Maneno Husika ya Mungu:
Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu. Leo, wale wote ambao hufuata maneno halisi ya Mungu wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu; wale ambao ni wageni kwa maneno halisi ya Mungu wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na watu hao hawasifiwi na Mungu.
Huduma ambayo imetenganishwa na matamshi halisi ya Roho Mtakatifu ni huduma ambayo ni ya mwili, na ya dhana, na haiwezi kuwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Kama watu huishi miongoni mwa dhana za kidini, basi hawawezi kufanya lolote lenye kustahili kwa mapenzi ya Mungu, na hata ingawa wao humhudumia Mungu, wao huhudumu katikati ya mawazo na dhana zao, na hawawezi kabisa kuhudumu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Wale ambao hawawezi kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu hawaelewi mapenzi ya Mungu, na wale ambao hawaelewi mapenzi ya Mungu hawawezi kumhudumia Mungu. Mungu hutaka huduma inayoupendeza moyo Wake mwenyewe; Hataki huduma ambayo ni ya dhana na mwili. Kama watu hawawezi kuzifuata hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, basi wao huishi katikati ya dhana, na huduma ya watu hao hukatiza na huvuruga. Huduma hiyo huenda kinyume na Mungu, na hivyo wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu hawawezi kumhudumia Mungu; wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu humpinga Mungu bila shaka, na ni wasioweza kulingana na Mungu. "Kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu" kuna maana ya kufahamu mapenzi ya Mungu leo, kuweza kutenda kwa mujibu wa masharti ya sasa ya Mungu, kuweza kutii na kumfuata Mungu wa leo, na kuingia kwa mujibu wa matamshi mapya zaidi ya Mungu. Huyu pekee ndiye mtu ambaye hufuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Watu hao hawawezi tu kupokea sifa za Mungu na kumwona Mungu, lakini wanaweza pia kujua tabia ya Mungu kutoka kwa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na ukaidi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutoka kwa kazi Yake ya karibuni zaidi; pia, wanaweza kutimiza polepole mabadiliko katika tabia yao wakati wa huduma yao. Ni watu kama hawa pekee ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata kwa halisi njia ya kweli. Wale ambao huondoshwa na kazi ya Roho Mtakatifu ni watu wasioweza kufuata kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na ambao huasi dhidi ya kazi ya karibuni zaidi ya Mungu. Kwamba watu hao humpinga Mungu waziwazi ni kwa sababu Mungu amefanya kazi mpya, na kwa sababu picha ya Mungu si sawa na ile iliyo ndani ya dhana zao—kutokana na hilo wao humpinga Mungu waziwazi na kumhukumu Mungu, kusababisha wao kuchukiwa na kukataliwa na Mungu.
kutoka kwa "Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Je, si watu wengi humpinga Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui kazi mbalimbali na tofautitofauti ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kwa sababu wanamiliki maarifa na mafundisho duni ya kupima kazi ya Roho Mtakatifu? Ingawa uzoefu wa watu kama hawa ni wa juujuu tu, ni wenye majivuno na wadekezi katika asili yao, na wanatazama kazi ya Roho Mtakatifu kwa dharau, wanapuuza masomo ya Roho Mtakatifu na, hata zaidi, wanatumia hoja zao ndogo ndogo zee kudhibitisha kazi ya Roho Mtakatifu. Pia wanajifanya, na wanashawishika kabisa na elimu yao na maarifa yao, na kuwa wanaweza kusafiri duniani kote. Je, watu hawa si ni wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na je, si wataondolewa na enzi mpya? Je, si wale wanaokuja mbele ya Mungu na kumpinga waziwazi ni watu wadogo wasioona mbali, wanaojaribu kuonyesha tu jinsi walivyo werevu? Kwa maarifa haba ya Biblia, wanajaribu kupotosha "wasomi" wa dunia, kwa mafundisho duni ya dini ili kuwafunza watu, wanajaribu kurudisha nyuma kazi ya Roho Mtakatifu, na kujaribu kuifanya ihusu mchakato wao wanavyofikiria, na kwa kuwa hawaoni mbali, wanajaribu kuona kwa mtazamo mmoja miaka 6,000 ya kazi ya Mungu. Je, watu hawa wana mantiki yoyote ya kuzungumzia? Kwa kweli, maarifa ya watu kumhusu Mungu yanavyozidi kuwa mengi, ndivyo wanavyokuwa wagumu wa kuhukumu kazi Yake. Zaidi ya hayo, wanazungumzia tu machache kuhusu maarifa yao ya kazi ya Mungu leo, lakini si wepesi wa kuhukumu. Kadri watu wanavyojua machache kumhusu Mungu, ndivyo wanavyozidi kuwa wenye majivuno na wenye kujiamini sana, na ndivyo wanavyozidi kutangaza nafsi ya Mungu kwa utundu—ilhali wanazungumzia tu nadharia, na wala hawapeani ushahidi wowote halisi. Watu kama hawa hawana thamani yoyote kabisa. Wale wanaoona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo ni wenye upuzi! Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wanaopayuka, ni wepesi wa kuhukumu wanaoruhusu silika yao ya kiasili kukana haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na pia kuitusi na kuikufuru—je, watu hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu? Je, si wao ndio, zaidi ya hayo, wale wasiojua, wenye majivuno ya asili na wasioweza kutawalwa? Hata ikiwa siku itakuja ambapo watu hawa watakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, bado Mungu hatawavumilia. Hawadharau tu wale wanaofanya kazi ya Mungu, bali pia wanamkufuru Mungu Mwenyewe. Watu kama hawa jasiri pasi na hadhari hawatasamehewa, katika enzi hii ama enzi itakayokuja na wataangamia kuzimuni milele! Watu kama hawa wasio na heshima, wenye kujifurahisha, wanajifanya kuwa wanamwamini Mungu, na kadiri wanavyozidi kufanya vile, ndivyo wanavyozidi kukosea amri za utawala wa Mungu. Je, si hao mafidhuli ambao kiasili hawazuiliki, na hawajawahi kumtii yeyote, wote hupitia njia hii? Je, si wao humpinga Mungu siku baada ya siku, Yeye ambaye daima huwa mpya na wala hazeeki?
kutoka kwa "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mtu kama huyu daima anakuwa na uadui dhidi ya kazi mpya ya Mungu, haonyeshi nia ya kujisalimisha, na hajawahi kutii ama kujinyenyekea kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe hajisalimishi kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi kwa kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi hazina anazomiliki, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiriwa kwa wengine, na kutumiwa kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni "mashujaa wasioshindwa," kizazi baada ya kizazi kinakaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanafikiria kuhubiri neno (mafundisho ya dini) ni wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wanatekeleza kwa nguvu wajibu wao "mtakatifu na usiokiukwa". Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna anayethubutu kuwapinga kwa uwazi. Walikuwa "mfalme" kwa nyumba ya Mungu, wakitenda kama dikteta kupitia enzi nyingi.
kutoka kwa "Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi , unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi, na kazi yako inaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe. Kwa hakika, utakuwa msumbufu zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hii ni uzoefu na mafunzo ya kibinadamu. Ni filosofia ya maisha ya binadamu. Watu kama hawa wanapatikana miongoni mwa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini.
kutoka kwa "Sitisha Huduma ya Kidini" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi katika akili ya mwanadamu inafikiwa kwa urahisi sana na mwanadamu. Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa kidini, kwa mfano, wanategemea karama zao na nafasi zao katika kufanya kazi zao. Watu wanaowafuata kwa muda mrefu wataambukizwa na karama zao na kuvutwa na vile walivyo. Wanalenga karama za watu, uwezo na maarifa ya watu, na wanamakinikia mambo ya kimiujiza na mafundisho mengi yasiyokuwa na uhalisi (kimsingi, haya mafundisho hayawezi kutekelezeka). Hawalengi mabadiliko ya tabia za watu, badala yake wanalenga kuwafundisha watu uwezo wao wa kuhubiri na kufanya kazi, kuboresha maarifa ya watu na mafundisho makuu ya kidini. Hawalengi kuona ni kwa kiasi gani tabia ya watu imebadilika au ni kwa kiasi gani watu wanauelewa ukweli. Wala hawajali utu wa watu, wala kujua hali za watu za kawaida na zisizo za kawaida. Hawapingi mitazamo ya watu au kufunua mitazamo yao, achilia mbali kurekebisha hali yao ya dhambi. Watu wengi wanaowafuata wanahudumia kwa karama zao za asili, na kile wanachokidhihirisha ni maarifa na ukweli wa kidini usioeleweka, ambayo ni nje ya mguso wa uhalisia na kuwapatia watu uzima. Kimsingi, kiini cha kazi yao ni kulea talanta, kumlea mtu kuwa mhitimu mwenye talanta aliyemaliza mafunzo ya kidini ambaye baadaye anakwenda kufanya kazi na kuongoza.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Unaweza kuzungumza maarifa mengi kama mchanga wa bahari, lakini hakuna yaliyo na njia ya kweli. Katika hili, je huwadanganyi watu? Je, wewe si mtu wa maneno matupu bila vitendo? Kutenda kwa namna hii ni hatari kwa watu! Kadri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokosa uhalisia, na ndivyo inavyokosa uwezo wa kuwapeleka watu katika uhalisia; kadri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokufanya kumuasi na kumpinga Mungu. Usizichukulie nadharia za kiwango cha juu kama hazina ya thamani; zina madhara, na hazina kazi yoyote! Pengine baadhi ya watu wanaweza kuzungumza juu ya nadharia za juu sana—lakini nadharia hizo hazina kitu chochote cha uhalisia, maana watu hawa hawajawa na uzoefu binafsi nazo, na kwa hiyo hawana njia ya kutenda. Watu kama hao hawawezi kumwongoza mwanadamu katika njia nzuri, na watawapotosha tu watu. Je, hii si hatari kwa watu? Kwa kiwango cha chini kabisa, unapaswa uweze kutatua shida za sasa na kuwaruhusu watu kupata kuingia; hii tu ndiyo inahesabika kama ibada, na baada ya hapo ndipo utakuwa na sifa za kufaa kumfanyia Mungu kazi. Siku zote usizungumze maneno mazuri, ya kibunifu, na usiwalazimishe watu kukutii wewe pamoja na vitendo vyako visivyofaa. Kufanya hivyo hakutaleta matokeo mazuri, na kutaongeza tu mkanganyiko wa watu. Kuwaongoza watu namna hii kutazalisha taratibu nyingi, ambazo zitafanya watu wakuchukie. Huu ndio udhaifu wa mwanadamu, na kwa kweli hauvumiliki.
kutoka kwa "Sisitiza Zaidi Kwa Uhalisia" katika Neno Laonekana katika Mwili
Maarifa yenu yanaweza kuwakimu watu kwa muda tu. Wakati unapoendelea, ukiendelea kusema kitu kile kile, watu kadhaa wataweza kutambua; watasema wewe ni mtu wa juu juu sana, aliyekosa kina sana. Hutakuwa na budi ila kujaribu kuwadanganya watu kwa kuongea mafundisho, na kama wewe daima huendelea hivi, wale walio chini yako watafuata namna yako, nyayo, na mfano wa kumwamini Mungu na kupitia, na watatia maneno na mafundisho hayo katika vitendo, na hatimaye, unapoongea katika njia hii, watakutumia kama mfano. Unachukua mwongozo kuongea mafundisho, na wale walio chini yako watajifunza mafundisho kutoka kwako, na vitu vinapoendelea utakuwa umechukua njia ambayo si sawa. Wale walio chini yako wanafuata njia yako … Tazama viongozi wa kila madhehebu na faraka. Wote ni wa kujigamba na kujisifu, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ujuzi fulani, na wanaweza kuongea mafundisho kiasi, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa, ambao kupitia kwake wamewaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu—lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na wale wanaohubiri njia ya kweli, baadhi yao wangesema, "Lazima tutafute ushauri kwake kuhusu imani yetu katika Mungu." Tazama jinsi wanavyohitaji ridhaa ya mtu ili kumwamini Mungu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli?
kutoka kwa "Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kutoa kwenu "muhtasari kuhusu ukweli" hakufanywi ili kuwawezesha watu kupata maisha au kupata mabadiliko katika tabia zao kutoka kwa ukweli. Badala yake, kunafanywa ili watu waweze kuwa weledi wa maarifa na mafundisho fulani kutoka kwa ukweli. Wao huonekana kana kwamba wanaelewa lengo lililokusudiwa katika kazi ya Mungu, wakati kwa kweli wamekuwa weledi wa baadhi ya maneno ya mafundisho tu. Hawaelewi maana iliyokusudiwa ya ukweli, na si tofauti na kusomea theolojia au kusoma Biblia. Wewe unakusanya vitabu hivi au vifaa hivyo, na hivyo unapata umiliki wa kipengele hiki cha mafundisho au kipengele kile cha ujuzi. Wewe ni msemaji wa kiwango cha juu wa mafundisho—lakini huwaje unapomaliza kusema? Watu basi hawana uwezo wa kupitia, hawana ufahamu wa kazi ya Mungu na hawana ufahamu wao wenyewe pia. Mwishowe, vitu vyote watakavyokuwa wamepata ni fomyula na sheria … Kwa kuuliza swali baada ya swali kuhusu maneno hayo, kisha kujibu, kufanya muhtasari, unadhani kuwa wale walio chini wanaweza kuelewa kwa urahisi. Mbali na kuwa rahisi kukumbuka, wao wana uhakika juu ya maswali haya kwa tazamo la haraka, na unafikiri ni vizuri kufanya mambo kwa njia hii. Lakini kile wanachokielewa siyo maana iliyokusudiwa ya ukweli; inatofautiana na ukweli na ni maneno ya mafundisho tu. Hivyo ingekuwa bora zaidi kama wewe hungefanya mambo haya hata kidogo. Unafanya mambo haya kuwaongoza watu kuelewa ujuzi na weledi wa elimu. Wewe huwaleta wengine katika mafundisho, katika dini, na kuwafanya wamfuate Mungu na kumwamini Mungu ndani ya mafundisho ya dini. Je, si wewe ni sawa tu na Paulo? … Mwishowe wao wangeletwa mahali ambapo hawawezi kupata ukweli na hawawezi kupitia neno la Mungu, mahali ambapo wanaweza kujiandaa tu na kujadili mafundisho na ni mahali ambapo hawawezi kumwelewa Mungu. Yote ambayo wangeweza kuzungumza yangekuwa mafundisho yenye kupendeza, mafundisho sahihi, lakini hakungekuwa na uhalisi ndani yao na hawangekuwa na njia ya kutembelea. Aina hii ya kuongoza kweli hufanya madhara makubwa!
kutoka kwa "Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wengine wanajihami tu na ukweli fulani kwa wakati wa dharura ama kujitelekeza wenyewe na kuwasaidia wengine, sio kutatua shida zao wenyewe; tunawaita "watu wasio na ubinafsi." Wanawaona wengine kama vikaragosi wa ukweli na wenyewe kama mabwana wa ukweli, wakiwafunza wengine kuushikilia ukweli na wasiwe wasiojihususha, ilhali wao wenyewe ni watazamaji kando kando mwa uwanja—hao ni watu wa aina gani? Wakiwa wamejihami na baadhi ya maneno ya ukweli ili kuwahubiria wengine tu, wakikosa kufanya chochote kujizuia kutokana na kuangamia kwao wenyewe—inasikitishaje! Kama maneno yao yanaweza kuwasaidia wengine, mbona wasijisaidie wenyewe? Tunafaa kuwaita wanafiki wasio na ukweli. Wanatoa maneno ya ukweli kwa wengine na kuwaambia wengine wayaweke katika matendo, lakini hawafanyi juhudi yoyote kuyatenda wenyewe—je sio wa kudharauliwa? Kwa hakika hawawezi kulifanya wenyewe, ilhali wanawalazimisha wengine kuweka maneno ya ukweli katika matendo—hii ni njia ya ukatili iliyoje! Hawatumii ukweli kuwasaidia wengine; hawawatolei wengine kwa moyo wa upendo wa mama; wanawadanyanya tu watu na kuwapotosha watu. Hili likiendelea—na kila mtu akipitisha maneno ya ukweli kwa anayefuata—je kila mmoja mwishowe hatakuwa na uelewa tu wa maandishi ya ukweli wakikosa uwezo wa kuyatenda?
kutoka kwa "Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Wale wanaosoma Biblia kwa makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu wabovu, kila mmoja akisimama juu kumfundisha Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga makusudi. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, mapepo yanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Ingawa wenye "mwili imara," wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni maadui wa Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?
kutoka kwa "Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mbona Nasema wale walio katika dunia ya kidini hawaamini katika Mungu na ni waovu, walio sawa na ibilisi? Ninaposema ni watenda maovu, ni kwa sababu hawaelewi matakwa ya Mungu, wala kuona hekima Yake. Hakuna wakati ambao Mungu anadhihirisha kazi Yake kwao; ni vipofu, wasioona matendo ya Mungu. Wao ndio walioachwa na Mungu na hawamiliki kabisa utunzaji na ulinzi wa Mungu, sembuse kazi ya Roho Mtakatifu. Wale walio bila kazi ya Mungu ni watenda maovu na humpinga Mungu.
kutoka kwa "Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ushirika wa Mtu:
Wajibu wa wafanyakazi ni kutenda kazi yao na kuyaongoza makanisa kulingana na mapenzi ya Mungu na kwa mujibu wa mahitaji na mipango ya Mungu. Kazi kama hii hubarikiwa na Mungu. Ikiwa wafanyakazi hawana urazini kama huo, na hukiuka mapenzi ya Mungu kwa kufanya mambo kwa njia yao wenyewe, wakichukua nafasi ya mchungaji na kuwafundisha watu jinsi wanavyopenda, wakitoa dhana zao, mawazo, na mafundisho na kuwafanya wengine kuyakubali, basi wafanyakazi kama hawa wamekuwa wachungaji wa uongo. Kuna mifano mingi ya wafanyakazi kuwa wachungaji wa uongo, na idadi kubwa wameondoshwa na Mungu katika kila hatua ya kazi Yake. Mungu wakati mmoja Alisema kuwa katika kila enzi kuna watu wengi wanaomtumikia Mungu na bado pia humpinga, hata hatimaye huwafanya wengine wawatii na kuwaabudu kama wao ni Mungu. Hili ni dhihirisho la "wachungaji wa uongo." Sote tunapaswa kuchukua hili kama onyo; wafanyakazi wanapaswa kuzingatia mabadiliko katika tabia, na ikiwa watazembea na kutokuwa waangalifu kwa hili, basi ni rahisi mno kwao kuwa wachungaji wa uongo. Kazi ya wachungaji wa uongo ina mkazo maalum juu ya kuwaongoza watu kulingana na maana ya wachungaji wa uongo wenyewe. Yote wanayofanya, kusema, na kutafuta ni ya mpango wao wenyewe, na hulichukulia hili kama ukweli safi mno kuliko ukweli wote, na wao hudhani kuwa wanaweza kuwafundisha watu kuwa wanadamu na kuwaruhusu watu kupata ukweli kulingana na mpango wao wenyewe. Haya ni maonyesho ya kiburi cha juu kabisa na hali ya kujidai ya wachungaji wa uwongo. Kwa wale ambao kweli ni wa busara, wanapoamini kuwa wako sahihi hasa wangetafuta na kuwasiliana ukweli kwa karibu , na kutenga uangalifu wao kwa kusikia maoni na maarifa tofauti ya wengine ili kuthibitisha kama yote waliyoyaelewa ni sahihi. Wale wote ambao wamepitia kupogolewa na kushughulikiwa kwa Mungu wanapaswa kuweza kuweka kando baadhi ya hali zao za kujidai na majisifu. Wanapofanya kazi, wao ni waangalifu katika hatua zao ili kuepuka kukiuka mapenzi ya Mungu na kuchukua njia mbaya. Matokeo yao kuwa wachungaji wa uongo hayawezi kufikiriwa. Kila mfanyakazi ana matendo yake mwenyewe, wote wana nadharia zao wenyewe ambazo wao hutumia kunyunyizia watu; kwa kweli, hakuna yeyote anayeweza kufahamu kabisa ni kiasi gani cha ukweli au thamani njia yao wenyewe inacho. Watu wamekosa hali ya kujitambua, hawana bidii au tafakari ya kina sana katika maarifa yao ya ukweli, na wao huchukua kiholela vitu visivyo na maana na kuvichukulia kama hazina za kutolewa kwa wengine. Si matendo kama hayo yanaashiria mchungaji wa uwongo? Si hili linawadhuru wengine pamoja na wao wenyewe? Bila kujali ni kazi kiasi gani wachungaji wa uwongo hufanya, hawana uwezo kabisa wa kuwaleta watu mbele ya Mungu na kuwaruhusu wamjue na kumtii Mungu. Yote yanayofunguliwa na wachungaji wa uongo ni maneno na mafundisho tu, na mawazo na fikra, na hakuna kitu ambacho huzuia kazi ya Mungu au kumpinga Yeye zaidi.
kutoka kwa "Maana ya 'Wachungaji Kondoo wa Uongo'" katika Ushirikiano Kutoka kwa wa Juu
Huduma kulingana na mbinu za kidini inamaanisha kufanya kila kitu kulingana na njia za desturi za dini na utaratibu wa huduma, kuzingatia kwa imara sherehe mbalimbali za kidini, na kuwaongoza watu tu kulingana na maarifa ya Biblia. Kwa kuonekana, yaelekea kuwa yenye bidii na nguvu, inaashiria dini, inafaa barabara kwa mawazo ya watu, na hawana vipingamizi. Lakini haina kabisa kazi ya Roho Mtakatifu, kinachohubiriwa si kitu ila mafundisho ya kidini na elimu ya Biblia, imejaa mawazo ya kidini, haina chochote kuhusu upataji wa nuru ya Roho Mtakatifu, na mikutano imetuama na kukosa uhai. Kwa huduma kama hii, miaka inavyoendelea watu waliochaguliwa wa Mungu bado wanabaki bila ukweli, hawana maarifa ya Mungu au utii kwa Mungu, na hawajaingia kwenye njia sahihi ya imani kwa Mungu–kwa kuwa kile watu hufuatilia sio wokovu bali ni neema na baraka, kiasi kwamba hakuna dalili za mabadiliko katika tabia ya maisha yao. Baada ya kuhudumu kwa miaka kadhaa, hawa watu bado wako mikono mitupu, bila ushahidi wa kitu walichopata wenyewe. Haya ndiyo matokeo ya huduma kulingana na mbinu za kidini. Ni dhahiri kuwa, watu kama hawa wanaomtumikia Mungu hawajui kazi ya Mungu, hawaelewi mapenzi ya Mungu, na hawajui maana ya kushirikiana na kazi ya Roho Mtakatifu. Ni jambo dhahiri la vipofu wakiwaongoza vipofu, huwapotosha watu waliochaguliwa wa Mungu , kama Mafarisayo humwamini Mungu na bado humpinga Mungu, hawamjui Mungu, na kimsingi hawawezi kufanikisha wokovu wa Mungu.
kutoka kwa "Wale tu Wanaoingia Kwenye Njia Sahihi ya Imani katika Mungu Ndio Wanaweza Kuchukua njia Sahihi ya Huduma kwa Mungu" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirika na Mipangilio ya Kazi ya Kanisa (I)
Wachungaji wa jamii ya kidini hutumia kila fursa ya kutangaza kiwango cha maarifa yao na kutoa sura ya uchaji Mungu. Lengo lao ni kuwafanya watu wawastahi na kuwaabudu, na wao hutumia taswira yao wenyewe kuwavuta watu kwao ili wawatii na kuwafuata, matokeo yakiwa ni wao kuwaongoza watu kuabudu maarifa ya Biblia, kuabudu hadhi na nguvu, na kuabudu ustadi katika kuhubiri. Kwa njia hii, kwa kila hatua huwaongoza watu katika njia ya kumpinga Mungu. Wale wanaoongozwa na wapinga Kristo humwamini Mungu asiye yakini, wao ni wazuri kwa kuzungumzia mafundisho matupu na yasiyo na maana, na wenye ujuzi katika unafiki, na wao wote humwamini Mungu na bado humpinga na kumwasi Mungu. Hakuna shaka kwamba njia ambayo viongozi wa uongo na wapinga Kristo hufanyia kazi–ile ambayo wao hutumia kumtumikia Mungu na bado kumpinga Yeye–ni ya kuwadhuru watu sana.
kutoka kwa "Kulinda Dhidi ya Wapinga Kristo na Njia ya Wapinga Kristo Ni ya Umuhimu Mkuu" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirika na Mipangilio ya Kazi ya Kanisa (II)
Chanzo: Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu (Mambo Muhimu ya Muumini Mpya)
Kujua zaidi: Maswali na Majibu ya Injili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni