Maneno ya Mwenyezi Mungu | Hitimisho
Ijapokuwa maneno haya yote si maonyesho ya Mungu, yanatosha kwa ajili ya watu kutimiza makusudi ya kumjua Mungu na badiliko katika tabia. Labda kuna wengine ambao wanafikiri kuwa kwa sababu kazi ya Mungu katika bara ya China imekwisha, hili linathibitisha kuwa Amemaliza kutamka maneno yote ambayo Anapaswa kutamka, na kwamba hawezi kamwe kuwa na matamshi mapya kwani haya ndiyo maneno ambayo Mungu anaweza kunena. Zaidi ya hayo, kuna watu wanaoamini kuwa Neno Laonekana katika Mwili linajumuisha maonyesho yote ya Mungu katika Enzi ya Ufalme, na kwamba kupokea kitabu hiki ni sawa na kupokea kila kilicho cha Mungu, au kwamba kitabu hiki kitawaongoza wanadamu katika siku za usoni kama ilivyofanya Biblia. Ninaamini kwamba watu wanaoshikilia mitazamo hii si wachache, kwa kuwa watu daima wanapenda kumlazimishia Mungu mipaka. Ijapokuwa wote wanatangaza kuwa Mungu ni mwenye kudura na Amezunguka kila kitu, asili ya watu bado inawafanya kuwa wepesi wa kumwekea Mungu mipaka katika upeo fulani. Wakati uleule ambapo kila mtu anapata kumjua Mungu, vilevile wanamuasi na kumwekea mipaka.
Kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme ndiyo tu imeanza. Matamshi yote ya Mungu katika kitabu hiki yalilengwa tu kwa wale waliomfuata wakati ule, na ni sehemu tu ya maonyesho ya Mungu katika kupata mwili Kwake kwa sasa, na hayawakilishi kila kitu cha Mungu. Zaidi ya hayo, haiwezi kusemwa kuwa ni kazi yote ambayo Mungu mwenye mwili atafanya wakati huu. Mungu atayalenga maneno Yake kwa watu wa makabila na asili tofauti, na Atawashinda wanadamu wote na kuitamatisha enzi ya zamani, hivyo basi Angekamilisha vipi baada ya kuonyesha sehemu ndogo kama hiyo ya maneno Yake? Ni kwamba tu kazi ya Mungu imegawanywa katika vipindi tofautitofauti vya wakati na hatua tofautitofauti. Anafanya kazi kulingana na mpango Wake na kuonyesha maneno Yake kulingana na hatua Zake. Ni vipi mwanadamu angeweza kuelewa kudura na busara za Mungu? Ukweli Ninaoufafanua hapa ni huu: Kile Mungu alicho na anacho milele hakiishi wala hakina mipaka. Mungu ni chanzo cha uhai na vitu vyote. Mungu hawezi kueleweka na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Mwishowe, ni lazima bado Nimkumbushe kila mtu: Msimwekee Mungu mipaka katika vitabu, maneno, au tena katika matamshi Yake yaliyopita. Kuna neno moja tu kwa sifa ya kazi ya Mungu—mpya. Hapendi kuchukua njia za zamani au kurudia kazi Yake, na zaidi ya hayo Hapendi watu kumwabudu kwa kumwekea mipaka katika upeo fulani. Hii ndiyo tabia ya Mungu.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni