I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu
9. Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?
Aya za Biblia za Kurejelea:
"Na itatimia katika siku za mwisho, kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utawekwa imara juu ya milima, na utainuliwa juu zaidi ya vilima; na mataifa yote yatamiminika kwenda kwake. Na watu wengi wataenda na kusema, Njoo, na hebu twende juu ya mlima wa Yehova, kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo; na atatufunza kuhusu njia zake, nasi tutatembea kwa njia zake: kwani sheria itatoka Zayuni, na neno la Mungu litatoka Yerusalemu. Naye atahukumu miongoni mwa mataifa, na atawakemea watu wengi: nao wata, nao watafua panga zao ili ziwe majembe, na mikuki yao ili iwe mundu: hakuna taifa litakaloinua upanga dhidi ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena. Enyi wa nyumba ya Yakobo, njooni, tutembee katika nuru ya Yehova" (ISA 2:2-5).
Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Ujio wa Mungu katika mwili wa siku za mwisho umehitimisha Enzi ya Neema. Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, kutumia maneno ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, kumwangazia na kumpa nuru mwanadamu, na kumwondoa Mungu asiye yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii sio hatua ya kazi ambayo Yesu Aliifanya Alipokuja. Yesu Alipokuja, Alifanya miujiza mingi, Aliponya wagonjwa na kutoa mapepo, na Alifanya kazi ya wokovu ya msalaba. Na matokeo yake ni kwamba, katika dhana za mwanadamu, mwanadamu anaamini kwamba hivi ndivyo Mungu Anapaswa kuwa. Maana Yesu Alipokuja, hakufanya kazi ya kuondoa taswira ya Mungu asiye yakini moyoni mwa mwanadamu; Alipokuja, Alisulubishwa, Aliponya wagonjwa na kutoa mapepo, na Alieneza injili ya ufalme wa mbinguni. Kwa upande mmoja, Mungu katika mwili katika siku za mwisho Anaondoa nafasi iliyochukuliwa na Mungu asiye yakini katika dhana za mwanadamu, ili taswira ya Mungu asiye yakini isiwepo kabisa katika moyo wa mwanadamu. Kwa kutumia maneno Yake halisi na kazi Yake halisi, Anazunguka katika nchi zote, na kazi Anayoifanya miongoni mwa wanadamu ni halisi kabisa na ya kawaida, kana kwamba mwanadamu anakuja kujua uhalisia wa Mungu na Mungu asiye yakini Anapoteza nafasi Yake moyoni mwake. Kwa upande mwingine, Mungu Anatumia maneno yaliyozungumzwa na mwili Wake ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, na kukamilisha vitu vyote. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu Ataikamilisha wakati wa siku za mwisho.
kutoka kwa "Kuijua Kazi ya Mungu Leo" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni leo tu, Nikujapo binafsi miongoni mwa mwanadamu na kuongea maneno Yangu, ndipo mwanadamu anapata maarifa kidogo kunihusu, kutoa nafasi "Yangu" ndani ya mawazo yao, badala yake kutengeneza mahali pa Mungu wa vitendo ndani ya fahamu zake. Mwanadamu ana dhana na amejawa na udadisi; ni nani ambaye hangetaka kumwona Mungu? Ni nani ambaye hangetamani kukutana na Mungu? Lakini bado kitu pekee kilicho na nafasi ya uhakika ndani ya moyo wa mwanadamu ni Mungu ambaye mwanadamu anahisi kuwa dhahania na asiye dhahiri. Nani angetambua haya kama Singewaeleza wazi? Nani angeamini kwa kweli Mimi nipo? Kwa hakika bila shaka yoyote? Kuna tofauti kubwa kati ya "Mimi" aliye ndani ya mwanadamu na "Mimi" wa ukweli, na hakuna anayeweza kuwalinganisha. Nisingekuwa mwili, mwanadamu hangewahi Nijua, na hata angekuja kunijua, je, maarifa kama hayo bado hayangekuwa dhana? …
… Kwa sababu mwanadamu amejaribiwa na kupotoshwa na Shetani, kwa sababu amechukuliwa na kufikiria kwa dhana, Nimekuwa mwili ili kuwashinda binafsi wanadamu wote, kufichua dhana zote za mwanadamu, na kupasua mawazo ya mwanadamu. Matokeo yake ni kuwa mwanadamu hajionyeshi mbele Yangu tena, na hanitumikii tena akitumia dhana zake mwenyewe, na hivyo, "Mimi" katika dhana za mwanadamu ameondoka kabisa.
kutoka kwa "Tamko la Kumi na Moja" la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika ujenzi wa ufalme Ninatenda moja kwa moja katika hali ya uungu Wangu, na kuruhusu watu wote kujua kile Nilicho nacho na nilicho nimejiweka msingi juu ya maarifa ya maneno Yangu, hatimaye kuwaruhusu kupata ufahamu Wangu Mimi Niliye katika mwili. Hivyo hukomesha harakati zote za wanadamu kutafuta Mungu asiye dhahiri, na hukomesha nafasi ya "Mungu mbinguni" katika moyo wa mwanadamu, ambayo ni kusema, unaruhusu mwanadamu kujua matendo Yangu katika mwili Wangu, na hivyo unahitimisha wakati Wangu duniani.
kutoka kwa "Tamko la Nane" la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa wale wote ambao wanaishi katika mwili, kubadilisha silika zao kunahitaji kuwe na malengo ya kufuata, na kumjua Mungu kunahitaji kushuhudia matendo halisi na sura halisi ya Mungu. Yote haya yanaweza kufikiwa tu na Mungu mwenye mwili, na yote yanaweza kukamilishwa na mwili wa kawaida na halisi. Hii ndiyo maana kufanyika mwili ni muhimu, na kwa nini kunahitajika na wanadamu wote wapotovu. Kwa kuwa watu wanahitajika kumjua Mungu, taswira za Mungu wa kufikirika na wa kimiujiza inapaswa iondolewe kutoka katika mioyo yao, na kwa kuwa wanahitajika kutupilia mbali silika yao iliyopotoka, kwanza wanapaswa kujua silika yao iliyopotoka. Ikiwa mwanadamu anafanya kazi ili kuondoa taswira za Miungu wasio dhahiri kutoka katika mioyo ya watu, basi atashindwa kupata matokeo sahihi. Taswira za Miungu wasio dhahiri katika mioyo ya watu haziwezi kuwekwa hadharani, kutupwa, au kufukuzwa kabisa kwa maneno pekee. Kwa kufanya hivyo, mwisho wake haitawezekana kuondoa vitu hivi vilivyokita mizizi kwa watu. Ni Mungu anayeonekana tu na mwenye taswira halisi ya Mungu ndiyo inayoweza kuchukua nafasi ya vitu hivi visivyo dhahiri na vya kimiujiza ili kuwaruhusu watu kuvielewa taratibu, na ni kwa njia hii pekee ndipo matokeo mazuri yanaweza kupatikana. Mwanadamu anatambua kwamba Mungu aliyekuwa anamtafuta huko nyuma ni asiye dhahiri na wa kimiujiza. Kile ambacho kinaweza kufanikiwa hapa sio uongozi wa moja kwa moja wa Roho, na wala sio mafundisho ya mtu fulani, bali ni Mungu mwenye mwili. Mitazamo ya mwanadamu inakuwa wazi pale ambapo Mungu mwenye mwili atafanya kazi Yake rasmi, kwa sababu ukawaida na uhalisi wa Mungu mwenye mwili ni kinyume na nadharia za Mungu asiye dhahiri na wa kufikirika katika fikra za mwanadamu. Mitazamo asilia ya mwanadamu inaweza tu kudhihirishwa kupitia tofauti zao na Mungu mwenye mwili. Bila ulinganisho na Mungu mwenye mwili, mitazamo ya mwanadamu isingefunuliwa; kwa maneno mengine, bila tofauti ya uhalisi vitu visivyo dhahiri visingefunuliwa. Hakuna anayeweza kutumia maneno ili kufanya kazi hii, na hakuna anayeweza kuizungumzia kazi hii kwa kutumia maneno. Ni Mungu Mwenyewe Pekee Ndiye anayeweza kufanya kazi Yake, na hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya kazi hii kwa niaba Yake. Haijalishi lugha ya mwanadamu ni pevu kiasi gani, hawezi kuzungumzia uhalisi na ukawaida wa Mungu. Mwanadamu anaweza kumjua Mungu zaidi kwa matendo, na anaweza kumwona kwa uwazi ziadi, ikiwa Mungu anafanya kazi miongoni mwanadamu na anaonyesha kikamilifu sura Yake na uungu Wake. Athari hizi haziwezi kupatwa na mwanadamu yeyote yule mwenye mwili. Bila shaka, Roho wa Mungu pia hawezi kupata matokeo haya.
kutoka kwa "Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati Mungu anapofanya kazi katika mwili wake, wale wanaofuata wanakuwa hawatafuti tena vitu hivyo visivyo yakini, na wanaacha kukisia mapenzi ya Munguasiye yakini. ... Mwanadamu hawezi kumgusa Roho, na wala hawezi kumwona, na kazi ya Roho haiwezi kuacha ushahidi au ukweli wowote zaidi wa kazi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu kamwe hataweza kuuona uso halisi wa Mungu, na siku zote ataamini katika Mungu asiye yakini ambaye hayupo. Mwanadamu hataweza kuutazama uso wa Mungu, hataweza kusikia maneno yaliyozungumzwa na Mungu moja kwa moja. Hata hivyo picha anazozijenga mwanadamu kumhusu Mungu, sio halisi na haziwezi kuchukua nafasi ya uso halisi wa Mungu; silika ya asili ya Mungu, na kazi ya Mungu Mwenyewe haiwezi kuigizwa na mwanadamu. Mungu wa mbinguni asiyeonekena na kazi Yake inaweza kuletwa tu duniani na Mungu mwenye mwili ambaye Yeye binafsi anafanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Hii ndiyo njia halisi ambayo Mungu anaonekana kwa mwanadamu, ambayo kwayo mwanadamu anamwangalia Mungu na kuujua uso wa kweli wa Mungu, na haiwezi kufanikishwa na Mungu asiyekuwa katika mwili.
kutoka kwa "Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wote watakapokuwa na ufahamu mkubwa zaidi kuhusu Mimi baada ya kukubali matamshi Yangu ni wakati ambapo watu Wangu kuishi kulingana na Mimi, ni wakati ambapo kazi Yangu katika mwili imekamilika, na wakati ambapo uungu Wangu unaishi kwa kudhihirishwa kabisa katika mwili. Wakati huu, watu wote watajaribu kunijua Mimi katika mwili, na kweli wataweza kusema kwamba Mungu huonekana katika mwili, na hili litakuwa ndilo tunda. ... Hatimaye, watu wa Mungu wataweza kumpatia Mungu sifa ambayo ni ya kweli, si ya kulazimishwa, na ambayo inatoka mioyoni mwao. Hiki ndicho kipo katika kiini cha mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka 6,000. Yaani, ni udhihirisho wa mpango huu wa usimamizi wa miaka 6,000: kuwafanya watu wote kujua umuhimu wa kupata mwili kwa Mungu—kuwafanya kumjua Mungu kupata mwili kwa vitendo, ambayo ni kusema, matendo ya Mungu katika mwili—ili kwamba wamkane Mungu asiye yakini, na kumjua Mungu ambaye ni wa leo na pia wa jana, na zaidi ya hilo, Mungu wa kesho, ambaye kwa kweli Ameishi toka milele hadi milele. Ni baada ya hapo tu, ndipo Mungu ataingia pumzikoni!
kutoka kwa "Ufafanuzi wa Tamko la Tatu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kitu kizuri kuhusu kazi Yake katika mwili ni kwamba anaweza kuacha maneno sahihi na ya kusihi, na mapenzi Yake kwa mwanadamu kwa wale wanaomfuata, ili kwamba hapo baadaye wafuasi wake waweze kueneza kazi Yake yote katika mwili kwa usahihi zaidi na kwa udhabiti na mapenzi Yake kwa wanadamu wote kwa wanaoikubali njia hii. Ni kazi ya Mungu mwenye mwili pekee miongoni mwa wanadamu ndiyo inayokamilisha ukweli wa Mungu kuwa na kuishi pamoja na mwanadamu. Ni kazi hii pekee ndiyo inayotimiza shauku ya mwanadamu kuutazama uso wa Mungu, kushuhudia kazi ya Mungu, na kusikia neno la Mungu. Mungu mwenye mwili anahitimisha enzi ambayo Yehova alionekana mgongo tu, na pia anahitimisha enzi ya mwanadamu kuamini katika Mungu asiye dhahiri. Kwa umahususi, kazi ya Mungu mwenye mwili wa mwisho inawaleta wanadamu wote katika enzi ambayo ni halisi zaidi, ya matendo zaidi na nzuri zaidi. Hahitimishi tu enzi ya sheria na mafundisho ya kidini; la umuhimu zaidi, anamfunulia mwamadamu Mungu ambaye ni halisia na wa kawaida ambaye ni mwenye haki na mtakatifu, ambaye anafungua kazi ya mpango wa usimamizi na kuonesha siri za hatma ya mwanadamu, ambaye alimuumba mwanadamu na kuhitimisha kazi ya usimamizi, na ambaye amebakia sirini kwa maelfu ya miaka. Anaihitimisha enzi ya Mungu asiye yakini, anaihitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanatamani kuutafuta uso wa Mungu lakini wanashindwa, anahitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanamtumikia Shetani, na anawaongoza wanadamu wote katika enzi mpya kabisa. Haya yote ni matokeo ya Mungu mwenye mwili badala ya Roho wa Mungu.
kutoka kwa "Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu Anakuja miongoni mwa wanadamu siku ya leo kwa kusudi la kubadilisha mawazo na roho zao, na taswira ya Mungu katika mioyo yao ambayo wamekuwa nayo kwa maelfu ya miaka. Kupitia fursa hii, Atamfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Yaani, kupitia maarifa ya mwanadamu, Atabadilisha namna wanavyomfahamu na mitazamo yao Kwake, ili kwamba maarifa yao juu ya Mungu, yaweze kuanza katika rekodi safi, na mioyo yao itakuwa imesafishwa upya na kubadilishwa. Kushughulika na nidhamu ni njia, na ushindi na kufanya upya ni malengo. Kuondoa mawazo ya kishirikina aliyonayo mwanadamu kuhusu Mungu asiye dhahiri ndilo limekuwa kusudi la Mungu milele, na hivi karibuni limekuwa suala la haraka kwake. Ni matumaini Yangu kwamba watu wote watalifikiria hili zaidi.
kutoka kwa "Kazi na Kuingia (7)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kimsingi, Ujio wa Mungu katika mwili ni kuwawezesha watu kuona matendo halisi ya Mungu, kumfanya Roho asiye na umbo kuwa bayana katika mwili, na kuwapa watu fursa ya kumwona na kumgusa. Kwa njia hii, wanaokamilishwa Naye wataishi kwa kumfuata Yeye, watamfaidi na kuupendeza moyo Wake. Mungu angalinena kutoka mbinguni tu, na hakika asije duniani, basi bado watu hawangeweza kumjua, wangeweza tu kuyahubiri matendo ya Mungu kwa kutumia nadharia tupu, na hawangekuwa na maneno ya Mungu kama uhalisi. Mungu amekuja duniani kimsingi kuwa mfano na kielelezo kwa wale ambao wamepatwa na Mungu; ni kwa njia hii pekee ndio watu wanaweza kumjua Mungu kwa hakika, na kumgusa Mungu, na kumwona, na hapo ndipo wanaweza kupatikana na Mungu kwa kweli.
kutoka kwa "Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwanadamu atakuwa hana asili ya kutenda dhambi baada ya kusafishwa, kwa sababu Mungu atakuwa amemshinda Shetani, ambayo ina maana kuwa hakutakuwepo na kuvamiwa na vikosi vya uhasama, na hakuna vikosi vya uhasama ambavyo vinaweza kushambulia mwili wa mwanadamu. Na kwa hivyo mwanadamu atakuwa huru, na mtakatifu—yeye atakuwa ameingia ahera. Ni kama tu vikosi vya uhasama wa giza vitakuwa vimefungwa ndipo mwanadamu atakuwa huru kokote aendako, na bila uasi au upinzani. Shetani ni sharti awe amefungwa ili mwanadamu awe sawa; leo, hayuko sawa kwa sababu[a] Shetani bado huchochea shida kila mahali hapa duniani, na kwa sababu kazi nzima ya usimamizi wa Mungu bado haijafika mwisho wake. Punde tu shetani anaposhindwa, mwanadamu atakuwa amekombolewa kikamilifu; wakati mwanadamu anampata Mungu na anatoka katika kumilikiwa na Shetani, atatazama jua ya haki. Maisha atakayolipwa mwanadamu wa kawaida yatarejeshwa; yote yale ambayo ni lazima yamilikiwe na mwanadamu wa kawaida—kama uwezo wa kupambanua mema na mabaya, na kufahamu jinsi ya kula na kujivisha mwenyewe, na uwezo wa kuishi kama kawaida—yote haya yatarejeshwa. Hata kama Hawa hakuwa amejaribiwa na nyoka, mwanadamu ni lazima angekuwa na maisha kama haya ambayo ni ya kawaida baada ya kuumbwa hapo mwanzo. Ni lazima angekula, angevishwa, na kuendelea na maisha ya mwanadamu wa kawaida hapa duniani. Ila baada ya mwanadamu kupotoshwa, maisha haya yakakuwa ndoto, na hata leo mwanadamu hathubutu kufikiri mambo kama haya. Kwa kweli, maisha haya ya kupendeza ambayo mwanadamu anatamani ni haja yake: Iwapo mwanadamu angekuwa hana hatima kama hii, basi maisha yake ya duniani yaliyopotoshwa kamwe hayangekoma, na kama hakungekuwepo na maisha yakupendeza kama haya, basi hakungekuwa na hitimisho la majaliwa ya Shetani au kwa enzi ambayo Shetani ana utawala duniani kote. Mwanadamu ni sharti awasili kwenye ufalme ambao huwezi kufikiwa na nguvu za giza, na wakati atawasili, hii itathibitisha ya kwamba Shetani amekwisha shindwa. Kwa njia hii, punde tu hakuna usumbufu wa Shetani, Mungu mwenyewe atamdhibiti mwanadamu, na Yeye ataamuru na kudhibiti maisha yote ya mwanadamu; hii tu ndiyo itahesabika kama kushindwa kwa Shetani.
kutoka kwa "Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kufuatia kukamilika kwa maneno Yangu, ufalme utaumbwa duniani hatua kwa hatua na mwanadamu atarudishwa kwa ukawaida hatua kwa hatua, na hivyo basi kutaanzishwa duniani ufalme ndani ya moyo Wangu. Katika ufalme, watu wote wa Mungu hupata tena maisha ya mwanadamu wa kawaida. Msimu wa barafu yenye baridi kali umeenda, umebadilishwa na dunia ya miji ya majira ya chipuko, ambapo majira ya chipuko yanashuhudiwa mwaka mzima. Kamwe, watu hawakumbwi tena na ulimwengu wa mwanadamu wenye huzuni na wenye taabu, na hawavumilii kuishi kwenye baridi kali ya dunia ya mwanadamu. Watu hawapigani na wenzao, mataifa hayaendi vitani dhidi ya wenzao, hakuna tena uharibifu na damu imwagikayo kutokana na uharibifu huo; maeneo yote yamejawa na furaha, na kila mahali pote panafurikwa na joto baina ya wanadamu. Naenda Nikipitia dunia nzima, Nafurahia kutoka juu ya kiti Changu cha enzi, Naishi miongoni mwa nyota. Na malaika Wananipa nyimbo mpya na dansi mpya. Udhaifu wao hausababishi machozi kutiririka nyusoni mwao tena. Sisikii tena, mbele Yangu, sauti za malaika wakilia, na kamwe hakuna tena anayenung’unika kuwa ana shida Kwangu.
kutoka kwa "Tamko la Ishirini" la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati ambapo watu wote watakuwa wamefanywa kamili na mataifa yote ya dunia kugeuka kuwa ufalme wa Kristo, basi huo utakuwa wakati ambapo radi saba zitanguruma. Siku ya sasa ni hatua ndefu ya kwenda mbele katika mwelekeo wa hatua hiyo, shambulio limeachiliwa huru kwa muda ujao. Huu ni mpango wa Mungu—hivi karibuni utafanikishwa. Hata hivyo, Mungu tayari amefanikisha yote ambayo Amesema. Hivyo, ni dhahiri kwamba mataifa ya dunia ni makasri tu yaliyo mchangani yanayotetemeka bamvua linapokaribia: Siku ya mwisho iko karibu sana na joka kubwa jekundu litaanguka chini ya neno la Mungu. Ili kuhakikisha kwamba mpango wa Mungu unatekelezwa kwa ufanisi, malaika wa mbinguni wameshuka juu ya dunia, wakifanya kila wanaloweza kumridhisha Mungu. Mungu Mwenyewe mwenye mwili Amejipanga katika uwanja wa vita kupigana na adui. Po pote ambapo Aliyepata mwili huonekana, adui anaangamiziwa mahali hapo. Uchina ni ya kwanza kuangamizwa, kuharibiwa kabisa kwa mkono wa Mungu. Mungu haipi Uchina upande wowote kabisa. Thibitisho la kuendelea kuanguka kwa joka kubwa jekundu linaweza kuonekana katika ukomavu wa watu unaoendelea. Hili linaweza kuonekana wazi na mtu yeyote. Ukomavu wa watu ni ishara ya kifo cha adui. Huu ni ufafanuzi kidogo wa kile kinachomaanishwa na "kufanya vita."
kutoka kwa "Ufafanuzi wa Tamko la Kumi" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi hii lazima itekelezwe kwa njia ya Mungu kusababisha mabaa mbalimbali duniani. Lakini Mungu hataonekana; kwa sababu, wakati huu, nchi ya joka kubwa jekundu bado itakuwa ni nchi ya uchafu, Mungu hataonekana, lakini ataibuka tu kwa njia ya kuadibu. Hiyo ndiyo tabia ya Mungu yenye haki, na hakuna anayeweza kuiepuka. Katika wakati huu, vyote vinavyoishi katika taifa la joka kubwa jekundu vitapitia maafa, ambavyo kwa kawaida ni pamoja na ufalme ulio duniani (kanisa). Huu ndio hasa wakati ambao ukweli hujitokeza, na kwa hiyo unapitiwa na watu wote, na hakuna anayeweza kuepuka. Hili limejaaliwa na Mungu. Ni kwa sababu ya hatua hii ya kazi hasa ndio Mungu asema, "Huu ndio wakati wa mtu kutumia vizuri sana vipaji vyake." Kwa sababu, katika siku za baadaye, hakutakuwa na kanisa duniani, na kwa ajili ya majilio ya machafuko, watu hawawezi kufikiria kuhusu kitu chochote kingine, na ni vigumu kwao kumfurahia Mungu katikati ya machafuko, hivyo, watu wanatakiwa kumpenda Mungu kwa moyo wao wote katika wakati huu wa ajabu, ili wasikose nafasi. Ukweli huu unapopita, Mungu amelishinda kabisa joka kubwa jekundu, na hivyo kazi ya ushuhuda wa watu wa Mungu imefika mwisho; baadaye Mungu ataanza hatua inayofuata ya kazi, Akifanya uharibifu kwa nchi ya joka kubwa jekundu, na hatimaye kuwagongomelea watu juu chini msalabani kotekote katika ulimwengu, baadaye Atawaangamiza wanadamu wote—hizi ni hatua za siku za baadaye za kazi ya Mungu.
kutoka kwa "Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini na Mbili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Nichukuapo kirasmi mamlaka Yangu na kutawala kama Mfalme katika ufalme, watu Wangu wote watakamilishwa na Mimi baada ya muda. Wakati mataifa yote ya dunia yatavurugwa, hapo ndipo hasa ufalme Wangu utaanzishwa na kupata umbo na pia Nitabadilika na kurejea kwa ulimwengu mzima. Wakati huo, watu wote watauona uso Wangu tukufu, watauona uso Wangu wa kweli.
kutoka kwa "Tamko la Kumi na Nne" la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati mataifa na watu wa dunia watakaporudi mbele ya kiti Changu cha enzi, basi Nitachukua fadhila ya mbinguni na kuiweka kwa sababu ya ulimwengu wa binadamu, ili, kwa mujibu Wangu, itajazwa na fadhila isiyo ya kufananisha. Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikipitisha wazi amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayeyakiuka:
Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa viwango tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Ubinadamu wote utafuata aina yake, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.
kutoka kwa "Tamko la Ishirini na Sita" la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Tanbihi:
a. Maandishi ya asilia yanasoma "leo, ni kwa sababu."
kutoka katika Mashahidi wa Kristo wa Siku za Mwisho
Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? , Maswali na Majibu ya Injili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni