Kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni mojawapo ya hatua muhimu sana za kuingia katika maneno ya Mungu, na ni funzo ambalo watu wote sasa wana haja ya haraka kuingia ndani. Njia za kuingia za kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni:
1. Ondoa moyo wako kwa mambo ya nje, tulia mbele ya Mungu, na uombe Mungu kwa moyo uliolenga.
3. Yafanye mazoea ya kawaida kutafakari na kuzingatia maneno ya Mungu na kufikiri kazi ya Mungu na moyo wako.
Kwanza anza na jambo la sala. Kuwa na nia moja, na uombe wakati usiobadilika. Haijalishi umepungukiwa na muda namna gani, au uwe na shughuli vipi, au chochote kitakachokufanyikia, omba kila siku kama kawaida, na ule na kunywa maneno ya Mungu kama kawaida. Mradi unakula na kunywa maneno ya Mungu, haijalishi mazingira yako ni yapi, roho yako hufurahia hasa, wala husumbuliwi na watu, matukio, au mambo yanayokuzunguka. Unapotafakari juu ya Mungu kwa kawaida ndani ya moyo wako, kinachoendelea nje hakiwezi kukusumbua wewe. Hii ndiyo maana ya kuwa na kimo. Anzia kwa maombi: Kuomba kwa amani mbele ya Mungu huzaa matunda zaidi. Baada ya hapo, kuna kula na kunywa maneno ya Mungu, kuweza kuelewa mwangaza ulio kwenye maneno ya Mungu, kuweza kupata njia ya kutenda, kujua maazimio ya matamshi ya Mungu ni yapi, na kuelewa bila mkengeuko. Kwa kawaida, lazima moyo wako uweze kusongea karibu na Mungu kwa kawaida, lazima uweze kuzingatia upendo wa Mungu, kutafakari juu ya maneno ya Mungu, na usiweze kuathiriwa na kuingiliwa kwa dunia ya nje. Moyo wako unapokuwa na amani mbele ya Mungu kiasi kwamba unaweza kutafakari, ukiwa, ndani yako mwenyewe, unazingatia upendo wa Mungu, na kusonga karibu na Mungu kwa kweli, bila kujali mazingira uliyomo, na, kwa hakika ukiwa umefika kiwango ambacho unapeana sifa moyoni mwako, na ni bora zaidi hata kuliko kuomba, basi katika hili utakuwa wa kimo fulani. Ikiwa una uwezo wa kutimiza hali iliyoelezewa hapa juu, basi hii itathibitisha kuwa moyo wako kwa kweli uko na amani mbele ya Mungu. Hii ni hatua ya kwanza; ni ujuzi wa kimsingi. Ni baada tu ya kuwa na uwezo wa kuwa na amani mbele ya Mungu ndipo watu wanaweza kuguswa na Roho Mtakatifu, na kupata nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu, ni hapo tu ndipo wanaweza kuwasiliana kwa karibu kwa kweli na Mungu, na kuweza kushika mapenzi ya Mungu na mwongozo wa Roho Mtakatifu—na katika hii, watakuwa wameingia katika njia sahihi katika maisha yao ya kiroho. Kujizoeza mwenyewe kuishi mbele ya Mungu kufikia kina fulani ili uweze kujiasi mwenyewe, kujidharau mwenyewe, na kuishi katika maneno ya Mungu, hii kweli ni kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Kuweza kujidharau, kujilaani, na kujiasi ni matokeo ambayo kazi ya Mungu hutimiza, na watu hawawezi kufanya hili. Kwa hivyo mazoezi ya kuutuliza moyo wa mtu mbele ya Mungu ni funzo ambalo watu wanapaswa kuingia ndani mara moja. Watu wengine hawawezi tu kwa kawaida kuituliza mioyo yao mbele ya Mungu, lakini mioyo yao hata haitulii mbele ya Mungu wanapoomba. Hii kwa jumla ni mbali sana na viwango vya Mungu! Ikiwa moyo wako hauwezi kutulia mbele ya Mungu unaweza kusisimuliwa na Roho Mtakatifu? Ikiwa huwezi kutulia mbele ya Mungu, unaweza kuvurugwa mawazo mtu akija, unaweza kuvurugwa mawazo watu wanapoongea, na moyo wako unaweza kuvutwa mbali watu wengine wanapofanya mambo, kwa hiyo wewe si mtu anayeishi mbele ya Mungu. Ikiwa moyo wako kweli umetulia mbele ya Mungu hutasumbuliwa na chochote kinachoendelea huko nje duniani, na hakuna mtu, tukio au jambo litakalokumiliki. Ikiwa mmeingia katika hili, basi zile hali mbaya au mambo yote mabaya, kama vile dhana za binadamu, falsafa ya maisha, mahusiano yasiyo ya kawaida na watu, na mawazo ndani ya moyo wako yatatoweka kwa kawaida. Kwa sababu kila mara unatafakari maneno ya Mungu, na moyo wako kila mara unasonga karibu na Mungu na kumilikiwa na maneno ya sasa ya Mungu, mambo hayo mabaya huvuliwa bila kufahamu. Mambo mapya mazuri yanapokumiliki, mambo ya zamani mabaya hayatakuwa na nafasi, kwa hiyo usitilie maanani mambo hayo mabaya. Huhitaji kufanya jitihada za kujaribu kuyadhibiti. Tilia maanani kutulia mbele ya Mungu, kula na kunywa maneno zaidi ya Mungu na kuyafurahia, imba nyimbo nyingi zaidi za dini ukimsifu Mungu, na wacha Mungu awe na nafasi ya kukushughulikia, kwa sababu Mungu wakati huu anataka binafsi kuwakamilisha watu, Anataka kuupata moyo wako, Roho Wake husisimua moyo wako, na ukiishi mbele ya Mungu ukifuata uongozi wa Roho Mtakatifu utamridhisha Mungu. Ukitilia maanani kuishi katika maneno ya Mungu na kushiriki zaidi kuhusu ukweli ili kupata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, basi dhana hizo za kidini, kujidai na kujikweza vitatoweka vyote, na kisha utajua namna ya kugharimia rasilmali kwa ajili ya Mungu, kujua namna ya kumpenda Mungu, na namna ya kumridhisha Mungu. Mambo hayo nje ya Mungu kisha husahaulika bila kufahamu.
Kutafakari juu ya maneno ya Mungu na kusali juu ya maneno ya Mungu kwa wakati sawa na kula na kunywa maneno ya sasa ya Mungu—hii ndiyo hatua ya kwanza ya kuwa na amani mbele ya Mungu. Iwapo unaweza kuwa na amani kwa uhakika mbele ya Mungu, basi utafuatwa na nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu.
Maisha yote ya kiroho hutimizwa kwa kutegemea kutulia mbele ya Mungu. Katika kuomba lazima utulie mbele ya Mungu kabla ya kuweza kusisimuliwa na Roho Mtakatifu. Kwa kutulia mbele ya Mungu unapokula na kunywa maneno ya Mungu unaweza kupata nuru na kuangaziwa na kuweza kutimiza kwa kweli ufahamu wa maneno ya Mungu. Katika tafakuri na ushirika wako wa kawaida, na wakati unasonga karibu na Mungu na moyo wako, ni wakati unapotulia tu mbele ya Mungu ndipo unaweza kuwa na ukaribiano halisi na Mungu, ufahamu halisi wa upendo wa Mungu na kazi ya Mungu, na uangalifu wa kweli kwa makusudi ya Mungu. Kadri unavyoweza kwa kawaida kutulia mbele ya Mungu ndivyo unavyoweza kuangaziwa zaidi, na ndivyo unavyoweza kufahamu tabia yako mwenyewe ya upotovu zaidi, unachokosa, unachopaswa kuingia, shughuli unayopaswa kuhudumu, na pale ulipo na dosari. Haya yote hutimizwa kwa kutegemea kuwa mtulivu mbele ya Mungu. Ikiwa utafikia kweli kina fulani cha kuwa mtulivu mbele ya Mungu, unaweza kugusa miujiza fulani katika roho, kugusa kile ambacho Mungu wakati huu anataka kufanya juu yako, kugusa ufahamu wa kina wa maneno ya Mungu, na kugusa asili ya maneno ya Mungu, kiini cha maneno ya Mungu, nafsi ya maneno ya Mungu, na unaweza kuona njia ya kutenda kwa kweli zaidi na sawasawa zaidi. Ikiwa huwezi kutulia katika roho yako kwa kina fulani, utaweza kusisimuliwa tu kiasi na Roho Mtakatifu, ndani utahisi nguvu, na furaha na amani kiasi, lakini hutagusa chochote kwa kina zaidi. Nimesema hapo awali, ikiwa mtu hatumii nguvu zake zote, itakuwa vigumu kwake kusikia sauti Yangu au kuona uso Wangu. Hii inanena juu ya kutimiza kina katika kutulia mbele ya Mungu, sio kwa juhudi za nje. Mtu anayeweza kuwa mtulivu kwa kweli mbele ya Mungu anaweza kujiachilia huru kutoka kwa vifungo vyote vya kidunia na anaweza kutimiza kumilikiwa na Mungu. Watu wote wasioweza kutulia mbele ya Mungu ni wafisadi na wasiozuiwa kwa yakini. Wale wote wanaoweza kutulia mbele ya Mungu ni watu ambao ni wacha Mungu mbele ya Mungu, watu wanaomtamani Mungu. Ni watu walio watulivu tu mbele ya Mungu ndio wanaotilia maanani maisha, wanaotilia maanani ushirika katika roho, walio na kiu ya maneno ya Mungu, na wanaofuatilia ukweli. Wale wote wasiotilia maanani kutulia mbele ya Mungu, wasiofanya mazoezi ya kuwa watulivu mbele ya Mungu ni watu ovyo ambao wamejifunga kabisa kwa dunia, wasio na uzima; hata wakisema wanaamini katika Mungu wanaunga mkono kwa maneno matupu tu. Wale ambao Mungu hukamilisha na kufanya kamili hatimaye ni watu wanaoweza kuwa watulivu mbele ya Mungu. Kwa hivyo, watu walio watulivu mbele ya Mungu ni watu walioneemeshwa na baraka nyingi. Watu ambao mchana hutumia muda mchache kula na kunywa maneno ya Mungu, ambao wameshughulika kabisa na mambo ya nje, na hawatilii maanani kuingia katika uzima wote ni wanafiki wasiokuwa na matarajio ya kuendelea katika siku za usoni. Ni wale wanaoweza kutulia mbele ya Mungu na kushiriki kwa uhalisi na Mungu ndio watu wa Mungu.
Kuja mbele ya Mungu kukubali maneno Yake kama uzima wako, lazima kwanza uwe mtulivu mbele ya Mungu. Ni wakati unapokuwa tu mtulivu mbele ya Mungu ndio Mungu atakupa nuru na kukufanya uelewe. Kadri watu wanavyokuwa watulivu zaidi mbele ya Mungu, ndivyo wanavyoweza kupata nuru na mwangaza wa Mungu zaidi. Haya yanawahitaji watu kuwa na uchaji Mungu na imani. Ni hivyo tu ndivyo wanaweza kutimiza ukamilifu. Zoezi la msingi la kuingia katika maisha ya kiroho ni kuwa mtulivu mbele ya Mungu. Mazoezi yako yote ya kiroho yatafaa tu ikiwa unatulia mbele ya Mungu. Ikiwa huwezi kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu huwezi kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ikiwa moyo wako umetulia mbele ya Mungu haijalishi unachofanya basi wewe ni mtu unayeishi mbele ya Mungu. Ikiwa moyo wako umetulia mbele ya Mungu na unasonga karibu na Mungu haijalishi unachofanya, hii inathibitisha kuwa wewe ni mtu uliye mtulivu mbele ya Mungu. Unapozungumza na wengine, unapotembea, unaweza kusema, "Moyo wangu unasonga karibu na Mungu, na haulengi mambo ya nje, na naweza kutulia mbele ya Mungu." Huyu ni mtu aliyetulia mbele ya Mungu. Usiingiliane na vitu vinavyoweza kuelekeza moyo wako kwa mambo ya nje, na usiingiliane na watu wanaoweza kuondoa moyo wako kwa Mungu. Achana na chochote kile kinachoweza kuvuta moyo wako usiwe karibu na Mungu, au kukaa mbali nacho. Njia hiyo ni ya manufaa zaidi kwa maisha yako. Huu ndio wakati wa kazi kuu ya Roho Mtakatifu. Ni wakati ambao Mungu Mwenyewe anawakamilisha watu. Ikiwa kwa wakati huu huwezi kutulia mbele ya Mungu basi wewe si mtu unayerudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ikiwa unafuatilia vitu badala ya Mungu hakuna uwezekano wa kukamilishwa na Mungu. Wale ambao leo wanaweza kusikia matamshi kama haya kutoka kwa Mungu na bado hawawezi kutulia mbele ya Mungu ni watu wasiopenda ukweli, watu wasiompenda Mungu. Ikiwa hutajitoa sasa utafanya hivyo lini? Kujitoa mwenyewe ni kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Huku ni kujitoa kwa halisi. Yeyote anayetoa moyo wake kwa Mungu sasa kwa kweli bila shaka anaweza kukamlishwa na Mungu. Hakuna chochote, haijalishi ni nini, kinaweza kukusumbua, ikiwa ni cha kukupogoa, au kukushughulikia, au ikiwa wewe hukutana na kuvunjwa moyo au kutofaulu, moyo wako unapaswa kila mara kutulia mbele ya Mungu. Haijalishi watu wanakutendea vipi, moyo wako unapaswa kutulia mbele ya Mungu. Haijalishi unakabiliwa na mazingira gani, iwe ni dhiki, taabu, au mateso, au ikiwa aina nyingi ya majaribio yanakukumba, moyo wako unapaswa kila mara kutulia mbele ya Mungu. Hii ni njia ya kukamilishwa. Ikiwa tu mmetulia kwa kweli mbele ya Mungu ndipo mtaelewa kuhusu maneno ya sasa ya Mungu, kutenda kwa usahihi zaidi mwanga na kupata nuru kwa Roho Mtakatifu na kutopotoka, kuweza kugusa kwa wazi makusudi ya Mungu na kuwa na mwelekeo wazi zaidi katika huduma yako, kuweza kugusa sawasawa kusisimua na uongozi wa Roho Mtakatifu na kuwa na uhakika wa kuishi chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Haya ndiyo matokeo ambayo kuwa mtulivu kwa kweli mbele ya Mungu hutimiza. Wakati watu hawaelewi kuhusu maneno ya Mungu, hawana njia ya kutenda, hawawezi kuyagusa makusudi ya Mungu, au hawana kanuni za kutenda, hii ni kwa sababu mioyo yao haijatulia mbele ya Mungu. Kusudi la kuwa mtulivu mbele ya Mungu ni kuwa mwenye ari na wa vitendo na kutafuta usahihi na uangavu katika maneno ya Mungu, hatimaye kutimiza kufahamu ukweli na kumjua Mungu.
Ikiwa moyo wako hauwezi siku zote kutulia mbele ya Mungu, Mungu hawezi kukukamilisha. Ikiwa mtu hana nia iliyo sawa na kukosa moyo, na watu wasio na mioyo hawawezi kutulia mbele ya Mungu. Hawajui ni kazi kiasi gani ambayo Mungu hufanya au kiasi gani Yeye husema, wala hawajui namna ya kuyaweka katika vitendo. Je, hawa si watu wasio na mioyo? Watu wasio na mioyo wanaweza kutulia mbele ya Mungu? Mungu hawezi kuwakamilisha watu wasio na mioyo, nao wako miongoni mwa wanyama. Mungu amenena wazi sana na kikamilifu, ilhali moyo wako bado hauwezi kusisimuliwa na bado huwezi kutulia mbele ya Mungu; je, huku sio kuwa mnyama? Watu wengine hupotoka katika kufanya mazoezi ya kutulia mbele ya Mungu. Ikiwa ni wakati wa kupika hawapiki, na ikiwa ni wakati wa kufanya kazi hawafanyi kazi, lakini wanaendelea tu kuomba na kutafakari. Kutulia mbele ya Mungu hakumaanishi kutopika au kutofanya kazi, wala kuyapuuza maisha, lakini kuweza kuutuliza moyo wa mtu mbele ya Mungu, kuweza kuweka nafasi ya Mungu ndani ya moyo wa mtu katika hali zote za kawaida. Unapoomba, piga magoti chini vizuri mbele ya Mungu kuomba; unapofanya kazi au kutayarisha chakula, tuliza moyo wako mbele ya Mungu, tafakari maneno ya Mungu au imba nyimbo za dini. Haijalishi ni mazingira gani uko ndani, una njia ya kufanya mazoezi, fanya kila uwezalo kuwa karibu na Mungu, fanya kila uwezalo kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Hali zinaporuhusu, omba kwa nia moja; hali zisiporuhusu, mkaribie Mungu ndani ya moyo wako unapofanya kazi hiyo kwa mikono yako. Unapoweza kula na kunywa maneno ya Mungu basi kula na kunywa maneno ya Mungu; unapoweza kuomba basi omba; unapoweza kumtafakari Mungu basi mtafakari Yeye; fanya kila uwezalo kujizoeza kwa ajili ya kuingia kwa kutegemea mazingira yako. Watu wengine wanaweza kutulia mbele ya Mungu wakati hakuna kinachotokea, lakini punde tu jambo hufanyika mioyo yao humwacha Mungu. Huko si kutulia mbele ya Mungu. Njia sahihi ya kupata uzoefu ni kwamba moyo wa mtu usimwache Mungu kwa hali yoyote ile, au kuhisi kusumbuliwa na watu, matukio, au mambo ya nje: Huyu ni mtu ambaye ametulia kweli mbele ya Mungu. Watu wengine husema kwamba wanapoomba katika mikutano mioyo yao huweza kutulia mbele ya Mungu, lakini wakiwa katika ushirika hawawezi kutulia mbele ya Mungu na mawazo yao huvurugwa. Huku si kutulia mbele ya Mungu. Watu wengi sana wakati huu wako katika hali hii, na mioyo yao haiwezi kila mara kutulia mbele ya Mungu. Kwa hiyo mnahitaji kuongeza juhudi zaidi katika kujizoeza katika eneo hili, kuingia hatua kwa hatua katika njia sahihi ya uzoefu wa maisha na kutembea juu ya njia ya kukamilishwa na Mungu.
Chanzo: Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni