Mungu kukwepa jozi moja ya macho baada ya nyingine, wanavyoeneza injili, na kumshuhudia Mungu.

Jumanne, 22 Januari 2019

Maonyesho ya Mungu | "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu"

Maonyesho ya Mungu | "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu"

Mwenyezi Mungu anasema, "Sababu mwanadamu hana ufahamu wa umuhimu wa Mungu kumwokoa na umuhimu wa kazi ya usimamizi wa Mungu, na hafahamu jinsi Mungu Anavyotamani zaidi wanadamu wawe. Je, ni wanadamu mfano wa Adamu na Hawa, wasiopotoshwa na Shetani? Hapana! Usimamizi wa Mungu ni kwa ajili ya kupata kikundi cha watu ambao humwabudu Mungu na kujitoa kwake. Hawa wanadamu wamepotoshwa na Shetani, lakini hawamwoni Shetani kama baba yao: hutambua uso usiopendeza wa Shetani, na kuukataa, na kuja mbele Zake Mungu na kukubali hukumu na kuadibu Kwake.

Jumatatu, 21 Januari 2019

Swahili Christian Video "Bwana Anakuja Kwa Namna Gani Hasa?" (Mazungumzo Chekeshi) | The Son of Man Has Come to Earth

Swahili Christian Video "Bwana Anakuja Kwa Namna Gani Hasa?" (Mazungumzo Chekeshi) | The Son of Man Has Come to Earth

Katika siku za mwisho, hali ya moyo ya Wakristo wanaongoja kurudi kwa Bwana Yesu inakuwa kali sana, lakini ni kwa vipi, hasa, Bwana atarudi? Baadhi wanasema, "Bwana Yesu atakuja na mawingu." Wengine wanasema, "Unabii unaotabiri kurudi Kwake nao unasema, 'Tazama, mimi nakuja kama mwizi' (Ufu 16:15). 'Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki' (Luka 17:25). 'Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha' (Mat 25:6).

Jumapili, 20 Januari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fasiri ya Mafumbo ya Maneno ya Mungu | Sura ya 12

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fasiri ya Mafumbo ya Maneno ya Mungu | Sura ya 12

Watu wote wanapotilia maanani, wakati vitu vyote vinafanywa upya na kuhuishwa, wakati kila mtu anamtii Mungu bila shaka, na yuko tayari kubeba jukumu zito la mzigo wa Mungu—hapa ndipo wakati umeme wa mashariki unatoka, ukiangaza yote kutoka Mashariki hadi Magharibi, ukiyatisha yote ya ulimwengu na ujaji wa mwanga huu; na wakati huu, Mungu tena huanza maisha Yake mapya. Ambayo ni kusema, wakati huu Mungu huanza kazi mpya duniani, akitangaza kwa watu wa ulimwengu wote kwamba “Wakati umeme unatoka Mashariki—ambapo pia ni wakati hasa Naanza kunena—wakati umeme unakuja, mbingu yote inaangaziwa, na nyota zote zinaanza kubadilika.” Hivyo, ni wakati upi ambao umeme unatoka kutoka Mashariki? 

Jumamosi, 19 Januari 2019

The Words the Holy Spirit Says to the Churches | "Sauti Nzuri Ajabu" | Filamu za Injili

The Words the Holy Spirit Says to the Churches | "Sauti Nzuri Ajabu" | Filamu za Injili

Dong Jingxin ni mhubiri katika kanisa la nyumba nchini Uchina. Amemsadiki Bwana kwa miaka thelathini, na anapenda ukweli, mara kwa mara yeye husoma maneno ya Bwana na yanamsisimua. Anajitumia kwa ajili ya Bwana kwa shauku kubwa. Kwa sababu ya kazi yake ya kuhubiri, alikamatwa na polisi wa serikali ya Kikomunisti ya Kichina na akafungwa gerezani ambako alivumilia ukatili na mateso. Maneno ya Bwana ndiyo yaliyomwongoza kwa kustahamili miaka saba ya maisha ya gerezani yasiyokuwa ya kibinadamu .

Ijumaa, 18 Januari 2019

Maonyesho ya Mungu | "Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu"

Maonyesho ya Mungu | "Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu"

Mwenyezi Mungu anasema, "Mwanadamu hana ufahamu wa umuhimu wa Mungu kumwokoa na umuhimu wa kazi ya usimamizi wa Mungu, na hafahamu jinsi Mungu Anavyotamani zaidi wanadamu wawe. Je, ni wanadamu mfano wa Adamu na Hawa, wasiopotoshwa na Shetani? Hapana! Usimamizi wa Mungu ni kwa ajili ya kupata kikundi cha watu ambao humwabudu Mungu na kujitoa kwake.

Alhamisi, 17 Januari 2019

2. Kupata Mwili Ni Nini? Ni Nini Kiini cha Kupata Mwili?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Bwana Yesu

I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

2. Kupata Mwili Ni Nini? Ni Nini Kiini cha Kupata Mwili?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli" (YN. 1:14).
"Mimi ndiye njia, ukweli na uhai" (YN. 14:6).
"Yesu akasema kwake, nimekuwa nanyi kwa muda mrefu, na bado hujanijua, Filipo? Yeye ambaye ameniona amemwona Baba; na unasemaje basi, Tuonyeshe Baba? Huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi? Maneno ninenayo kwenu sineni juu yangu, ila Baba aishiye ndani yangu, anazifanya kazi hizo. Niamini kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi, la sivyo niamini kwa ajili ya kazi hizo" (YN. 14:9-11).

Jumatano, 16 Januari 2019

Maonyesho ya Mungu | "Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu"

Maonyesho ya Mungu | "Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu"

Mwenyezi Mungu anasema, "Kuamini katika Mungu na kutafuta maarifa ya Mungu si jambo rahisi. Hayawezi kupatikana kwa kukusanyika pamoja na kusikiliza mahubiri, na huwezi kukamilishwa kwa kupenda tu. Lazima upitie uzoefu, na ujue, na kuongozwa na kanuni katika matendo yako, na kupata kazi za Roho Mtakatifu. Utakapopitia katika uzoefu, utakuwa na uwezo wa kutofautisha mambo mengi—utakuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya jema na baya, kati ya haki na uovu, kati ya kile ambacho ni cha mwili na damu na kile ambacho ni cha kweli.

Jumanne, 15 Januari 2019

I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yesu

1. Bwana Yesu Mwenyewe alitabiri ya kwamba Mungu angepata mwili katika siku za mwisho na kuonekana kama Mwana wa Adamu ili kufanya kazi.

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja" (LK. 12:40).
"Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki" (LK. 17:24-25).
"Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha" (MT. 25:6).

Jumatatu, 14 Januari 2019

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Fasiri ya Mafumbo ya Maneno ya Mungu | Nyongeza ya 2: Sura ya 2

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Fasiri ya Mafumbo ya Maneno ya Mungu | Nyongeza ya 2: Sura ya 2

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wanapomwona Mungu wa vitendo, wanapoishi maisha yao binafsi na, wanapotembea sako kwa bako na, na wanapoishi na Mungu Mwenyewe, wao huweka kando udadisi ambao umekuwa ndani ya mioyo yao kwa miaka mingi sana. Ufahamu wa Mungu uliozungumziwa awali ni hatua ya kwanza tu; ingawa watu wana ufahamu wa Mungu, bado kuna mashaka mengi ya kuchagiza ndani ya mioyo yao: Mungu alitoka wapi?

Jumapili, 13 Januari 2019

Mashahidi wa Kristo wa Siku za Mwisho | Dibaji

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mashahidi wa Kristo wa Siku za Mwisho | Dibaji

Katika mwaka wa 1991, Mwenyezi Mungu mwenye mwili alionekana na kuanza kufanya kazi nchini China. Ameonyesha maneno milioni kadhaa, na amekuwa akifanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho akianzia na nyumba ya Mungu. Amehitimisha Enzi ya Neema, akaanza Enzi ya Ufalme, na akaanzisha injili ya ufikaji wa ufalme wa mbinguni.

Jumamosi, 12 Januari 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?"

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?"

Mwenyezi Mungu anasema, "Hata ingawa wamenusurika mpaka siku hii, ni nani angefikiri kuwa wamepewa sumu na yule mwovu kwa muda mrefu? Je, umesahau kuwa wewe ni mmoja wa waathiriwa? Kwa ajili ya upendo wako kwa Mungu, una nia ya kufanya kila uwezalo kuwaokoa walionusurika? Je, huna nia , ya kutumia nguvu zako zote kulipiza Mungu anayempenda binadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe? Unaitafsiri vipi hali ya kutumiwa na Mungu kuishi maisha yako yasiyo ya kawaida? Je, unao kweli uamuzi na matumaini ya kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana ya mtu mcha Mungu anayemtumikia Mungu?"

Ijumaa, 11 Januari 2019

Swahili Christian Variety Show | "Mchungaji wetu alisema …" (Mazungumzo Chekeshi)

Swahili Christian Variety Show | "Mchungaji wetu alisema …" (Mazungumzo Chekeshi)

Yu Shunfu ni muumini katika ulimwengu wa dini ambaye huenzi na huabudu wachungaji na wazee wa kanisa. Yeye hufikiri "wachungaji na wazee wa kanisa wote walikuzwa na Mungu, na kutii wachungaji na wazee wa kanisa ni kutii Mungu, "kwa hivyo yeye humsikiza mchungaji wake katika yote anayofanya, hata katika mambo ya kukaribisha kuja kwake Bwana.

Alhamisi, 10 Januari 2019

Mchezo Mfupi wa Kuchekesha "Kukusanyika katika Zizi la Ng'ombe" | A Horrible Experience in a Meeting

Kwa sasa, mateso ya Wakristo ya serikali inayomkana Mungu ya CCP yanaongezeka kila siku. Waumini wanakabiliwa na kizuizi kwa kutenda imani yao mara kwa mara; hata hawawezi kupata pahali pa kukutana kwa amani. Bila chaguo jingine, Liu Xiumin anaweza tu kutayarisha mkutano na ndugu katika zizi lake la ng'ombe. Lakini wakati wanapokutana, makada wa kijiji wanakuja mmoja baada ya mwingine kuangalia kila pahali, wakitoa visingizio mbalimbali, na kisha hata kuwaleta polisi wa CCP ndani.... Je, Liu Xiumin na ndugu zake wataweza kufanikiwa kufanya mkutano wao? Je, watagunduliwa?

Jumatano, 9 Januari 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" (Official Video)

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" (Official Video)

Mwenyezi Mungu anasema, "Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu.

Jumanne, 8 Januari 2019

Swahili Christian Movie "Ujinga Angamizi" | Why Can’t Foolish Virgins Enter the Kingdom of Heaven?

Swahili Christian Movie "Ujinga Angamizi" | Why Can’t Foolish Virgins Enter the Kingdom of Heaven?

Zheng Mu'en ni mfanyakazi mwenza katika kanisa la Kikristo nchini Marekani, amemwamini Bwana kwa miaka mingi, na anafanya kazi kwa bidii na humtumia Bwana. Siku moja, shangazi yake anashuhudia kwake kwamba Bwana Yesu amerudi kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya kumhukumu na kumtakasa mtu katika siku za mwisho, habari ambazo zinampendeza sana.

Jumatatu, 7 Januari 2019

Wimbo wa Maneno ya Mungu | "Jinsi ya Kujua Kuonekana na Kazi ya Kristo wa Siku za Mwisho"


Wimbo wa Maneno ya Mungu | "Jinsi ya Kujua Kuonekana na Kazi ya Kristo wa Siku za Mwisho"

I
Mwili wa Mungu utajumlisha kiini cha Mungu na maonyesho Yake.
Atakapofanywa mwili, Ataleta matunda ya kazi Aliyopewa
ajidhihirishe na Alete Ukweli kwa wote,
awape uhai na awaonyeshe njia.
Mwili wowote usiokuwa na dutu Yake sio Mwili wa Mungu.

Jumapili, 6 Januari 2019

Swahili Christian Skit | "Polisi Waenda kwa Ziara ya Mwaka Mpya" (Kichekesho)

Zheng Xinming, mwanamume mzee wa karibu miaka sabini, ni Mkristo wa dhati. Kwa sababu ya imani yake katika Bwana, aliwekwa kizuizini na kufungwa gerezani, na kuhukumiwa miaka nane. Alipoachiliwa, bado alikuwa ameorodheshwa na Polisi wa Kikomunisti wa China kama mlengwa wa ufuatiliaji wa kuzingatiwa. Hasa, baada ya mzee huyo kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, polisi walikuja karibu kila siku kumtisha, kumuogofya na kumsumbua.

Jumamosi, 5 Januari 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu"

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu"

Mwenyezi Mungu anasema, "Kama huelewi tabia ya Mungu, basi itakuwa haiwezekani kwako wewe kufanya kazi unayofaa kumfanyia. Kama hujui dutu ya Mungu, ndivyo pia haitawezekana kubakiza hali ya kumcha na kumwogopa Yeye, utakuwa ni uzembe na kuepuka kusema ukweli wote kwa kutojali, na zaidi, kukufuru kusikorekebishika. Kuelewa tabia ya Mungu kwa kweli ni muhimu sana, na maarifa ya dutu ya Mungu hayawezi kupuuzwa, ilhali hakuna yeyote amewahi kuchunguza kwa umakinifu au kudadisi suala hili.

Ijumaa, 4 Januari 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Waovu Lazima Waadhibiwe"

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Waovu Lazima Waadhibiwe" (Official Video)

Mwenyezi Mungu anasema, "Mwanadamu kila wakati huamini kuwa Mungu habalidiliki na humfafanua kulingana na Bibilia, kana kwamba mwanadamu ameona ndani ya usimamizi wa Mungu, kana kwamba kila kitu Atendacho Mungu kiko mikononi mwa mwanadamu. Wanadamu ni wa kufanya mzaha pakubwa, wana kiburi kikubwa sana, na wote wana kipaji cha lugha ya kushawishi ya kujivuna.

Alhamisi, 3 Januari 2019

Best Swahili Christian Music Video 2018 "Upendo kwa Mungu" | The Love of God Never Leaves Us

Best Swahili Christian Music Video 2018 "Upendo kwa Mungu" | The Love of God Never Leaves Us

I
Ee Bwana,
Nimefurahia nyingi ya neema Yako.
Kwa nini mimi daima huhisi tupu ndani?
Je, sijapata ukweli na uzima?
II
Kusoma maneno haya kunaweza kuyajibu maswali yako.
"Kristo wa siku za mwisho huleta uzima,
na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele.
Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima,
na njia pekee ambayo
mtu atajua Mungu na kuidhinishwa na Mungu.

Jumatano, 2 Januari 2019

Video za Kikristo "Kuamka Kutoka kwa Ndoto" | Kufichua Fumbo la Kuingia katika Ufalme wa Mbinguni

Video za Kikristo "Kuamka Kutoka kwa Ndoto" | Kufichua Fumbo la Kuingia katika Ufalme wa Mbinguni

Kama wafuasi wengi wa Bwana Yesu, Yu Fan aliangazia kuhusu kusoma Biblia, akaacha kila kitu ili kulipa gharama ya kuteseka kwa ajili ya Bwana, na akatafuta kumtumikia Bwana kwa ari. Alifikiri kuwa kwa kufuata imani yake kwa jinsi hii, Bwana atakaporudi bila shaka atanyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni.

Jumanne, 1 Januari 2019

Wimbo wa Maneno ya Mungu "Mamlaka na Nguvu Anayoonyesha Mungu Anapopata Mwili"

Wimbo wa Maneno ya Mungu "Mamlaka na Nguvu Anayoonyesha Mungu Anapopata Mwili"

I
Mungu alikuja duniani hasa kutimiza ukweli wa "Neno kuwa mwili."
(tofauti na Agano la Kale, katika siku za Musa,
Mungu alizingumza moja kwa moja kutoka mbinguni).
Kisha, yote yatatimizwa katika enzi ya Ufalme wa Milenia
kuwa ukweli ambao watu wanaweza kuona,
ili watu waweze kuona utimizaji hasa kwa macho yao wenyewe.
Hii ni maana ya kina ya Mungu kuwa mwili.
Yaani, kazi ya Roho imekamilika kupitia kwa mwili na neno.
Hii ni maana ya kweli ya "Neno kuwa mwili, Neno kuonekana katika mwili."