A. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Maarifa Kumpotosha Mwanadamu |
Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
(Sehemu ya Tatu)
Kiini cha Shetani ni ovu, kwa hivyo matokeo ya vitendo vya Shetani bila shaka ni ovu, ama kwa kiwango cha chini kabisa, yanahusiana na uovu wake, tunaweza kusema hayo? (Ndiyo.) Kwa hivyo, je Shetani anampotosha mwanadamu vipi? Kwanza lazima tuangalie hasa—uovu uliofanywa na Shetani duniani na miongoni mwa ubinadamu ambao unaonekana, tunaoweza kuhisi; mmewahi kuyafikiria haya awali? Pengine hamkuyafikiria sana, kwa hivyo wacha Nitaje pointi kadhaa muhimu ili muweze kuona jinsi Shetani anampotosha mwanadamu.
Kuna nadharia inayoitwa mageuko; kila mtu anajua kuihusu, siyo? Mageuko na uyakinifu huu, si sehemu ya maarifa yanayosomwa na mwanadamu? (Ndiyo.) Hivyo, Shetani kwanza anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu, na kisha anatumia sayansi kuamsha mvuto wa wanadamu kwa maarifa, sayansi, na vitu vya ajabu, ama kwa vitu ambavyo watu wanataka kuchunguza; hii ni kusema, Shetani anatumia maarifa ya kisayansi kumpotosha mwanadamu. Vitu vifuatavyo vinavyotumiwa na Shetani kumpotosha mwanadamu ni desturi ya kitamaduni na ushirikina, na baada ya vitu hivyo, anatumia mienendo ya kijamii. Hivi vyote ni vitu ambavyo watu wanapatana navyo katika maisha yao ya kila siku na hivi vyote vinahusiana na vitu vilivyo karibu na watu, vitu wanavyoona, wanavyosikia, wanavyogusa na wanavyopitia. Mtu anaweza kusema kwamba vinazunguka kila mtu, haviwezi kutorokwa na kuepukika. Wanadamu hawana njia ya kuepuka kuathiriwa, kuambukizwa, kudhibitiwa, na kufungwa na vitu hivi; hawana nguvu za kuvisukuma mbali.
Mwenyezi Mungu alisema,Kwanza tutazungumza kuhusu maarifa. Si kila mtu angechukulia maarifa kuwa kitu chema? Ama kwa kiwango cha chini kabisa, watu wanafikiri kwamba kidokezo cha neno “maarifa” ni chema badala ya hasi. Kwa hivyo mbona tunataja hapa kwamba Shetani anatumia maarifa kwanza kumpotosha mwanadamu? Si nadharia ya mageuko ni kipengele cha maarifa? Si sheria za kisayansi za Newton ni sehemu ya maarifa? Si mvuto wa dunia ni sehemu ya maarifa, siyo? (Ndiyo.) Hivyo mbona maarifa yametajwa miongoni mwa maudhui anayoyatumia Shetani kumpotosha mwanadamu? Maoni yenu hapa ni yapi? Je, maarifa yana hata chembe cha ukweli ndani yake? (La.) Kwa hivyo ni nini kiini cha maarifa? (Yanaenda kinyume na ukweli.) Maarifa ambayo mwanadamu anatafiti yanafunzwa kwa msingi upi? Yanalingana na nadharia ya mageuko? Si maarifa ambayo mwanadamu amechunguza, ujumla wake, unatokana na ukanaji Mungu? (Ndiyo.) Hivyo, kuna sehemu yoyote ya maarifa haya ambayo ina uhusiano na Mungu? Je, yanahusiana na kumwabudu Mungu? Yanahusiana na ukweli? (La.) Shetani anatumiaje maarifa kumpotosha mwanadamu? Nimetoka tu kusema kwamba hakuna sehemu yoyote ya maarifa haya inahusiana na kumwabudu Mungu ama na ukweli. Watu wengine wanayafikiria hivi: “Yanaweza kutokuwa na chochote kuhusiana na ukweli, lakini hayawapotoshi watu.” Mnafikiri nini kuhusu haya? Ulifundishwa na maarifa kwamba furaha ya watu ilitegemea kile walichokiumba na mikono yao? Je, maarifa yaliwahi kukufunza kwamba hatima ya mwanadamu ilikuwa mikononi mwake? (Ndiyo.) Haya ni mazungumzo ya aina gani? (Ni upuuzi.) Sahihi! Ni upuuzi! Maarifa yanatatiza kujadili. Unaweza kuiweka kwa urahisi kwamba eneo la maarifa ni maarifa tu. Hili ni eneo la maarifa linalofunzwa kwa msingi wa ukanaji Mungu na kutokuwa na uelewa kwamba Mungu aliumba mambo yote. Watu wanaposoma aina hii ya maarifa, hawaoni Mungu anatawala mambo yote, hawaoni Mungu anaongoza ama anasimamia mambo yote. Badala yake, wanayofanya tu ni kutafiti, kuchunguza, na kutafuta majibu ya kisayansi bila kikomo kwa sehemu hiyo ya maarifa. Hata hivyo, iwapo watu hawamwamini Mungu na badala yake wanatafiti tu, kamwe hawatapata majibu ya kweli, siyo? Maarifa yanakupa tu riziki, yanakupa tu kazi, yanakupa tu mapato ili usiwe na njaa, lakini kamwe hayawezi kukusaidia kumjua Mungu, hayatakusaidia kumwamini Yeye, kumtii Yeye, na maarifa kamwe hayatakuweka mbali na maovu. Kadiri unavyosoma maarifa, ndivyo utatamani zaidi kuasi dhidi ya Mungu, kumtafiti Mungu, kumjaribu Mungu, na kwenda kinyume na Mungu. Hivyo sasa, tunaona yapi ambayo maarifa yanawafunza watu? Yote ni filosofia ya Shetani. Je, filosofia za Shetani na kanuni za kuishi zinazopatikana kwa wanadamu potovu zina uhusiano wowote na ukweli? (La.) Hazina uhusiano wowote na ukweli na, kwa kweli, ni kinyume cha ukweli. Watu mara nyingi husema, “Maisha ni mwendo”; haya ni mazungumzo ya aina gani? (Upuuzi.) Watu pia wanasema, “Mwanadamu ni chuma, mchele ni chuma, mwanadamu huhisi anataabika kwa njaa asipokula mlo”; hii ni nini? (Upuuzi, maneno ya Shetani.) Hata ni uwongo mbaya zaidi na inachukiza kuisikia. Hivyo, maarifa ni kitu ambacho pengine kila mtu anakijua. Kwa yanayoitwa maarifa ya mwanadamu, Shetani amejaza kidogo filosofia yake ya maisha na kufikiria kwake. Na wakati Shetani anafanya haya, Shetani anamruhusu mwanadamu kuomba kufikiria kwake, filosofia, na mtazamo wake ili mwanadamu aweze kukana uwepo wa Mungu, kukana utawala wa Mungu juu ya mambo yote na utawala juu ya hatima ya mwanadamu. Kwa hivyo, masomo ya mwanadamu yanapoendelea, anahisi uwepo wa Mungu kuwa usio yakini anapopata maarifa zaidi, na mwanadamu anaweza hata kuhisi kwamba Mungu hayupo kwa sababu ya mitazamo, dhana, na fikira ambazo Shetani ameongeza kwa akili ya mwanadamu. Shetani anapoweka fikira hizi ndani ya akili ya mwanadamu, si watu wanapotoshwa na mambo haya? (Ndiyo.) Ni nini msingi wa maisha ya mwanadamu sasa? Kweli anategemea maarifa haya? La; msingi wa maisha ya mwanadamu ni fikira, mitazamo na filosofia za Shetani ambazo zimefichwa kwa maarifa haya. Hapa ndipo kiini cha upotovu wa Shetani wa mwanadamu unafanyika, hili ndilo lengo la Shetani na mbinu yake ya kumpotosha mwanadamu.
A. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Maarifa Kumpotosha Mwanadamu
Kwanza tutazungumzia kipengele cha juujuu zaidi cha mada hii. Mlipokuwa mnafunzwa Kiswahili shuleni, je, lugha na maandishi yaliweza kuwapotosha watu? Hayangeweza. Maneno yanaweza kupotosha watu? (La.) Maneno hayapotoshi watu; ni chombo kinachowaruhusu watu kuongea na chombo ambacho watu wanatumia kuwasiliana na Mungu. Zaidi, lugha na maneno ni jinsi ambavyo Mungu anawasiliana na watu sasa, ni vyombo, ni vya umuhimu. Moja ongeza moja ni mbili, haya ni maarifa, siyo? Mbili zidisha kwa mbili ni nne, haya ni maarifa, siyo? Lakini yanaweza kukupotosha? Hii ni akili ya wote na kanuni kwa hivyo haiwezi kupotosha watu. Kwa hivyo ni maarifa gani yanayopotosha watu? Ni maarifa ambayo yamechanganywa mitazamo na fikira za Shetani, Shetani anataka kujaza mitazamo na fikira hizi ndani ya ubinadamu kupitia maarifa. Kwa mfano, katika insha, kuna chochote kibaya na maneno yaliyoandikwa? (La.) Hivyo, shida inaweza kuwa wapi? Mitazamo na nia ya mwandishi alipoandika insha hiyo na pia maudhui ya fikira zake—haya ni mambo ya kiroho—yanaweza kuwapotosha watu. Kwa mfano, iwapo ungekuwa ukitazama kipindi kwa runinga, ni mambo yapi ndani yake yangeweza kubadili mtazamo wako? Je, yale yaliyosemwa na wasanii, maneno yenyewe, yangeweza kuwapotosha watu? (La.) Ni mambo yapi ambayo yangeweza kuwapotosha watu? Ingekuwa fikira na maudhui ya kiini ya kipindi, ambayo yangewakilisha mitazamo ya mwelekezi, na taarifa iliyo kwa mitazamo hii ingeshawishi mioyo na akili za watu. Siyo? (Ndiyo.) Je, mnajua Narejelea nini katika mjadala Wangu wa Shetani kutumia maarifa kuwapotosha watu? (Ndiyo, tunajua.) Hutafahamu vibaya, siyo? Hivyo unaposoma riwaya ama insha tena, unaweza kutathmini iwapo fikira zilizoelezwa katika insha hiyo zinapotosha ama hazipotoshi mwanadamu ama kuchangia kwa ubinadamu? (Tunaweza kufanya hivyo kidogo.) Hiki ni kitu ambacho lazima kisomwe na kupitiwa polepole, si kitu kinachoeleweka kwa urahisi mara moja. Kwa mfano, unapotafiti ama kusoma sehemu ya maarifa, baadhi ya vipengele vyema vya maarifa hayo vinaweza kukusaidia kuelewa baadhi ya akili ya wote kuhusu eneo hilo, na kile ambacho watu wanapaswa kuepukana nacho. Chukua mfano wa “umeme,” hili ni eneo la maarifa, siyo? Ungekuwa mjinga kama hungejua kwamba umeme unaweza kuwatetemesha watu, siyo? Lakini utakapoelewa sehemu hii ya maarifa, hutakuwa na uzembe kuhusu kugusa kitu cha umeme na utajua jinsi ya kutumia umeme. Haya yote ni mambo mema. Unaelewa kile tunachojadili kuhusu jinsi maarifa yanawapotosha watu? (Ndiyo, tunaelewa.) Iwapo unaelewa hatutaendelea kukizungumzia zaidi kwa sababu kuna aina nyingi za maarifa ambazo zinasomwa duniani na lazima mchukue wakati wenu kuzitofautisha wenyewe.
B. Jinsi ambavyo Shetani Anatumia Sayansi Kupotosha Mwanadamu
Sayansi ni nini? Si sayansi imewekwa kwa hadhi ya juu na kuchukuliwa kuwa muhimu katika akili za karibu kila mtu? (Ndiyo, imewekwa kwa hadhi ya juu.) Sayansi inapotajwa, si watu wanahisi, “Hiki ni kitu ambacho watu wa kawaida hawawezi kuelewa, hii ni mada ambayo tu watafiti wa kisayansi ama wataalam wanaweza kugusia. Haina uhusiano wowote na sisi watu wa kawaida”? Je, ina uhusiano lakini? (Ndiyo.) Shetani anatumiaje sayansi kuwapotosha watu? Hatutazungumza kuhusu mambo mengine isipokuwa mambo ambayo watu mara nyingi wanapatana nayo katika maisha yao binafsi. Umesikia kuhusu “jeni,” siyo? (Ndiyo.) Nyote mnalijua neno hili, siyo? Je, jeni ziligunduliwa kupitia sayansi? Jeni zinamaanisha nini hasa kwa watu? Hazifanyi watu kuhisi kwamba mwili ni kitu cha ajabu? Wakati watu wanajulishwa kwa mada hii, si kutakuwa na watu—hasa wenye kutaka kujua—ambao watataka kujua zaidi ama kutaka maelezo zaidi? Hawa watu wanaotaka kujua wataweka nguvu zao zote kwa mada hii na wakati hawana shughuli watatafuta maelezo kwa vitabu na intaneti kujifunza maelezo zaidi kuihusu. Sayansi ni nini? Kuongea waziwazi, sayansi ni fikira na nadharia ya vitu ambavyo mwanadamu anataka kujua, vitu visivyojulikana, na ambavyo hawajaambiwa na Mungu; sayansi ni fikira na nadharia za siri ambazo mwanadamu anataka kuchunguza. Unafikiria wigo wa sayansi ni upi? Unaweza kusema kwamba unajumuisha mambo yote, lakini mwanadamu anafanya vipi kazi ya sayansi? Je, ni kupitia utafiti? Inahusiana na kutafiti maelezo na sheria za vitu hivi na kuweka mbele nadharia zisizoaminika ambazo watu wote wanafikiria, “Wanasayansi hawa ni wakubwa mno! Wanajua mengi na wana maarifa mengi kuelewa mambo haya!” Wanapendezwa sana na watu hao, siyo? Watu wanaotafiti sayansi, wana mitazamo ya aina gani? Hawataki kutafiti ulimwengu, kutafiti mambo ya ajabu ya maeneo ya maslahi yao? Matokeo ya mwisho ya haya ni nini? Baadhi ya sayansi ina watu wanaofikia mahitimisho yao kwa kubahatisha, nyingine ina watu wanaotegemea uzoefu wa binadamu kwa mahitimisho yao na hata eneo lingine la sayansi litakuwa na watu wanaofikia mahitimisho yao kutokana na uzoefu ama uchunguzi wa kihistoria na usuli. Sivyo? (Ndiyo.) Hivyo, sayansi inawafanyia nini watu? Kile sayansi inafanya ni kwamba inawaruhusu tu watu kuona vyombo katika ulimwengu wa maumbile na tu kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu; haimruhusu mwanadamu kuona sheria ambazo Mungu anatumia kutawala mambo yote. Mwanadamu anaonekana kupata majibu kutoka kwa sayansi, lakini majibu hayo yanachanganya na yanaleta tu uradhi wa muda mfupi, uradhi ambao unawekea moyo wa mwanadamu mipaka kwa ulimwengu wa maumbile. Mwanadamu anahisi kwamba tayari amepata majibu kutoka kwa sayansi kwa hivyo licha ya suala litakaloibuka, anaamini kwa dhati mitazamo yao ya kisayansi kulithibitisha ama kulikubali. Moyo wa mwanadamu unamilikiwa na sayansi na kushawishiwa nayo hadi pahali ambapo mwanadamu tena hana akili ya kumjua Mungu, kumwabudu Mungu, na kuamini kwamba mambo yote yanatoka kwa Mungu na mwanadamu anapaswa kumwangalia kupata majibu. Hii si ukweli? Unaweza kuona kwamba kadiri ambavyo mtu anaamini sayansi, anakuwa mjinga zaidi, akiamini kwamba kila kitu kina suluhisho la sayansi, kwamba utafiti unaweza kutatua chochote. Hamtafuti Mungu na haamini kwamba Yupo; hata watu wengine ambao wamemfuata Mungu kwa miaka mingi wataenda na kutafiti vimelea kwa msukumo ama kutafuta baadhi ya maelezo ili kupata majibu. Mtu kama huyo haangalii masuala kwa mtazamo wa ukweli na wakati mwingi anataka kutegemea mitazamo na maarifa ya kisayansi ama majibu ya kisayansi kutatua shida; lakini hamtegemei Mungu na hamtafuti Mungu. Je, watu kama hao wana Mungu katika mioyo yao? (La.) Hata kuna watu wengine wanaotaka kutafiti Mungu kwa njia sawa na vile wanasoma sayansi. Kwa mfano, kuna wataalam wengi wa kidini walioenda mahali safina ilisimama baada ya mafuriko makubwa. Wameiona safina, lakini katika kuonekana kwa safina hawaoni uwepo wa Mungu. Wanaamini tu hadithi na historia na haya ni matokeo ya utafiti wao wa kisayansi na utafiti wa dunia ya maumbile. Ukitafiti vitu yakinifu, viwe mikrobiolojia, falaki, ama jiografia, hutawahi kupata matokeo yanayosema kwamba Mungu yupo ama kwamba anatawala mambo yote, Sivyo? (Ndiyo.) Kwa hivyo sayansi inamfanyia nini mwanadamu? Si inamweka mbali na Mungu? Si hii inawaruhusu watu kumtafiti Mungu? Si hii inawafanya watu kuwa na shaka zaidi kuhusu uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo Shetani anataka kutumia vipi sayansi kumpotosha mwanadamu? Si Shetani anataka kutumia mahitimisho ya kisayansi kuwadanganya na kuwanyima watu hisia? Shetani anatumia majibu yenye maana nyingi kushikilia mioyo ya watu ili wasitafute ama kuamini uwepo wa Mungu, na hivyo watakuwa wenye tuhuma kwa Mungu, kumkanusha Mungu na kuwa mbali na Yeye. Hivyo, hii ndiyo sababu tunasema ni njia moja Shetani anawapotosha watu.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni