Jumatano, 26 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (6)

Leo, watu wengi hawana hata urazini au kujitambua kwa Paulo, ambaye, ingawa aliangushwa na Bwana Yesu, tayari alikuwa na azimio la kufanya kazi na kuteseka kwa ajili Yake. Yesu alimpa ugonjwa, na baadaye, Paulo aliendelea kuvumilia ugonjwa huu mara alipoanza kufanya kazi. Kwa nini alisema alikuwa na mwiba mwilini mwake? Mwiba, kwa kweli, ulikuwa ugonjwa, na kwa Paulo, ulikuwa ugonjwa wa kufisha. Haijalishi alivyofanya kazi vizuri au jinsi azimio lake kuteseka lilivyokuwa kuu, alikuwa na ugonjwa huu kila mara. Paulo alikuwa mwenye uhodari thabiti zaidi kuliko ninyi watu wa leo; hakuwa tu mwenye uhodari mzuri, lakini pia alikuwa na kujitambua na alikuwa na urazini zaidi kuwaliko ninyi. Leo, usijali kutimiza urazini wa Petro—watu wengi hawawezi hata kutimiza urazini wa Paulo. Baada ya Paulo kuangushwa na Yesu, alikoma kuwatesa wanafunzi, na akaanza kuhubiri na kuteseka kwa ajili ya Yesu. Na ni nini kilichotia msukumo kuteseka kwake? Paulo aliamini kwamba, kwa vile alikuwa ameona nuru kuu, lazima awe na ushuhuda kwa Bwana Yesu, lazima asiwatese tena wanafunzi wa Yesu, na lazima asiipinge tena kazi ya Mungu. Baada ya yeye kuiona nuru kuu, alianza kuteseka kwa ajili ya Mungu, na kujitoa kwa dhati kwa Mungu, na akaweka azimio lake. Baada ya “nuru kuu” kumwangaza, alianza kumfanyia Mungu kazi, na aliweza kuweka azimio lake, lililothibitisha kwamba alikuwa na urazini. Katika dini, Paulo alikuwa mtu mwenye cheo kikubwa sana. Alikuwa mwenye maarifa mengi sana na mwenye kipaji, aliwadharau watu wengi zaidi, na alikuwa na nafsi thabiti zaidi kuliko wengi zaidi. Lakini baada ya “nuru kuu” kumwangaza, alisema kwamba lazima amfanyie Bwana Yesu kazi—na huu ulikuwa urazini wake. Wakati ambapo aliwatesa wanafunzi, Yesu alionekana kwake na kusema: “Paulo, mbona wanitesa Mimi?” Paulo alianguka chini papo hapo na kusema: “Wewe ni nani?” Sauti kutoka mbinguni ikasema: “Mimi ndimi Bwana Yesu, unayemtesa.” Mara moja, Paulo akaamka, akaelewa, na wakati huo tu ndipo alijua kwamba Yesu alikuwa Kristo, kwamba alikuwa Mungu. Lazima nitii, Mungu amenipa neema hii, na nilimtesa Yeye hivyo, ilhali Yeye hakuniangusha, wala Yeye hakunilaani mimi—lazima niteseke kwa ajili Yake. Paulo aligundua kwamba alikuwa amemtesa Bwana Yesu Kristo na sasa alikuwa akiwaua wanafunzi Wake, kwamba Mungu hakuwa amemlaani, bali alimwangazia nuru; hili lilimpa msukumo, na akasema: “Ingawa sikuuona uso Wake, niliisikia sauti Yake na kuiona nuru Yake kuu. Ni sasa tu ndipo naona kweli kwamba Mungu ananipenda kwa kweli, na kwamba Bwana Yesu Kristo kweli ni Mungu ambaye huwa na rehema kwa mwanadamu na Yeye husamehe dhambi za mwanadamu milele. Naona kweli kwamba mimi ni mwenye dhambi.” Ingawa, baadaye, Mungu alivitumia vipaji vya Paulo kufanya kazi, sahau hili kwa sasa. Azimio lake wakati huo, urazini wake wa binadamu wa kawaida, na kujitambua kwake—hamna uwezo wa kuyatimiza mambo haya. Leo, hamjapokea nuru tele? Je, watu wengi hawajaona kwamba tabia ya Mungu ni ile ya uadhama, ghadhabu, hukumu, na kuadibu? Mara nyingi laana, majaribio, na usafishaji vimewafika watu—na wamejifunza nini? Umepata chochote kutoka kwa kufunzwa nidhamu na kushughulikiwa kwako? Maneno makali, kuangamiza, na hukumu vimekufika wewe mara nyingi, ilhali huvitilii maanani. Wewe huna hata urazini kidogo ambao Paulo alikuwa nao—wewe sio mwenye maendeleo kidogo mno? Kulikuwa na mengi ambayo Paulo hakuyaona kwa dhahiri. Alijua tu kwamba nuru ilikuwa imemwangaza, na hakutambua kwamba alikuwa ameangushwa. Katika imani yake mwenyewe, baada ya nuru kumwangaza, lazima atumike kwa ajili ya Mungu, ateseke kwa ajili ya Mungu, afanye kila kitu ili kumwandalia Yesu Kristo njia, na kupata wenye dhambi wengi wakombolewe na Bwana. Hili lilikuwa azimio lake, na lengo pekee la kazi yake—lakini wakati ambapo alifanya kazi, ugonjwa bado haukumwacha, mpaka kufikia kifo chake. Paulo alifanya kazi kwa zaidi ya miaka ishirini. Alivumilia mengi, na alipitia mateso na majonzi mengi, ingawa, bila shaka, majaribio yake yalikuwa machache zaidi kuliko yale ya Petro. Ni la kusikitisha vipi kama ninyi hamna hata urazini wa Paulo? Katika hili, ni vipi ambavyo Mungu angeanzisha hata kazi kubwa zaidi ndani yenu?
Wakati ambapo alieneza injili, Paulo alivumilia mateso makubwa. Azimio lake, kazi aliyofanya, imani yake, uaminifu, upendo, uvumilivu, na unyenyekevu wakati huo, na tabia za nje nyingine nyingi alizoishi kwa kudhihirisha, zilikuwa za juu zaidi kuliko ninyi watu wa leo. Kuyaeleza kwa ukali zaidi, hakuna urazini wa kawaida ndani yenu! Ninyi hata hamna dhamiri au ubinadamu wowote—mnakosa mengi sana! Hivyo, wakati mwingi, katika yale mnayoishi kwa kudhihirisha hakuna urazini wa kawaida unaoweza kupatikana, na hakuna ishara ya kujitambua kokote. Ingawa mwili wa Paulo ulipatwa na ugonjwa, aliendelea kuomba na kutafuta: Huu ni ugonjwa gani—nimemfanyia Bwana kazi hii yote, kwa nini hauniachi? Yaweza kuwa kwamba Bwana Yesu ananijaribu? Je, Ameniangusha? Kama Angeniangusha, ningekufa wakati huo, na singeweza kumfanyia kazi hii yote, wala singeweza kupokea nuru tele hivi. Yeye pia alitambua azimio langu. Paulo kila mara alihisi kwamba ugonjwa huu ulikuwa ni kujaribiwa kwake na Mungu, kwamba ulikuwa unatuliza imani yake na utashi—hili ndilo alilofikiri. Kwa kweli, ugonjwa wake ulikuwa matokeo kutoka kwa wakati Bwana Yesu alipomwangusha yeye. Ulimweka chini ya shinikizo la akili, na kuondoa nyingi ya tabia yake asi. Mkijikuta katika hali za Paulo, mngefanya nini? Je, azimio lenu lingekuwa kuu kuliko la Paulo? Mna uwezo zaidi wa kuteseka kuliko yeye? Wakati ambapo watu wa leo huumizwa na ugonjwa fulani mdogo au kupitia majaribio makuu, kuteseka kwao huwaacha wametiwa wasiwasi kabisa. Kama mngefungiwa ndani ya tundu la ndege na kutotolewa nje kamwe mngekuwa sawa. Na kila kitu ambacho mngehitaji kula na kunywa lazima kiandaliwe, la sivyo mngekuwa kama mbwa mwitu. Kupitia kikwazo au ugumu kidogo ni vyema kwenu; kama mngepewa utulivu kuhusu hilo mngepotezwa, na ungewezaje kulindwa? Leo, ni kwa sababu ninyi huadibiwa, hulaaniwa, na huhukumiwa ndipo ninyi hupewa ulinzi. Ni kwa sababu mmepitia mengi ndipo ninyi hulindwa. La sivyo, mngekuwa mmetumbukia katika uharibifu zamani. Sifanyi mambo yawe magumu kwenu kwa kudhamiria—asili ya mwanadamu imefanywa madhubuti kwa imara, na lazima iwe hivi ili tabia za watu zibadilishwe. Leo, ninyi hamna hata urazini au kujitambua kwa Paulo, wala hamna dhamiri yake. Ninyi kila mara lazima mshurutishwe, na ninyi kila mara lazima muadibiwe na kuhukumiwa ili kuamsha roho zenu. Kuadibu na hukumu ndivyo vilivyo bora zaidi kwa maisha yenu. Na kama inabidi, lazima pia kuwe na kuadibu kwa ufikaji wa ukweli; ni wakati huo tu ndipo utatii kwa ukamilifu. Asili zenu ni kiasi kwamba bila kuadibu na laana, mngekuwa hamko radhi kuinamisha vichwa vyenu, mngekuwa hamko radhi kutii. Bila ukweli mbele ya macho yenu, hakungekuwa na athari. Ninyi ni duni mno na wasio thamani katika hulka! Bila kuadibu na hukumu, ingekuwa vigumu ninyi kushindwa, na vigumu kwa udhalimu na kutotii kwenu kukomeshwa. Asili yenu ya zamani imekita mizizi sana. Kama mngewekwa juu ya kiti cha enzi, hamngekuwa na habari kuhusu kimo cha mbingu na kina cha dunia, sembuse mlikokuwa mkielekea. Ninyi hata hamjui mlikotoka, kwa hiyo mngemjuaje Muumba? Bila kuadibu na laana ya wakati wa kufaa ya leo, siku zenu za mwisho zingekuwa zimefika kitambo. Sembuse majaliwa yenu—hilo haliko hatarini hata zaidi? Bila kuadibu na hukumu hii ya wakati wa kufaa, nani ajuaye vile mngekuwa wenye kiburi, na nani ajuaye vile mngekuwa wapotovu. Kuadibu huku na hukumu imewafikisha leo, na imehifadhi kuishi kwenu. Kama bado “mngefunzwa” kwa kutumia mbinu sawa na zile za “baba” yenu, nani ajuaye ni ulimwengu upi ambao mngeingia ndani! Hamna uwezo wowote wa kudhibiti na kutafakari kuhusu ninyi wenyewe. Inatosha kwa watu kama ninyi, kufuata tu, kutii, na kutoingilia au kuvuruga ili malengo Yangu yatimie. Hampaswi kutenda bora zaidi katika kukubali kuadibu na hukumu ya leo? Ni machaguo gani mengine mliyonayo? Paulo alipomwona Bwana Yesu, bado hakuamini. Baadaye, baada ya Bwana Yesu kugongomelewa msalabani, alijua ukweli huu, ilhali aliendelea kutesa na kupinga. Hii ndiyo maana ya kutenda dhambi kwa hiari, na kwa hivyo aliangushwa. Hapo mwanzo, alijua kulikuwa na Mfalme miongoni mwa Wayahudi aliyeitwa Yesu, alikuwa amesikia hili. Baadaye, alipotoa mahubiri katika hekalu na kuhubiri kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa nchi, alimpinga Yesu, na alikataa kwa kiburi kumtii mwanadamu yeyote. Mambo haya yalikuwa kizuizi kikubwa mno kwa kazi wakati huo. Yesu alipokuwa akifanya kazi, Paulo hakuwatesa na kuwashika watu moja kwa moja, bali alitumia kuhubiri na maneno kuivuruga kazi. Baadaye, wakati ambapo Bwana Yesu Kristo aliwekwa juu ya msalaba, alianza kuwashika wanafunzi, akikimbia kila mahali na kufanya yote ambayo angeweza ili kuwasumbua. Ni baada tu ya “nuru” kumwangaza ndipo aliamshwa na kupitia majuto makuu. Baada ya yeye kuangushwa, ugonjwa wake haukumwacha. Wakati mwingine, alihisi kwamba mateso yake yalizidi kuwa mabaya, na hangeweza kusimama. Alifikiri[a]: “Ni nini kinaendelea? Je, nimeangushwa kweli?” Kisha, bila kujua vile lilifanyika, angejikuta alikuwa na nafuu tena, na angeanza kufanya kazi tena. Lakini ugonjwa haukumwacha kamwe, na ilikuwa kwa sababu ya ugonjwa huu ndio alifanya kazi nyingi. Inaweza kusemwa kwamba Yesu aliweka ugonjwa huu ndani ya Paulo kwa sababu ya kiburi na majivuno yake; ilikuwa ni adhabu kwake, lakini pia kwa ajili ya kazi kuu zaidi ya Yesu—Yesu alitumia vipaji vya Paulo kwa ajili ya kazi Yake. Kwa kweli, halikuwa kusudi la Yesu kumwokoa Paulo, bali kumtumia yeye. Ilhali tabia ya Paulo ilikuwa ya kiburi na ya kusudi mno, na kwa hiyo “mwiba” uliwekwa ndani yake. Kuna wengi miongoni mwenu kama Paulo, lakini kama kweli mna azimio la kufuata mpaka mwisho kabisa, hamtateswa. Hatimaye, kufikia wakati ambapo Paulo alimaliza kazi yake, ugonjwa huo haukuonekana wa kuumiza sana kwake, na hivyo baadaye aliweza kuyasema maneno “Nimepigana vita vizuri, nimeutimiza mwendo wangu, nimeihifadhi imani: Kutoka sasa kuendelea taji la haki limewekwa kwangu”—aliyosema kwa sababu hakujua. Hatutazungumza kuhusu jambo lingine lolote, hebu tuendelee na sehemu yake ambayo ilikuwa nzuri na ya kustahili kusifiwa. Alikuwa na dhamiri, na baada ya nuru kumwangaza alijitolea kwa Mungu na akateseka kwa ajili ya Mungu. Kwa kawaida, huu ni upande wake wa kustahili kusifiwa, huu ulikuwa uwezo wake. Hatutazungumza kuhusu vile aliasi na kupinga; sisi huzungumza hasa kuhusu urazini wake wa mwanadamu wa kawaida, na kama alikuwa na kujitambua au la. Kama kuna wale ambao huamini hilo, kwa sababu alikuwa na uwezo, hili linathibitisha kwamba alikuwa mtu aliyebarikiwa, ambao huamini kwamba hakuadibiwa kwa lazima, basi haya ni maneno ya watu wasio na akili.
Mara Ninapomaliza kuzungumza nao ana kwa ana, watu wengi mara nyingine huwa wapotovu bila Mimi kujua, wakikosa kufikiria maneno Yangu ni muhimu. Mara kwa mara Mimi huzungumza, Nikifichua safu baada ya safu, na mpaka safu ya chini kabisa ifichuliwe, wao “hupata amani,” na kutosababisha taabu zaidi. Hali zenu zikiwa kama zilivyo leo, bado lazima ninyi mshambuliwe na kufichuliwa kikatili, na kuhukumiwa utondoti kwa utondoti, ili msiweze hata kuziba pumzi yenu. Ninyi lazima kila mara mpigwe na kufichuliwa, na kwenu ninyi inaonekana kana kwamba kuadibu hakuwaachi kamwe, kwamba laana, pia, haiondoki kamwe kwenu, wala hukumu kali, kuwakubalia ninyi kuona kwamba mkono wa amri za usimamizi wa Mungu haziondoki kwenu kamwe. Hili ni bora zaidi, ni kama wakati ambapo Haruni aliona kwamba Yehova hakumwacha yeye kamwe. (Lakini alichoona ni uongozi na ulinzi wa daima wa Yehova; uongozi mnaoona leo ni kuadibu, laana, na hukumu.) Leo, mkono wa amri za usimamizi wa Yehova hauwaachi ninyi pia, lakini kuna jambo moja mnaloweza “kupumzika” kulihusu: Haijalishi vile mnapinga, mnaasi, na kuhukumu, hakutakuwa na madhara kwa mwili wenu. Lakini kuna watu ambao hukiuka mipaka katika upinzani wao, ambao haukubaliki; kuna mpaka, na haikubaliki kwako kuizuia kazi ya Mungu. Leo, unaweza kuzungumza na kutenda bila matokeo hasi—lakini usiingilie au kuyavuruga maisha ya kanisa, usiingilie kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa mengine, unaweza kufanya unalotaka. Unasema hutayafuatilia maisha na ungependa kurudi ulimwenguni. Basi harakisha na uende! Mnaweza kufanya lolote mpendalo, maadamu halizuii kazi ya Mungu. Ilhali kuna jambo moja lazima ulijue: Mwishowe, watenda dhambi wa hiari hivyo wataondoshwa. Leo, hata hivyo, hushutumiwi. Mwishowe, ni sehemu tu ya watu wataweza kuwa na ushuhuda—na wengine watakuwa hatarini. Kama hupendi kuwa katika mkondo huu, ni sawa. Watu wa leo hutendewa kwa ustahimilivu; Siwawekei mipaka. Ni sawa maadamu wewe huogopi kuadibu kwa kesho. Lakini kama uko katika mkondo huu, lazima uwe na ushuhuda, na lazima uadibiwe. Ikiwa wewe husema kwamba huwezi kuvumilia tena, na ungependa kuchukua muda fulani kupumzika, hilo ni sawa—hakuna anayekuzuia! Lakini Sitakuruhusu kufanya kazi ambayo ni ya uharibifu na ambayo huvuruga kazi ya Roho Mtakatifu—wewe huwezi tu kusamehewa kwa hilo! Kuhusu kile ambacho macho yako huona na masikio yako husikia watu gani huadibiwa, na ambao familia zao hulaaniwa—kuna kikomo na mipaka kwa hili. Roho Mtakatifu hafanyi vitu kwa wepesi. Kwa kutegemea dhambi za mwanadamu na yote ambayo mmefanya, kama mngetendewa na kufikiriwa kwa uzito kwa kadri ya udhalimu wenu wenyewe, nani kati yenu angeweza kuendelea kuishi? Taabu kuu ingewajia ninyi—na mwanadamu angekuwa bado sawa wakati huo? Ilhali leo, watu wengine hutendewa kwa stahamala. Ingawa ninyi huhukumu, huasi, na hupinga, maadamu hamwingilii, basi nitawakabili kwa tabasamu. Kama kweli ninyi hufuatilia uzima, basi lazima mpitie kuadibu kidogo, na lazima mstahimili, lazima mstahimili maumivu ya kuachana na mnachopenda ili kwenda juu ya meza ya kupasulia kufanyiwa upasuaji, lazima uvumilie maumivu, kukubali majaribio na kuteseka kama Petro. Leo, mko mbele ya kiti cha hukumu. Katika siku za usoni, lazima mwende katika “bamba la kukata kichwa,” ndio utakuwa wakati ambapo mtajitoa mhanga wenyewe.
Wakati wa hatua ya mwisho ya kazi ya siku za mwisho, ninyi nyote lazima mjue kwamba unaweza kuamini kwamba Mungu hataangamiza mwili wako, na inaweza kusemwa kwamba huenda usipate ugonjwa wowote hata ingawa wewe humpinga Yeye na kumhukumu Yeye—lakini wakati ambapo maneno makali ya Mungu huja kwako, huwezi kujificha, na huwa na hofu kubwa na mwenye wasiwasi. Lakini leo, lazima muwe na dhamiri kidogo. Msiwe wale ambao hupinga na kuasi dhidi ya Mungu, msiwe walio waovu. Lazima uwachane na babu zako wa zamani; hili pekee ndilo huonyesha una kimo cha kweli, na hivyo pia huu ni ubinadamu unaopaswa kuwa nao. Wewe kila mara huwezi kuweka kando matarajio yako mwenyewe au raha za leo. Mungu asema: Maadamu ninyi hufanya yote mmwezayo ili kunifuata Mimi, Nitawafanya wakamilifu bila shaka. Baada ya ninyi kufanywa wakamilifu, kutakuwa na matumaini mazuri—mtaletwa ndani ya ufalme Wangu kufurahia baraka pamoja na Mimi. Ninyi mna makusudio, ilhali matakwa kwenu hayajapungua. Kuna sharti pia: Katika mahali hapa, haijalishi kama ninyi mtashindwa au kufanywa wakamilifu, leo lazima mpitie kuadibu kiasi, na mateso kiasi, lazima muangamizwe, na kufundishwa nidhamu, lazima msikilize maneno Yangu, mfuate njia Yangu, na kufanya mapenzi ya Mungu—hili ndilo ninyi binadamu mnapaswa kufanya. Haijalishi vile unafuatilia, lazima usikie njia hii kwa dhahiri. Kama umeona kwa halisi, kwa hakika, basi unaweza kuendelea kufuata. Kama unaamini kwamba hakuna matarajio au matumaini hapa, basi unaweza kwenda. Maneno haya yamenenwa kwako kwa dhahiri, lakini kama kweli ungependa kwenda, hili linaonyesha tu kwamba huna dhamiri hata kidogo; kitendo hiki chako kinatosha kuthibitisha kwamba wewe ni pepo. Ingawa unasema kwamba yote yanapaswa kuachiwa Mungu, kutegemea kile unachoishi kwa kudhihirisha, na mwili wako, wewe bado unaishi kwa kumilikiwa na Shetani. Ingawa Shetani pia yuko mikononi mwa Mungu, wewe mwenyewe ni wa Shetani, na bado hujaokolewa kweli na Mungu, kwani bado unaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Ni vipi ambavyo ni lazima ufuatilie ili uokolewe kabisa? Chaguo ni lako: Unaweza kukimbia, unaweza kwenda ghafla, unaweza kwenda kokote unakotaka, ni juu yako—unapaswa kuchagua njia unayopaswa kufuata. Hatimaye, kama unaweza kusema: Sina kitu bora zaidi, nalipa upendo wa Mungu na dhamiri yangu, na lazima niwe na ubinadamu kidogo. Siwezi kutimiza chochote cha juu zaidi, wala uhodari wangu hauko juu; mimi sielewi maono na maana ya kazi ya Mungu. Mimi hulipa tu upendo wa Mungu, mimi hufanya lolote ambalo Mungu hutaka, na mimi hufanya yote niwezayo—mimi hutekeleza wajibu wangu kama kiumbe wa Mungu—na, kwa njia hii, mimi huhisi maliwazo. Huu ndio ushuhuda wa juu zaidi ambao unaweza. Hiki ni kiwango kikuu zaidi kinachohitajika kwa sehemu ya watu: kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Lazima ufanye kadri unavyoweza. Matakwa ya Mungu kwako si ya juu sana; maadamu unafanya unachoweza, basi katika hili unakuwa na ushuhuda.
Tanbihi:
a. Maandishi ya asili yanaacha “Alifikiri.”
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni