Alhamisi, 10 Januari 2019

Mchezo Mfupi wa Kuchekesha "Kukusanyika katika Zizi la Ng'ombe" | A Horrible Experience in a Meeting

Kwa sasa, mateso ya Wakristo ya serikali inayomkana Mungu ya CCP yanaongezeka kila siku. Waumini wanakabiliwa na kizuizi kwa kutenda imani yao mara kwa mara; hata hawawezi kupata pahali pa kukutana kwa amani. Bila chaguo jingine, Liu Xiumin anaweza tu kutayarisha mkutano na ndugu katika zizi lake la ng'ombe. Lakini wakati wanapokutana, makada wa kijiji wanakuja mmoja baada ya mwingine kuangalia kila pahali, wakitoa visingizio mbalimbali, na kisha hata kuwaleta polisi wa CCP ndani.... Je, Liu Xiumin na ndugu zake wataweza kufanikiwa kufanya mkutano wao? Je, watagunduliwa? Je, watakamatwa? Mchezo huu mfupi wa kuchekesha Kukusanyika katika Zizi la Ng'ombe unakufichulia jinsi Wakristo katika China wanaweza kushikilia katika imani yao chini ya mateso ya serikali ya CCP.
Aya za Biblia za Kurejelea:
Bwana Yesu alisema, "Kwa maana atakayeyaokoa maisha yake, atayapoteza: na yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa sababu yangu atayapata." (Mathayo 16:25)
Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, "Wale wanaoitwa washindi na Mungu ni wale ambao bado wanaweza kusimama kama mashahidi, wakidumisha imani yao, na ibada yao kwa Mungu wanapokuwa chini ya ushawishi wa Shetani na kuzingirwa na Shetani, hiyo ni, wanapokuwa katika nguvu za giza. Kama bado unaweza kudumisha moyo wa utakaso na upendo wako wa kweli kwa Mungu kwa vyovyote vile, unasimama shahidi mbele ya Mungu, na hii ndio Mungu Anaita kuwa mshindi."
kutoka kwa “Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni