Jumatano, 30 Oktoba 2019

Sura ya 4

Kanisa la Mwenyezi Mungu


Watu Wangu wote wanaohudumu mbele Zangu wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita: Je, upendo wenu Kwangu ulikuwa umetiwa doa na uchafu? Je, uaminifu wenu Kwangu ulikuwa safi na wa moyo wako wote? Je, ufahamu wenu kunihusu ulikuwa wa kweli? Je, Nilikuwa na nafasi kiasi gani katika nyoyo zenu? Je, Nilikuwa Nimejaza nyoyo zenu zote? Je, maneno Yangu yalitimiza kiasi gani ndani yenu? Msinichukue kama mpumbavu! Hivi vitu viko wazi kabisa Kwangu! Leo, sauti ya wokovu Wangu inapopazwa nje, je, kumekuwa na ongezeko la upendo wenu Kwangu?  Je, sehemu ya uaminifu wenu Kwangu imekuwa safi? Je, ufahamu wenu kunihusu umezidishwa? Je, sifa ya zamani iliweka msingi dhabiti kwa maarifa yenu leo hii? Je, ni kiasi gani cha undani wenu kinamilikiwa na Roho Wangu? Mfano Wangu unamiliki sehemu kiasi gani ndani yenu? Je, matamshi Yangu yamewagonga katika sehemu yenu ya udhaifu? Je, mnahisi kwa kweli kuwa hamna mahali pa kuficha aibu yenu? Je, mnaamini kwa kweli kuwa hamjafuzu kuwa watu Wangu? Iwapo hutambui kabisa maswali haya, basi hii inaashiria kuwa unafanya kazi gizani, kwamba uko tu pale kuongeza idadi, na kwamba katika muda ulioamuliwa na Mimi kabla ya siku hii, kwa hakika utaangamizwa na kutupwa katika shimo lisilo na mwisho kwa mara ya pili. Haya ni maneno Yangu ya onyo, na yeyote anayeyachukulia kwa wepesi atapigwa na hukumu Yangu, na, kwa wakati ulioteuliwa atapatwa na janga. Sivyo? Je, bado Ninahitaji kutoa mifano ili kueleza hili? Je, inanilazimu kuzungumza kwa uwazi zaidi ili Niweke kigezo kwa ajili yenu? Tangu wakati wa uumbaji mpaka sasa, watu wengi wamekosa kutii maneno Yangu na hivyo wametupwa nje na kutolewa katika mtiririko wa urejesho Wangu; hatimaye, miili yao inaangamia na roho zao zinatupwa kuzimu, na mpaka wa leo bado wanapitia adhabu kali. Watu wengi wameyafuata maneno Yangu, lakini wameenda kinyume na nuru na mwanga Wangu, na hivyo wametupwa kando na Mimi, wakaanguka katika miliki ya Shetani na kuwa wale wanaonipinga. (Leo hii wote wanaonipinga moja kwa moja wanatii ujuu juu wa maneno Yangu peke yake, na kuasi kiini cha maneno Yangu.) Kumekuwa na wengi, pia, ambao wameyasikiza tu maneno Niliyonena jana, ambao wameshikilia vikorokoro vya kale na hawajathamini mazao ya siku hii. Watu hawa hawajafanywa tu wafungwa na Shetani, bali wamekuwa watenda dhambi wa milele na kuwa adui Zangu, na wananipinga moja kwa moja. Watu wa aina hii ndio viumbe Nitakaohukumu wakati wa ghadhabu Yangu kali, na leo hii wao bado ni vipofu, wakiwa bado ndani ya jela zenye giza (ambayo ni kusema, watu kama hawa wameoza, maiti zisizo na hisia ambazo zinadhibitiwa na Shetani; kwa sababu macho yao yamefunikwa na Mimi, Ninasema kuwa wao ni vipofu). Ingekuwa vema kutoa mfano kwa ajili ya kurejelea kwenu, ili mpate funzo kutoka kwa mfano huu:

Kwa kumtaja Paulo, mtafikiria historia yake, na baadhi ya hadithi kumhusu zisizo sahihi na zisizo sawa na hali halisi. Yeye alifunzwa na wazazi wake kutoka umri mdogo, na akapata uhai Wangu, na kwa sababu ya maajaliwa Yangu alipata kuwa na ubora wa tabia Ninaohitaji. Akiwa na umri wa miaka 19, alisoma vitabu kadhaa kuhusu maisha; hivyo Sihitaji kueleza kwa kina kuhusu vile, kwa sababu ya ubora wake wa tabia, na kwa sababu ya nuru na mwanga Wangu, hakuweza tu kuzungumza na baadhi ya utambuzi kuhusu mambo ya kiroho, bali pia aliweza kufahamu nia Yangu. Bila shaka, hili haliachi nje muungano wa mambo ya ndani na ya nje. Hata hivyo, udhaifu wake mmoja ulikuwa kwamba, kwa sababu ya talanta zake, mara nyingi angekuwa mwepesi wa kusema maneno yasiyo ya kweli na mwenye kujigamba. Kwa sababu ya hili, kwa ajili ya kutotii kwake, ambako kwa kiasi kuliwakilisha malaika mkuu, Nilipokuwa mwili mara ya kwanza, alijaribu kabisa kuniasi Mimi. Alikuwa mmojawapo wa wale wasiojua maneno Yangu, na nafasi Yangu katika moyo wake ilikuwa tayari imeshapotea. Watu wa aina hii moja kwa moja wanaasi uungu Wangu, na wanaangamizwa na Mimi, na wanainama na kutubu dhambi zao mwishowe tu. Hivyo, baada ya Mimi kumaliza kutumia uwezo wake—ambayo ni kusema, baada ya yeye kunifanyia kazi kwa muda fulani—alirudi tena katika njia zake za zamani, na hata ingawa hakuasi maneno Yangu moja kwa moja, alipuuza mwongozo Wangu na nuru Yangu ya ndani, na hivyo yote aliyokuwa amefanya mbeleni yalikuwa bure; kwa maneno mengine, taji la utukufu alilozungumzia lilikuwa limekuwa maneno tupu, matokeo ya mawazo yake, kwa kuwa hata leo, yeye bado yuko katika hukumu yangu katika minyororo Yangu.

Kutokana na mfano huo hapo juu inaweza kuonekana kuwa yeyote anayeniasi (na sio kuuasi tu mwili Wangu lakini la muhimu zaidi, maneno Yangu na Roho Wangu—ambayo ni kusema, uungu Wangu), anapata hukumu Yangu katika mwili wake. Wakati Roho Wangu Anakuwacha, unaporomoka kwenda chini, unateremka moja kwa moja mpaka kuzimu. Na hata ingawa mwili wako wa nyama uko duniani, wewe ni kama mtu aliye na ugonjwa wa akili: Umepoteza akili yako, na ghafla unahisi ni kama wewe ni maiti, mpaka unanisihi Niutoe mwili wako bila kungoja. Wengi wenu ambao mmejawa na Roho mnao uwezo wa kuelewa hali hii kwa undani, na Mimi sihitaji kuenda katika maelezo mengi zaidi. Katika siku zilizopita, Nilipofanya kazi katika ubinadamu wa kawaida, watu wengi walikuwa tayari wamejipima dhidi ya ghadhabu Yangu na uadhama Wangu, na tayari walijua kiasi kidogo kuhusu hekima na tabia Yangu. Leo hii, Ninazungumza na kutenda moja kwa moja katika uungu, na bado kuna baadhi ya watu ambao wanaona ghadhabu na hukumu Yangu kwa macho yao wenyewe; zaidi ya hayo, kazi muhimu ya sehemu ya pili ya enzi ya hukumu ni kuwafanya watu Wangu wote wajue matendo Yangu katika mwili moja kwa moja, na kuwafanya ninyi nyote muone tabia Yangu moja kwa moja. Ilhali kwa sababu Niko katika mwili, Mimi bado ni mwenye huruma kwa udhaifu wenu. Matumaini Yangu ni kuwa hamtachukua roho, nafsi na mwili wenu kama vitu vya kuchezea, na bila kujali mvikabidhi kwa Shetani. Ni vema mthamini vyote mlivyo navyo, na kutovichukulia kama mchezo, kwa maana vitu hivyo vinahusiana na majaliwa yenu. Je, kweli mnao uwezo wa kuyaelewa maneno Yangu? Je, kweli mnao uwezo wa kujali hisia Zangu za kweli?

Je, mnayo nia ya kustarehe katika baraka Zangu duniani, baraka zilizo sawa na zile za mbinguni? Je, mko tayari kuchukua kuelewa kwao kunihusu, na kufurahia kwa maneno Yangu na ufahamu wako kunihusu, kama vitu vya thamani zaidi na vya muhimu zaidi katika maisha yenu? Je, kweli mnaweza kuwa watiifu Kwangu kikamilifu, bila fikira kwa matarajio yenu wenyewe? Je, kweli mna uwezo wa kujiruhusu kuuwawa na Mimi, na kuongozwa na Mimi, kama kondoo? Je, kunao kati yenu walio na uwezo wa kutimiza vitu kama hivi? Inawezekana kuwa wote wanaokubaliwa na Mimi na kupokea ahadi Zangu ndio wanaopokea baraka Zangu? Je, mmeelewa chochote kutoka katika maneno haya? Nikiwajaribu, je, mnaweza kweli kujiweka wenyewe katika huruma Yangu, na, katikati ya majaribu haya, mtafute nia Yangu na mulewe moyo Wangu? Mimi sitamani wewe uweze kuongea maneno mengi matamu, au utoe hadithi nyingi za kufurahisha; badala yake Ninauliza kuwa uweze kuwa na ushuhuda mzuri Kwangu, na kwamba unaweza kuingia kikamilifu na kwa kina katika hali halisi. Kama Singezungumza moja kwa moja, je, ungewacha kila kitu kilicho karibu na wewe na ukubali kutumiwa na Mimi? Je, hii siyo hali halisi Ninayohitaji? Je, ni nani aliye na uwezo wa kuelewa maana iliyo katika maneno Yangu? Ilhali Ninauliza kuwa msishushwe na wasiwasi tena, kwamba mwe msitari ya mbele katika kuingia kwenu na muelewe kiini cha maneno Yangu. Hii itazuia hali ya nyinyi kutoelewa maneno Yangu, na hali ya kutokuwa na uwazi kuhusu maana Yangu, na hivyo kukiuka amri Zangu za utawala. Natumaini kuwa mtaelewa Nia Yangu kwenu katika maneno Yangu. Msifikiri juu ya matarajio yenu tena, na mtende vile ambavyo mmeamua mbele Yangu kutii mipango ya Mungu katika kila kitu. Wale wote wanaosimama miongoni mwa kaya Yangu wanapaswa kufanya mengi kiasi wanachoweza; unafaa utoe hali yako bora zaidi kwa sehemu ya mwisho ya kazi Yangu duniani. Je, unayo nia ya kuviweka vitu vya aina hii katika matendo?

Februari 23, 1992


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni