Maneno ya Roho Mtakatifu | “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” (Sehemu ya Kwanza)
Mwenyezi Mungu anasema, "Kazi Aifanyayo Mungu ni kwa ajili ya wanadamu wote na mawazo Yake daima ni mema. Kwa mwanadamu, kwa hivyo, kazi ya Mungu na mawazo ya Mungu kwa mwanadamu (yaani mapenzi ya Mungu) ni “maono” ambayo yanafaa kutambuliwa na mwanadamu. Maono kama hayo pia ni usimamizi wa Mungu, na kazi ambayo haiwezi kufanywa na mwanadamu. Mahitaji ambayo Mungu anatarajia kutoka kwa mwanadamu wakati wa kazi Yake, wakati uo huo, yanaitwa “vitendo” vya mwanadamu.
Maono ni kazi ya Mungu Mwenyewe au ni mapenzi Yake kwa mwanadamu au madhumuni na umuhimu wa kazi Yake. Maono pia yanaweza kusemekana kuwa sehemu ya usimamizi, kwani usimamizi huu ni kazi ya Mungu, iliyokusudiwa kwa mwanadamu, kwa maana kwamba ni kazi ambayo Mungu anaifanya miongoni mwa wanadamu. Kazi hii ni ushahidi na njia ambayo kwayo mwanadamu anamfahamu Mungu na ni ya umuhimu wa hali ya juu kwa mwanadamu. Iwapo wanadamu hawatatilia maanani kuijua kazi ya Mungu na badala yake kutilia maanani mafundisho ya dini kuhusu imani kwa Mungu au kutilia maanani vitu vidogo visivyo na maana, hawatamjua Mungu, na, aidha, hawatakuwa wanautafuta moyo wa Mungu. Kazi ya Mungu inamsaidia sana mwanadamu kumfahamu Mungu na inaitwa maono. Maono haya ni kazi ya Mungu, mapenzi, madhumuni na umuhimu wa kazi ya Mungu na yote ni kwa manufaa ya mwanadamu. Vitendo vinamaanisha yale ambayo yanafaa kufanywa na mwanadamu, yale ambayo yanafaa yafanywe na viumbe wanaomfuata Mungu. Ni wajibu wa mwanadamu pia."
Sikiliza zaidi: Maneno ya Roho Mtakatifu | "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" (Sehemu ya Pili)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni