Neno la Mwenyezi Mungu | Utendaji (1)
Mbeleni, kulikuwa na kupotoka kwingi katika jinsi watu walipata uzoefu, na kungeweza hata kuwa kwa ajabu. Kwa sababu tu hawakuelewa viwango vya mahitaji ya Mungu, kulikuwa na maeneo mengi ambayo uzoefu wa watu ulienda kombo. Sharti la Mungu kwa mtu ni kwao kuwa na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida. Njia za mtu wa kisasa kuhusiana na chakula na mavazi, kwa mfano. Wanaweza kuvaa suti na tai na wanaweza kujifunza kiasi kuhusu sanaa ya kisasa, na katika muda wao wa ziada wanaweza kuwa na kiasi fulani cha fasihi na maisha ya burudani.
Wanaweza kuchukua baadhi ya picha za kumbukumbu na wanaweza kusoma na kupata kiasi cha elimu, na kuwa na mazingira mazuri kiasi ya kuishi. Haya ndiyo maisha ambayo yanastahili ubinadamu wa kawaida, ilhali watu wanayaona kama kitu kinachochukiwa na Mungu. Utendaji wao tu ni wao kufuata kanuni chache, na hii huwasababisha kuishi maisha yanayochosha sana, bila maana yoyote. Katika hali halisi, Mungu hajawahi kumhitaji mtu kufanya hivyo. Watu wanataka kukatiza tabia zao wenyewe, wakiomba bila kukoma katika roho zao ili wawe karibu na Mungu, mawazo yao daima yakiwa yamemilikiwa na kufikiria kuhusu mambo ya kimungu, macho yao mara kwa mara yakiangalia huku na kule, wakiangalia suala hili na suala lile, wakihofia kwa kiasi kikubwa kwamba uhusiano wao kwa Mungu utatengwa kwa namna fulani. Haya ni mambo yote ambayo mtu amejijumlishia mwenyewe; ni sheria ambazo zimewekwa kwa ajili ya mtu na mtu wenyewe. Usipoelewa kiini chako mwenyewe au kile kiwango ambacho mwenyewe unaweza kufikia, basi hutakuwa na namna yoyote ya kufahamu hasa viwango ni vipi ambavyo Mungu anahitaji kwa ajili ya mtu, na basi hutakuwa na namna yoyote ya kupata matendo ambayo yanatekelezwa katika hatua mwafaka. Akili yako daima inageuka upande huu na ule, unafikiria kila namna iwezekanayo kujifunza na kuhisi njia yako jinsi gani unaweza kusisimuliwa na kupata nuru kwa Roho Mtakatifu, na matokeo kwamba unaweka muhtasari seti za njia za kutenda ambazo unadhani zitakusaidia kupata kuingia. Unapotenda kwa njia hii, hujui nini hasa ambacho Mungu anataka kutoka kwako; unatenda tu kwa njia yako mwenyewe, ukihisi starehe kabisa, bila kujali kuhusu matokeo wala kujali hata kidogo kuhusu iwapo kupotoka na makosa yapo. unapoendelea kwa njia hii, kutenda kwako kunakosa mambo mengi makubwa, kama vile pongezi ya Mungu, uthibitisho na Roho Mtakatifu na matokeo yanayopatikana kwa matakwa ya Mungu. Hata inakosa ubinadamu wowote wa kawaida au hisia za kawaida za mtu za mantiki. Kutenda kwako ni kufuata sheria tu, au kwamba uendelee kuongeza mzigo wako kimakusudi ili ujizuie, ili ujidhibiti. Na hata unafikiri kuwa kutenda kwako kuko sahihi, bila kujua kwamba sehemu kubwa ya kile unachotenda ni mchakato au utunzaji ambao si lazima. Kuna wengi ambao wanatenda hivi kwa miaka mingi bila mabadiliko kimsingi katika tabia zao, bila ufahamu mpya, na bila kuingia kupya. Wanazitekeleza kwa kutojua asili zao za kinyama, hata hadi hatua ambapo kuna mara nyingi wakati wanafanya mambo bila busara, mambo ya kinyama na mara nyingi wakifanya mambo ambayo huwapa watu kusita na ambayo hayaeleweki. Je, si aina hii ya mtu ni mtu ambaye amebadilika?
Sasa, kuzungumza kwa kiasi, watu huomba kidogo sasa ikilinganishwa na mbeleni kwa kuwa sasa si enzi ya kutafuta na kuhisi njia ya mtu ya kufuata. Sasa ni enzi ya ufunuo, Enzi ya Ufalme, ni maisha ya ufahamu ambapo vitu vyote vinaelezwa waziwazi kwa mtu, na mtu haachwi tena kuihisi njia katika maisha. Kuhusu masuala ya ndoa, mambo ya kidunia, maisha, chakula, mavazi na malazi, mahusiano kati ya watu, jinsi mtu anaweza kuhudumu katika njia ambayo inayakidhi mapenzi ya Mungu, jinsi mtu anavyoweza kuuacha mwili..., yepi kati ya haya hayajaambiwa kwenu? Je, bado mnahitaji kwenda kutafuta? Je, bado mnahitaji kuomba? Haina haja kweli! Kama bado unafanya vitu hivi, si unaongeza safu nyingine ya urasmi? Si lazima! Muhimu ni kama una azimio au la. Baadhi ya watu wanatenda kosa kwa kujua, na wanajua wazi kwamba kutembea njia ya dunia si vizuri, kwamba huleta hasara kwa maisha ya mtu na kuchelewesha maendeleo yao ya maisha, lakini wanasisitiza kulifanya, nao wanafanya hivyo baada ya kuomba na kutafuta. Je, si hii ni kutenda kosa kwa kujua? Kama wale wanaotamani sana anasa za mwili na kushikilia utajiri, ambaye baadaye anamwomba Mungu akisema: “Mungu! Je, Unaniruhusu nishikilie anasa za mwili na kushikilia utajiri? Je, ni mapenzi Yako nipate fedha kwa njia hii?” Je, hii ni njia ya kufaa kuomba? Ikiwa wanajua vizuri kabisa kwamba Mungu hafurahii mambo haya basi yanapaswa kuachiliwa, lakini mambo haya yameimarishwa katika mioyo nao wanaomba na kutafuta ili kumlazimisha Mungu kuwakubalia na kumfanya Mungu awape jibu. Kisha kuna wale ambao huwaleta ndugu wa kanisa upande wao na kuanzisha falme huru zao wenyewe. Unajua vizuri sana kwamba matendo haya yanamwasi Mungu, lakini bado unaenda kumtafuta na kumwomba Mungu. Wewe ni sugu na, ukifanya mambo hivi, bado unaweza kuonekana ukimwomba Mungu kwa ujasiri mkubwa na utulivu. Kweli huna aibu! Kuhusu kutembea njia ya dunia, hili limehubiriwa kwa muda mrefu mbeleni. Linachukiwa sana na Mungu, lakini bado unaomba, ukisema: “Ee Mungu! Unaniruhusu kutembea njia ya kidunia? Naweza kuyakidhi mapenzi Yako kwa njia hii? Kwa kweli, nia zangu ni sahihi. Sifanyi hivi kwa ajili ya mwili; nafanya hivi ili jina Lako lisitiwe aibu, nafanya hivyo kwa utukufu Wako, ili watu wa kidunia waweze kuona utukufu Wako ndani yangu. “Je, si njia hii ya kuomba ni upuuzi? Huoni aibu? Na si wewe unakuwa mjinga zaidi kufikiri kwamba hiki ni kitu cha thamani cha kufanya? Huna nia ya kupata uzoefu wa maisha ya mwanga, badala yake unakwenda kwa makusudi kuyaonja yale maisha katika giza na kuteseka. Hivyo si wewe unatafuta tu kuteseka? Umeambiwa jinsi ya kuishi maisha ya kiroho, maisha ya ubinadamu wa kawaida na umeambiwa kuhusu masuala yote ya ukweli. Kama huelewi kitu basi kiangalie moja kwa moja. Je, bado unahitaji kuyafunga macho yako na kuomba? Kama bado unaenda kutafuta kwa kuyaelekeza macho yako mbinguni, si bado unamwamini Mungu wa mashaka? Awali uliona matokeo kutokana na kutafuta kwako na kuomba na Roho Mtakatifu Aliisisimua roho yako kwa kiasi fulani kwa sababu wakati huo alikuwa Enzi ya Neema. Hukuweza kumwona Mungu hivyo hukuwa na chaguo lakini unaihisi njia yako mbele na kwenda kutafuta hivyo. Sasa Mungu Amekuja kati ya mtu na Neno limeonekana katika mwili. Sasa unaweza kumwona Mungu, na hivyo Roho Mtakatifu Hafanyi kazi tena kama Alivyofanya mbeleni. Enzi imebadilika na pia namna ambavyo Roho Mtakatifu hufanya kazi. Ingawa maombi yanaweza kutekelezwa kidogo zaidi kuliko awali, kwa sababu Mungu yuko duniani mtu sasa anayo nafasi ya kumpenda Mungu. Wanadamu wameingia katika enzi ya kumpenda Mungu nao wanayo ndani yao ukaribu sahihi kwa Mungu: “Ee Mungu! Hakika Wewe ni mzuri, nami niko tayari kukupenda!” Maneno machache tu ya wazi na rahisi hutoa sauti kwa upendo wa Mungu ndani ya moyo wako na ni kuimarisha tu upendo kati yako na Mungu. Wakati mwingine unaweza kujiona ukionyesha uasi kiasi, ukisema: “Ee Mungu! Mbona mimi ni mwovu sana?” Kweli unataka kujipiga, na machozi machoni mwako. Kwa wakati huu, moyo wako unahisi kujuta na kuwa na dhiki lakini huna namna ya kuionyesha. Hii ni kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, lakini hili ni jambo tu ambalo wale wanaotafuta maisha wanaweza kufikia. Unahisi kwamba Mungu anao upendo mkubwa kwako nawe unahodhi hisia maalum, lakini huna maneno ya kuomba kwa uwazi. Daima unahisi, hata hivyo, kwamba upendo wa Mungu ni kama kina cha bahari lakini huna namna ya kuonyesha hali hii, daima ukiuhisi katika moyo wako lakini kamwe huna maneno sahihi ya kuuonyesha. Hii ni hali ambayo mara nyingi hutokea katika roho. Aina hii ya maombi na ushirika ndani ya moyo wako kwamba inalenga kuwa karibu na Mungu ni ya kawaida.
Ingawa sasa maisha ya kuhisi njia ya mtu ya kwenda mbele na kutafuta yameisha, hii si kusema kwamba watu wasiombe kamwe, wala si kusema kwamba watu hawahitaji kuyasubiri mapenzi ya Mungu kujifunua kabla ya kuendelea na kazi; hizi ni baadhi tu ya mawazo ya mtu kabla ya kuona. Mungu amekuja miongoni mwa mtu kuishi naye na kuwa mwanga wa mtu, maisha ya mtu na njia ya mtu, na huu ni ukweli. Bila shaka, katika kuja kwa Mungu duniani ni muhimu Kwake kumletea mtu njia ya vitendo ambayo inafaa vimo vyao na maisha kwao kufurahia—Hajaja kuharibu njia zote za matendo ya mtu. Mtu haishi tena kwa kuihisi njia yake kwenda mbele na kutafuta kwa sababu hii imebadilishwa na kuja kwa Mungu duniani kufanya kazi na kunena Neno Lake. Amekuja kumweka huru mtu kutoka katika maisha ya giza na kumpa maisha ya mwanga. Kazi ya sasa ni kuonyesha mambo kwa uwazi, kusema kwa uwazi, kumwambia mtu moja kwa moja na kufafanua mambo waziwazi, ili mtu aweze kuweka mambo haya katika matendo. Kama vile Yehova alivyowaongoza watu wa Israeli, akiwaambia jinsi ya kutoa sadaka na jinsi ya kujenga hekalu, hivyo huna haja tena ya kuishi maisha ya kutafuta kama ulivyofanya Bwana Yesu alipoondoka. Je, ni muhimu kwenu kuihisi njia yenu kwa ajili ya kazi ya baadaye ya kueneza injili? Je, ni muhimu kwenu kuihisi njia yenu ili mjue jinsi mnavyopaswa kuishi? Je, ni muhimu kwenu kuihisi njia yenu ili mjue jinsi mnavyopaswa kutekeleza majukumu yenu? Je, ni muhimu kwenu kujisujudu ardhini na kwenda kutafuta ili mjue jinsi mnapaswa kutoa ushahidi? Je, ni muhimu kwenu kufunga na kuomba ili mjue jinsi mnapaswa kuvaa au kuishi? Je, ni muhimu kwenu kustahimili katika maombi yenu kwa Mungu mbinguni ili mjue jinsi mnapaswa kukubali kushindwa? Je, ni muhimu kwenu kuomba bila kukoma siku nzima na usiku kucha ili mjue jinsi mnapaswa kutii? Kuna wengi miongoni mwenu wanaosema kwamba hamwezi kutenda kwa sababu hamwelewi. Watu kweli hawaizingatii kazi ya leo! Mengi ya mambo haya nimeyasema muda mrefu uliopita, ni kwamba tu hamkuzingatia, hivyo si ajabu hamjui. Bila shaka, katika enzi ya leo Roho Mtakatifu bado Hajawasisimua watu ili kuwaruhusu kuhisi starehe, Naye anaishi pamoja na mtu. Hizi ni baadhi ya hisia maalum na zenye kuanisi ambazo mara nyingi hutokea katika maisha yako. Kila mara moja kwa wakati siku inakuja ambapo unahisi kwamba Mungu ni wa kupendeka sana nawe huwezi kutenda lingine ila kumwomba Mungu: “Ee Mungu! Upendo wako ni mzuri sana na picha Yako ni kubwa sana. Natamani kukupenda kwa undani zaidi. Natamani kutoa yote niliyo ili kuyatumia maisha yangu yote. Mradi ni kwa ajili Yako, natamani kutoa kila kitu kwako, ili tu kwamba iweze kukupenda Wewe....” Hii ni hisia ya furaha uliyopewa na Roho Mtakatifu. Si kupata nuru, wala mwangaza, ni kuchochea. Aina hii ya uzoefu itatokea mara kwa mara, kama vile ukielekea kazini. Utaomba na kujihisi karibu na Mungu, kiasi kwamba machozi yataulowesha uso wako, utaongozwa kiasi kwamba huwezi kujizuia nawe utakuwa na wasiwasi wa kupata mazingira ya kufaa ambapo unaweza kuonyesha hamasa zote moyoni mwako.... Wakati mwingine utakuwa katika shughuli ya umma nawe utahisi kwamba upendo unaofurahia ni mwingi mno, na kwamba bahati yako si ya kawaida, na zaidi utahisi kwamba wewe ni bora zaidi kuliko mwingine yeyote. Utajua kwa undani kwamba Mungu anakuinua, kwamba huu ni upendo mkuu wa Mungu kwa ajili yako. Katika maficho ya ndani kabisa ya moyo wako utahisi kuwa kuna aina ya upendo kuhusu Mungu usioelezeka na usiosomeka; ni kama unaujua lakini huna namna ya kuuonyesha, siku zote ukikufanya ufikirie kwa makini lakini ukikuacha usiweze kuuonyesha kabisa. Wakati kama huu, hata utasahau ulipo, hadi pale ambapo utazungumza: “Ee Mungu! Ni vigumu sana kukuelewa, lakini Wewe unapendwa sana! “Wakati mwingine unaweza hata kufanya baadhi ya vitendo vya ajabu na vya kipkee ambavyo watu kuviona visivyoelezeka, na haya ni mambo yote ambayo yanaweza kutokea mara nyingi .... Aina hii ya maisha ni magumu mno katika uzoefu wenu na mambo haya ni maisha ambayo Roho Mtakatifu amekupa leo, na maisha ambayo unapaswa kuishi sasa. Si kukufanya uache kuishi maisha, bali kwamba namna unavyoishi inabadilika. Ni hisia ambazo haziwezi kuelezeka au kuonyeshwa. Pia ni hisia ya kweli ya mtu na hata zaidi ni kazi ya Roho Mtakatifu. Inakufanya uelewe katika moyo wako, lakini huna namna ya kuionyesha wazi kwa mtu yeyote hata kidogo. Si kwa sababu wewe si mwepesi wa kusema au kwamba wewe ni kigugumizi, lakini kwa sababu ni aina ya hisia ambayo haiwezi kuelezwa katika maneno. Anakuruhusu kufurahia mambo haya leo kwa sababu haya ni maisha unayopaswa kuishi. Bila shaka, maisha yako mengine si matupu, kwamba tu kusisimuliwa kwa njia hii kunakuwa aina ya furaha katika maisha yako ambayo yanakufanya kutaka kufurahia misisimko ya Roho Mtakatifu siku zote. Lakini unapaswa kujua kwamba kuhamasishwa kwa namna hii sio kwamba uweze kujitenga kutoka kwenye mwili na kwenda mbingu ya tatu, au kusafiri duniani, bali ni kuwa uweze kupata uzoefu wa upendo wa Mungu leo, upate uzoefu wa umuhimu wa kazi ya Mungu leo, kumbukia utunzaji na ulinzi wa Mungu. Mambo haya yote ni kwa ajili yako kuwa na maarifa zaidi ya kazi ya Mungu hufanya leo na kuwa na uwezo wa kuhisi na kupata uzoefu zaidi wa upendo wa Mungu ambao unaufurahia leo—hili ni lengo la kazi hii.
Maisha ya kutafuta na kuihisi njia ya mtu yalikuwa wakati Mungu alikuwa bado hajakuwa mwili. Wakati huo watu hawangeweza kumwona Mungu na hivyo hawakuwa na chaguo lakini kutafuta na kuihisi njia yake kuendelea. Leo unaweza kumwona Mungu naye Anakwambia moja kwa moja jinsi unapaswa kutenda ili usihitaji tena kuihisi njia yako hapa na pale au kutafuta tena. Njia inayooongozwa naye ni njia ya ukweli na yale Anayomwelezea mtu, kile mtu anachokipata ni maisha na ukweli. Unaweza kuwa na njia nau kweli wa maisha, hivyo haja gani ipo kwenda kutafuta mahali popote? Roho Mtakatifu hawezi kufanya hatua mbili za kazi kwa pamoja. Kama, wakati Nimemaliza kuzungumza neno Langu, watu bado wanahitaji kuomba na kutafuta, hiyo haitamaanisha kwamba hatua hii ya kazi Ninayoifanya inafanywa bure? Ingawa Naweza kuwa nimemaliza kunena neno Langu, watu bado hawaelewi kabisa, na hii ni kwa sababu wanakosa ubora. Tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa njia ya maisha ya kanisa na kupitia kushiriki mmoja kwa mwingine. Mbeleni, Mungu aliyekuwa mwili hakuanza kazi, hivyo Roho Mtakatifu alifanya kazi kwa njia hiyo wakati huo na kuidumisha kazi. Wakati huo Roho Mtakatifu aliifanya kazi, lakini sasa ni Mungu aliyekuwa mwili Mwenyewe ambaye anaifanya, baada ya kuchukua nafasi ya kazi ya Roho Mtakatifu. Wakati watu waliomba mbeleni, walipata amani, furaha, lawama na nidhamu na hii yote ilikuwa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Sasa hali hizi ni chache na nadra. Mbona wakati Petro aliomba hakuwa na hisia za amani au za lawama, na kwa nini Paulo na wengine pia walihisi hivyo walipoomba? Hii ilikuwa kwa sababu ulikuwa ni wakati ambao kuonekana kwa Mungu hakukuwa kumeonekana, na zaidi ya hayo ulikuwa wakati wa Enzi ya Neema wakati Mungu alifanya kazi tofauti. Roho Mtakatifu anaweza tu kufanya aina moja ya kazi katika enzi yoyote ile. Kama Angefanya aina mbili za kazi wakati huo huo, mwili ukifanya aina moja na Roho Mtakatifu Akifanya aina nyingine ndani ya watu, na kama kile mwili ulisema haikuwa halali na kile Roho Alifany kilikuwa, basi Kristo asingekuwa na ukweli wowote, njia au maisha ya kuyataja. Huku kungekuwa kujipinga, na kungekuwa makosa katika chanzo hasa.
Watu walipotoka sana na walifanya makosa mengi mno katika uzoefu wao wa zamani. Awali kulikuwa na baadhi ya mambo ambayo watu wa ubinadamu wa kawaida walikuwa wamenuiwa kuwa nayo, na kunuiwa kufanya, au kulikuwa na makosa yasiyoepukika ambayo yalinuiwa kuonekana katika maisha ya binadamu, na wakati mambo hayo yalitendwa vibaya, waliliweka jukumu hilo kwa Mungu. Kulikuwa na dada ambaye alikuwa na wageni nyumbani kwake. Maandazi yake yaliyochomeka hayakuchemshwa vyema, hivyo akafikiri:: “Hii inaweza kuwa nidhamu ya Mungu. Mungu anaushughulika moyo wangu usiofaa. Mimi sifai kabisa.” Kwa kweli, alimradi njia ya kawaida ya mtu ya kufikiri inavyohusu, wageni wanapokuja unapata msisimko na kukimbia huku na kule, bila kujua nini cha kufanya kwanza na bila kuwa umepangwa unachofanya, matokeo yake ni kwamba ikiwa wali hautaishia kuungua, basi vyakula vyako vina na chumvi nyingi sana. Kwa kawaida, bila wageni uko sawa, lakini wakati ambapo watu wanakuja kila kitu kinakwenda mrama. Hali hii inasababishwa na hisia za msisimko, lakini watu huishia kudhania kuwa ni “nidhamu ya Mungu.” Kwa kweli, hii inafungamana na makosa katika maisha ya binadamu. Je, hungekumbana pia na aina hii ya kitu iwapo hukumwamini Mungu? Si aina hii ya kitu tukio la mara kwa mara? Kuna mambo mengi yanayofungamana na makosa ya watu; watu hufanya makosa, lakini hayafanywi na Roho Mtakatifu na hayamhusu Mungu. Kama unavyojiuma ulimi unapokula—yawezekana kuwa hii ni nidhamu ya Mungu? Nidhamu ya Mungu ina kanuni na kwa kawaida huonekana wakati unatenda kosa kwa kujua. Mungu humfundisha mtu nidhamu na mambo yanayohusu jina Lake, au wakati inahusu ushuhuda Wake au kazi Yake. Watu huuelewa ukweli vya kutosha sasa ili kuwa na ufahamu wa ndani wa mambo ya wanayoyafanya, kwa mfano: Je, unaweza kutohisi kitu unapozibadhiri fedha za kanisa au kuzitumia bila kujali? Utahisi kitu unapofanya hivyo. Haiwezekani kufanya kitu na kisha kuanza kuhisi kitu baadaye. Uko wazi moyoni mwako kuhusu mambo unayoyafanya ambayo yanaenda kinyume na dhamiri yako. Ingawa wanaweza kuujua ukweli kwa wazi, kwa sababu kila mtu anayo anayoyapenda, wao hujiingiza tu, hivyo baada ya wao kufanya kitu hawana hisia za wazi ya shutuma. Kama hawana nidhamu wakati wanapofanya makosa, nidhamu gani inaweza kuweko baadaye? Nidhamu gani inaweza kuweko baada ya fedha zote kubadhiriwa? Wao wana ufahamu kabisa wa nini wanachokifanya wanapofanya hivyo na kuhisi lawama. Usiposikiliza basi Mungu hatakupa usikivu. Utakapofika wakati ambapo hukumu ya haki inatokea, adhabu ataletwa juu ya kila mmoja kulingana na matendo yake. Kama mtu wa kawaida mwenye hisia ya mantiki, mtu ambaye ana dhamiri, una ufahamu wa kila kitu unachokifanya, hasa unapofanya kitu kibaya. Je, bado kuna watu wachache kanisani ambao hubadhiri fedha? Je, bado kuna watu wachache ambao hawaweki mipaka wazi kati ya wanaume na wanawake? Je, bado kuna watu wachache wanaohukumu, kupinga na kujaribu kuvunja mambo kwa siri? Kwa nini bado kila kitu kiko sawa nanyi? Nyote mnao ufahamu, hisia na aibu mioyoni mwenu na kwa sababu hii wakati mwingine mnateseka kuadibiwa na utakaso. Ni kwamba tu watu hawana aibu! Kama nidhamu kweli ingewafika, bado wangethubutu kutenda kwa njia hii? Wakati ambapo watu wa dhamiri hufanya mambo, wanahisi kufadhaika wakati dhamiri yao inachomwa kidogo tu, na kwa hiyo wana uwezo wa kuiacha miili yao. Kama wale wanaotenda dhambi kati ya wanaume na wanawake. Wanao ufahamu wa kile wanachofanya wakati huo, lakini tamaa yao ni kubwa mno na hawawezi kujidhibiti. Hata kama Roho Mtakatifu anatoa nidhamu, haitakuwa bure, hivyo Roho Mtakatifu hajishughulishi nawe tena. Wakati huo, kama Roho Mtakatifu hakukufundisha nidhamu, kukulaumu au kukifanyia chochote mwili wako, lawama gani ingeweza kutokea baadaye? Nidhamu gani inaweza kuwa baada ya tendo kufanyika? Inathibitisha tu kwamba huna aibu na unapuuzwa. Wewe ni fidhuli usiye na maana! Roho Mtakatifu hafanyi kazi bila sababu. Ikiwa unaujua ukweli vizuri sana lakini hushirikiani na una uwezo wa kufanya kitu chochote kabisa, basi unaweza kusubiri tu hadi siku ile ambayo inakuja wakati ambapoutaadhibiwa pamoja na yule mwovu. Huu ni mwisho bora kwako! Sasa Nimehubiri nikirudia kuhusu dhamira, kwa kuwa hiki ni kiwango cha chini zaidi. Bila dhamira, watu pia watapoteza nidhamu ya Roho Mtakatifu, na wanaweza kufanya chochote wanachopenda. Ikiwa kweli mtu ana dhamira, basi wakati ambapo Roho Mtakatifu anamshutumu anapitia vita vya ndani, na basi hana uwezekano wa kufanya kitu chochote kikubwa mno. Haijalishi jinsi Roho Mtakatifu anafundisha nidhamu ama kuadibu, kwa ujumla watu wote watakuwa na hisia kiasi wanapofanya kitu kibaya. Hivyo watu sasa wanaelewa kila aina ya ukweli na kama hawautendi basi hiyo ni shauri yao. Siwajibu watu kama hawa, wala sishikilii tumaini lolote kwao. Unaweza kufanya unavyopenda!
Baadhi ya watu huja pamoja na kuliweka neno la Mungu upande mmoja, daima wakizungumza kuhusu jinsi mtu huyu au mtu yule alivyo. Bila shaka ni vizuri kuwa na upambanuzi mdogo, kwa kuwa bila kujali unapokwenda hutadanganywa kwa urahisi, wala hautalaghaiwa au kupumbazwa kwa urahisi; hiki pia ni kipengele ambacho watu wanapaswa kumiliki. Lakini usilenge tu katika suala hili kwa kuwa linafungamanishwa na mambo ambayo ni hasi. Macho yasikaziwe daima kwa watu. Ufahamu wako wa jinsi Roho Mtakatifu anafanya kazi sasa ni kidogo mno, imani yako katika Mungu ni ya juujuu sana, nawe unayo mambo machache mno mazuri. Yule unayemwamini ni Mungu, Yule unayehitaji kumwelewa ni Mungu, si Shetani. Ikiwa unaelewa tu jinsi Shetani anafanya kazi na kuwa na ufahamu wa njia zote ambazo roho mbaya zinafanya kazi, lakini huna ujuzi wa Mungu kwa lolote, haya yatakuwa na maana gani? Je, si ni Mungu unayemwamini leo? Kwa nini ufahamu wako hauhusishi mambo haya mazuri? Hutilii tu maanani kipengele chanya cha kuingia na huna ufahamu wake, hivyo nini unachotaka kupata? Je, hujui jinsi unapaswa kutafuta? Unavyo vifaa vingi hasi “vya kufundishia” lakini unaambulia patupu na suala chanya la kuingia, hivyo ni jinsi gani kimo chako kitawahi kukua? Mtu akizungumza tu kuhusu vita na Shetani, ni matarajio yapi ya baadaye ya maendeleo mtu huyo atakuwa nayo? Si kuingia kwako kumepitwa na wakati sana? Mambo gani utakayoweza kupata kutokana na kazi ya sasa ukiendelea kwa njia hii? Kile ambacho ni muhimu sasa ni wewe uelewe nini Mungu anataka kufanya sasa, jinsi binadamu anapaswa kushirikiana, jinsi wanavyopaswa kumpenda Mungu, jinsi wanavyopaswa kuielewa kazi ya Roho Mtakatifu, jinsi wanavyopaswa kuingia katika maneno yote ambayo Mungu anasema leo, jinsi wanavyopaswa kuyaona, kuyaelewa na kuwa na uzoefu kwayo, jinsi yanavyopaswa kuyakidhi mapenzi ya Mungu, kushindwa kabisa na Mungu na kutii mbele za Mungu .... Unapaswa kulenga mambo haya kwa kuwa haya ni mambo yanayopaswa kuingiwa sasa. Je, unaelewa? Kuna faida gani kulenga tu juu kuhusu utambuzi wa watu? Unaweza kumtambua Shetani hapa, kuzitambua roho mbaya huko, unauweza kutambua mambo mengi, kuwa na ufahamu kamili wa roho mbaya na kuijua moja mara tu unapoiona. Lakini kama huwezi kusema chochote kuhusu kazi ya Mungu, utambuzi wako unaweza kuchukua nafasi ya ufahamu wako kuhusu Mungu? Hapo awali Nimeshiriki kuhusu maonyesho ya kazi ya roho mbaya, lakini hili si jambo kuu. Bila shaka watu wanapaswa pia kuwa na ufahamu kidogo kwa kuwa hili ni suala ambalo wale wanaomtumikia Mungu wanapaswa kumiliki ili kuepuka kufanya mambo ya kipuuzi na kuikatiza kazi ya Mungu. Lakini jambo muhimu zaidi linabaki kuwa na elimu ya kazi ya Mungu na kuelewa mapenzi ya Mungu. Ni ufahamu gani ulio nao wa hatua hii ya kazi ya Mungu? Je, unaweza kusema ni nini ambacho Mungu anafanya, mapenzi ya Mungu ni yepi, na unaweza kusema mapungufu yako ni yapi na mambo unayopaswa kujiandaa nayo? Je, unaweza kusema kuingia kwako kupya zaidi ni nini? Unapaswa kuelewa maingio yepi ya zamani yalikuwa mikengeuko na makosa, na maingio yepi yalikuwa yamepitwa na wakati. Unapaswa kupata tuzo na ufahamu katika maingio yako mapya. Usijidai kuwa ujinga; lazima ufanye juhudi katika maingio yako mapya ili uimarishe uzoefu na ufahamu wako mwenyewe, na hata zaidi lazima ufahamu sana hasa maingio yako mapya zaidi na njia sahihi zaidi ya kupata uzoefu. Lazima pia ujue jinsi ya kuzitupilia mbali mbinu zako za kutenda zilizopitwa na wakati na kuingia katika uzoefu mpya. Hata zaidi hivyo unapaswa kutambua kutenda kwako kulikopitwa na wakati kutokana na kazi mpya na kuingia. Haya ni mambo ambayo sasa unahitaji kuelewa kwa haraka na kuingia ndani yake. Lazima ufahamu tofauti na uhusiano kati ya maingizo yako ya zamani na mapya. Kama huna ufahamu wa hali ya juu wa mambo haya, basi hutakuwa njia ya yoyote ya kuendelea, kwa kuwa hutaweza kuendelea na kazi ya Roho Mtakatifu. Sehemu kubwa ya kuingia kwako kwa zamani na uzoefu iliungamanishwa na njia ya kutenda ya kupotosha na yenye makosa, na sehemu kubwa ya huku ilikuwa namna ya kupata uzoefu ambao ulikuwa wa wakati uliopita; lazima uelewe jinsi unavyopaswa kuwa na mtazamo wa vitu hivyo. Kwa njia ya kula kwa sahihi na kunywa neno la Mungu na kupitia ushirika mzuri, lazima uwe na uwezo wa kubadilisha dhana zako za kutenda za zamani na dhana zako za desturi za jadi, ili uweze kuingia katika kutenda kupya, na kuingia katika kazi mpya. Haya ni mambo unayopaswa kupata. Sasa Sikusihi kwamba ujielewe hadi kiwango kidogo zaidi; Sikusihi ulichukue hili kwa umakini sana.. Badala yake Nakusihi kuchukulia kwa umakini kuingia kwako na ufahamu wa kipengele chanya. Ingawa unaweza “kujijua,” haifuati kwa lazima kwamba hii ni kimo chako cha kweli. Lakini kama unaweza kupata uzoefu wa kutenda na kuingia kwa kazi mpya, hadi pale ambapo unaweza kufahamu na dhana zako binafsi zilikuwa nini au kutokuelewana, basi hiki ni kimo wako cha kweli nacho ni kitu unapaswa kumiliki. Haya ni mambo ambayo kila mtu kati yenu anapaswa kupata.
Kuna mambo mengi ambayo ninyi hamjui tu jinsi ya kutenda, hata zaidi kujua jinsi Roho Mtakatifu anafanya kazi. Wakati mwingine unafanya kitu ambacho kwa wazi hakimtii Roho Mtakatifu. Tayari una ufahamu wa kanuni ya kitu kupitia kula kwako na kunywa, hivyo unasumbuliwa kwa ndani na hisia ya lawama na kufadhaika na bila shaka hii ni hisia kuwa mtu ataihisi kwa misingi ya kuujua ukweli. Kutoshirikiana na kutofanya mambo kulingana na neno leo huipinga kazi ya Roho Mtakatifu na mtu lazima atahisi kufadhaika ndani mwake. Unaelewa kanuni za kipengele hiki lakini hutendi ipasavyo, hivyo unateswa na hisia ya lawama kwa ndani. Lakini kama huelewi kanuni hii, na hujala wala kunywa suala hili la ukweli, kama huijui kabisa, basi si lazima uhisi hali ya lawama katika suala hili. Kuzalisha shutuma ya Roho Mtakatifu ni kwa masharti. Unafikiri kwamba kwa sababu hujaomba, hujashirikiana na Roho Mtakatifu, hujauachilia mzigo unaoubeba ndani yako, umeichelewesha kazi ya Roho Mtakatifu. Katika hali halisi haiwezi kucheleweshwa, na kama hutasema kitu basi Roho Mtakatifu Atamchochea mtu mwingine kukisema; Roho Mtakatifu Hazuiliwi nawe. Unahisi kutubu kwa Mungu na hili ni jambo unalopaswa kuhisi. Lakini Mungu hadhanii chochote na basi ni la zamani. Kama unaweza kupata kitu chochote au la ni shauri yako. Wakati mwingine dhamiri yako inahisi kama inateswa na shutuma, lakini hii si kupata nuru au mwangaza katika Roho Mtakatifu wakati huo, wala si lawama ya Roho Mtakatifu. Badala yake ni hisia katika dhamiri yako. Kama inahusisha jina la Mungu, ushuhuda wa Mungu au kazi ya Mungu, na wewe unatenda ovyo ovyp, basi Yeye hatakuachilia. Lakini ina kikomo, na kwa mambo ambayo ni vigumu kuyataja, Hatajishughulisha nawe, Atakupuuza, na hivyo hili ni jambo ambalo unapaswa kulihisi katika dhamiri yako. Baadhi ya mambo ni yale ambayo watu wa ubinadamu wa kawaida wanapaswa kuyafanya na baadhi ni mambo ya maisha ya binadamu ya kawaida. Kwa mfano, huchemshi maandazi vyema na kusema kuwa Mungu Anakuadhibu—hii ni kitu kisicho na mantiki kabisa kusema. Kabla ya kuja kumwamini Mungu, aina hii ya kitu hakikutokea mara nyingi? Je, ilikuwa ni Shetani akikuadhibu hapo awali? Kwa kweli unapotenda zaidi kuhusu jambo hili, hutakuwa na uwezekano wa kutenda makosa, ni ubongo wako tu ambao unafanya makosa. Unahisi kwamba inaonekana kuwa nidhamu ya Roho Mtakatifu wakati kwa kweli hivi sivyo (baadhi hali za kipekee kando), kwa sababu kazi hii haifanywi kabisa na Roho Mtakatifu, lakini badala yake ni hisia tu ambazo watu wanazo. Lakini kufikiri kwa namna hii kile wale ambao wana imani sahihi katika Mungu wanapaswa kufanya. Hungeweza kufikiri hivi wakati ambapo hukumwamini Mungu. Mara ulipokuja kumwamini Mungu, moyo wako unatumia juhudi zote katika suala hili na kwa kutojua ulianza kufikiri kwa namna hii. Hii inatokana na mawazo ya kawaida ya watu na pia inafungamana na mawazo yao wenyewe. Lakini acha Nikwambie, hiki si kitu ambacho kiko chini ya eneo la kazi ya Roho Mtakatifu. Jambo hili linafungamana na mjibizo wa kawaida aliyopewa mtu na Roho Mtakatifu kwa njia ya kufikiri kwake mwenyewe; lakini lazima uelewekwamba mjibizo huu si kazi ya Roho Mtakatifu. Kuwa na aina hii ya “maarifa” haithibitishi kwamba unayo kazi ya Roho Mtakatifu. Uwlewa wako haufungamani na kupata nuru kwa Roho Mtakatifu, kiasi kidogo ni kazi ya Roho Mtakatifu. Ni mjibizo tu wa kufikiri kwa kawaida kwa watu na hauhusiani kamwe na kupata nuru au mwanga wa Roho Mtakatifu. Hayo ni mambo mawili tofauti kabisa na halifanywi kabisa na Roho Mtakatifu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ili kuwapa watu nuru, Yeye kwa ujumla kuwapa ufahamu wa kazi ya Mungu, na ya kuingia kwao ya kweli na hali ya ukweli, na pia Huwapa azimio, huwaruhusu kuelewa kusudi la hamu la Mungu na mahitaji yake kwa ajili ya mtu leo, Huwapa azimio la kufungua njia zote. Hata wakati ambapo watu wanapitia umwagaji damu na sadaka ni lazima watende kwa ajili ya Mungu, na hata kama wanakumbana na mateso na dhiki, lazima bado wampende Mungu, na wasiwe na majuto, na lazima wawe shahidi kwa Mungu. Azimio la aina hii ni misisimko ya Roho Mtakatifu, na kazi ya Roho Mtakatifu—lakini jua kwamba hujamilikiwa na misismko kama hii kila wakati. Wakati mwingine katika mikutano unaweza kuhisi kuongozwa mno na kupata msukumo nawe unatoa sifa kubwa zaidi na unacheza. Unahisi kwamba una ufahamu usioaminika wa yale wengine wanashiriki, unahisi mpya kabisa kwa ndani, na moyo wako uko wazi kabisa bila hisia yoyote ya utupu—haya yote yanaungamanishwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kama wewe ni mtu ambaye huongoza, na Roho Mtakatifu anakupa nuru na mwangaza usio wa kawaida unapoenda kanisani kufanya kazi, akikufanya uwe mwenye bidii wa kushangaza, mwenye kuwajibika na kitilia maanani kazi yako, hii inafungamanisha kazo ya Roho Mtakatifu.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni