Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)
Asili ya mwanadamu ni tofauti kabisa na kiini Changu; hii ni kwa kuwa asili potovu ya mwanadamu inatokana kabisa na Shetani na asili ya mwanadamu imemilikiwa na kupotoshwa na Shetani. Yaani, mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa uovu na ubaya wake. Mwanadamu hakui katika ulimwengu wa ukweli au mazingira matakatifu, na aidha haishi katika mwanga. Kwa hivyo, haiwezekani ukweli kumilikiwa kiasili katika asili ya kila mtu, na zaidi ya hayo, hawawezi kuzaliwa na kiini cha kumwogopa, kiini cha kumheshimu Mungu.