Jumapili, 22 Septemba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (2)


Kazi na kuingia kwenu ni duni kabisa; mwanadamu hafikirii kwamba kazi ni muhimu na hata yeye ni mzembe zaidi na kuingia. Mwanadamu haoni haya kuwa mafunzo mazuri anayopaswa kuingia ndani; kwa hivyo, katika uzoefu wake wa kiroho, kwa kweli yote ambayo mwanadamu huona ni njozi. Si mengi yanatakiwa kutoka kwenu kuhusu uzoefu wenu katika kazi, lakini, kama yule anayetakiwa kukamilishwa na Mungu, mnapaswa kujifunza kumfanyia Mungu kazi ili hivi punde muweze kuupendeza moyo wa Mungu. Kotekote katika enzi, wale waliofanya kazi wameitwa wafanyakazi au mitume, ambayo inahusu idadi ndogo ya watu waliotumiwa na Mungu. Hata hivyo, kazi Niizungumziayo leo haihusu wafanyakazi au mitume hao pekee; inaelekezwa kwa wote watakaokamilishwa na Mungu. Labda kuna wengi walio na hamu kidogo katika hili, lakini, kwa ajili ya kuingia, ingekuwa bora zaidi kujadili ukweli huu.
Kazi inapozungumziwa, mwanadamu anaamini kwamba kazi ni kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu, akihubiri kila sehemu, na kugharimia rasilmali kwa ajili ya Mungu. Ingawa imani hii ni sahihi, ni ya kuegemea upande mmoja sana; kile ambacho Mungu anamwomba mwanadamu si kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu; ni huduma zaidi na kujitoa ndani ya roho. Ndugu wengi hawajawahi kufikiria juu ya kumfanyia Mungu kazi hata baada ya miaka mingi sana ya uzoefu, maana kazi kama mwanadamu anavyoielewa haipatani na ile ambayo Mungu anaitaka. Kwa hiyo, mwanadamu havutiwi kwa namna yoyote ile na kazi ya Mungu, na hii ndiyo sababu kuingia kwa mwanadamu ni kwa kuegemea upande mmoja kabisa. Nyinyi nyote mnapaswa kuingia kwa kumfanyia Mungu kazi, ili muweze kupata uzoefu wa vipengele vyake vyote. Hiki ndicho mnapaswa kuingia ndani. Kazi haimaanishi kutembea huku na huko kwa ajili ya Mungu; maana yake ni iwapo maisha ya mwanadamu na kile ambacho mwanadamu anaishi kwa kudhihirisha ni kwa ajili ya Mungu kufurahia. Kazi inamaanisha mwanadamu kutumia uaminifu alio nao kwa Mungu na maarifa aliyo nayo juu ya Mungu ili kumshuhudia Mungu na kumhudumia mwanadamu. Huu ndio wajibu wa mwanadamu, na yote ambayo mwanadamu anapaswa kutambua. Kwa maneno mengine, kuingia kwenu ni kazi yenu; mnatafuta kuingia wakati wa kazi yenu kwa ajili ya Mungu. Kupata uzoefu wa Mungu sio tu kuweza kula na kunywa neno Lake; na muhimu zaidi, mnapaswa kuweza kumshuhudia Mungu, kumtumikia Mungu, na kumhudumia na kumkimu mwanadamu. Hii ni kazi, na pia kuingia kwenu; hiki ndicho kila mwanadamu anapaswa kukitimiza. Kuna watu wengi ambao wanatilia mkazo tu katika kusafiri huku na huko kwa ajili ya Mungu, na kuhubiri kila sehemu, lakini hawazingatii uzoefu wao binafsi na kupuuza kuingia kwao katika maisha ya kiroho. Hiki ndicho kinasababisha wale wanaomtumikia Mungu kuwa watu wanaompinga Mungu. Kwa miaka mingi sana, wale wanaomtumikia Mungu na kumhudumia mwanadamu wanaona kufanya kazi na kuhubiri kuwa ndio kuingia, na hakuna anayechukulia uzoefu wake binafsi wa kiroho kuwa kuingia muhimu. Badala yake, wanatumia nuru ya kazi ya Roho Mtakatifu kuwafundisha wengine. Wanapohubiri, wanakuwa na mzigo mkubwa sana na wanapokea kazi ya Roho Mtakatifu, na kupitia hili wanatoa sauti ya Roho Mtakatifu. Wakati huo, wale wanaofanya kazi wanahisi kuridhika kana kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni uzoefu wao binafsi wa kiroho; wanahisi kwamba maneno yote wanayoyazungumza wakati huo ni ya yao wenyewe, na pia kana kwamba uzoefu wao si wazi kama walivyoeleza. Kuongezea, wao hawana fununu ya nini cha kusema kabla ya kunena, lakini Roho Mtakatifu anapofanya kazi ndani yao, wao huwa na mtiririko wa maneno usioisha na usiosita. Baada ya kuwa umehubiri kwa namna hiyo, unahisi kwamba kimo chako halisi sio kidogo kama ulivyoamini. Baada ya Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yako kwa namna ile ile mara kadhaa, basi unaamini kwamba tayari una kimo na unaamini kimakosa kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kuingia kwako na asili yako mwenyewe. Unapopitia uzoefu huu kwa mfululizo, unakuwa mzembe kuhusu kuingia kwako. Halafu unakuwa mvivu bila kujua, na kutozingatia kabisa kuingia kwako mwenyewe. Kwa hiyo, unapowahudumia wengine, unapaswa kutofautisha waziwazi kati ya kimo chako na kazi ya Roho Mtakatifu. Hii itasaidia zaidi kuingia kwako na kunufaisha zaidi uzoefu wako. Mwanadamu akidhani kazi ya Roho Mtakatifu ni uzoefu wake binafsi ndio mwanzo wa upotovu. Hivyo, kazi yoyote mnayoifanya, mnapaswa kuzingatia kuingia kwenu kama somo muhimu.
Mtu anafanya kazi ili kutimiza mapenzi ya Mungu, kuwaleta wale wote wanaoutafuta moyo wa Mungu mbele Yake, kumleta mwanadamu kwa Mungu, na kuitambulisha kazi ya Roho Mtakatifu na uongozi wa Mungu kwa mwanadamu, kwa kufanya hivyo atakuwa anayakamilisha matunda ya kazi ya Mungu. Kwa sababu hii, ni muhimu kuelewa kiini cha kufanya kazi. Kama mtu anayetumiwa na Mungu, watu wote wanafaa kumfanyia kazi Mungu, yaani, wote wana fursa ya kutumiwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo kuna hoja moja mnayopaswa kuielewa: Mwanadamu anapofanya kazi ya Mungu, mwanadamu anakuwa na fursa ya kutumiwa na Mungu, lakini kile kinachosemwa na kujulikana na mwanadamu sio kimo cha mwanadamu kabisa. Mnaweza tu kujua vizuri kasoro zako katika kazi yenu, na kupokea nuru kubwa kutoka kwa Roho Mtakatifu, kwa kufanya hivyo mtakuwa mnaweza kupata kuingia kuzuri katika kazi yenu. Ikiwa mwanadamu anachukulia uongozi wa Mungu kuwa ni kuingia kwake mwenyewe na kile kilichomo ndani ya mwanadamu, hakuna uwezo wa mwanadamu kuongezeka kimo. Roho Mtakatifu humpatia mwanadamu nuru anapokuwa katika hali ya kawaida; katika nyakati kama hizo, mara nyingi mwanadamu anadhani nuru anayopokea ni kimo chake mwenyewe katika uhalisi, maana Roho Mtakatifu huangazia katika njia ya kawaida: kwa kutumia kile ambacho ni cha asili kwa mwanadamu. Mwanadamu anapofanya kazi na kuzungumza, au wakati mwanadamu anapofanya maombi katika shughuli zake za kiroho, ndipo ukweli utawekwa wazi kwao. Hata hivyo, katika uhalisi, kile ambacho mwanadamu anakiona ni nuru tu iliyoangaziwa na Roho Mtakatifu (kwa kawaida, hii inahusiana na ushirikiano kutoka kwa mwanadamu) na sio kimo halisi cha mwanadamu. Baada ya kipindi cha kupitia uzoefu ambao mwanadamu anakabiliana na shida nyingi, kimo cha kweli cha mwanadamu hudhihirika katika mazingira kama hayo. Ni katika muda huo ndipo mwanadamu anagundua kwamba kimo cha mwanadamu sio kikubwa hivyo, na ubinafsi, fikira zake mwenyewe, na tamaa za mwanadamu vyote huibuka. Ni baada tu ya mizunguko kadhaa ya uzoefu kama huo ndipo wengi wa jinsi hiyo ambao wameamshwa ndani ya roho zao watatambua kwamba haukuwa uhalisi wao hapo nyuma, bali ni mwangaza wa muda tu kutoka kwa Roho Mtakatifu, na mwanadamu alipokea nuru tu. Roho Mtakatifu anapompa mwanadamu nuru ili aelewe ukweli, mara nyingi inakuwa katika namna ya wazi na tofauti, bila muktadha. Yaani, Hayajumuishi matatizo ya mwanadamu katika ufunuo huu, na badala yake Anatoa ufunuo moja kwa moja. Mwanadamu anapokabiliana na matatizo katika kuingia, basi mwanadamu anaijumuisha nuru ya Roho Mtakatifu, na huu unakuwa uzoefu halisi wa mwanadamu. Kwa mfano, dada ambaye hajaolewa ananena hivi wakati wa ushirika: “Hatutafuti sifa kuu na utajiri au kutamani furaha ya upendo kati ya mume na mke; sisi hutafuta tu kuutoa moyo wa utakatifu na umakini kwa Mungu.” Anaendelea kusema: “Mara tu watu wanapoolewa au kuoa, kuna mengi ambayo huwazonga, na moyo wao wa kumpenda Mungu si halisi tena. Mioyo yao daima hushughulishwa na familia zao na wake au waume zao, na kwa hiyo mioyo yao huwa yenye utata zaidi....” Anapozungumza, ni kana kwamba maneno ayanenayo ni yale anayofikiria moyoni mwake; maneno yake ni ya kuvuma na yenye nguvu, kana kwamba yote anenayo yanatoka ndani kabisa ya moyo wake. Anatamani angejitolea kabisa kwa Mungu na anatumaini kwamba ndugu kama yeye wanashiriki azimio lilo hilo. Inaweza kusemwa kwamba azimio lako na hisia ya kusisimuliwa wakati huu yote hutoka kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Wakati ambapo mbinu ya kazi ya Mungu hubadilika, umekua miaka michache kwa umri; unaona kwamba wanafunzi wenzako wote na marafiki wa umri wako wana waume, au unasikia kwamba baada ya fulani na fulani kuolewa, mume wake alimpeleka mjini kuishi na akapata kazi huko. Unapomwona, moyo wako huanza kuona wivu. Unaona kwamba amejaa uzuri na mkao toka utosini hadi wayoni; anapozungumza, ana mwenendo wa kidunia na amepoteza kabisa maringo ya kishamba. Hili husisimua hisia ndani yako. Wewe, baada ya kugharimia rasilmali kwa ajili ya Mungu wakati huu wote, huna familia au kazi, na umevumilia kushughulikiwa kwingi; kitambo sana, uliingia katika umri wa makamo, na ujana wako ukaponyoka kimya, kana kwamba umepumbaa. Umefika umbali huu wote mpaka siku hii, lakini hujui ni wapi utatulia. Ni wakati huo ndipo unakuwa katika kimbunga cha mawazo, kana kwamba wewe ni mwenye wazimu. Ukiwa mpweke na usiyeweza kulala fofofo, ukiona ugumu kupata usingizi usiku wote, wewe, kabla hujajua, unaanza kufikiri juu ya azimio lako na nadhiri zako za dhati kwa Mungu. Kwa nini hali hizi zimekufika? Punde si punde, machozi ya kimyakimya yanakutoka na unahisi uchungu kabisa. Unakuja mbele za Mungu kuomba na unaanza kufikiria juu ya urafiki wa karibu sana na kukaribiana kwa kutotengana kwa wakati wa siku zako za furaha na Mungu. Onyesho baada ya onyesho linaonekana mbele ya macho yako, na nadhiri uliyoweka siku hiyo inabaki mara tena akilini mwako, “Je, Mungu si mwandani wangu wa pekee?” Kufikia wakati huo, unamamia: “Mungu! Mungu mpenzi! Nimeshakupa Wewe moyo wangu wote. Ningependa kuahidiwa Kwako milele, na nitakupenda Wewe bila kubadilika maisha yangu yote....” Ni wakati ambao unang’ang’ana tu katika mateso hayo ya kuzidi kiasi ndiyo unahisi kweli jinsi Mungu alivyo wa kupendeza, na wakati huo tu ndipo unatambua kwa dhahiri: Nilijitolea kabisa kwa Mungu kitambo sana. Baada ya pigo kama hilo, unakuwa na uzoefu zaidi katika jambo hili na kuona kwamba kazi ya Roho Mtakatifu wakati huo si miliki ya mwanadamu. Katika uzoefu wako baadaye, wewe hauzuiwi tena katika kuingia huku; ni kana kwamba makovu yako yamefaidisha sana kuingia kwako. Wakati wowote unapokabiliwa na hali kama hizo, mara moja utakumbuka machozi yako tangu siku hiyo, kana kwamba unaunganishwa tena na Mungu. Una woga siku zote wa kuuvunja uhusiano wako na Mungu tena na kuharibu penzi la hisia (uhusiano wa kawaida) kati yako na Mungu. Hii ni kazi yako na kuingia kwako. Kwa hiyo, mnapoipokea kazi ya Roho Mtakatifu, mnapaswa kujikita zaidi katika kuingia kwenu, na wakati huo huo, kuona kipi ni kazi ya Roho Mtakatifu na kipi ni kuingia kwenu, vilevile kujumuisha kazi ya Roho Mtakatifu katika kuingia kwenu, ili kwamba muweze kukalishwa Naye vizuri na kuruhusu hulka ya kazi ya Roho Mtakatifu kuletwa pamoja ndani yenu. Wakati mnapitia uzoefu wenu wa kazi ya Roho Mtakatifu, mnamjua Roho Mtakatifu, vilevile nyinyi wenyewe, na katikati ya mateso makali, mnajenga uhusiano wa kawaida pamoja na Mungu, na uhusiano baina yenu na Mungu unakuwa wa karibu siku kwa siku. Baada ya michakato mingi ya kupogolewa na kusafishwa, mnakuza upendo wa kweli kwa Mungu. Hii ndiyo sababu mnapaswa kutambua kwamba mateso, mapigo, na dhiki havitishi; kinachoogopesha ni kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu tu lakini sio kuingia kwenu. Siku inapofika kwamba kazi ya Mungu imemalizika, mtakuwa mmefanya kazi bure; ingawa mmepitia uzoefu wa kazi ya Mungu, hamtakuwa mmemjua Roho Mtakatifu au kuwa na kuingia kwenu wenyewe. Nuru anayopewa mwanadamu na Roho Mtakatifu si ya kudumisha hisia za mwanadamu; ni kufungua njia kwa ajili ya kuingia kwa mwanadamu, vilevile kumruhusu mwanadamu kumjua Roho Mtakatifu, na kuanzia hapo anakuza moyo wa uchaji na ibada kwa Mungu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni