Ijumaa, 7 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (1)

maneno-ya-Mungu, ukweli
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (1)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (1)

Kazi Yangu iko karibu kukamilika. Miaka mingi ambayo tumeshinda pamoja imekuwa kumbukumbu zisizovumilika za siku za nyuma. Nimeendelea kurudia maneno Yangu na Sijakoma kuendelea katika kazi Yangu mpya. Bila shaka, ushauri Wangu ni sehemu muhimu katika kila sehemu ya kazi Ninayoifanya. Bila ushauri Wangu, ninyi nyote mtapotea, na kuchanganyikiwa hata zaidi. Kazi Yangu sasa karibu inakamilika na kuisha; bado Nataka kufanya kazi fulani katika kutoa ushauri, hiyo ni, kutoa baadhi ya maneno ya ushauri ili muyasikilize. Natumai tu kwamba hamtapoteza juhudi Zangu zenye kujitahidi na zaidi ya hayo, kwamba mnaweza kuelewa utunzaji wote na fikira ambazo Nimetumia, mkiyachukulia maneno Yangu kama msingi wa jinsi mnavyotenda kama binadamu. Iwe ni maneno ambayo mko tayari kuyasikiliza au la, iwe ni maneno ambayo mnafurahia kuyakubali au mnayakubali bila raha, lazima muyachukulie kwa uzito. Vinginevyo, tabia na mielekeo yenu isiyokuwa ya kujali itanifadhaisha Mimi kweli na hata zaidi, kuniudhi. Natumai sana kwamba nyote mnaweza kuyasoma maneno Yangu tena na tena—mara elfu kadhaa—na hata kuyakariri. Ni kwa namna hiyo tu ndiyo hamtayaacha matarajio Yangu kwa ajili yenu. Hata hivyo, hakuna hata mmoja wenu anayeishi hivi sasa. Hata, nyote mmezama katika maisha fisadi ya kula na kunywa hadi kushiba, na hakuna mmoja wenu anayeyatumia maneno Yangu kusitawisha mioyo na nafsi zenu. Hii ndiyo sababu Nimehitimisha kuwa uso wa kweli wa mwanadamu ni ule ambao utanisaliti siku zote na hakuna mtu anayeweza kuwa mwaminifu kabisa kwa maneno Yangu.
“Mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani kiasi kwamba hana sura ya mwanadamu tena.” Usemi huu sasa umepata utambuzi kidogo kutoka kwa idadi kubwa ya watu. Inasemwa hivyo kwa sababu “utambuzi” hapa ni kukiri juu juu tu kinyume na maarifa ya kweli. Kwa kuwa hakuna yeyote kati yenu anayeweza kujitathmini kwa usahihi wala kujichanganua kabisa, daima mnaamini nunu nusu, mnayashuku maneno Yangu nusu nusu. Lakini wakati huu Nautumia ukweli kuelezea tatizo kubwa zaidi mlio nalo, na hilo ni “usaliti.” Nyote mnao uzoefu wa neno “usaliti” kwa sababu watu wengi wamefanya kitu kuwasaliti wengine awali, kama vile mume kumsaliti mke wake, mke kumsaliti mume wake, mwana kumsaliti baba yake, binti kumsaliti mama yake, mtumwa kumsaliti bwana wake, marafiki kusalitiana, jamaa kusalitiana, wauzaji kuwasaliti wanunuzi, na mengineyo. Mifano hii yote ina asili ya usaliti. Kwa kifupi, usaliti ni aina ya tabia ambayo mtu huvunja ahadi, hukiuka kanuni za maadili, au huenda dhidi ya maadili ya kibinadamu, na ambayo huonyesha kupoteza ubinadamu. Kama mwanadamu, bila kujali kama unakumbuka iwapo umewahi kufanya kitu cha kumsaliti mwingine au ikiwa tayari umewasaliti wengine mara nyingi, kuzungumza kwa ujumla, kama ninyi mmezaliwa katika dunia hii basi mmefanya kitu kuusaliti ukweli. Kama una uwezo wa kuwasaliti wazazi au marafiki basi una uwezo wa kuwasaliti wengine, na zaidi ya hayo una uwezo wa kunisaliti Mimi na kufanya mambo ambayo Ninayadharau. Kwa maneno mengine, usaliti si aina ya utovu wa maadili tu kwa nje, lakini ni kitu ambacho hakikubaliani na ukweli. Aina hii ya kitu hasa ni chanzo cha upinzani wa mwanadamu na uasi kuhusiana na Mimi. Hii ndio sababu Nimeufupisha katika maelezo yafuatayo: Usaliti ni asili ya mwanadamu. Asili hii ni adui wa kimaumbile wa kila mtu kuwa sambamba na Mimi.
Tabia ambayo haiwezi kunitii kabisa ni usaliti. Mwenendo ambao hauwezi kuwa mwaminifu Kwangu ni usaliti. Kunidanganya na kutumia uongo kunilaghai ni usaliti. Kujawa na dhana na kuzieneza kila mahali ni usaliti. Kutozilinda shuhuda na maslahi Yangu ni usaliti. Kubuni tabasamu wakati mtu ameniacha moyoni mwake ni usaliti. Tabia hizi ni mambo yote ambayo daima mna uwezo wa kuyafanya, na pia ni za kawaida kati yenu. Hakuna mmoja wenu anayeweza kufikiri kwamba hilo ni tatizo, lakini Mimi sifikirii hivyo. Siwezi kuchukulia kunisaliti kama jambo dogo, na zaidi ya hayo siwezi kulipuuza. Nafanya kazi miongoni mwenu sasa lakini bado mko hivi. Kama siku moja hakutakuwa na mtu wa kuwalinda na kuwaangalia, si nyote mtakuwa wafalme wa kilima?[a] Kwa wakati huo, nani atavisafisha vitu tena na kuondoa uchafu mnaposababisha janga kubwa? Mnaweza kufikiri kwamba baadhi ya vitendo vya usaliti ni kitu cha mara moja tu badala ya tabia ya kuendelea, na hakipaswi kutajwa kwa uzito hivi, kikiwasababisha kuadhirika. Kama kweli mnaamini hivyo, basi mnakosa wepesi wa kuhisi. Zaidi mtu anavyofikiri hivi, ndivyo anavyokuwa mtundu na muasi zaidi. Asili ya mtu ni maisha yake, ni kanuni ambayo anaitegemea ili kuendelea kuishi, na anashindwa kuibadilisha. Jinsi ilivyo hali ya usaliti—kama unaweza kufanya kitu ili kumsaliti ndugu au rafiki, hii inathibitisha kwamba ni sehemu ya maisha yako na hali ambayo ulizaliwa nayo. Hiki ni kitu ambacho hakuna mtu anaweza kukikana. Kwa mfano, kama mtu anapenda kuiba vitu vya watu wengine, basi hii “kupenda kuiba” ni sehemu ya maisha yake. Ni kwamba tu wakati mwingine anaiba, na wakati mwingine haibi. Bila kujali kama anaiba au la, haiwezi kuthibitisha kwamba kuiba kwake ni aina ya tabia. Badala yake, inathibitisha kwamba kuiba kwake ni sehemu ya maisha yake, yaani, asili yake. Baadhi ya watu watauliza: Kwa kuwa ni asili yake, basi kwa nini wakati mwingine anaona vitu vizuri lakini haviibi? Jibu ni rahisi sana. Kuna sababu nyingi kwa nini haibi, kama vile kama bidhaa ni kubwa mno kwake kuinyakua akitazamwa na watu, au hakuna wakati mzuri wa kutenda, au bidhaa ni ghali sana, imelindwa vikali, au hana nia hasa ya kitu kizuri kama hicho, au bado hajafikiria matumizi ya kitu hicho, na mengineyo. Sababu hizi zote zinawezekana. Lakini haidhuru, akikiiba au la, hii haiwezi kuthibitisha kuwa hiyo dhana humjia akilini kwa muda tu. Kinyume chake, hii ni sehemu ya asili yake ambayo ni ngumu kuirudia tena. Mtu kama huyo haridhiki na kuiba mara moja tu, lakini mawazo ya kudai vitu vya wengine kama vyake huamshwa wakati wowote anapokutana na kitu kizuri au hali inayofaa. Hii ndiyo sababu Nasema kwamba wazo hili haliinuki kila mara, lakini linatokana na asili ya mtu huyu mwenyewe.
Mtu yeyote anaweza kutumia maneno na vitendo vyake wenyewe kuwakilisha tabia yake halisi. Sura hii ya kweli bila shaka ni asili yake. Kama wewe ni mtu anayeongea bila kuwa dhahiri, basi una asili mbovu. Kama asili yako ni yenye hila sana, basi namna ambayo unafanya mambo ni janja na laghai sana, nawe unafanya iwe rahisi sana kwa watu kulaghaiwa nawe. Kama asili yako ni mbovu sana, huenda maneno yako ni mazuri kusikiliza, lakini vitendo vyako haviwezi kuficha njia zako mbovu. Kama asili yako ni vivu sana, basi kila kitu unachosema vyote vinalenga kukwepa lawama na wajibu wa uzembe na uvivu wako, na vitendo vyako vitakuwa vya polepole sana na vizembe, na vizuri sana katika kuuficha ukweli. Kama asili yako ni yenye uwezo wa kuhisi maono ya wengine sana, basi maneno yako yatakuwa yenye busara na hatua zako pia zitalingana sana na ukweli. Kama asili yako ni aminifu sana, basi maneno yako lazima yawe ya dhati na namna ambayo unafanya mambo lazima iwe yenye kuhusika na mambo halisi, bila mengi ya kufanya bwana wako asikuamini. Kama asili yako ni yenye tamaa sana au ni yenye tamaa ya fedha, basi moyo wako mara nyingi utajazwa na mambo haya na utafanya baadhi ya mambo yaliyopotoka bila kukusudia, mambo maovu ambayo hufanya iwe vigumu kwa watu kusahau na zaidi ya hayo yatawaudhi. Kama Nilivyosema, kama una asili ya usaliti basi ni kujinasua kutoka kwake kwa nadra sana. Msiamini kuwa hivyo ndivyo ilivyo kwamba hamna asili ya usaliti kwa sababu hamjamkosea mtu yeyote. Kama hivyo ndivyo unavyofikiri basi unachukiza sana. Maneno ambayo Nimenena kila wakati yamewalenga watu wote, sio tu mtu mmoja au aina ya mtu. Kwa sababu tu hujanisaliti Mimi kwa jambo moja haithibitishi kwamba huwezi kunisaliti katika mambo yote. Baadhi ya watu hupoteza imani yao katika kuutafuta ukweli wakati wa kipingamizi katika ndoa zao. Baadhi ya watu hupoteza wajibu wao wa kuwa waaminifu Kwangu wakati wa kuvunjika kwa familia. Baadhi ya watu huniacha kwa ajili ya kutafuta wakati wa furaha na msisimko. Baadhi ya watu afadhali waanguke katika korongo lenye giza kuliko kuishi katika mwanga na kupata furaha ya kazi ya Roho Mtakatifu. Baadhi ya watu hupuuza ushauri wa marafiki kwa ajili ya kuridhisha tamaa zao kwa ajili ya mali, na hata sasa hawawezi kuyakubali makosa yao na kugeuka. Baadhi ya watu huishi tu kwa muda chini ya jina Langu ili wapate ulinzi Wangu, wakati wengine hujitolea tu kidogo kwa sababu wameyashikilia maisha na wanahofu kifo. Si vitendo hivi na vingine viovu na zaidi ya hayo visivyofaa tabia tu ambazo watu wamenisaliti kwa muda mrefu ndani ya mioyo yao? Bila shaka, Najua usaliti wa watu haukuwa umepangwa mapema, lakini ni ufunuo wa kimaumbile wa asili zao. Hakuna mtu anayetaka kunisaliti, na zaidi ya hayo hakuna mtu aliye na furaha kwa sababu amefanya kitu kunisaliti. Kinyume chake, wanatetemeka kwa hofu, sivyo? Hivyo mnafikiri kuhusu jinsi mnavyoweza kuzikomboa saliti hizi, na jinsi mnavyoweza kubadili hali ya sasa?
Tanbihi:
a. Msemo wa Kichina, maana halisi ambayo ni “magaidi wanaoimiliki milima na kujitangaza kama wafalme.”
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni