Jumapili, 31 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Sita)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia,

10. Hukumu ya Mafarisayo kwa Bwana Yesu
Marko 3:21-22 Na wakati marafiki zake walisikia kuhusu hilo, walitoka kumshika: kwani walisema, Yeye si wa akili sawa. Nao waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema, Ana Beelzebubi, na kupitia mwana wa mfalme wa mapepo huwaondoa mapepo.
11. Mafarisayo Kukemewa na Bwana Yesu
Mat 12:31-32 Ndiyo sababu nawaambieni, Wanadamu watasamehewa kila namna ya dhambi na kukufuru: lakini wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Na yeyote ambaye atasema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa: ila yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.

Jumamosi, 30 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Tano)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yesu,
Mwenyezi Mungu anasema, Halafu, hebu tuangalie vifungu vifuatavyo katika maandiko.
9. Bwana Yesu Atenda Miujiza
1) Bwana Yesu Awalisha Watu Elfu Tano
Yohana 6:8-13 Mmoja wa wanafunzi wake, Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akasema kwake, Kuna mvulana hapa, aliye na mikate mitano ya shayiri nao samaki wawili wadogo: lakini ni yapi miongoni mwa watu wengi? Naye Yesu akasema, Wafanye watu waketi chini. Na kulikuwa na nyasi nyingi pahali hapo.

Ijumaa, 29 Desemba 2017

Upendo wa Mungu | "Kama Nisingeokolewa na Mungu" | Swahili Gospel Music Video

Upendo wa Mungu | "Kama Nisingeokolewa na Mungu" | Swahili Gospel Music Video


Kama Nisingeokolewa na Mungu
Kama nisingeokolewa na Mungu, ningekuwa bado nazurura ulimwenguni humu,
nikipambana kwa bidii na maumivu katika dhambi; kila siku huwa ya taabu isiyo na tarajio.
Kama nisingeokolewa na Mungu, bado ningekuwa nimepondwa chini ya miguu ya shetani,
kama nimenaswa katika dhambi na starehe zake, bila kujua maisha yangu yangekuwaje.
Kama nisingeokolewa na Mungu, nisingekuwa na baraka zangu leo,
wala kujua kwa nini sisi tuendelee kuishi ama maana ya maisha yetu.

Alhamisi, 28 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Nne)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, neema,
Kanisa la Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu anasema, Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba mambo mengi yalifanyika Bwana Yesu alipozaliwa. Kubwa zaidi miongoni mwa hayo lilikuwa kutafutwa na mfalme wa ibilisi, hadi kufikia kiwango cha watoto wote wenye umri wa miaka miwili na chini katika eneo hilo kuchinjwa. Ni dhahiri kwamba Mungu alichukua hatari kubwa kwa kuwa mwili miongoni mwa binadamu; gharama kubwa Aliyolipia kwa ajili ya kukamilisha usimamizi Wake wa kumwokoa mwanadamu pia ni wazi. Matumaini makubwa ambayo Mungu alishikilia kwa ajili ya kazi Yake miongoni mwa wanadamu katika mwili pia ni wazi.

Jumatano, 27 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Tatu)

Mwenyezi Mungu anasema, Kifuatacho tutaangalia mfano uliozungumziwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema.
3. Mfano wa Kondoo Aliyepotea
Mat 18:12-14 Mnafikiri vipi? Iwapo mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao apotee, je, hawaachi hao tisini na tisa, na kuenda milimani, na amtafute huyo ambaye amepotea? Na iwapo atampata, kweli nawaambia, anafurahi zaidi kwa sababu ya huyo kondoo, kuliko wao tisini na tisa ambao hawakupotea. Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.

Jumanne, 26 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Pili)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yesu,
Mwenyezi Mungu anasema, Kama hii ilikuwa habari ya shangwe au ya kisirani kwa binadamu ilitegemea kiini chao kilikuwa kipi. Inaweza kusemekana kwamba hizi hazikuwa habari za shangwe, lakini zilikuwa habari za kisirani kwa baadhi ya watu, kwa sababu Mungu alipoanza kazi Yake mpya, watu hao ambao walifuata tu sheria na masharti, ambao walifuata tu kanuni lakini hawakumcha Mungu wangeegemea upande wa kutumia kazi nzee ya Mungu ili kuishutumu kazi Yake mpya. Kwa watu hawa, hizi zilikuwa habari za kisirani; lakini kwa kila mtu aliyekuwa hana hatia na aliyekuwa wazi, aliyekuwa mwenye ukweli kwa Mungu na aliyekuwa radhi kupokea ukombozi Wake, Mungu kuwa mwili kwa mara ya kwanza zilikuwa habari zenye shangwe sana.

Jumatatu, 25 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Kwanza)

Mwenyezi Mungu anasema,Vikao hivi kadhaa vya ushirika vimekuwa na athari kubwa kwa kila mmoja wa watu. Kwa sasa, watu wanaweza hatimaye kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu na kwamba Mungu kwa hakika yuko karibu sana na wao. Ingawa watu wamemwani Mungu kwa miaka mingi, hawajawahi kuelewa kwa kweli mawazo na fikira Zake kama wanavyozielewa sasa, wala hawajawahi kupata kwa kweli uzoefu wa matendo Yake halisi kama walio nao kwa sasa.

Jumapili, 24 Desemba 2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufalme wa Milenia Umewasili

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufalme wa Milenia Umewasili

Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani. Musa alipokuwa jangwani, Mungu alimwelekeza na kuzungumza naye moja kwa moja.

Jumamosi, 23 Desemba 2017

Swahili Christian Movie Trailer | "Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China"

Swahili Christian Movie Trailer | "Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China"

Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani.

Ijumaa, 22 Desemba 2017

2. Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Wakristo,

2. Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Xiaoxiao Jijini Xuzhou, Mkoani Jiangsu
Kwa sababu ya mahitaji ya kazi ya kanisa, nilihamishwa mpaka mahali pengine ili kutimiza wajibu wangu. Wakati huo, kazi ya injili mahali pale ilikuwa katika hali duni, na hali ya akina kaka na dada kwa kawaida haikuwa nzuri. Lakini kwa kuwa nilikuwa nimeguswa na Roho Mtakatifu, bado nilijitwisha kila kitu nilichoaminiwa nacho kwa matumaini kamili. Baada ya kukubali kuaminiwa, nilihisi uwajibikaji kamili, kupata nuru kamili, na hata nikafikiri kwamba nilikuwa na uamuzi kiasi fulani.

Alhamisi, 21 Desemba 2017

Sura ya 12. Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yesu,

Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana

1. Usijishughulishe na Ikiwa Umejaaliwa na Mungu, bali Ujishughulishe na Ufuatiliaji Wako
Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi hawaelewi mapenzi ya Mungu; wanafikiri kuwa kila mtu ambaye ameamuliwa na Mungu ataokolewa bila kuepuka na wanafikiri kuwa kila mtu asiyeamuliwa na Mungu hataokolewa hata wakiyafanya mambo vyema zaidi. Wanafikiri kwamba Mungu hataamua matokeo ya watu kulingana na utendaji na tabia yao. Iwapo unafikiri hivi, basi unamwelewa Mungu visivyo kabisa. Iwapo Mungu angefanya hili kweli, basi Mungu angekuwa mwenye haki? Mungu huamua matokeo ya watu kulingana na kanuni: Mwishowe matokeo ya watu yataamuliwa kulingana na utendaji wao wa kibinafsi na tabia.

Jumatano, 20 Desemba 2017

Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Leo, tutawasiliana hasa jinsi watu wanavyostahili kumhudumia Mungu katika imani yao kwa Mungu, masharti yanayopaswa kutimizwa na ukweli unaopaswa kufahamika na watu wanaomhudumia Mungu, na mikengeuko ipi iliyoko katika huduma yako. Unapaswa kufahamu haya yote. Masuala haya yanagusia jinsi unavyomwamini Mungu, jinsi unavyotembea katika njia ya kuongozwa na Roho Mtakatifu, na jinsi unatii mipango ya Mungu katika mambo yote, na yatakuwezesha kujua kila hatua ya kazi ya Mungu ndani yako.

Jumanne, 19 Desemba 2017

Swahili Christian Movie Trailer | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Saa ya Giza Kabla ya Mapambazuko"

Swahili Christian Movie Trailer | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Saa ya Giza Kabla ya Mapambazuko"

Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani.

Jumatatu, 18 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II (Sehemu ya Tisa)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, maombi,
Kanisa la Mwenyezi Mungu

Ayubu Atumia Nusu ya Mwisho ya Maisha Yake Katikati ya Baraka za Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Ingawaje baraka Zake wakati huo zilikuwa tu zinajumuisha kondoo, ng'ombe, ngamia, na rasilimali za dunia, na kadhalika, baraka ambazo Mungu alitaka kumpa Ayubu katika moyo Wake zilikuwa mbali zaidi na hizi. Kwa wakati huo ziliporekodiwa, ni aina gani za ahadi za milele ambazo Mungu alipenda kumpa Ayubu? Katika baraka Zake kwa Ayubu, Mungu hakugusia au kutaja kuhusu mwisho wake, na haijalishi umuhimu au cheo ambacho Ayubu alishikilia ndani ya moyo wa Mungu, kwa ujumla Mungu alikuwa akitambua katika baraka Zake.

Jumapili, 17 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II | (Sehemu ya Nane)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia,

Ingawaje Mungu Amefichwa Kutoka kwa Binadamu, Matendo Yake Miongoni mwa Mambo Yote Yanatosha Binadamu Kumjua Yeye

Mwenyezi Mungu alisema, Ayubu alikuwa hajauona uso wa Mungu, wala kusikia matamshi yaliyoongelewa na Mungu, isitoshe yeye mwenyewe binafsi alikuwa hajapitia kazi ya Mungu, lakini kumcha kwake Mungu na ushuhuda aliyokuwa nao wakati wa majaribio kunashuhudiwa na kila mmoja, na kunapendwa, kunafurahiwa, na kupongezwa na Mungu na watu wakayaonea wivu na kuvutiwa nayo, na vilevile, wakaimba nyimbo zao za sifa.

Jumamosi, 16 Desemba 2017

Jinsi ya Kuujua Uhalisi | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Jinsi ya Kuujua Uhalisi | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi.

Ijumaa, 15 Desemba 2017

Mungu ni Mkuu | "Upendo wa Kweli wa Mungu" Swahili Gospel Song | Asante Mungu | Haleluya

Mungu ni Mkuu | "Upendo wa Kweli wa Mungu" Swahili Gospel Song | Asante Mungu | Haleluya


Upendo wa Kweli wa Mungu
Nasimama mbele ya Mungu wangu tena leo.
Moyo wangu una mengi ya kusema
ninapoona uso Wake wa kupendeza.
Nimeacha siku zangu za zamani za kuzurura nyuma yangu.
Neno Lake linanijaza na raha
na furaha kutoka kwa neema Yake.

Alhamisi, 14 Desemba 2017

Mungu ni upendo | "Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu" | Best Swahili Gospel Worship Song

Mungu ni upendo | "Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu" | Best Swahili Gospel Worship Song


Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu
Sasa kwa kushangilia sana, utakatifu wa Mungu na haki
vinakua ulimwenguni kote,
ikitukuka sana kati ya wanadamu wote.
Miji ya mbinguni inacheka, falme za dunia zinacheza.
Ni nani asiyesherehekea? Ni nani asiyetoa machozi?
Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde;
jua linaaangaza kotekote.

Jumatano, 13 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II (Sehemu ya Saba)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, upendo wa Mungu,
Kanisa la Mwenyezi Mungu

Uhusiano Kati ya Uwakilishi wa Mungu ya Ayubu na Shetani na Malengo ya Kazi ya Mungu

Ingawaje watu wengi sasa wanatambua kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, utambuzi huu hauwapi uelewa mkubwa zaidi wa nia ya Mungu. Wakati huohuo wakionea wivu ubinadamu na ushughulikaji wa Ayubu, wanamuuliza Mungu swali lifuatalo: Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu sana, watu walimpenda sana, kwa hivyo kwa nini Mungu akamkabidhi kwa Shetani na kumpitishia maumivu haya makali? Maswali kama hayo yanatarajiwa kuwepo katika mioyo ya watu wengi—au, kushuku huku ndiko hasa swali katika mioyo ya watu wengi. Kwa sababu kushuku huku kumeshangaza watu wengi sana, lazima tuliwasilishe swali hili waziwazi na kulielezea kikamilifu.

Jumanne, 12 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II (Sehemu ya Sita)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumpenda Mungu,

Kuhusu Ayubu

Mwenyezi Mungu alisema, Baada ya kusikia namna Ayubu alivyopitia majaribio, kunao uwezekano kwamba wengi wenu watataka kujua maelezo zaidi kuhusu Ayubu mwenyewe, hasa kuhusiana na siri iliyomfanya akapata sifa za Mungu. Hivyo basi leo, hebu tuzungumzie kuhusu Ayubu!

Katika Maisha ya Kila Siku ya Ayubu Tunaona Utimilifu, Unyofu, Kumcha Mungu, na Kujiepusha na Maovu

Kama tutazungumzia Ayubu, basi lazima tuanze na namna ambavyo alitathminiwa kwa mujibu wa matamshi kutoka kwa kinywa cha Mungu mwenyewe: “hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu.”

Jumatatu, 11 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II (Sehemu ya Tano)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kutotikisika kwa Uadilifu wa Ayubu Kunaleta Aibu Kwake Shetani na Kusababisha Shetani Kutoroka kwa Wasiwasi

Mwenyezi Mungu alisema, Na ni nini ambacho Mungu alifanya wakati Ayubu alipopitia mateso haya? Mungu aliangalia, na kutazama, na Akasubiri matokeo. Wakati Mungu Alipokuwa akiangalia na kutazama, Alihisi vipi? Alihisi kuwa mwenye huzuni, bila shaka. Lakini, kutokana na huzuni Yake, Aliweza kujuta ruhusa Yake kwa Shetani ya kumjaribu Ayubu? Jibu ni, La, Asingefanya hivyo. Kwani Yeye alisadiki kwa dhati kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu, kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu alikuwa amempa Shetani tu fursa ya kuthibitisha uhaki wa Ayubu mbele ya Mungu, na kufichua maovu yake Shetani na hali ya kudharauliwa kwake binafsi.

Jumapili, 10 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II | (Sehemu ya Nne)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu

(Sehemu ya Nne)

Mwenyezi Mungu alisema, Kuanzia mwanzo hadi leo, ni binadamu tu ambaye ameweza kuzungumza na Mungu. Yaani, miongoni mwa viumbe wote walio hai na viumbe wa Mungu, hakuna yeyote isipokuwa binadamu ameweza kuzungumza na Mungu. Binadamu anayo masikio yanayomwezesha kusikia, na macho yanayomwezesha kuona, anayo lugha na fikira zake binafsi, na pia anao uhuru wa kuamua chochote. Anamiliki kila kitu kinachohitajika kusikia Mungu akiongea, na kuelewa mapenzi ya Mungu, na kukubali agizo la Mungu, na hivyo basi Mungu anayaweka matamanio yake yote kwake binadamu, Akitaka kumfanya binadamu kuwa mwandani Wake ambaye anayo akili sawa na Yeye na ambaye anaweza kutembea na Yeye.

Jumamosi, 9 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II(Sehemu ya Tatu)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kwenye kipindi sawa na kile cha Ibrahimu, Mungu pia aliliangamiza jiji. Jiji hili liliitwa Sodoma. Bila shaka, watu wengi wanaijua hadithi ya Sodoma, lakini hakuna yeyote aliyejua fikira za Mungu zilikuwa usuli wa kuangamiza Kwake jiji hili.

Na hivyo leo, kupitia mazungumzo yake Mungu na Ibrahimu hapa chini, tutajifunza fikira Zake wakati huo, huku pia tukijifunza kuhusu tabia Yake. Kinachofuata, hebu tusome vifungu vya maandiko.

Ijumaa, 8 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II | (Sehemu ya Pili)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kazi ya Usimamizi wa Mungu na Wokovu wa Mwanadamu Yaanza kwa Sadaka ya Isaka ilivyotolewa na Ibrahimu

Baada ya kumpa mtoto Ibrahimu, maneno ambayo Mungu alikuwa ametamka kwa Ibrahimu yakawa yametimizwa. Hii haimaanishi kwamba mpango wa Mungu ulifikia mwisho hapa; kinyume cha mambo ni kwamba, mpango wa ajabu wa Mungu wa usimamizi na wokovu wa mwanadamu ndipo ulikuwa tu umeanza, na baraka Yake ya mwana kwa Ibrahimu ilikuwa tu ni utangulizi wa mpango wa usimamizi Wake kwa ujumla. Wakati huo, ni nani aliyejua kwamba vita vya Mungu na Shetani vilikuwa vimeanza kimya kimya wakati Ibrahimu alipomtoa Isaka?

Alhamisi, 7 Desemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II | (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

(Sehemu ya Kwanza)


Kwenye mkutano wetu wa mwisho tuliweza kuzungumzia mada muhimu sana. Je, wakumbuka mada hiyo ilikuwa kuhusu nini? Hebu Niirudie. Mada ya ushirika wetu wa mwisho ilikuwa: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Je, mada hii ni muhimu kwako? Ni sehemu gani katika mada hii ni muhimu kwako? Kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, au Mungu Mwenyewe? Ni sehemu ipi inakuvutia zaidi? Ni sehemu ipi unayotaka kusikiliza kuhusu zaidi?

Jumatano, 6 Desemba 2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 11. Kutatua Asili na Kutenda Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kutatua Asili na Kutenda Ukweli

1. Uhusiano Kati ya Ubinadamu na Uwezo wa Kutenda Ukweli
Watu husema kuwa kutenda ukweli ni vigumu kabisa. Basi mbona watu wengine wanaweza kutenda ukweli? Watu wengine husema ni kwa sababu kwa asili wanaipokea kazi ya Roho Mtakatifu ikifanya kazi juu yao, na pia kwa sababu ni wazuri kiasili. Hoja hii ina kiwango fulani cha mantiki. Watu wengine ni wazuri kiasili; wana uwezo wa kutenda ukweli. Ubinadamu wa watu wengine ni mnyonge, hivyo ni vigumu kwao kutenda ukweli; hii inamaanisha kuwa watakumbana na matatizo fulani.

Jumanne, 5 Desemba 2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 10. Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu

1. Kama hali ya Watu Ni Ya Kawaida Inategemea na Kama Wanapenda Ukweli au La
Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi wameibua suala lifuatalo: Baada ya ushirika wa juu, wanahisi wazi kabisa, wanakuwa na nguvu zaidi, na hawana hisia hasi—lakini hali kama hiyo inabaki tu kwa karibu siku kumi, ambapo baadaye hawawezi kudumisha hali ya kawaida. Suala ni nini? Je mmewahi kujiuliza kinachosababisha hili? Mbona hali zenu ni nzuri sana katika siku hizo takriban kumi za kwanza? Wengine wanasema kuwa hili ni tokeo la kutolenga ukweli. Lakini hivyo ungeweza vipi kufikia kiwango hiki cha kawaida baada ya kusikia ushirika? Mbona ulikuwa na furaha sana baada ya kuusikia ukweli? Wengine wanasema ni kwa sababu ya kazi ya Roho Mtakatifu.

Jumatatu, 4 Desemba 2017

Video za Kikristo | Kuelezea Wazi Uhusiano Kati ya Biblia na Mungu | "Biblia na Mungu" (Swahili Subtitles)

Video za Kikristo | Kuelezea Wazi Uhusiano Kati ya Biblia na Mungu | "Biblia na Mungu" (Swahili Subtitles)

Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba “Biblia ni ufunuo wa Mungu,” “Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu.” Moyoni mwake, Biblia ni kuu. Kwa sababu ya upendo na imani yake pofu katika Biblia, hajawahi kutafuta au kuitazama kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Hadi siku moja, alipowazuia waumini kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu mtandaoni, akawa na fursa ya kukutana na wahubiri kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Baada ya kupitia majadiliano makali kuhusu ukweli, aliweza hatimaye kuona wazi uhusiano kati ya Biblia na Mungu? Je, aliweza kusonga mbali na Biblia kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima? Je, atachukuliwa kwenda mbinguni mbele ya Mungu?

Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki

Jumapili, 3 Desemba 2017

Waovu Lazima Waadhibiwe | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Waovu Lazima Waadhibiwe

Kukagua kama unatenda uhaki katika kila jambo unalotenda, na iwapo matendo yako yanachunguzwa na Mungu, ni tabia za kanuni za wale wanaomwamini Mungu. Utaitwa mwenye haki kwa sababu una uwezo wa kukidhi matakwa ya Mungu, na kwa sababu umekubali utunzaji na ulinzi wa Mungu. Machoni pa Mungu, wote wanaokubali utunzaji, ulinzi na ukamilishaji Wake na wale waliopatwa Naye, ni wenye haki na hutazamwa kwa upendo sana Mungu. Zaidi ya unavyokubali neno la Mungu wakati huu, ndivyo unavyoweza kupokea na kuelewa mapenzi ya Mungu zaidi, na hivyo ndivyo unavyoweza kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu na kukidhi mahitaji Yake.

Jumamosi, 2 Desemba 2017

Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watii kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini. Imani kama hii ni kujidanganya, kujihakikishia, na kujishukuru.

Ijumaa, 1 Desemba 2017

Swahili Christian Movie Trailer | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Kuficha Uhalifu"



Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani. Filamu hii ya hali halisi inayoonyesha kifo cha ghafla na kisichotarajiwa cha Mkristo Mchina aliyeitwa Song Xiaolan–kifo ambacho kwacho polisi wa CCP walitoa maelezo yasiyopatana na yaliyogongana.