Jumatano, 30 Oktoba 2019

Sura ya 4

Kanisa la Mwenyezi Mungu


Watu Wangu wote wanaohudumu mbele Zangu wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita: Je, upendo wenu Kwangu ulikuwa umetiwa doa na uchafu? Je, uaminifu wenu Kwangu ulikuwa safi na wa moyo wako wote? Je, ufahamu wenu kunihusu ulikuwa wa kweli? Je, Nilikuwa na nafasi kiasi gani katika nyoyo zenu? Je, Nilikuwa Nimejaza nyoyo zenu zote? Je, maneno Yangu yalitimiza kiasi gani ndani yenu? Msinichukue kama mpumbavu! Hivi vitu viko wazi kabisa Kwangu! Leo, sauti ya wokovu Wangu inapopazwa nje, je, kumekuwa na ongezeko la upendo wenu Kwangu? 

Jumapili, 27 Oktoba 2019

Utofautishaji Kati ya Kazi ya Mungu na Ile ya Mwanadamu

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ya Mungu Mwenyewe inahusisha kazi ya wanadamu wote, na pia inawakilisha kazi ya enzi nzima. Hii ni kusema kwamba, kazi ya Mungu mwenyewe inawakilisha harakati na mwelekeo wa kazi yote ya Roho Mtakatifu, ilhali kazi ya mitume inafuata kazi ya Mungu na wala haiongozi enzi, na wala haiwakilishi mwelekeo wa kufanya kazi wa Roho Mtakatifu katika enzi nzima.

Alhamisi, 24 Oktoba 2019

Jumatatu, 21 Oktoba 2019

Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni hukumu ya kiti cha enzi kikubwa, cheupe, kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo

Aya za Biblia za Kurejelea:

Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17).
Na nikaona kiti kikubwa cha enzi, cheupe, na yeye akiketiye, ambaye kutoka kwa uso wake nchi na mbingu zilitoroka; na hapakupatikana mahali pao. Na nikawaona waliokufa, wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya Mungu; na vitabu vilifunguliwa: na kitabu kingine pia kikafunguliwa, ambacho ni kitabu cha uhai: na waliokufa walihukumiwa kwa mambo yale yaliyokuwa yameandikwa katika vitabu hivyo, kulingana na vitendo vyao. Nayo bahari ikawatoa waliofariki ambao walikuwa ndani yake; na kifo na kuzimu zikawatoa waliofariki ambao walikuwa ndani zao: na kila mtu alihukumiwa kulingana na vitendo vyake. Na kifo na kuzimu zikarushwa katika ziwa la moto. Hiki ndicho kifo cha pili. Na yeyote ambaye hakupatikana ameandikwa ndani ya kitabu cha uzima alirushwa katika ziwa la moto” (Ufunuo 20:11-15).
Maneno Husika ya Mungu:
“Hukumu” katika maneno yaliyonenwa awali—hukumu itaanza na nyumba ya Mungu—inarejelea hukumu ambayo Mungu anatoa leo kwa wale wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi katika siku za mwisho.

Ijumaa, 18 Oktoba 2019

Ni jinsi gani hatua tatu za kazi ya Mungu kwa pole pole huongeza uketo ili watu waokolewe na kukamilishwa?

Maneno Husika ya Mungu:
Usimamizi mzima wa Mungu umegawika katika hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayofaa yanatakiwa kutoka kwa mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu wote huwa ya juu hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa “kuonekana kwa Neno katika mwili,” na kwa njia hii mahitaji ya mwanadamu huwa ya juu hata zaidi, na mahitaji ya mwanadamu kutoa ushuhuda huwa ya juu hata zaidi.

Jumanne, 15 Oktoba 2019

Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” | Mtazamo Kimbele Uliorefushwa



Wimbo wa kusisimua wa ufalme umevuma, ukitangazia ulimwengu wote kuwasili kwa Mungu kati ya mwanadamu! Ufalme wa Mungu umefika! Watu wote washangilia, vitu vyote vyafurahi! Kila kitu mbinguni kote kina furaha tele. Mandhari haya yanayopendeza mno ya shangwe ni yapi?

Jumamosi, 12 Oktoba 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini”

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini”


Mwenyezi Mungu anasema, “Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako? Ni mara ngapi umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha. Badala yake, huku ni kutenda ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu. Vitendo kama hivi pekee ndivyo humridhisha Mungu. Desturi yoyote inayompendeza Mungu si kanuni bali ni kutenda ukweli.”

Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu


Nimewapa maonyo mengi na kuwapa ukweli mwingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyohisi hapo zamani, kuelewa kanuni nyingi za jinsi mtu anavyopaswa kuwa, na kumiliki kiasi kikubwa cha maarifa ya kawaida ambayo watu waaminifu wanapaswa kuwa nayo. 

Jumatano, 9 Oktoba 2019

Kuinuka Kupitia Ukandamizaji wa Giza

Mo Zhijian Mkoa wa Guangdong

Nilizaliwa katika eneo maskini, la mbali lenye milima ambako tumefukiza na kumwabudu Budha kwa vizazi vingi. Kuna hekalu za Budha sehemu hiyo kote ambako familia zote zingekwenda kuchoma uvumba; hakuna mtu yeyote aliyewahi kumwamini Mungu kamwe. Katika mwaka wa 1995, mimi na mke wangu tulikuwa katika sehemu nyingine ya nchi ambapo tulimwamini Bwana Yesu; baada ya sisi kurudi tulianza kushiriki injili na idadi ya watu ambao waliikubali ilikua polepole hadi watu zaidi ya 100. Kwa sababu watu zaidi na zaidi walikuwa wakimwamini Mungu, liliishtua serikali ya mitaa. Siku moja mwaka wa 1997, polisi waliniita kwenda kituo cha polisi cha mahali palepale, ambapo mkuu wa Ofisi ya Usalama wa Umma ya Wilaya, Mkuu wa Ofisi ya Usalama wa Taifa, mkuu wa Ofisi ya Dini na mkuu wa kituo cha polisi na vilevile maafisa wachache wa polisi walikuwa wananisubiri.