Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (5)
Wakati wa Enzi ya Neema, Yesu alizungumza maneno kiasi na Akatekeleza hatua moja ya kazi. Kulikuwa na muktadha kwayo, na yalikuwa ya kufaa kwa hali za watu kwa wakati huo; Yesu alinena na kufanya kazi kama ilivyostahili muktadha wa wakati huo. Pia Alinena unabii kiasi. Alitabiri kwamba Roho wa ukweli angekuja wakati wa siku za mwisho, wakati ambapo Roho wa ukweli angetekeleza hatua ya kazi. Ambalo ni kusema, nje ya kazi ambayo Yeye Mwenyewe alikuwa Afanye wakati wa enzi hiyo, Hakuwa dhahiri kuhusu lingine lolote; yaani, kulikuwa na mipaka kwa kazi iliyoletwa na Mungu mwenye mwili. Hivyo, Alifanya tu kazi ya enzi hiyo, na hakufanya kazi nyingine ambayo haikuwa na uhusiano na Yeye.
Wakati huo, Hakufanya kazi kwa kadri ya hisia au maono, bali ilivyostahili wakati na muktadha. Hakuna aliyemwongoza au kumwelekeza Yeye. Uzima wa kazi Yake ulikuwa Alichokuwa, ambayo ilikuwa kazi iliyopaswa kutekelezwa na Roho wa Mungu aliyepata mwili—ilikuwa kazi yote iliyoanzishwa na kupata mwili. Labda, neema na amani ya Enzi ya Neema vimesababisha uzoefu wako kuwa na mengi yanayohusika na hisia au kiwango cha hisi cha binadamu. Yesu alifanya kazi tu kwa kadri ya kile ambacho Yeye Mwenyewe aliona na kusikia. Kwa maneno mengine, Roho alifanya kazi moja kwa moja; hakukuwa na haja ya wajumbe kuonekana Kwake na kumpa Yeye ndoto, wala kwa nuru yoyote kubwa kuangaza juu Yake na kumkubalia Yeye kuona. Alifanya kazi kwa huru na kwa nadra, ambayo ilikuwa kwa sababu kazi Yake haikutegemea hisia. Kwa maneno mengine, Alipofanya kazi hakutafuta kwa kupapasa na kubahatisha, lakini Alifanya mambo kwa utulivu, kufanya kazi na kunena kwa kadri ya mawazo Yake mwenyewe na kile alichoona Yeye kwa macho Yake mwenyewe, ambacho Alitoa mara moja kwa wanafunzi waliomfuata Yeye. Hii ndiyo tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya watu: Wakati ambapo watu hufanya kazi, wao hutafuta na kupapasa, wakiiga kila mara na kufikiri sana kwa kutegemea msingi uliowekwa na wengine ili kutimiza kuingia kwa ndani zaidi. Kazi ya Mungu ni kiasi kinachotolewa cha kile Alicho, Yeye hufanya kazi ambayo Yeye Mwenyewe hupaswa kufanya, na hatoi kwa kanisa kwa kutumia ufahamu uliotoka kwa kazi ya mwanadamu yeyote; badala yake, Yeye hufanya kazi ya sasa kwa kutegemea hali za watu. Hivyo, kufanya kazi kwa njia hii ni mara maelfu huru zaidi kuliko wakati ambapo watu hufanya kazi. Kwa watu, hata huonekana kwamba Mungu hatii wajibu Wake na Hufanya kazi kwa hali yoyote Anayopenda. Lakini kazi yote ambayo Yeye hufanya ni kazi mpya, na unapaswa kujua kwamba kazi ya Mungu mwenye mwili kamwe haitegemei hisia.
Wakati ambapo wanafunzi waliomfuata Yesu wakati huo walikuwa wamepata uzoefu kwa kiwango fulani, walihisi kwamba siku ya Mungu ilikuwa imefika, na wangekutana na Bwana mara moja. Hiyo ilikuwa hisia waliyokuwa nayo, na kwa wao, hisia hii ilikuwa muhimu sana. Lakini kwa kweli, hisia zilizo ndani ya watu si za kutegemea. Ndani, wanafunzi walihisi kwamba labda takriban wamefika mwisho wa safari yao, au kwamba yote waliyofanya na kupitia yaliamuriwa na Mungu. Na Paulo alisema kwamba alikuwa amemaliza mwendo wake, alikuwa amevipiga vita vilivyo vizuri, na alikuwa amewekewa taji ya haki. Hizo zilikuwa hisia alizokuwa nazo, na aliziandika katika nyaraka na kuzituma kwa makanisa. Vitendo kama hivyo vilitoka kwa mzigo alioubeba kwa ajili ya makanisa, na hivyo Roho Mtakatifu hakutilia maanani kazi hii. Wakati huo, aliposema, "nimewekewa taji ya haki," hakuhisi shutuma ndani yake mwenyewe—hakuwa na hisi ya mashaka, wala hakushutumiwa, kwa hiyo aliamini kwamba hisia hii ilikuwa ya kawaida sana na ya kweli kabisa. Aliamini kwamba ilitoka kwa Roho Mtakatifu. Lakini ikitazamwa leo, haikutoka kwa Roho Mtakatifu. Ilikuwa tu njozi ya mwanadamu. Kulikuwa na njozi nyingi ndani ya wanadamu. Wakati huo, Mungu hakuzitilia maanani au kuonyesha wazo lolote. Kazi nyingi sana ya Roho Mtakatifu haitekelezwi kupitia kwa hisia za watu—Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani ya hisia za watu. Isipokuwa kwa nyakati ngumu, za giza kabla ya Mungu kupata mwili, au kipindi ambapo hakukuwa na mitume au wafanyakazi; wakati wa hatua hii kazi ya Roho Mtakatifu iliwapa watu hisia fulani maalumu. Kwa mfano: Wakati ambapo watu hawakuwa na uongozi wa maneno ya Mungu, walipoomba wangekuwa na hisi ya furaha isiyoelezeka, ndani ya mioyo yao kulikuwa na hisia ya raha, na walikuwa na amani, na starehe. Wakati ambapo walikuwa na uongozi wa maneno, roho za watu zilikuwa dhahiri, na vitendo vyao vilipata nuru kwa maneno. Kwa kawaida, wao pia walikuwa na hisia za amani na kuwa starehe. Wakati ambapo watu huwa katika hatari, au Mungu aliwazuia kufanya mambo fulani, ndani ya mioyo yao walihisi kufadhaishwa na kuona haya, lakini haikuwa kana kwamba koo zao zilikuwa zimebanwa na hawangeweza kupumua. Wakati ambapo watu walikuwa na hisia hii ingekuwa ni kwa sababu mazingira yalikuwa ya kutisha sana au ya uhasama, yaliyosababisha hisia ya hofu ndani yao, na hivyo walikuwa wenye wasiwasi kabisa. Lakini hakuwa Roho Mtakatifu aliyewafanya wenye woga kwa kiasi hicho. Katika nyakati hizo, nusu ya hisia hii ilitoka kwa athari ya wasiwasi ya watu, na siyo yote ilitoka kwa Roho Mtakatifu. Watu kila mara huishi katikati ya hisia zao wenyewe, na wamefanya hivyo kwa miaka mingi sana. Wakati ambapo wao huwa na amani ndani ya mioyo yao, wao hutenda (wakiamini kuwa radhi kwao ni hisia ya amani), na wakati ambapo hawana amani ndani ya mioyo yao, wao hawatendi (wakiamini kutopenda au kutotaka kwao kuwa hisia ya wasiwasi). Mambo yakiendelea kwa urahisi, wao hudhani kwamba yalikuwa mapenzi ya Mungu. (Kwa kweli, ni jambo ambalo lilipaswa kuendelea kwa urahisi sana, hii ikiwa sheria asilia ya mambo.) Mambo yasipoendelea kwa urahisi, wao hudhani hayakuwa mapenzi ya Mungu, na wao huvunja ahadi yao kwa haraka sana. Lakini wakati mwingi, watu wanapopitia matukio kama hayo, ni sheria asilia ya mambo. Kama ungetia bidii zaidi ndani, wewe kwa hakika ungeshughulikia jambo hilo vizuri, na lingeendelea kwa urahisi zaidi na zaidi. Chukulia wakati ambapo wewe huenda kununua kabeji, kwa mfano. Bei ya soko ni jiao[a] mbili kwa jin,[b] lakini wewe huhisi kwamba inapaswa kuwa jiao moja kwa jin. Kwa kweli, hili ni lile ambalo wewe hufikiria tu moyoni mwako, na unapojaribu na kununua kwa bei hii, hufanikiwi kamwe, na wewe huamini kwamba Mungu hataki ununue kabeji.
Maisha ya watu yana hisia nyingi sana. Hasa, tangu wakati ambapo wao huanza kumwamini Mungu, hisia za watu huongezeka kila siku, kuwaacha wamechanganyikiwa na waliokanganyikiwa wakati wote. Hawajui waanzie wapi, na huwa hawana hakika kuhusu mambo mengi—lakini katika hali nyingi sana, wanapotenda na kunena kwa kadri ya hisia zao, maadamu si jambo ambalo hukiuka kanuni kuu, Roho Mtakatifu hajibu. Ni kama taji ya haki iliyoguswa na Paulo: Kwa miaka mingi, hakuna aliyeamini kwamba hisia zake zilikuwa si sahihi, wala Paulo mwenyewe hakuhisi kamwe kwamba hisia zake zilikuwa na makosa. Hisia za watu hutoka wapi? Hizo, bila shaka, ni athari ya akili zao. Hisia tofauti husababishwa kwa kadiri ya mazingira tofauti, na mambo tofauti. Wakati mwingi, watu huamua kutokana na mantiki ya binadamu na hupata seti ya fomyula, ambalo husababisha uundaji wa hisia nyingi za binadamu. Bila kulitambua, watu huingia katika uamuzi wao wenyewe wenye mantiki, na kwa njia hii, hisia hizi huwa kile ambacho watu hutegemea katika maisha yao, hizo huwa gongo la hisia katika maisha yao (kama taji ya Paulo, au "kukutana na Bwana hewani" kwa Witness Lee) Mungu takribani hana njia ya kusihi katika hisia hizi za mwanadamu, na lazima Azikubalie zikue kwa hiari zao wenyewe. Leo, Nanena nawe kwa dhahiri, na ukiendelea kuzifuata hisia zako, bado huishi katika yasiyo dhahiri? Wewe huyakubali maneno ambayo yameonyeshwa kwa dhahiri kwako, na kila mara hutegemea hisia zako binafsi. Katika hili, wewe si kama kipofu anayegusa ndovu? [c] Na ni nini ambacho utapata hatimaye?
Leo, kazi yote ambayo hufanywa na Mungu mwenye mwili ni halisi. Hiki si kitu ambacho unaweza kugusa, au kitu unachoweza kufikiria, sembuse kitu ambacho unaweza kuamua—ni kitu tu ambacho utaweza kuelewa wakati ambapo mambo ya hakika yatafanyika kwako. Wakati mwingine, hata yanapofanyika, wewe bado huwezi kuona kwa dhahiri, na wakati ambapo tu Mungu hufanya mambo mwenyewe, kuleta uwazi mkuu kwa mambo ya hakika ya kweli ya kile kinachotokea, ndipo watu wanaweza kuelewa. Wakati huo, kulikuwa na njozi nyingi miongoni mwa wanafunzi wa Yesu. Waliamini kwamba siku ya Mungu ilikuwa karibu kufika na wao wangemfia Yesu hivi punde na waweze kukutana na Bwana Yesu—ilhali wakati huo bado haukufika. Petro alikuwa mwepesi sana kuhisi kwa hisia hii. Alingoja miaka mizima saba, kila mara akihisi kwamba wakati ulikuwa umefika—lakini bado haukuwa umefika. Walihisi kwamba maisha yao yalikuwa yamekomaa, na hisia zao zilizidi na hisia hizi zikawa nyepesi kuhisi—lakini walipitia kushindwa kwingi na hawakuweza kufanikiwa. Wao wenyewe hawakujua kilichokuwa kikiendelea. Je, kile ambacho kilitoka kwa Roho Mtakatifu kwa hakika hakingeweza kutimizwa? Hisia za watu si za kutegemewa. Kwa sababu watu wana akili, fikira, na mawazo yao wenyewe, kutegemea muktadha na hali wakati huo, wao huunda mwungano wa akili wenye mawazo wao wenyewe. Hasa, wakati ambapo jambo hutendeka kwa watu wenye urazini wa akili wenye afya, wao huwa wenye kusisimuka mno, na hawawezi kuzuia ila kuunda mwungano wa akili wenye mawazo. Hili hasa linahusika na "mabingwa" wenye maarifa na nadharia ya fahari sana, ambao mwungano wa akili wao huwa hata mwingi zaidi baada ya miaka mingi ya kushughulika na ulimwengu; bila wao kuligundua, huo hutwaa fikira zao, na kuwa hisia zenye nguvu kabisa—na kupitia hili mabingwa huridhishwa. Wakati ambapo watu hutaka kufanya jambo, hisia na mawazo hutokea, na watu hudhani kwamba hizo ni sahihi. Baadaye, wanapoona kwamba hazijatimizwa, watu hawawezi kutoa jawabu la kile kilifanyika vibaya. Labda wao huamini kwamba Mungu ameubadilisha mpango Wake.
Miongoni mwa watu wa Enzi ya Sheria, watu wengi pia walikuwa na hisia fulani, lakini makosa katika hisia zao yalikuwa machache kuliko ya watu wa leo. Hilo ni kwa sababu, hapo awali, watu waliweza kutazama kuonekana kwa Yehova, na wangeona wajumbe, na walikuwa na ndoto. Watu wa leo hawawezi kuona maono au wajumbe, na hivyo kuna makosa mengi zaidi katika hisia zao. Ni lisiloepukika kwamba watu wana hisia. Watu wa Agano la Kale pia walikuwa na hisia, na waliamini kwamba hisia hizo zilikuwa sahihi kabisa, lakini wajumbe wangeonekana mara kwa mara miongoni mwao, ambalo hupunguza makosa ya hisia zao. Wakati ambapo watu wa leo huhisi kwamba jambo fulani ni sahihi hasa, na kwenda kulitia katika vitendo, Roho Mtakatifu hawashutumu. Ndani, hawana hisia kwa vyovyote vile, na wao wako na amani. Baada ya wao kumaliza, ni kupitia tu kwa ushirikiano au kusoma maneno ya Mungu ndipo wao hugundua walikuwa na makosa. Kuhusu suala moja, hakuna wajumbe wanaoonekana kwa watu, ndoto ni haba, na watu hawaoni chochote kuhusu maono katika anga. Kuhusu suala lingine, Roho Mtakatifu haongezi shutuma Yake na kufundisha nidhamu ndani ya watu; kuna kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya watu kwa nadra sana. Hivyo, kama watu hawali na kunywa maneno ya Mungu,[d]hawaelewi njia ya kuelekea kwa utendaji, na hawatafuti kwa kweli, basi hawatavuna chochote. Kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu ni kama zifuatazo: Hazingatii kile ambacho hakihusu kazi Yake; ikiwa jambo haliko ndani ya eneo la mamlaka Yake, Yeye hasihi kamwe, Akiwakubalia watu wafanye matatizo yoyote wapendayo. Unaweza kutenda vyovyote utakavyo, lakini siku itakuja ambapo hujui la kufanya. Mungu hufanya kazi kwa lengo moja tu katika mwili Wake mwenyewe, Yeye haingilii kamwe au kujihusisha katika kazi na ulimwengu mdogo wa wanadamu; badala yake, Mungu hujiepusha na ulimwengu wako, na Hufanya kazi ambayo Anapaswa kuifanya. Leo, hushutumiwi ukitumia fedha zaidi kwa mao tano, wala hutuzwi ukiokoa mao tano. Haya ni mambo ya binadamu, na hayana uhusiano hata kidogo na kazi ya Roho Mtakatifu—vitendo vyako katika suala hili haviko ndani ya eneo la kazi Yangu.
Wakati huo, Petro alinena maneno mengi na alifanya kazi nyingi. Yawezekana kwamba hakuna kati yake iliyotoka kwa mawazo ya binadamu? Kwa hiyo kuweza kutoka kabisa kwa Roho Mtakatifu haiwezekani. Petro alikuwa tu kiumbe wa Mungu, alikuwa mfuasi, alikuwa Petro, sio Yesu, na dutu zao hazikuwa sawa. Ingawa Petro alitumwa na Roho Mtakatifu, siyo yote aliyofanya na kusema[e] yalitoka kwa Roho Mtakatifu, kwani alikuwa, hata hivyo, mwanadamu. Paulo alinena maneno mengi na aliandika nyaraka nyingi kwa makanisa, ambazo zimekusanywa katika Biblia. Roho Mtakatifu hakuonyesha maoni yoyote, kwani wakati ambao alikuwa akiandika nyaraka ulikuwa wakati ambapo alikuwa akitumiwa na Roho Mtakatifu. Yeye aliona maono, na kuyaandika chini na kuyapisha kwa ndugu zake waliokuwa katika Bwana. Yesu hakuonyesha maoni, na hakuwa na athari. Kwa nini Roho Mtakatifu alitenda hivyo? Kwa nini Roho Mtakatifu hakumkomesha? Kwa sababu uchafu mwingine hutoka kwa fikira za kawaida za watu, na hauepukiki. Aidha, vitendo vyake havikuanzia kwa pingamizi, na havikuharibu hali za kawaida za watu; wakati ambapo kuna kazi kama hiyo ya ubinadamu, watu huona rahisi zaidi kuikubali. Ni kawaida kwa mawazo ya kawaida ya watu kuchanganywa ndani, bora tu uchafu huu haujiingizi katika chochote. Kwa maneno mengine, watu wenye fikira za kawaida wote wana uwezo wa kufikiria kwa njia hiyo. Wakati ambapo watu huishi katika mwili, wao huwa na mawazo yao wenyewe—lakini hakuna njia ya kutoa hizi fikira za kawaida. Ikiwa mna akili, basi lazima muwe na fikira. Hata hivyo, baada ya kuipitia kazi ya Mungu kwa muda, kutakuwa na fikira chache ndani ya akili za watu. Wakati ambapo wamepitia mambo mengi, wataweza kuona kwa dhahiri, na hivyo watapinga kidogo zaidi; kwa maneno mengine, wakati ambapo fikira za watu na uamuzi wenye mantiki hukanushwa, hisia zao zisizo za kawaida zitakuwa chache zaidi. Wale wanaoishi katika mwili wote huwa na fikira zao wenyewe, lakini mwishowe, kazi ya Mungu ndani yao itafikia kiwango ambacho fikira zao hazitaweza kuwasumbua, hawategemei tena hisia kuishi, kimo chao halisi hukomaa, na wao huweza kuishi kwa maneno ya Mungu kwa uhalisi, na hawafanyi tena mambo ambayo si dhahiri na tupu, kisha hawataweza kufanya mambo yanayosababisha pingamizi. Kwa njia hii, watakoma kuwa na njozi, na kuanza wakati huu kuendelea mbele vitendo vyao vitakuwa kimo chao halisi.
Tanbihi:
a. "Jiao" (inayojulikana pia kama "mao") ni kitengo cha fedha ya Uchina. Katika taifa la China, kitengo cha msingi cha fedha ni yuan. Kuna jiao kumi katika yuan moja.
b. "Jin" ni kipimo cha uzito cha Uchina, jin moja ni gramu 500.
c. "Kipofu anayegusa ndovu" inatoka kwa hadithi ya mafumbo ya kipofu na ndovu. Inaeleza juu ya vipofu kadhaa ambao wote waliigusa ndovu, kila mmoja akiamini kwamba sehemu aliyogusa iliwakilisha mnyama mzima. Hadithi hii ya mafumbo ni sitiari ya jinsi watu huchukulia visivyo kutazama au maoni yasiyo kamili kuwa ukweli kamili.
d. Maandishi ya asili yameacha "maneno ya Mungu."
e. Maandishi ya asili yameacha "aliyofanya na kusema."
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni