Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia
Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kuyasikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu anayemfuata Yesu angependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewazia hili: Mtamjua Yesu kweli Atakaporejea? Je, mtaelewa kweli kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali kweli, bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake.
Nyote mmetazamia kufika kwa wakati huo, na uaminifu wenu ni wa kusifika, imani yenu kweli ni ya kuleta wivu, lakini mnatambua kuwa mmefanya kosa kuu? Yesu Atarejea kwa namna gani? Mnaamini kuwa Yesu Atarudi juu ya wingu jeupe, lakini Nawauliza: Wingu hili jeupe linaashiria nini? Na kwa kuwa wafuasi wengi wa Yesu wanangoja kurejea Kwake, Atashuka miongoni mwa watu wapi? Iwapo ninyi ni wa kwanza kati ya wale ambao Yesu Atawashukia, Je, wengine hawataona jambo hili kama lisilo la haki sana? Najua kuwa nyinyi mna ukweli mkubwa na utiifu kwa Yesu, lakini mmewahi kukutana na Yesu? Mnajua tabia Yake? Mmewahi kuishi na Yeye? Mnaelewa kiasi gani kumhusu kwa kweli? Wengine watasema kuwa maneno haya yanawaweka katika tatizo gumu. Watasema, “Nimesoma Biblia kuanzia mwanzo hadi mwisho mara nyingi sana. Nitakosaje kumwelewa Yesu? Usijali kuhusu tabia ya Yesu—najua hata rangi ya nguo Alizopenda kuvaa. Je, haushushi hadhi yangu ukisema simwelewi?” Napendekeza kuwa usiyapinge masuala haya; ni heri utulie na kufanya ushirika juu ya maswali yafuatayo: Kwanza, unajua uhalisi ni nini, na nadharia ni nini? Pili, unajua dhana ni nini, na ukweli ni nini? Tatu, unajua kile kinachowazwa na kile kilicho halisi?
Watu wengine wanakataa ukweli kuwa hawamwelewi Yesu. Ilhali Nasema hammwelewi hata kidogo, na hamwelewi hata neno moja la Yesu. Hiyo ni kwa sababu kila mmoja wenu anamfuata Yeye kwa sababu ya matukio ya Biblia, kwa sababu ya yale yaliyosemwa na wengine. Hamjawahi kumwona Yesu, sembuse kuishi na Yeye, na hata hamjapata kushinda na Yeye hata kwa muda mfupi. Hivyo, je, kuelewa kwenu kuhusu Yesu sio nadharia pekee? Je, si kuelewa kwenu kunakosa uhakika? Labda watu wengine wameiona picha ya Yesu, ama wengine wametembea nyumbani kwa Yesu kibinafsi. Labda wengine wamegusa mavazi ya Yesu. Ilhali kuelewa kwako kumhusu bado ni kwa nadharia na ila si kwa vitendo, hata kama umeonja chakula kilicholiwa na Yesu binafsi. Haijalishi ni hali ipi, hujawahi kumwona Yesu, na hujawahi kuwa pamoja na Yeye katika hali ya kimwili, na hivyo, kuelewa kwako kumhusu Yesu kutabaki kuwa nadharia tupu daima ambako hakuna ukweli. Pengine maneno Yangu yana uvutio mdogo kwako, lakini Nakuuliza hivi: Ingawa labda umesoma maandishi mengi yaliyoandikwa na mwandishi unayempenda, je, unaweza kumwelewa kikamilifu bila kuwahi kukaa na yeye kwa muda? Je, unajua tabia yake ilivyo? Je, unajua ni maisha ya aina gani anayoishi? Unajua chochote kuhusu hali ya hisia zake? Huwezi hata kumwelewa kikamilifu mwanadamu unayempenda, sasa utawezaje kumwelewa Yesu Kristo? Kila kitu unachoelewa kumhusu Yesu kimejaa mawazo na dhana, na hakina ukweli wowote wala uhalisi. Kinanuka, na kimejaa mwili. Kuelewa kwa aina hii kutakuwezesha vipi kustahili kukaribisha kurejea kwa Yesu? Yesu hatawakaribisha wale waliojawa na mawazo na dhana za mwili. Wale wasiomwelewa watafaa vipi kuwa waumini Wake?
Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha, na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuonyesha heshima tupu kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni zaidi, kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale wote ambao hawakumfahamu Masiha walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, wa kumkataa Yesu, wa kumpaka Yeye tope. Watu wote wasiomwelewa Yesu wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kama uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliyerudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale yote ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe kwa upofu, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni kundi ambalo litaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia ulimwengu wa mbinguni wenye raha, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupokea ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, na kisha kuzikiri, tena na tena? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?
Uaminifu wenu uko kwa maneno pekee, maarifa yenu ni ya kiakili tu na ya dhana, kazi yenu ni kwa sababu ya kupata baraka za mbinguni, na kwa hivyo imani yenu inafaa kuwa vipi? Hata leo, bado mnapuuza kila neno la ukweli. Hamjui Mungu ni nini, hamjui Kristo ni nini, hamjui jinsi ya kumcha Yehova, hamjui jinsi ya kuingia katika kazi ya Roho Mtakatifu, na hamjui jinsi ya kutofautisha kati ya kazi ya Mungu Mwenyewe na uongo wa mwanadamu. Unajua tu kukashifu neno lolote la ukweli linaloelezwa na Mungu lisilolingana na mawazo yako. Unyenyekevu wako uko wapi? Utiifu wako uko wapi? Uaminifu wako uko wapi? Tamaa yako ya kupata ukweli iko wapi? Uchaji Mungu wako uko wapi? Nawaambieni, wale wanaoamini katika Mungu kwa sababu ya ishara hakika ni kikundi ambacho kitapata kuangamizwa. Wale wasio na uwezo wa kukubali maneno ya Yesu Ambaye Amerudi kwa mwili kwa hakika ni vizazi vya kuzimu, vizazi vya malaika mkuu, kikundi ambacho kitakabiliwa na kuangamizwa kwa milele. Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayeidaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Utaashiria mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi, na utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba “Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo” watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Atawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wenye kiburi sana. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika. Nawashauri mtembee katika njia ya kuamini katika Mungu kwa uangalifu. Msiwe wepesi wa kuamua bila kuzingatia suala zima; kilicho zaidi, msiwe kawaida na wenye kutojali katika imani yenu kwa Mungu. Mnafaa kujua kwamba, angalau, wale wanaoamini Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wenye kucha. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali wanaudharau ni wajinga na wapumbavu. Wale ambao wameusikia ukweli ilhali bila kujali wanaamua mambo bila kuzingatia kila kitu ama kuukashifu wamejawa na kiburi. Hakuna anayeamini katika Yesu anastahili kuwalaani au kuwahukumu wengine. Nyote mnafaa kuwa watu walio wenye mantiki na wanaoukubali ukweli. Pengine, baada ya kusikia njia ya kweli na kusoma neno la uzima, unaamini kuwa neno moja tu kati ya maneno haya elfu kumi ndiyo yanayolingana na dhana zako na Biblia, na kisha unafaa kuendelea kutafuta katika moja kati ya elfu kumi ya maneno haya. Bado Nawashauri muwe wanyenyekevu, msijiamini sana, na msijiinue juu sana. Moyo wako ukiwa na uchaji mdogo kama huu kwa Mungu, utapata mwanga mkuu. Ukichunguza kwa makini na kurudia kutafakari maneno haya, utapata kuelewa iwapo ni ukweli au la, na iwapo ni ya uzima au la. Pengine, baada ya kusoma tu sentensi chache, watu wengine watakashifu kwa upofu maneno haya, wakisema, “Hiki sicho chochote ila nuru kiasi ya Roho Mtakatifu,” ama, “Huyu ni Kristo wa uongo ambaye amekuja kuwadanganya watu.” Wale wanaosema vitu kama hivyo wamepofushwa na ujinga! Unaelewa kiasi kidogo sana kuhusu kazi na hekima ya Mungu, na Nakushauri uanze tena kutoka mwanzo! Hamfai kuyakashifu kwa upofu maneno yaliyonenwa na Mungu kwa sababu ya kutokea kwa Makristo wa uongo katika siku za mwisho, na hampaswi kuwa watu wanaomkufuru Roho Mtakatifu kwa sababu mnaogopa kudanganywa. Je, hiyo haitakuwa hali kubwa ya kuhuzunisha? Iwapo, baada ya uchunguzi mwingi, bado unaamini kuwa maneno haya si ukweli, si njia, na si maonyesho ya Mungu, basi utaadhibiwa hatimaye, na kuwa bila baraka. Iwapo huwezi kukubali ukweli kama huu ulionenwa wazi sana na kwa kawaida sana, basi wewe si ni asiyefaa kwa wokovu wa Mungu? Je, wewe si mtu ambaye hana bahati ya kutosha kurejea mbele za kiti cha enzi cha Mungu? Waza kuhusu hili! Usiwe mwenye pupa wala wa haraka, na usiichukulie imani kwa Mungu kama mchezo. Fikiria kwa ajili ya hatima yako, kwa ajili ya matarajio yako, kwa ajili ya maisha yako, na usifanye mchezo na nafsi yako. Je, unaweza kuyakubali maneno haya?
Chanzo: Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia
Tufuate: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni