Jumamosi, 15 Juni 2019

Je, Wale Wasiojifunza na Wasiojua Chochote si Wanyama tu?

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Ni mbinu gani iliyo ya kufaa zaidi ya ufukuziaji katika njia ya leo? Ni umbo la aina gani unalopaswa kujiona mwenyewe kama katika ufukuziaji wako? Unapaswa kujua namna ya kushughulikia kila kitu kinachokufika wewe sasa, yawe ni majaribio au mateso, kuadibu bila huruma au laana—unapaswa kufikiria kwa makini haya yote. Mbona Nasema hili? Kwa sababu hata hivyo, kinachokufika wewe sasa ni jaribio moja fupi baada ya lingine. Labda sio mfadhaiko mkuu kwako sasa kwa hiyo unaacha mambo yaelekee kwa mwelekeo fulani, sio kuuchukulia kama utajiri wa thamani kwa ufukuziaji wako wa maendeleo. Wewe ni mzembe sana! Wewe kwa kweli huchukulia utajiri huu wa thamani kama mawingu yanayoelea mbele ya macho yako, na huthamini mifano hii mifupi ya mapigo makali, ambayo haionekani kuwa ya shida kwako. Wewe huchunguza tu kwa dharau na huyazingatii moyoni, lakini huyaona tu kama yanayogonga mwamba mara chache. Wewe ni mwenye kiburi sana! Wewe huchukua mtazamo wa dharau kwa shambulio moja kali, la dhoruba baada ya lengine, na wakati mwingine wewe hata hutabasamu kwa dharau, kufichua sura ya kutojali. Hili ni kwa sababu hujawahi kufikiria kuhusu kwa nini wewe hupitia aina hii ya "msiba" tena na tena. Yaweza kuwa kwamba Mimi sina haki kiasi hicho kwa watu? Je, Natafuta makosa madogo madogo tu kwako? Ingawa kufikiria kwenu si kwa maana kama Nilivyoeleza, huo mwenendo mtulivu umeeleza ulimwengu wa ndani wa moyo wako waziwazi sana. Ni wazi kwamba, kilichofichwa ndani sana ya moyo wako ni shutuma zisizojali tu na dalili zisizoisha za huzuni ambazo wengine hawawezi kuziona. Ni kwa sababu umepitia aina hizi za majaribio ndiyo unahisi kwamba si haki kabisa, hivyo unavurumisha shutuma huku. Ni kwa sababu ya majaribio haya ndiyo unahisi ulimwengu unahuzunisha sana, hivyo umejawa ghamu. Wewe huoni pigo baada ya pigo na kufundishwa nidhamu baada ya kufundishwa nidhamu kama ulinzi bora zaidi, bali unayaona kama uchokozi usio na busara kutoka Mbinguni au adhabu ya kufaa kwako. Wewe ni mjinga sana! Wewe umefungia bila huruma nyakati bora zaidi katika giza, na wewe huona mara kwa mara majaribio na kufundisha nidhamu kuzuri kama mashambulio kutoka kwa adui. Wewe huwezi kubadili kwa ajili ya mazingira, na hata zaidi, wewe hutaki kubadili. Hili ni kwa sababu wewe hutaki kupata chochote kutoka kwa kuadibu baada ya kuadibu unakoona kuwa katili. Wewe hutafuti au kuchunguza jambo kwa makini, na umekubali bila kulalamika mapenzi ya Mbinguni—popote unapoishia ndipo ulipo. Kurudi unakoona kama katili hakujaubadilisha moyo wako kabisa, wala hakujaumiliki moyo wako. Badala yake, kumeudhuru tu. Wewe umeona tu "kuadibu huku katili" kama adui yako katika maisha haya lakini hujapata chochote. Wewe ni wa kujidai sana! Wewe huamini mara chache kwamba unapitia aina hizi za majaribio kwa sababu wewe ni mwenye kustahili dharau sana, badala yake, wewe huamini kwamba ni wa bahati mbaya sana na zaidi ya hayo, wewe husema kwamba Mimi kila mara Hutafuta makosa madogo madogo kwako. Hadi sasa, ni ufahamu kiasi gani ulionao wewe kwa kweli wa kile ambacho Mimi husema na kile ambacho Mimi hufanya? Usidhani kwamba wewe ni mtu mwenye kipaji cha kuzaliwa, aliyepungukiwa na mbinguni kwa sehemu ndogo sana na anayeenda juu sana ya dunia. Wewe si stadi zaidi kuliko watu wengine, na inaweza kusemwa kwamba wewe ni mpumbavu zaidi vizuri kuliko mtu mwingine yeyote wa busara duniani kwa sababu wewe hujiona mwenyewe kuwa muhimu sana; hujawahi kuwa na hisi ya udhalili. Inaonekana kwamba wewe huona kila kitu Nifanyacho dhahiri kabisa. Ukweli ni kwamba wewe siyo mtu wa busara hata kidogo. Hili ni kwa sababu huna habari ya kile Niendacho kufanya, na hujui hata kidogo kile Nifanyacho sasa. Hiyo ndiyo maana Mimi husema kwamba huwezi tu kulinganisha na mkulima mkongwe ambaye hana utambuzi wa maisha ya binadamu ilhali hutegemea baraka kutoka Mbinguni kwa ajili ya ukulima. Wewe ni wa kupuuza sana kuhusu maisha yako mwenyewe na hata wewe hujui kuhusu sifa, na una hata kujijua kidogo zaidi. Wewe ni "mwenye majivuno" mno! Nasikitishwa kweli kuhusu vile wapenda sana starehe au mabibi wadhaifu kama wewe wataweza kuhimili mashambulio ya, pepo na mawimbi makuu zaidi ya dhoruba? Hao wapenda sana starehe hawajali kabisa kuhusu aina ya mazingira ambayo yamewajia sasa. Linaonekana kuwa jambo hafifu—hawana staha kwa mambo haya. Wao si wabaya na hawajioni wenyewe kuwa duni. Badala yake, wao bado wanatembeatembea na kutembea polepole katika "barabara zenye miti kandokando" wakijipungia hewa wenyewe. "Watu" hawa wasiojifunza na wasiojua chochote hawana habari kwa nini Mimi husema mambo haya kwao. Wao hujijua tu wenyewe kidogo sana na mtazamo wa kutaka ugomvi, na baada ya hilo njia zao za uovu hazibadiliki. Baada ya kuondoka Kwangu wao huendelea kukimbia na kuenea pote katika ulimwengu na hutamba na hulaghai. Sura yako hubadilika haraka mno—wewe bado unanidanganya Mimi kwa njia hii. Una ujasiri mno! Na wale mabibi chipukizi wadhaifu ni wa kuchekesha kwa kweli. Wao huyasikia matamshi Yangu muhimu, wao huona mazingira walio ndani na hawawezi kufanya lolote ila kutoa machozi; wao hunengua mwili wao kila mahali kana kwamba wanajaribu kuduwaza. Linachukiza sana! Yeye huona kimo chake mwenyewe na hulala kitandani na hushinda huko, hulia bila kukoma, ni kana kwamba anakaribia kukosa hewa. Kutokana na maneno haya yeye huuona uchanga na uduni wake mwenyewe, na baada ya hilo yeye hujazwa mno na ukanushaji. Yeye hukodoa kwa kutoonyesha hisia, na hakuna nuru katika macho yake; yeye halalamiki, na hanichukii Mimi—yeye ni wa kukanusha sana mpaka hata hasongi. Yeye pia hajifunzi na hajui chochote. Baada ya kuondoka Kwangu yeye mara tena ni mwenye mzaha na wa kucheza, na hicho "kicheko kama kengele ya fedha" ni kama tu "binti mfalme wa kengele ya fedha." Wao ni wadhaifu mno na vilevile wanaokosa mno kujihurumia! Ninyi nyote, bidhaa zilizoharibika miongoni mwa wanadamu—ninyi mnakosa sana ubinadamu! Ninyi hamjui kujipenda au kujilinda, hamwelewi maana, ninyi hamtafuti njia ya kweli au kupenda nuru ya kweli, na hasa hamjui jinsi ya kujithamini wenyewe. Mmesukuma maneno ya mafunzo Yangu mara kwa mara nyuma ya akili zenu na hata mumeyatumia kwa ajili ya burudani katika wakati wenu wa mapumziko. Ninyi mumeyatumia kila mara kama hirizi yenu wenyewe. Wakati ambapo Shetani hukushitaki, wewe huomba kidogo tu. Wakati ambapo wewe ni mbaya, wewe hulala, na wakati ambapo wewe huwa na furaha wewe hukimbia kila mahali kama mwenye wazimu. Wakati ambapo Mimi hukukemea, wewe hukubali kwa kichwa na kuinama, lakini wakati ambapo wewe huniacha wewe hucheka kishenzi. Miongoni mwa watu wewe kila mara ndiwe wa juu zaidi na hujawahi kujifikiri mwenyewe kuwa mwenye kiburi zaidi. Wewe kila mara ni mwenye majivuno mno, wa kujiona mno na mwenye kiburi sana. Ni vipi ambavyo aina hiyo ya "kijana wa kiume," "kijana wa kike," "mwanamume," au "bibi" asiyejifunza na asiyejua chochote anaweza kuyachukulia maneno Yangu kama hazina ya thamani? Nitakuuliza zaidi—ni nini ambacho umejifunza kutoka kwa maneno Yangu na kazi Yangu kwa muda huu wote? Hila zako ni janja zaidi? Mwili wako ni mstaarabu zaidi? Mtazamo wako Kwangu ni wa dharau zaidi? Nitakwambia kwa wazi, hii kazi Yangu nyingi kwa kweli imefanya ujasiri wako, ambao ulikuwa ule wa panya, kuwa mkuu zaidi. Woga wako Kwangu hupungua kila siku kwa sababu Mimi ni mwenye huruma sana. Sijawahi kutumia mbinu kali sana kuadhibu mwili wako. Labda vile unavyoona, Nazungumza tu kwa ukali, lakini wakati mwingi Mimi hukutazama kwa tabasamu na Mimi hukukosoa bayana kwa nadra sana. Na hasa ni kwa sababu Mimi kila mara hujali kuhusu udhaifu wako ndiyo imesababisha wewe kunichukulia Mimi kama vile nyoka humchukulia mkulima mwenye huruma. Mimi hupenda kwa kweli ustadi wa wanadamu katika kutathmini watu wengine kwa uangalifu—ni wa kusifika kwa kweli, mzuri sana! Nitakwambia ukweli. Kama una moyo wa uchaji leo au la ni isiyo na maana. Mimi si mwenye woga au wa wasiwasi, lakini Nitakwambia pia wewe "mtu mwenye kipaji" asiyejifunza na asiyejua chochote utaharibika mwishowe ndani ya ujanja wa kujiona kwako mwenyewe. Wewe ndiwe utakayeteseka, na wewe ndiwe utakayeadibiwa. Singekuwa mpumbavu hivyo kuendelea kufuatana na wewe mpaka jehanamu na kuendelea kuteseka, kwa sababu wewe na Mimi si wa aina moja. Usisahau kwamba wewe ni kiumbe aliyelaaniwa na Mimi, na ambaye hufunzwa na kuokolewa na Mimi. Hakuna chochote ndani yako Ninachotamani sana. Haijalishi wakati ambapo Mimi hufanya kazi, Mimi sipaswi kutii umiliki wa hila wa watu, matukio, au vitu vyovyote. Inaweza kusemwa kwamba mtazamo Wangu kwa, na maoni kuhusu wanadamu yamebaki vilevile kila mara. Sina upendeleo wowote kwako kwa sababu wewe ni kiungo katika usimamizi Wangu; wewe bila shaka huna nguvu kuu nyingi zaidi kuliko kingine chochote. Nakushauri wewe kukumbuka kila mara kwamba wewe si kitu zaidi ya kiumbe tu! Ingawa wewe huishi na Mimi, unapaswa kuijua hali yako na usijione kuwa wa sifa za juu zaidi. Hata kama Sikukosoi wewe au kukushughulikia, na Nakutazama na tabasamu, hili halithibitishi kwamba wewe na Mimi ni wa aina moja. Unapaswa kujua kwamba unatafuta ukweli, wewe mwenyewe siyo ukweli! Lazima ubadilike kulingana na maneno Yangu wakati wowote—huwezi kuepuka hili. Nakushauri ujifunze kitu wakati upo katikati ya nyakati hizi za ajabu, wakati nafasi hii adimu iko hapa, na usijaribu kunidanganya Mimi. Huhitaji kutumia sifa isiyostahilika kunidanganya Mimi. Ninyi kunitafuta Mimi siyo kwa ajili Yangu mwenyewe tu—ni kwa ajili yenu!
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni