Kwenye Siku ya Sita, Muumba Aongea, na Kila Aina ya Kiumbe Hai Akilini Mwake Chajitokeza, Kimoja Baada ya Kingine
Mwenyezi Mungu alisema, Bila kuchoka, kazi ya Muumba ya kuumba viumbe vyote ilikuwa imeendelea kwa siku tano, na punde tu baada ya hapo ndipo Muumba alipokaribisha siku ya sita ya uumbaji Wake wa viumbe vyote. Siku hii ilikuwa mwanzo mwingine mpya, na siku nyingine isiyo ya kawaida.
Nini, basi, kilikuwa mpango wa Muumba mkesha wa siku hii mpya? Ni viumbe vipi vipya ambavyo Angezalisha, je, Angeviumba? Sikiliza, hii ndiyo sauti ya Muumba….
“Naye Mungu aksema, Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake, mifugo, na kitu kinachotambaa, na wanyama wa mwituni kwa namna yake: na ikafanyika. Naye Mungu akaumba wanyawa wa mwituni kwa namna yake, na mifugo kwa namna yake, na chote kinachotambaa duniani kwa namna yake: na Mungu akaona kwamba ni vizuri” (Mwa 1:24-25). Viumbe hai gani ndivyo vinavyojumuishwa hapa? Maandiko yanasema: ng'ombe, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye siku hii hakukuweko tu na aina zote za viumbe hai kwenye nchi, lakini pia vyote vilikuwa vimeainishwa kulingana na aina, na, vilevile, “Mungu akaona ya kuwa ni vizuri.”
Kama tu kwenye siku zile tano za awali, na kwa sauti sawa, kwenye siku ya sita Muumba akashurutisha kuzaliwa kwa viumbe hai Alivyotamani, na vikajitokeza kwenye nchi, kila kimoja kulingana na aina yake. Wakati Muumba anapotekeleza mamlaka Yake, hakuna matamshi Yake yanayotamkwa bure bilashi, na kwa hivyo, kwenye siku ya sita, kila kiumbe hai ambacho Alikuwa amenuia kuumba kikajitokeza wakati ule Aliochagua. Muumba aliposema “Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake,” nchi ilijawa mara moja na maisha, na juu ya ardhi kukaibuka pumzi za aina zote za viumbe hai…. Kwenye jangwa lenye nyasi za kijani, ng’ombe wanene, wakichezesha mikia yao huku na kule, walijitokeza mmoja baada ya mwengine, kondoo waliokuwa wakitoa milio walikusanyika kwa makundi, na farasi waliotoa milio wakaanza kurukaruka…. Mara moja, nchi pana tambarare yenye utulivu ikajaa uhai…. Kujitokeza kwa mifugo hii mbalimbali kulikuwa mandhari ya kupendeza kwenye nchi ile tambarare iliyotulia, na kujitokeza huko kukaleta nguvu zisizo na mipaka…. Wangekuwa wenza wa nchi ile tambarare, na wenyeji wakuu wa nchi ile tambarare, kila mmoja akitegemea mwengine; na vilevile ndivyo pia wangekuwa walezi na walinzi wa ardhi hizi, ambazo zingekuwa makao yao ya kudumu, na ambazo zingewapa kila kitu walichohitaji, chanzo cha ukuzwaji wa milele kwa minajili ya kuwepo kwao …
Kwenye siku iyo hiyo ambayo mifugo hii mbalimbali ilijitokeza, kwa tamko la Muumba, wadudu wengi pia walijitokeza, mmoja baada ya mwengine. Hata ingawaje ndio waliokuwa viumbe hai wadogo zaidi miongoni mwa viumbe vyote, nguvu zao za uhai zilikuwa bado uumbaji wa kimiujiza wa Muumba, na hawakuwasili wakiwa wamechelewa sana…. Baadhi yao walipigapiga mabawa yao madogo, huku wengine wakitambaa polepole; baadhi waliruka juu kwa juu, wengine wakapepesuka; wengine walichimba wakienda mbele, huku wengine wakirudi nyuma kwa haraka; wengine walienda upandeupande, wengine wakaruka juu na chini…. Wote walishughulika kwa kujaribu kujitafutia makao: Baadhi walisukumana na kujipata kwenye nyasi, baadhi walianza kuyachimba mashimo ardhini, baadhi wakapaa hadi kwenye miti, wakiwa wamejificha kwenye msitu…. Ingawaje walikuwa wadogo kwa ukubwa, hawakuwa radhi kuvumilia mateso ya njaa, na baada ya kupata makao yao binafsi, walikimbia kutafuta chakula ili kuweza kujilisha. Baadhi yao walipanda juu ya nyasi ili wale ncha zake laini, baadhi yao walikamata uchafu kwenye vinywa vyao na kuanza kulisha matumbo yao, wakila kwa bidii na kwa furaha (kwao, hata uchafu ulikuwa mlo wenye ladha); wengine walikuwa wamejificha misituni, lakini hawakusita kupumzika, kwani majimaji ndani ya majani yale ya kijani kolevu cha kumetameta yaliwapa mlo wenye utomvu mwingi…. Baada ya wao kushiba, bado wadudu hawakusita kufanya shughuli zao; ingawa walikuwa wadogo kwa kimo, walimilikiwa na nishati ya ajabu pamoja na uchangamfu usio na mipaka, na kwa viumbe vyote wao ndio walikuwa amilifu zaidi na wenye bidii zaidi. Hawakuwahi kuwa wazembe, na hawakuhusika katika mapumziko yoyote. Baada ya kushiba, bado walifanya kazi na wakafanyiza miili yao bidii kwa minajili ya siku zao za usoni, wakiwa wamejishughulisha na kukimbia hapa na pale kwa minajili ya kesho yao ili waweze kuishi…. Kwa utaratibu waliweza kuimba nyimbo zenye midundo tofauti ili kuhimizana na kusihi kila mmoja wao aendelee na kazi. Waliweza pia kuongeza furaha kwenye nyasi, miti, na kila inchi ya udongo, huku wakifanya kila siku, na kila mwaka kuwa wa kipekee…. Wakiwa na lugha zao binafsi na kwa njia zao wenyewe, walipitisha taarifa kwa viumbe vyote vilivyokuwa ardhini. Na wakitumia mkondo wao binafsi maalum wa maisha, waliweka alama katika viumbe vyote, na baadaye wakaacha alama…. Walikuwa na uhusiano wa karibu sana na mchanga, nyasi, na misitu, na walipatia mchanga nguvu na uthabiti, vivyo hivyo kwenye nyasi, na misitu na wakaweza kuleta ushawishi na salamu za Muumba kwa viumbe hai vyote …
Mtazamo wa Muumba ulienea kotekote kwenye viumbe vyote ambavyo Alikuwa ameumba na wakati huu kwa muda huo macho Yake yalitulizia misitu na milima, akili Yake ikigeuka. Huku matamshi Yake yakitamkwa wazi kwenye misitu mingi, na juu ya milima, kulionekana aina ya viumbe fulani vilivyokuwa tofauti na vyovyote vile vilivyokuwa vimekuja hapo awali: Walikuwa wanyama wa mwitu waliotamkwa kwa kinywa cha Mungu. Walikuwa wamepitiliza muda mrefu ajabu, walitikisa vichwa vyao na kupigapiga mikia yao, huku kila mmoja wao akiwa na uso wake pekee. Baadhi yao walikuwa na manyoya mengi, baadhi yao walikuwa wamejikinga, baadhi yao walikuwa na meno ya sumu, baadhi yao walikuwa wanakenua, baadhi yao walikuwa na shingo-ndefu, baadhi yao walikuwa na mkia—mfupi, baadhi walikuwa na macho—mapana, baadhi walikuwa na mtazamo wa woga, baadhi walikuwa wamejiinamia ili wale nyasi, baadhi walikuwa na damu midomoni mwao, baadhi walikuwa wakidundadunda kwa miguu miwili, baadhi walikuwa wakirukaruka kwa kwato nne, baadhi walikuwa wakiangalia mbele juu ya mti, baadhi walikuwa wamejilalia tu wakisubiria misituni, baadhi walikuwa wakitafuta vyumba vya chini kwa chini ili kupumzika, baadhi walikuwa wakikimbiakimbia na kuonyesha furaha ya kipekee kwenye nchi tambarare, baadhi walikuwa wakinyatianyatia kwenye misitu…; baadhi walikuwa wakinguruma, baadhi walikuwa wakitoa milio mikali, baadhi walikuwa wakibweka, baadhi walikuwa wakilia…; baadhi walikuwa na sauti nyororo, baadhi walikuwa na sauti ya kati, baadhi walikuwa na sauti nzito, baadhi walikuwa na sauti safi na yenye mdundo wa kimuziki…; baadhi walikuwa wa kuogofya, na baadhi walikuwa warembo, na baadhi walikuwa wakitisha, baadhi walikuwa wa kuvutia, baadhi walikuwa wa kutishia, baadhi walikuwa wasio na hatia ila wachangamfu…. Mmoja baada ya mwengine, wote walikuja. Tazama namna walivyotembea, kwenye uhuru, wasijue chochote kuhusu wenzao waliokuwa kando yao, wasitake hata kuchukua muda kutazamana…. Kila mmoja akiwa na maisha fulani waliyopewa na Muumba, na umwitu wao binafsi, na ukatili, walionekana kwenye misitu na pia juu ya milima. Viumbe vya kudharauliwa kati ya vyote, na vyenye kuamrisha kabisa—ni nani aliyewafanya kuwa mabingwa wa kweli wa milimani na misituni? Kutoka muda ambao Kuonekna kwao kuliamriwa na Muumba, waliweza “kuweka madai” hayo katika misitu, na “kuweka madai” kwenye milima, kwani Muumba alikuwa tayari amepangilia mipaka yao na Akaamua upana wa uwepo wao. Hawa ndio waliokuwa mabwana wa kweli wa milimani na misitu, na ndiyo maana walikuwa na umwitu mwingi na kwa hivyo wenye dharau. Waliitwa “wanyama wa mwituni” kimsingi kwa sababu, kati ya viumbe vyote, ndio waliokuwa wasiowezekana, wenye unyama, na wasiofugwa. Wasingeweza kufugwa, hivyo basi wasingeweza kulelewa na wasingeishi kwa amani na mapatano na mwanadamu au kufanya kazi kwa niaba ya mwanadamu. Ni kwa Sababu hawakuweza kufugwa, hawakuweza kumfanyia kazi mwanadamu, ndiyo maana iliwalazimu kuishi kwa umbali fulani kutoka kwa mwanadamu, na wasingeweza kusongelewa na mwanadamu. Na ilikuwa kwa sababu waliishi umbali fulani kutoka kwa mwanadamu, na wasingeweza kukaribiwa na mwanadamu ndiposa waliweza kutimiza wajibu wao waliopewa na Muumba: kuilinda milima na misitu. Ule umwitu wao uliilinda milima na kulinda misitu, na ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi na wenye hakikisho la uwepo wao na utekelezaji wao. Wakati uo huo, umwitu wao uliendeleza na kuhakikisha usawazisho miongoni mwa viumbe vyote. Kuwasili kwao kulileta msaada na ukitaji mizizi kwenye milima na misitu; kuingia kwao kuliweza kuingiza nguvu na uthabiti zaidi kwenye milima ile mitupu na misitu mitupu. Kuanzia hapa kwenda mbele, milima na misitu ikawa ni makao yao ya kudumu, na wasingewahi kupoteza maskani yao, kwa sababu milima na misitu ilionekana na ikawepo kwa ajili yao, na wanyama wa mwituni wangetimiza wajibu wao na kufanya kila kitu ambacho wangeweza ili kuilinda. Kwa hivyo, pia, wanyama wa mwituni wangeweza kutii kwa umakinifu kule kusihiwa na Muumba ili waweze kushikilia eneo lao, na kuendelea kutumia asili yao ya kinyama ili kuendeleza usawazisho wa viumbe vyote vilivyoanzishwa na Muumba, na kuonyesha waziwazi mamlaka na nguvu za Muumba!
Katika Mamlaka ya Muumba, Viumbe Vyote ni Timilifu
Viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, vikiwemo vile vilivyoweza kusonga na vile visingeweza kusonga, kama vile ndege na samaki, kama vile miti na maua, na hata ikiwemo mifugo, wadudu na wanyama wa mwituni, wote walioumbwa kwenye siku ya sita—wote walikuwa wazuri mbele ya Mungu, na, vilevile, machoni mwa Mungu, viumbe hivi, kulingana na mpango Wake, vilikuwa vimetimiza kilele cha utimilifu, navyo vilikuwa vimefikia viwango ambavyo Mungu alitaka kutimiza. Hatua kwa hatua, Muumba alifanya kazi Aliyonuia kufanya kulingana na mpango Wake. Kimoja baada ya kingine, vitu hivi Alivyonuia kuumba vilijitokeza, na kujitokeza kwa kila kiumbe kulikuwa onyesho la Mamlaka ya Muumba, na uthibitishaji wa mamlaka Yake, na kwa sababu ya uthibitishaji huu, viumbe vyote visingeweza kufanya chochote kingine ila kushukuru kwa neema ya Muumba na riziki ya Muumba. Huku vitendo hivi vya kimiujiza vya Mungu vikijionyesha, ulimwengu huu ulijaa, vipande kwa vipande, ukiwa na viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, na ukabadilika kutoka kwa fujo na giza hadi kwa wazi na uangavu, kutoka kwenye utulivu wa kutisha hadi kwa uchangamfu na nguvu zisizokuwa na mipaka. Miongoni mwa viumbe vyote vya uumbaji, kutoka kwa wale wakubwa hata wadogo, toka kwa wadogo hata kwa wale wadogo zaidi, hakuna hata kiumbe kimoja ambacho hakikuumbwa kupitia kwa Mamlaka na nguvu za Muumba, na kukawa na upekee na haja ya ndani kwa ndani na thamani ya uwepo wa kila kiumbe. Licha ya tofauti zao katika maumbo na muundo, lazima viumbe hivi vingeumbwa na Muumba ili viwepo chini ya mamlaka ya Muumba. Wakati mwingine watu wataona mdudu, yule aliye na sura mbaya kabisa na watasema, “Mdudu yule ni sura mbaya kweli, hakuna vile ambavyo kiumbe chenye sura mbaya kama hicho kinaweza kuwa kiliumbwa na Mungu—hakuna njia ambayo Angeumba kitu chenye sura mbaya hivyo.” Mtazamo wa kijinga ulioje! Kile wanachofaa kusema ni, “ingawaje mdudu huyu ana sura mbaya sana, aliumbwa na Mungu, na kwa hivyo, lazima awe na kusudio lake la kipekee.” Kwenye fikira za Mungu, Alinuia kupatia kila mojawapo ya sura, na kazi na matumizi aina zote, katika viumbe mbalimbali vilivyo na uhai Alivyoumba, na hivyo basi hamna kati ya viumbe hivyo ambavyo Mungu aliumba vilivyoumbwa vikiwa vimefanana. Kuanzia sura yao ya nje hadi mkusanyiko wao wa ndani, kuanzia katika mazoea yao ya kuishi hadi mahali pa kuishi—kila kiumbe ni tofauti. Ng’ombe wana sura ya ng’ombe, punda wana sura ya punda, paa ana sura ya paa, na ndovu wana sura ya ndovu. Je, unaweza kusema ni kiumbe kipi kinachovutia zaidi na ni kipi kinachotisha zaidi kwa sura? Je, unaweza kusema ni kiumbe kipi chenye manufaa zaidi na uwepo wa kile ambacho hakihitajiki sana? Baadhi ya watu wanapenda namna ambavyo ndovu hufanana, lakini hakuna anayetumia ndovu kutayarisha mashamba ya kupanda: baadhi ya watu wanapenda namna simba na chui mkubwa mwenye milia walivyo, kwani sura inavutia zaidi miongoni mwa viumbe vyote, lakini je, unaweza kuwafuga nyumbani? Kwa ufupi, kuhusiana na viumbe vyote, binadamu anafaa kurejelea mamlaka ya Muumba, hivi ni kusema kwamba, rejelea mpangilio uliochaguliwa na Muumba katika viumbe vyote; huu ndio mtazamo wenye hekima zaidi. Mtazamo tu wa kutafutiza, na wa kuwa mtiifu, kwa nia ama makusudio ya mwanzo ya Muumba ndio ukubalifu wa kweli na hakika wa mamlaka ya Muumba. Ni vyema kwa Muumba, kwa hivyo ni sababu gani ambayo binadamu atakuwa nayo ya kusema kwamba si vyema?
Hivyo basi, viumbe vyote vilivyo katika mamlaka ya Muumba vitaweza kuchezesha mdundo mpya wa ukuu wa Muumba, vitaanza utangulizi mwema kwa minajili ya kazi Yake kwenye siku mpya, na kwa muda huu Muumba ataufungua ukurasa mpya katika kazi ya usimamizi Wake! Kulingana na sheria ya mimea ya machipuko, kukomaa kwa kiangazi, mavuno ya mapukutiko, na hifadhi ya kipupwe iliyochaguliwa na Muumba, viumbe hivi vyote vitaweza kutilia mkazo mpango wa usimamizi wa Muumba na vitakaribisha siku yao mpya, mwanzo mpya, na mkondo mpya wa maisha, na hivi karibuni vitu vitaweza kuzaana katika mfululizo usioisha ili kuweza kukaribisha kila siku katika ukuu wa mamlaka ya Muumba …
Hakuna Kiumbe Chochote Kati ya Vile Vilivyoumbwa na Vile Ambavyo Havikuumbwa Kinaweza Kubadilisha Utambulisho wa Muumba
Tangu Alipoanza uumbaji wa viumbe vyote, nguvu za Mungu zilianza kuonyeshwa na zikaanza kufichuliwa, kwani Mungu alitumia maneno kuumba vitu vyote. Haijalishi ni njia gani Alitumia, haijalishi ni kwa nini Aliviumba, viumbe vyote viliumbwa na kusimama imara na kuwepo kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba. Kwenye muda kabla ya mwanadamu kuumbwa ulimwenguni, Muumba alitumia nguvu na mamlaka Yake kuumba viumbe vyote kwa minajili ya mwanadamu, na Akatumia mbinu za kipekee kutayarisha mazingira yanayofaa kuishi mwanadamu. Kwa yote Aliyoyafanya, ilikuwa ni kwa kumtayarishia mwanadamu ambaye hivi karibuni angepokea pumzi Zake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye muda ule kabla ya mwanadamu kuumbwa, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa kupitia kwenye viumbe vyote tofauti na mwanadamu, na vitu vikubwa kama vile mbingu, nuru, bahari, na ardhi, na vile vilivyo vidogo kama vile wanyama na ndege, pamoja na wadudu na vijiumbe vyote vya kila aina, zikiwemo vimelea mbalimbali visivyoonekana kwa macho ya kawaida. Kila mojawapo kilipewa maisha kwa matamshi ya Muumba, na kila kiumbe mojawapo kilizaana kwa sababu ya matamshi ya Muumba na kila kimojawapo kiliishi chini ya ukuu wa Muumba kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Ingawaje hawakupokea pumzi za Muumba, bado walionyesha maisha na nguvu walizopewa na Muumba kupitia kwa mifumo na miundo yao mbalimbali; ingawaje hawakupokea uwezo wa kuongea aliopewa mwanadamu na Muumba, kila kimojawapo kilipokea njia ya kuelezea maisha yao ambayo walipewa na Muumba, na ambayo ilitofautiana na ile lugha ya Mwanadamu. Mamlaka ya Muumba hayatoi tu nguvu za maisha kwenye vifaa vinavyoonekana kuwa tuli, ili visiwahi kutoweka, lakini, vilevile, hupatia silika ya kuzaana na kuongezeka kwa kila kiumbe hai, ili visiwahi kutoweka, na ili kizazi baada ya kizazi, vitaweza kupitisha sheria na kanuni za kuishi walizopewa na Muumba. Namna ambavyo Muumba anatilia mkazo mamlaka Yake haikubaliani kwa lazima na mtazamo wa mambo makubwamakubwa au madogomadogo, na haiwekewi mipaka ya umbo lolote; Anaweza kuamuru utendaji mambo katika ulimwengu na kushikilia ukuu juu ya maisha na kifo cha viumbe vyote, na, vilevile, Anaweza kushughulikia viumbe vyote ili viweze kumhudumia Yeye; Anaweza kusimamia kazi zote za milima, mito, na maziwa, na kutawala viumbe vyote ndani yake, na, zaidi ya hayo, Anaweza kutoa kile ambacho kinahitajika na viumbe vyote. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya pekee ya Muumba miongoni mwa viumbe vyote mbali na mwanadamu. Maonyesho kama hayo si tu ya maisha tunayoishi, na hayatawahi kusita, au kupumzika, na hayawezi kubadilishwa au kuharibiwa na mtu yeyote au kitu chochote, wala hayawezi kuongezwa au kupunguzwa na mtu yeyote au kitu chochote—kwani hamna kile kinachoweza kubadilisha utambulisho wa Muumba, na, hivyo basi, mamlaka ya Muumba hayawezi kubadilishwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, na hayawezi kufikiwa na kiumbe chochote-ambacho hakikuumbwa. Chukulia wajumbe na malaika wa Mungu kwa mfano. Hawamiliki nguvu za Mungu, isitoshe hawamiliki mamlaka ya Muumba, na sababu ambayo hawana nguvu na mamlaka ya Mungu ni kwa sababu hawamiliki ile hali halisi ya Muumba. Vile viumbe ambavyo havikuumbwa, kama vile wajumbe na malaika wa Mungu, ingawaje vinaweza kufanya baadhi ya mambo kwa niaba ya Mungu, haviwezi kuwakilisha Mungu. Ingawaje wanamiliki nguvu fulani zisizomilikiwa na binadamu, hawamiliki mamlaka ya Mungu, hawamiliki mamlaka ya Mungu ya kuumba viumbe vyote, na kuamuru viumbe vyote, na kushikilia kuwa na ukuu juu ya viumbe vyote. Na kwa hivyo upekee wa Mungu hauwezi kubadilishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa, na vilevile, mamlaka na nguvu za Mungu haviwezi kusawazishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa. Kwenye Biblia, je, umewahi kusoma kuhusu mjumbe yeyote wa Mungu aliyeumba viumbe vyote? Na kwa nini Mungu hakuwahi kutuma mmojawapo wa wajumbe Wake au malaika kuumba viumbe vyote? Kwa sababu hawakumiliki mamlaka ya Mungu, na kwa hivyo hawakumiliki uwezo wa kutekeleza mamlaka ya Mungu. Sawa tu na viumbe vyote, viumbe vyote visivyoumbwa viko chini ya ukuu wa Muumba, na chini ya mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo, kwa njia ile ile, Muumba pia ni Mungu wao na pia ndiye Mtawala wao. Miongoni mwa kila mmoja wao—haijalishi kama wao ni sharifu au kina yahe, wenye nguvu nyingi au kidogo—hakuna hata mmoja anayeweza kuzidi mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo miongoni mwao, hakuna hata mmoja wao anayeweza kubadilisha utambulisho wa Muumba. Hawatawahi kuitwa Mungu, na hawatawahi kuweza kuwa Muumba. Huu ni ukweli na hoja zisizobadilika!
Kupitia ushirika uliotajwa hapo juu, je, tunaweza kusema yafuatayo: Muumba na Kiongozi wa viumbe vyote tu, Yule anayemiliki mamlaka ya kipekee na nguvu za kipekee, ndiye Anayeweza kuitwa Mungu Mwenyewe wa kipekee? Wakati huu, unaweza kuhisi kwamba swali kama hilo ni la kina sana. Wewe, kwa muda huu, huwezi kulielewa, na huwezi kung'amua kiini cha ndani na kwa hivyo kwa muda huu unahisi kwamba ni swali gumu kujibu. Kwa hivyo, Nitaendelea na ushirika Wangu. Kinachofuata, Nitakuruhusu kutazama vitendo halisi vya dhana nyingi za mamlaka na nguvu zinazomilikiwa na Mungu pekee, na hivyo basi Nitakuruhusu kuelewa kwa kweli, kushukuru, na kujua upekee wa Mungu, na maana ya mamlaka ya kipekee ya Mungu.
2. Mungu Hutumia Matamshi Yake Kuanzisha Agano na Binadamu
Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.
Baada ya Kuumba Viumbe Vyote, Mamlaka ya Muumba Yanathibitishwa na Kuonyeshwa kwa Mara Nyingine Tena Kwenye Agano la Upinde wa Mvua
Mamlaka ya Muumba siku zote yanaonyeshwa na kutekelezwa miongoni mwa viumbe vyote, Naye hatawali tu hatima ya viumbe vyote, lakini pia Anatawala mwanadamu, kiumbe maalum ambacho Aliumba kwa mikono Yake mwenyewe, na kinachomiliki muundo tofauti wa uhai na kinachopatikana kwa mfumo tofauti wa uhai. Baada ya kuumba viumbe vyote, Muumba hakusita kuonyesha mamlaka na nguvu Zake; kwake Yeye, mamlaka ambayo Alishikilia ukuu juu ya viumbe vyote na hatima ya mwanadamu kwa ujumla, ilianza rasmi tu pale ambapo mwanadamu alizaliwa kwa kweli kutoka kwenye mkono Wake. Alinuia kusimamia mwanadamu, kutawala mwanadamu, Alinuia kumwokoa mwanadamu, Alinuia kufaidi mwanadamu kwa kweli, kufaidi mwanadamu ambaye angetawala viumbe vyote, na Alinuia kumfanya mwanadamu kama huyo kuishi chini ya mamlaka Yake, na kujua mamlaka Yake, na kutii mamlaka Yake. Hivyo basi, Mungu akaanza kuonyesha rasmi mamlaka Yake miongoni mwa binadamu kwa kutumia matamshi Yake, na Akaanza kutumia mamlaka Yake kutambua matamshi Yake. Bila shaka, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa mbele katika sehemu zote wakati wa mchakato huu; Nimeweza kuchukua tu baadhi ya mifano mahususi, inayojulikana ambayo unaweza kuelewa na kujua upekee wa Mungu na kuelewa na kujua upekee wa mamlaka ya Mungu.
Mamlaka ya Muumba siku zote yanaonyeshwa na kutekelezwa miongoni mwa viumbe vyote, Naye hatawali tu hatima ya viumbe vyote, lakini pia Anatawala mwanadamu, kiumbe maalum ambacho Aliumba kwa mikono Yake mwenyewe, na kinachomiliki muundo tofauti wa uhai na kinachopatikana kwa mfumo tofauti wa uhai. Baada ya kuumba viumbe vyote, Muumba hakusita kuonyesha mamlaka na nguvu Zake; kwake Yeye, mamlaka ambayo Alishikilia ukuu juu ya viumbe vyote na hatima ya mwanadamu kwa ujumla, ilianza rasmi tu pale ambapo mwanadamu alizaliwa kwa kweli kutoka kwenye mkono Wake. Alinuia kusimamia mwanadamu, kutawala mwanadamu, Alinuia kumwokoa mwanadamu, Alinuia kufaidi mwanadamu kwa kweli, kufaidi mwanadamu ambaye angetawala viumbe vyote, na Alinuia kumfanya mwanadamu kama huyo kuishi chini ya mamlaka Yake, na kujua mamlaka Yake, na kutii mamlaka Yake. Hivyo basi, Mungu akaanza kuonyesha rasmi mamlaka Yake miongoni mwa binadamu kwa kutumia matamshi Yake, na Akaanza kutumia mamlaka Yake kutambua matamshi Yake. Bila shaka, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa mbele katika sehemu zote wakati wa mchakato huu; Nimeweza kuchukua tu baadhi ya mifano mahususi, inayojulikana ambayo unaweza kuelewa na kujua upekee wa Mungu na kuelewa na kujua upekee wa mamlaka ya Mungu.
Kunao mfanano kati ya fungu kwenye Mwanzo 9:11-13 na Mafungu yaliyo hapo juu yanayohusu rekodi za Mungu kuumba ulimwengu, ilhali kunayo pia tofauti. Mfanano ni upi? Mfanano umo katika matumizi ya matamshi na Mungu kuweza kufanya kile ambacho Alinuia, na tofauti ni kwamba, fungu hili ni mazungumzo ya Mungu na binadamu, ambapo Alianzisha agano na binadamu, na Akamwambia binadamu kuhusu kile ambacho kilikuwa ndani ya agano hilo. Utiliaji mkazo huu wa mamlaka ya Mungu ulitimizwa wakati wa mazungumzo Yake na Mungu, hivi ni kusema kwamba, kabla ya uumbaji wa mwanadamu, maneno ya Mungu yalikuwa maagizo, na amri ambavyo vilitolewa kwa viumbe ambavyo Alinuia kuumba. Lakini sasa kulikuwa na mtu wa kusikiliza matamshi ya Mungu, na hivyo basi matamshi Yake yalikuwa ya mazungumzo na binadamu, na pia himizo na onyo kwa binadamu, na zaidi, kulikuwa na amri zilizotolewa kwa viumbe vyote vilivyokuwa na mamlaka Yake.
Ni hatua gani ya Mungu imerekodiwa katika fungu hili? Inarekodi agano ambalo Mungu alianzisha na binadamu baada ya Yeye kuangamiza ulimwengu kwa gharika, linamwambia binadamu kwamba Mungu asingesababisha maangamizo katika ulimwengu tena, na kwamba, hadi mwisho huu, Mungu aliumba ishara—na ishara hii ilikuwa nini? Kwenye Maandiko inasemekana kwamba “naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.” Haya ni matamshi ya asili yaliyotamkwa na Muumba kwa mwanadamu. Aliposema matamshi haya, upinde wa mvua ulionekana mbele ya macho ya binadamu, ambapo ulibakia mpaka leo. Kila mmoja ameuona upinde wa mvua kama huo, na unapouona, je, unajua namna unavyojitokeza? Sayansi haiwezi kuthibitisha haya, au kutafuta chanzo chake, au kutambua mambo yanayosababisha upinde huu wa mvua. Hiyo ni kwa sababu, upinde wa mvua ni ishara ya agano lilioanzishwa kati ya Muumba na binadamu; hauhitaji msingi wowote wa kisayansi, haukuumbwa na binadamu, wala binadamu hawezi kuubadilisha. Ni maendelezo ya mamlaka ya Muumba baada ya Yeye kuongea matamshi Yake. Muumba alitumia mbinu fulani Yake mwenyewe kutii agano lake na binadamu na ahadi Yake, na hivyo basi matumizi Yake ya upinde wa mvua kama ishara ya agano ambalo Alianzisha ni maelekezo na sheria ya kimbinguni yatakayobakia milele hivyo, haijalishi kama ni kuhusiana na Muumba au mwanadamu aliyeumbwa. Ilhali sheria hii isiyobadilika ni, lazima isemwe, maonyesho mengine ya kweli ya mamlaka ya Muumba kufuatia uumbaji Wake wa viumbe vyote, na lazima isemwe kwamba mamlaka na nguvu za Muumba havina mipaka; matumizi Yake ya upinde wa mvua ni ishara ya maendelezo na upanuzi wa mamlaka ya Muumba. Hiki kilikuwa kitendo kingine kilichotekelezwa na Mungu kwa kutumia matamshi Yake, na kilikuwa ni ishara ya agano ambalo Mungu alikuwa ameanzisha na mwanadamu kwa kutumia matamshi. Alimwambia binadamu kuhusu kile ambacho Aliamua kuleta, na kwa njia gani kingekamilishwa na kutimizwa, na kwa njia hii suala liliweza kutimizwa kulingana na matamshi kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Mungu pekee ndiye anayemiliki nguvu kama hizo, na leo, miaka elfu kadhaa baada ya Yeye kuongea matamshi haya, binadamu angali bado anaweza kuangalia upinde wa mvua uliozungumziwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Kwa sababu ya matamshi hayo yaliyotamkwa na Mungu, kitu hiki kimebakia bila ya kusongezwa na kubadilishwa mpaka hadi leo. Hakuna anayeweza kuuondoa upinde huu wa mvua, hakuna anayeweza kubadilisha sheria zake, na upo kimsingi kutokana na matamshi ya Mungu. Haya kwa hakika ni mamlaka ya Mungu. “Mungu ni mzuri tu kama matamshi Yake, na matamshi Yake yataweza kukamilishwa, na kile ambacho kimekamilishwa kinadumu milele.” Matamshi kama haya kwa kweli yanaonyeshwa waziwazi hapa, na ni ishara na sifa wazi kuhusu mamlaka na nguvu za Mungu. Ishara au sifa kama hiyo haimilikiwi na au kuonekana katika viumbe vyovyote vile vilivyoumbwa, wala kuonekana kwenye viumbe vyovyote vile ambavyo havikuumbwa. Inamilikiwa tu na Mungu wa kipekee, na inapambanua utambulisho na hali halisi inayomilikiwa tu na Muumba kutoka ile ya viumbe. Wakati uo huo, ni ishara na sifa pia ambayo mbali na Mungu Mwenyewe, haitawahi kupitwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa.
Uanzishaji wa agano Lake Mungu na binadamu kilikuwa ni kitendo chenye umuhimu mkubwa, na ambao Alinuia kutumia ili kuwasilisha hoja kwa binadamu na kumwambia binadamu mapenzi Yake, na hadi hapa, Alitumia mbinu ya kipekee, kwa kutumia ishara maalum ya kuanzisha agano na binadamu, ishara ambayo ilikuwa ahadi ya agano ambalo Alikuwa ameanzisha na binadamu. Kwa hivyo, je, uanzishaji wa agano hili ulikuwa ni tukio kubwa? Na tukio hili lilikuwa kubwa vipi? Hii haswa ndiyo inayoonyesha namna ambavyo agano hili lilivyo maalum: si agano lililoanzishwa kati ya binadamu mmoja na mwengine, au kundi moja na jingine, au nchi moja na nyingine, lakini agano lililoanzishwa kati ya Muumba na wanadamu kwa ujumla, na litabakia halali mpaka siku ambayo Muumba atakomesha mambo yote. Mtekelezaji wa agano hili ni Muumba, na mwendelezaji pia ni Muumba. Kwa ufupi, uzima wa agano la upinde wa mvua ulioanzishwa pamoja na mwanadamu ulikamilishwa na kutimizwa kulingana na mazungumzo kati ya Muumba na mwanadamu, na umebakia vivyo hivyo mpaka leo. Ni nini kingine ambacho viumbe vinaweza kufanya mbali na kujinyenyekeza, na kutii, na kusadiki, na kushukuru, na kutolea ushuhuda, na kusifu mamlaka ya Muumba? Kwani hamna yeyote yule isipokuwa Mungu wa pekee anayemiliki nguvu za kuanzisha agano kama hilo. Kujitokeza kwa upinde wa mvua mara kwa mara, kunatangaza kwa mwanadamu na kumtaka azingatie agano lile kati ya Muumba na mwanadamu. Katika kujitokeza kwingine kwa agano kati ya Muumba na binadamu, kile kinachoonyeshwa kwa mwanadamu si upinde wa mvua au agano lenyewe, lakini ni mamlaka yenyewe yasiyobadilika ya Muumba. Kujitokeza kwa upinde wa mvua, mara kwa mara, kunaonyesha yale matendo ya kipekee na ya kimiujiza ya Muumba yanayopatikana kwenye sehemu zilizofichwa, na, wakati uo huo ni onyesho muhimu la mamlaka ya Muumba ambayo hayatawahi kufifia, na wala kubadilika. Je, hili si onyesho la dhana nyingine ya mamlaka ya kipekee ya Muumba?
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni