Kwenye Siku ya Tatu
Kwenye Siku ya Tatu, Matamshi ya Mungu Yazaa Ardhi na Bahari, na Mamlaka ya Mungu Yasababisha Ulimwengu Kujaa Maisha
Sasa, hebu na tusome sentensi ya kwanza ya Mwanzo 1:9-11:
“Naye Mungu akasema, Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane.” Ni mabadiliko gani yaliyotokea baada ya Mungu kusema tu, “Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane”? Na hii nafasi iliyokuwa katikati ya nuru na anga ilikuwa nini? Katika Maandiko, imeandikwa: “Naye Mungu akaiita nchi kavu Dunia: na kukonga kwa maji akakuita Bahari: naye Mungu akaona kwamba ni vyema.” Hivi ni kusema, kulikuwepo sasa na ardhi na bahari kwenye anga hii, nayo ardhi na bahari viliweza kutenganishwa. Kujitokeza kwa vitu hivi vipya kulifuata amri kutoka kwenye kinywa cha Mungu, “na kukawa vivyo hivyo.” Je, Maandiko yanafafanua Mungu akiwa ameshughulika kila pahali wakati Akifanya haya? Je, yanafafanua Mungu akiwa anajihusisha katika kazi ngumu? Kwa hivyo, haya yote yaliwezaje kufanywa na Mungu? Mungu aliwezaje kusababisha vitu hivi vipya kuumbwa? Tunaelewa wenyewe bila kuelezewa, kwamba Mungu alitumia matamshi kutimiza mambo haya yote, kuumba uzima wa haya yote.
“Naye Mungu akasema, Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane.” Ni mabadiliko gani yaliyotokea baada ya Mungu kusema tu, “Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane”? Na hii nafasi iliyokuwa katikati ya nuru na anga ilikuwa nini? Katika Maandiko, imeandikwa: “Naye Mungu akaiita nchi kavu Dunia: na kukonga kwa maji akakuita Bahari: naye Mungu akaona kwamba ni vyema.” Hivi ni kusema, kulikuwepo sasa na ardhi na bahari kwenye anga hii, nayo ardhi na bahari viliweza kutenganishwa. Kujitokeza kwa vitu hivi vipya kulifuata amri kutoka kwenye kinywa cha Mungu, “na kukawa vivyo hivyo.” Je, Maandiko yanafafanua Mungu akiwa ameshughulika kila pahali wakati Akifanya haya? Je, yanafafanua Mungu akiwa anajihusisha katika kazi ngumu? Kwa hivyo, haya yote yaliwezaje kufanywa na Mungu? Mungu aliwezaje kusababisha vitu hivi vipya kuumbwa? Tunaelewa wenyewe bila kuelezewa, kwamba Mungu alitumia matamshi kutimiza mambo haya yote, kuumba uzima wa haya yote.
Kwenye mafungu matatu yaliyo hapo juu, tumejifunza kunatokea matukio matatu makubwa. Matukio haya matatu makubwa yalionekana, na yakaumbwa kuwa hivyo, kupitia kwa matamshi ya Mungu, na ni kwa sababu ya matamshi Yake ndipo, moja baada ya lengine, yaliweza kujitokeza mbele ya macho ya Mungu. Kwa hivyo inaweza kuonekana kwamba “Mungu huongea, na ikatimizwa; huamuru, na ikawa imara” haya si maneno matupu. Hali hii halisi ya Mungu inathibitishwa wakati ule ambao fikira Zake zinaeleweka, na wakati ambapo Mungu hufungua kinywa Chake kuongea, hali Yake halisi inajionyesha kikamilifu.
Hebu na tuendelee hadi kwenye sentensi ya mwisho ya fungu hili: “Naye Mungu akasema, Na dunia izae majani, mche ambao unatoa mbegu, na mti wa matunda ambao unazaa tunda kwa aina yake, ambao mbegu zake ziko ndani yake, juu ya dunia: na kukawa vivyo hivyo.” Huku Mungu akiongea, mambo haya yote yaliumbika kufuatia fikira za Mungu, na kwa muda mfupi tu, mseto wa viumbe vidogo vinyonge vyenye maisha vilikuwa vinachomoza vichwa vyao kwa kusita huku vichwa vyao vikiwa juu kupitia kwenye ardhi, na hata kabla ya kukung’uta chembechembe za uchafu kutoka kwenye miili yao vilikuwa vikipungiana mikono kusalimiana kwa hamu, kuitikia na kuufurahia ulimwengu. Vilishukuru Muumba kwa maisha aliyovipatia, na kuutangazia ulimwengu kwamba vilikuwa sehemu ya viumbe vyote, na kwamba kila kimojawapo kingejitolea katika maisha yavyo ili viwe vinaonyesha mamlaka ya Muumba. Kama vile matamshi ya Mungu yalivyotamkwa, ardhi ikawa yenye rutuba na kijani, aina zote za miti ambayo ingeweza kufurahiwa na binadamu iliweza kuota na kuchipuka kutoka kwenye ardhi, na milima na nchi tambarare vyote vikawa na idadi kubwa ya miti na misitu…. Ulimwengu huu tasa, ambao hakukuwahi kuwepo na chembechembe zozote za maisha, ulifunikwa mara moja na wingi wa nyasi, mimea ya msimu na miti na ilikuwa ikifurika kwa kijani kibichi kingi…. Harufu nzuri ya nyasi na mnukio wa mchanga uliosambazwa kupitia hewani, na mseto wa mimea vyote vilianza kupumua kulingana na mzunguko wa hewa, na vikaanza pia mchakato wa kukua. Wakati uo huo, kutokana na maneno ya Mungu na kufuatia fikira za Mungu, mimea yote ilianza mizunguko isiyoisha ya maisha ambapo inakua, inanawiri, inazaa matunda na kuzaana na kuongezeka. Ilianza kutii kwa umakinifu mikondo yao husika ya maisha, na kuanza kutekeleza wajibu wao husika miongoni mwa viumbe vyote…. Yote ilizaliwa na kuishi, kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Ingepokea matoleo na ustawishi usiosita wa Muumba, na siku zote ingeendelea kuishi kwa shauku katika kila pembe ya ardhi ili kuonyesha mamlaka na nguvu za Muumba, na siku zote ingeonyesha nguvu za maisha walizopewa na Muumba …
Mwenyezi Mungu alisema, Maisha ya Muumba ni yale yasiyo ya kawaida, fikira Zake ni zile zisizo za kawaida, na mamlaka Yake ni yale yasiyokuwa ya kawaida, na kwa hivyo, wakati matamshi Yake yalipotamkwa, yale matokeo ya mwisho yalikuwa “na ikawa hivyo.” Ni wazi kwamba, Mungu hahitaji kufanya kazi kwa mikono Yake wakati Anapofanya matendo; Anatumia tu fikira Zake kutoa amri, na matamshi Yake ili kuagizia, na kwa njia hii mambo yanatimizwa. Kwenye siku hii, Mungu aliyakusanya maji katika mahali pamoja, na Akaiacha ardhi kavu kujitokeza, baada ya hapo Mungu aliifanya nyasi kuota kutoka kwenye ardhi, na papo hapo palimea mimea ya msimu iliyozaa mbegu, na miti ya kuzaa matunda, na Mungu akaainisha kila mojawapo kulingana na aina, na kusababisha kila mmea kuwa na mbegu yake. Haya yote yaliwezekana kulingana na fikira za Mungu na amri za matamshi ya Mungu, na kila mmea ulijitokeza, mmoja baada ya mwingine, kwenye ulimwengu huu mpya.
Wakati Alikuwa aanze kazi Yake, Mungu tayari alikuwa na picha ya kile Alichonuia kutimiza katika akili Zake na wakati ambapo Mungu alianza kutimiza mambo haya, na ndio wakati ambao pia Mungu alikifungua kinywa Chake kuongea kuhusu maudhui ya picha hii, mabadiliko katika viumbe vyote yalianza kufanyika kutokana na mamlaka na nguvu za Mungu. Bila ya kujali namna Mungu alivyofanya, au Alivyoonyesha mamlaka Yake, kila kitu kilitimizwa hatua kwa hatua kulingana na mpango wa Mungu na kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na mabadiliko ya hatua kwa hatua yalifanyika kati ya mbingu na ardhi kutokana na matamshi na mamlaka ya Mungu. Mabadiliko na matukio haya yote yalionyesha mamlaka ya Muumba, na nguvu za maisha ya Muumba zisizo za kawaida na zenye ukubwa. Fikira Zake si mawazo mepesi, au picha tupu, lakini mamlaka yanayomiliki nishati kuu na ile isiyo ya kawaida, na ndio nguvu zinazosababisha viumbe vyote kubadilika, kufufuka, kupata nguvu upya, na kuangamia. Na kwa sababu ya haya, viumbe vyote hufanya kazi kwa sababu ya fikira Zake, na, wakati uo huo, yote haya yanatimizwa kwa sababu ya matamshi kutoka kinywa Chake….
Kabla ya viumbe vyote kujitokeza, kwenye akili za Mungu mpango wa Mungu ulikuwa umeundwa kitambo, na ulimwengu mpya ulikuwa umetimizwa kitambo. Ingawaje kwenye siku ya tatu mimea aina yote ilijitokeza ardhini, Mungu hakuwa na sababu yoyote ya kusitisha hatua za uumbaji Wake kwa ulimwengu huu, Alinuia kuendelea kunena matamshi Yake, kuendelea kutimiza uumbaji wa kila kiumbe kipya. Angenena, angetoa amri Zake, na angeonyesha mamlaka Yake na kuendeleza nguvu Zake, na Alitayarisha kila kitu Alichokuwa amepanga ili kutayarishia viumbe vyote na mwanadamu ambaye Alinuia kuumba….
Kwenye Siku ya Nne
|
Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya Mwanadamu Iliumbika Huku Mungu Akionyesha Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena
Muumba alitumia matamshi Yake kutimiza mpango Wake, na kwa njia hii Alipitisha siku tatu zake za kwanza kwenye mpango Wake. Kwenye siku hizi tatu, Mungu hakuonekana kushughulika kila pahali, au kujichosha Yeye Mwenyewe; kinyume cha mambo ni kwamba, Alikuwa na siku tatu za kwanza nzuri katika mpango Wake na Alitimiza utekelezaji mkubwa wa mabadiliko makubwa ya ulimwengu. Ulimwengu mpya kabisa ulijitokeza mbele ya macho Yake, na, kipande kwa kipande, picha nzuri na ya kupendeza ambayo ilikuwa imefichwa ndani ya fikira Zake ilikuwa tayari imefichuliwa kwa matamshi ya Mungu. Kujitokeza kwa kila kiumbe kipya kulikuwa sawa na kuzaliwa kwa mtoto mchanga, na Muumba alifurahia sana picha hii ambayo iliwahi kuwa kwenye fikira Zake, lakini ambayo sasa ilikuwa imepewa uhai. Wakati huu, moyo Wake ulifaidi sehemu ndogo ya kutosheka, lakini mpango Wake ulikuwa ndio tu umeanza. Punde si punde, siku mpya ilikuwa imewadia—na ukurasa unaofuata ulikuwa upi kwenye mpango wa Muumba? Ni nini Alichosema? Na Aliwezaje kuonyesha mamlaka Yake? Na, wakati uo huo, ni mambo yapi mapya yaliyokuja kwenye ulimwengu huu mpya? Kufuatia mwongozo wa Muumba, kuangaza kwetu kwa macho kunatufikisha kwenye siku ya nne ya uumbaji wa Mungu wa viumbe vyote, siku ambayo ilikuwa ni mwanzo mpya. Bila shaka, kwa Muumba, bila tashwishi ilikuwa ni siku nyingine nzuri, na siku nyingine yenye umuhimu mkubwa kwa mwanadamu wa leo. Ilikuwa, bila shaka, siku yenye thamani isiyopimika. Ilikuwaje nzuri, ilikuwaje muhimu, na ilikuwaje yenye thamani isiyopimika? Hebu na tuweze kusikiliza matamshi yaliyotamkwa na Muumba….
“Naye Mungu akasema, Kuwe na mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kutenga mchana na usiku; na uwe ndio ishara; na majira, na siku na miaka: Na tena uwe ndio mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kupa nchi nuru; na ikawa vile” (Mwa 1:14-15). Haya yalikuwa maonyesho mengine ya mamlaka ya Mungu yaliyoonyeshwa kwa viumbe kufuatia uumbaji Wake wa ardhi kavu na mimea iliyokuwa ndani yake. Kwa Mungu, kitendo kama hicho kilikuwa rahisi kwa kiasi fulani, kwa sababu Mungu ana nguvu kama hizo; Mungu ni mzuri kama vile tu neno Lake lilivyo, na neno Lake litaweza kutimizwa. Mungu aliamuru nuru kujitokeza mbinguni, na nuru hizi hazikuangaza tu kwenye mbingu lakini pia kwenye ardhi, lakini pia zilihudumu kama ishara za mchana na usiku, kwa minajili ya misimu, siku, na miaka. Kwa njia hii, kama vile Mungu alivyoongea kwa matamshi Yake, kila kitendo ambacho Mungu alipenda kutimiza kilitimizwa kulingana na maana ya Mungu na kwa njia iliyoteuliwa na Mungu.
Nuru kwenye mbingu ni viumbe vilivyo kwenye mbingu vinavyoweza kuonyesha nuru; vinaweza kuangazia mbingu, na vinaweza kuangazia ardhi na bahari. Vinazunguka kulingana na mpigo na mara ngapi ambapo vimeamriwa na Mungu, na vinaangaza sehemu mbalimbali zenye vipindi tofauti vya muda kwenye ardhi, na kwa njia hii mizunguko ya kuzunguka kwa nuru hizi husababisha mchana na usiku kujitokeza upande wa mashariki na magharibi mwa ardhi, na wala si tu ishara za usiku na mchana, lakini kupitia kwa mizunguko hii tofauti inaweza kuadhimisha pia karamu na siku mbalimbali maalum za mwanadamu. Ndizo nyongeza na saidizi timilifu kwa misimu minne—mchipuko, kiangazi, mapukutiko, na kipupwe—iliyotolewa na Mungu, pamoja na vile ambavyo nuru hizi huhudumu kwa mpangilio maalum kama alama za mara kwa mara na sahihi kwa minajili ya vipimo mbalimbali, siku, na miaka ya mwanadamu. Ingawaje ilikuwa baada tu ya mwanzo wa kilimo ndipo mwanadamu alipoanza kuelewa na kukumbana na utofautishi wa vipimo vya muda, siku, na miaka iliyosababishwa na nuru hizi zilizoumbwa na Mungu, kwa hakika, vipindi vya muda, siku, na miaka ambavyo binadamu anaelewa leo vilianza kutolewa kitambo kwenye siku ya nne ya uumbaji wa viumbe vyote na Mungu, na vilevile ndivyo ilivyokuwa kwenye mizunguko inayobadilishana ya mchipuko, kiangazi, mapukutiko, na kipupwe ambavyo binadamu anapitia na vinaanza kitambo kwenye siku ya nne ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote. Nuru zile zilizoumbwa na Mungu zilimwezesha binadamu kuweza kutofautisha mara kwa mara, kwa hakika, na waziwazi usiku na mchana, na kuhesabu siku, na kuweza kufuatilia waziwazi vipindi vile vya muda na miaka. (Siku ya mwezi mzima ilikuwa kukamilika kwa mwezi mmoja, na kutokana na haya binadamu alijua kwamba kule kuangazia kwa nuru kulianzisha mzunguko mpya; siku ile ya nusu mwezi ilikuwa ni kukamilika kwa nusu moja ya mwezi, jambo ambalo lilimfahamisha binadamu kwamba kipindi kipya cha muda kilikuwa kimeanza, ambapo binadamu angeweza kujua ni mchana na usiku ngapi vilikuwa kwenye kipindi cha muda, na ni vipindi vingapi vya muda vilikuwa kwenye msimu, na ni misimu mingapi ilikuwa kwenye mwaka, na vyote hivi vilionyeshwa mara kwa mara.) Kwa hivyo, binadamu angeweza kufuatilia kwa urahisi vipindi vya muda, siku, na miaka iliyowekewa alama na mizunguko ya nuru hizo. Kuanzia sasa kusonga mbele, mwanadamu na viumbe vyote viliishi bila kufahamu miongoni mwa mabadiliko yenye mpangilio ya usiku na mchana na kubadilishwa kwa misimu iliyotokana na mizunguko ya nuru. Huu ndio ulikuwa muhimu wa uumbaji wa Muumba wa nuru kwenye siku ya nne. Vilevile, nia na umuhimu wa hatua hii ya Muumba vilikuwa bado haviwezi kutenganishwa na mamlaka na nguvu Zake. Na kwa hivyo, nuru zilizoumbwa na Mungu na thamani ambayo zingeleta hivi karibuni kwa binadamu ilikuwa ni mafanikio mengine katika uonyeshaji wa mamlaka ya Muumba.
Katika ulimwengu huu mpya, ambao mwanadamu bado alikuwa hajaonekana, Muumba alikuwa ametayarisha jioni na asubuhi, ile anga, ardhi na bahari, nyasi, miti isiyozaa na aina mbalimbali za miti, na nuru, misimu, siku, na miaka kwa minajili ya maisha mapya ambayo Angeumba hivi karibuni. Mamlaka na nguvu za Muumba vyote vilionyeshwa katika kila kiumbe kipya Alichokiumba, na maneno na kufanikiwa Kwake vyote vilifanyika sawia, bila ya hitilafu yoyote ndogo na bila ya kuchelewa kokote kudogo. Kujitokeza na kuzaliwa kwa viumbe hivi vyote vipya kulikuwa ithibati ya mamlaka na nguvu za Muumba: Yeye ni mzuri sawa tu na neno Lake, na neno Lake litakamilika, na kile kinachokamilika kinadumu milele. Hoja hii haijawahi kubadilika: ndivyo ilivyokuwa kale, ndivyo ilivyo leo, na ndivyo itakavyokuwa daima dawamu. Unapoyaangalia kwa mara nyingine maneno hayo ya maandiko, unahisi kwamba yangali mapya kwako? Je, umeyaona maudhui mapya, na kufanya ugunduzi mpya? Hii ni kwa sababu vitendo vya Muumba vimechangamsha moyo wako na kuongoza mwelekeo wa maarifa yako ya mamlaka na nguvu Zake, na yakakufungulia mlango wa ufahamu wa Muumba, na vitendo na mamlaka Yake vimeweza kupatia maneno haya uhai. Na kwa hivyo katika maneno haya binadamu ameona maonyesho halisi, na wazi ya mamlaka ya Muumba, na kuweza kushuhudia kwa kweli mamlaka makuu ya Muumba, na kutazama mamlaka yake yasiyokuwa ya kawaida na nguvu za Muumba.
Mamlaka na nguvu za Muumba hutoa muujiza baada ya muujiza na huvutia umakinifu wa binadamu, naye binadamu hawezi kukwepa haya ila kuyaangazia tu macho matendo haya ya kipekee yaliyozaliwa kutokana na utekelezwaji wa mamlaka husika. Nguvu zake za kipekee zafurahisha baada ya kufurahisha, na binadamu anabaki akishangaa na akijawa na furaha, naye anatweta kwa kuvutiwa, anastaajabishwa, na kushangilia; nini kingine tena, binadamu amefurahishwa kwa kumtazama alivyo, na kilichozaliwa ndani yake ni heshima, kustahi, na mtagusano wa karibu. Mamlaka na vitendo vya Muumba vinayo athari kwa roho ya binadamu na hutakasa roho ya binadamu na zaidi, kutosheleza roho ya binadamu. Kila mojawapo ya fikira Zake, kila mojawapo ya matamshi Yake, na kila ufunuo wa mamlaka Yake ni kiungo muhimu miongoni mwa viumbe vyote, na ni utekelezaji mkuu wenye thamani zaidi wa kuunda ufahamu na maarifa ya kina ya mwanadamu. Tunapohesabu kila kiumbe kilichozaliwa kutokana na matamshi ya Muumba, roho zetu zinavutiwa kwa maajabu ya nguvu za Mungu, na tunajipata tukifuata nyayo za Muumba hadi kwenye siku inayofuata: siku ya tano ya uumbaji wa Mungu wa viumbe vyote.
Hebu tuendelee kusoma Maandiko fungu hadi fungu, tunapoangalia vitendo vingi zaidi vya Muumba.
Kwenye Siku ya Tano
|
Kwenye Siku ya Tano, Maisha ya Maumbo Tofauti na Pana Yaonyesha Mamlaka ya Muumba kwa Njia Tofauti
Maandiko yanasema, “Na Mungu akasema, Na maji yalete kwa wingi kiumbe asongaye aliye na uhai, na ndege wanaoweza kuruka juu ya nchi katika anga wazi la mbingu. Naye Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na viumbe wote walio na uhai wasongao, ambao maji yalileta kwa wingi, kwa aina yao, na kila ndege anayeruka kwa aina yake: na Mungu akaona kuwa ilikuwa vizuri” (Mwa 1:20-21). Maandiko yanatwambia waziwazi kwamba, kwenye siku hii, Mungu aliumba viumbe vya majini na ndege wa hewani, hivi ni kusema kwamba Aliwaumba samaki na ndege mbalimbali, na akawaainisha kila mmoja wao kulingana na aina. Kwa njia hii, ardhi, mbingu, na maji vyote vilitajirishwa na uumbaji wa Mungu …
Kama vile maneno ya Mungu yalivyotamkwa, maisha mapya mazuri, kila mojawapo ikiwa na umbo tofauti, kwa ghafla vilipata uhai miongoni mwa matamshi ya Muumba. Viliingia ulimwenguni vikijitikisatikisa kwa minajili ya kupata nafasi, kuruka, kurukaruka kwa furaha…. Samaki wa maumbo na ukubwa wote waliweza kuogelea majini, samakigamba wa kila aina waliweza kukua kwenye michanga, viumbe vyenye magamba, vyenye maganda na vile visivyokuwa na uti wa mgongo viliweza kukua kwa haraka kwa maumbo tofauti, haijalishi kama vilikuwa vikubwa au vidogo, virefu au vifupi. Na ndivyo pia ilivyokuwa kwa aina tofauti za mwani kuanza kukua kwa haraka, ikiyumbayumba kutokana na msongo wa maisha mbalimbali ya majini, yasiyosita, na yanayosihi yale maji tulivu, ni kana kwamba yanataka kuyaambia: Tikisa mguu! Walete marafiki wako! Kwani hutawahi kuwa pekee tena! Kuanzia muda ule ambao viumbe mbalimbali vilivyo na uhai viliumbwa na Mungu na kuonekana majini, kila maisha mapya yalileta nguvu kwenye maji yaliyokuwa tulivu kwa muda mrefu, na kuweza kuanzisha enzi mpya…. Kuanzia hapo kwenda mbele, viumbe hivi viliishi pamoja, kimoja kando ya kingine na vikaweza kutangamana pamoja, na wala havikujiona tofauti. Yale maji yalikuwepo kwa minajili ya viumbe vilivyokuwa ndani yake, yakipatia uhai kila maisha yaliyokuwa karibu na kumbatio lake, na kila maisha yalikuwepo kwa minajili ya maji kwa sababu ya uhai wake. Kila moja ilipatia uhai mwenzake, na wakati uo huo, kila kimoja, kwa njia hiyo, kilitolea ushuhuda wa miujiza na ukubwa wa uumbaji wa Muumba, na kwa nguvu zisizoshindwa za mamlaka ya Muumba …
Kwa vile bahari haikuwa tulivu tena, ndivyo pia maisha yalivyoanza kujaza mbingu. Mmoja baada ya mwengine, ndege, wakubwa na wadogo, walipaa kwenye mbingu kutoka ardhini. Tofauti na viumbe vya baharini, walikuwa na mbawa na manyoya ambayo yalifunika maumbo yao membamba na yenye neema. Walipigapiga mbawa zao, kwa maringo na majivuno wakionyesha koti lao la kupendeza la manyoya na kazi zao maalum pamoja na mbinu walizopewa na Muumba. Walipaa kwa uhuru, na kwa mbinu walizokuwa nazo wakapaa katikati ya mbingu na ardhi, kotekote kwenye mbuga na misitu…. Walikuwa ndio wapenzi wa hewani, walikuwa ndio wapenzi wa viumbe vyote. Hivi punde ndio wangekuwa kiunganishi kati ya mbingu na ardhi, na wangepitisha ujumbe kwa viumbe vyote…. Waliimba, wakawa wanapaapaa kwa furaha kotekote, walileta vifijo, vicheko, na uchangamfu kwenye ulimwengu huu uliojaa utupu hapo mwanzoni…. Walitumia kuimba kwao kwa uwazi, kuvutia, na kutumia maneno yaliyokuwa ndani ya mioyo yao kusifu Muumba kwa maisha aliyowapa. Walicheza kwa uchangamfu ili kuonyesha utimilifu na miujiza ya uumbaji wa Muumba, na wangejitolea maisha yao yote kushuhudia agano la mamlaka ya Muumba kupitia kwenye maisha maalum ambayo Alikuwa amewapa …
Licha ya kama vilikuwa majini, au mbinguni, kwa amri ya Muumba, wingi huu wa viumbe hivi hai ulikuwepo katika mipangilio tofauti ya maisha, na kwa amri ya Muumba, vilikusanyika pamoja kulingana na aina zao mbalimbali—na sheria hii, kanuni hii, ilikuwa isiyoweza kubadilishwa na viumbe vyovyote. Havikuwahi kuthubutu kwenda nje ya mipaka viliyowekewa na Muumba, na wala visingeweza kufanya hivyo. Kama walivyoamriwa na Muumba, waliishi na kuzaana, na kutii kwa umakinifu mkondo wa maisha na sheria walizowekewa na Muumba, na kwa kufahamu wakafuata amri Zake zisizotamkwa na matamshi na maelekezi ya kimbinguni Aliyowapa, kutoka hapo hadi leo. Walizungumza na Muumba kwa njia yao wenyewe maalum, na wakashukuru maana ya Muumba, na wakatii amri Zake. Hakuna kati yao aliyewahi kukiuka mamlaka ya Muumba, na ukuu na amri Yake juu yao ilitekelezwa ndani ya fikira Zake; hakuna maneno yaliyotolewa, lakini mamlaka yaliyokuwa ya kipekee kwa Muumba yalidhibiti viumbe vyote kwa kimya ambacho hakikumiliki matumizi yoyote ya lugha, na iliyokuwa tofauti na mwanadamu. Utiliaji mkazo wa mamlaka Yake kwa njia hii maalum ulimshawishi binadamu kupata maarifa mapya, na kuufanya ufasiri mpya wa mamlaka ya kipekee ya Mungu. Hapa, lazima Niwaambie kwamba kwenye siku hii mpya, ule utiliaji mkazo wa mamlaka ya Muumba ulionyesha kwa mara nyingine ule upekee wa Muumba.
Kinachofuata, wacha tuangalie sentensi ya mwisho ya fungu hili la maandiko: “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Unafikiri hii inamaanisha nini? Hapa, tunapata kuziona hisia za Mungu. Mungu alitazama viumbe vyote Alivyokuwa ameumba vikiumbika na kusimama wima kwa sababu ya matamshi Yake, na kwa utaratibu vikianza kubadilika. Wakati huu, Mungu alikuwa ametosheka na mambo mbalimbali Aliyoyaumba kwa matamshi Yake, na vitendo mbalimbali Alivyokuwa ametimiza? Jibu ni kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Wewe unaona nini hapa? Kinawakilisha nini kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri”? Kusema hivi kunaashiria nini? Kunamaanisha kwamba Mungu alikuwa na nguvu na hekima ya kukamilisha kile Alichokuwa amepangilia na kushauri, kukamilisha shabaha Alizokuwa ameweka wazi ili kuzikamilisha. Baada ya Mungu kukamilisha kila kazi, je, Alijutia chochote? Jibu lingali kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Kwa maneno mengine, Hakujutia chochote, lakini Alitosheka. Ni nini maana ya Yeye kutojutia chochote? Tunaelezewa kwamba Mpango wa Mungu ni mtimilifu, kwamba nguvu na hekima Zake ni timilifu, na hiyo ni kutokana tu na mamlaka Yake kwamba utimilifu kama huo unaweza kukamilishwa. Wakati binadamu anapotekeleza kazi, je, anaweza, kama Mungu, kuona kwamba kazi hiyo ni nzuri? Je, kila kitu anachofanya binadamu kinaweza kukamilika na kuwa timilifu? Je, binadamu anaweza kukamilisha kitu mara moja na kikawa hivyo daima dawamu? Kama vile tu binadamu anavyosema, “hakuna kitu kilicho timilifu, kinaweza tu kuwa bora zaidi,” hakuna kitu ambacho binadamu hufanya kinaweza kufikia utimilifu. Wakati Mungu alipoona kwamba kile Alichokuwa amefanya na kutimiza kilikuwa kizuri, kila kitu kilichoumbwa na Mungu kiliwekwa kwa matamshi Yake, hivi ni kusema kwamba, wakati “Mungu akaona kwamba ni vizuri,” kila kitu Alichoumba kikachukua mfumo wa kudumu, kikaainishwa kulingana na aina, na kikapewa mahali maalum, kusudio, na kazi, kwa mara ya kwanza na kwa daima dawamu. Vilevile, wajibu wao miongoni mwa viumbe vyote na safari ambayo lazima waabiri kwenye usimamizi wa Mungu wa viumbe vyote, ulikuwa tayari umeamriwa na Mungu, na usingebadilishwa. Hii ilikuwa sheria ya kimbinguni iliyotolewa na Muumba kwa viumbe vyote.
“Mungu akaona kwamba ni vizuri,” matamshi haya mepesi, yasiyopongezwa, yanayopuuzwa mara nyingi, ndiyo matamshi ya sheria ya kimbinguni na maelekezo ya kimbinguni kwa viumbe vyote kutoka kwa Mungu. Ni mfano mwingine halisi wa mamlaka ya Muumba, mfano ambao ni wa kimatendo zaidi na unaojitokeza zaidi. Kupitia kwa matamshi Yake, Muumba hakuweza tu kufaidi kila kitu Alichoweka wazi ili kufaidi, na kutimiza kila kitu Alichoweka wazi ili kutimiza, lakini pia Aliweza kudhibiti mikononi Mwake, kila kitu Alichokuwa ameumba, na kutawala kila kitu Alichokuwa ameumba kulingana na mamlaka Yake, na, vilevile, kila kitu kilikuwa cha mfumo na cha kawaida. Viumbe vyote viliishi na kufa pia kwa matamshi Yake na, vilevile, kwa mamlaka Yake, vilikuwepo katikati ya sheria Aliyokuwa ameiweka wazi, na hakuna kiumbe kilichoachwa! Sheria hii ilianza punde tu “Mungu alipoona kuwa ni vyema,” na itakuwepo, itaendelea, na kufanya kazi kwa minajili ya mpango wa Mungu wa usimamizi mpaka siku ile itabatilishwa na Muumba! Upekee wa mamlaka ya Muumba ulionyeshwa si tu katika uwezo Wake wa kuumba viumbe vyote na kuamuru viumbe vyote kuwepo, lakini pia katika uwezo Wake wa kutawala na kushikilia ukuu juu ya viumbe vyote, na kupatia maisha na nguvu kwa viumbe vyote, na, vilevile, katika uwezo Wake kusababisha, kwa mara ya kwanza na kwa daima dawamu, viumbe vyote ambavyo Angeumba katika mpango Wake ili kuonekana na kuwepo katika ulimwengu ulioumbwa na Yeye kwa umbo timilifu, na kwa muundo wa maisha timilifu, na wajibu timilifu. Na ndivyo pia ilivyoonyeshwa kwa njia ambayo fikira za Muumba hazikutegemea vizuizi vyovyote, hazikuwekewa mipaka ya muda, nafasi, au jiografia. Kama mamlaka Yake, utambulisho wa kipekee wa Muumba utabakia vilevile milele hata milele. Mamlaka yake siku zote yatakuwa uwakilishi na ishara ya utambulisho Wake wa kipekee, na mamlaka Yake yatakuwepo milele sambamba na utambulisho Wake!
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni