Jumatano, 21 Machi 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V | Utakatifu wa Mungu (II) (Sehemu ya Nne)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
C. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Desturi ya Kitamaduni Kumpotosha Mwanadamu

Sehemu ya Nne)

C. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Desturi ya Kitamaduni Kumpotosha Mwanadamu
Mwenyezi Mungu alisema, Je, kuna mambo mengi yanayochukuliwa kuwa sehemu ya desturi ya kitamaduni? (Ndiyo.) Hii desturi ya kitamaduni inamaanisha nini? (Inapitishwa kutoka kwa mababu.) Inapitishwa kutoka kwa mababu, hiki ni kipengele kimoja. Familia, vikundi vya makabila, na hata jamii ya binadamu imepitisha njia yao ya maisha kutoka mwanzo, ama imepitisha mila, misemo, na kanuni, ambazo zimeingizwa kwa fikira za watu. Watu wanafikiria nini kuhusu mambo haya? Watu wanayachukulia kuwa yasiyoweza kutengwa na maisha yao. Wanayachukua mambo haya na kuyachukulia kuwa kanuni na uhai wa kutii, na daima hawako tayari kuyabadilisha ama kuyaacha mambo haya kwa sababu yalipitishwa kutoka kwa mababu. Kuna vipengele vingine vya desturi ya kitamaduni, kama kile kilichopitishwa na Confucius ama Mencius, ama mambo waliyofunzwa watu na Udao ama Uconfucius ambayo yamekuwa sehemu ya kila mtu hadi ndani kwa mifupa yao. Sivyo? (Ndiyo.) Desturi ya kitamaduni hii inajumuisha nini? Inajumuisha likizo ambazo watu wanasherehekea? Kwa mfano, hapo juu kuna Tamasha la Majira ya machipuko, Tamasha la Taa, Siku ya Kufagia Kaburi, Tamasha la Mashua ya Joka, na kuna Siku ya Kimataifa ya Leba, Siku ya Watoto, Tamasha ya Katikati ya Majira ya Kupukutika kwa Majani, na Siku ya Kitaifa. Baadhi za familia hata husherehekea likizo zingine, ama husherehekea wakati wazee wanahitimu umri fulani, ama wakati watoto wanahitimu umri wa mwezi 1 na wakati wako na umri wa siku 100. Hizi zote ni likizo za desturi. Je, si usuli wa likizo hizi unajumuisha desturi ya kitamaduni? Ni nini kiini cha desturi ya kitamaduni? Kina chochote kuhusu kumwabudu Mungu? Kina chochote kuhusu kuwaambia watu kuweka katika vitendo ukweli? (La.) Kuna likizo zozote za watu kutoa sadaka kwa Mungu, kwenda kwa madhabahu ya Mungu na kupokea neno Lake? Kuna likizo kama hizi? (La.) Watu hufanya nini katika likizo hizi zote? (Kumwabudu Shetani. Kula, kunywa na shughuli za burudani.) Katika nyakati za sasa zinaonekana kuwa hafla za kula, kunywa, na kujiburudisha. Basi ni nini chanzo cha desturi ya kitamaduni? Desturi ya kitamaduni imetoka kwa nani? (Shetani.) Imetoka kwa Shetani. Katika usuli wa hizi likizo za desturi, Shetani anaingiza mambo ndani ya mwanadamu, haya ni mambo gani? Kuhakikisha kwamba watu wanakumbuka mababu zao, hili ni mojawapo ya mambo haya? Kwa mfano, wakati wa Tamasha la Kufagia Kaburi watu husafisha makaburi na kutoa sadaka kwa mababu zao. Hivyo watu hawatasahau mababu zao, siyo? Pia, Shetani anahakikisha kwamba watu wanakumbuka kuwa wazalendo, kama katika Tamasha la Mashua ya Joka. Je, Tamasha la Katikati ya Majira ya Kupukutika kwa Majani? (Kupatana kwa familia.) Ni nini usuli wa kupatana kwa familia? Sababu zake ni nini? (Kuweka familia kwanza, na hisia.) Kuwasiliana na kuunganika kihisia, siyo? Bila shaka, iwapo ni kusherehekea Mkesha wa Mwaka Mpya wa Mwezi ama Tamasha la Taa, kuna njia nyingi za kuelezea sababu za usuli. Haijalishi mtu anaelezea sababu iliyo nyuma yazo, kila moja ni njia ya Shetani ya kuingiza filosofia yake na kufikiria kwake kwa watu, ili waweze kupotea kutoka kwa Mungu na wasijue kwamba kuna Mungu, na kwamba watoe sadaka ama kwa mababu zao au Shetani, ama kwamba ni udhuru wa kula, kunywa na kujifurahisha kwa ajili ya matamanio ya mwili. Kila ya likizo hizi inaposherehekewa, fikira na mitazamo ya Shetani yanapandwa kwa kina ndani ya akili za watu na hata hawajui. Wakati watu wanafika umri wa kati ama zaidi, mambo haya, fikira na mitazamo hii ya Shetani tayari yamekita mizizi ndani sana ya mioyo yao. Zaidi, watu wanafanya juhudi zao kabisa kueneza fikira hizi, ziwe sahihi ama si sahihi, kwa kizazi kifuatacho bila wasiwasi. Sivyo? (Ndiyo.) Hivyo desturi hii ya kitamaduni na likizo hizi zinapotosha vipi watu? (Watu wanawekewa mipaka na kufungwa na kanuni za hizi desturi kana kwamba hawana muda ama nguvu kumtafuta Mungu.) Hiki ni kipengele kimoja. Kwa mfano, kila mtu anasherehekea wakati wa Mwaka Mpya wa Mwezi, usingesherehekea, hungehisi huzuni? Hungehisi, “Haiya, sikusherehekea Mwaka Mpya. Siku hii ya Mwaka Mpya wa Mwezi ilikuwa mbaya sana, na haijasherehekewa; mwaka huu wote utakuwa mbaya”? Si ungehisi kutokuwa na utulivu? (Ndiyo.) Na pengine kuogopa kiasi, siyo? Kuna hata watu wengine ambao hawajatoa sadaka kwa mababu zao kwa miaka mingi na ghafla wamekuwa na ndoto ambapo mtu aliyekufa anawaomba pesa, watahisi nini ndani yao? “Inahuzunisha kwamba huyu mtu aliyekufa anahitaji pesa ya kutumia! Nitawachomea baadhi ya pesa ya karatasi, nisipo hiyo hakika haitakuwa sawa. Sisi tunaoishi tunaweza kupatana na shida kidogo nisipochoma baadhi ya pesa ya karatasi, ni nani anayeweza kusema wakati janga litatokea?” Daima watakuwa na wingu hili ndogo la hofu na wasiwasi katika mioyo yao. Hivyo ni nani anayewapa wasiwasi? (Shetani.) Shetani huleta wasiwasi. Si hii ndiyo njia moja ambayo Shetani anampotosha mwanadamu? Anatumia mbinu na udhuru mbalimbali ili kukudhibiti, kukutishia, kukufunga, hadi kiasi kwamba unachanganyikiwa na kumkubali na kumnyenyekea; hivi ndivyo Shetani anampotosha mwanadamu. Nyakati nyingi ambapo watu ni wanyonge ama hawaelewi vyema hali ilivyo, wanaweza bila kutaka, kufanya kitu kwa njia iliyochanganyikiwa, yaani, wanaanguka chini ya mshiko wa Shetani bila kusudi na wanaweza kufanya kitu bila kusudi na wasijue wanafanya nini. Hii ni njia ambayo Shetani anampotosha mwanadamu. Hata kuna watu wachache sasa ambao wanasita kuachana na desturi za kitamaduni ambazo zimekita mizizi na hawawezi tu kuziacha. Ni hasa wakati ni wanyonge na wasipoonyesha hisia ndipo wanataka kusherehekea likizo za aina hizi na wanataka kukutana na Shetani na kumridhisha Shetani tena, ambako kupitia huko wanaweza pia kujifariji ndani yao. Si mambo yanaenda hivi? (Ndiyo.) Ni nini usuli wa hizi desturi za kitamaduni? Mkono mweusi wa Shetani unavuta nyuzi nyuma ya pazia? Asili ovu ya Shetani inatawala na kudhibiti vitu? Shetani anadhibiti hivi vitu vyote? (Ndiyo.) Wakati watu wanaishi katika desturi ya kitamaduni na kusherehekea likizo za desturi za aina hizi, tunaweza kusema kwamba haya ni mazingira ambapo wanadanganywa na Shetani na kupotoshwa na Shetani? Si wana furaha kupotoshwa na Shetani? Si hivi ndivyo jinsi ilivyo? (Ndiyo.) Hiki ni kitu ambacho sisi wote tunakiri, siyo? Na kitu ambacho sote tunakijua.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
D. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Ushirikina Kumpotosha Mwanadamu
D. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Ushirikina Kumpotosha Mwanadamu
Mnalijua neno “ushirikina,” siyo? Katika ushirikina, watu mara nyingi wanakutana na nini? (Miungu ya uongo) Kuna usawa unaopatana na desturi ya kitamaduni hapa, lakini hatutazungumza kuhusu huo leo, badala yake Nitajadili unaokabiliwa mara nyingi: uganga, uaguzi, kuchoma ubani, na kuabudu Buddha. Watu wengine wanafanya uganga, wengine wanaabudu Buddha na kuchoma ubani, ilhali wengine wanabashiriwa ama wanaambiwa bahati zao kwa kumruhusu mtu kusoma vipengele vya uso yao. Wangapi kati yenu wameambiwa bahati zao ama wamesomwa uso? Hiki ni kitu ambacho watu wengi wanataka, siyo? (Ndiyo.) Mbona hivyo? Watu wanapata faida ya aina gani kutoka kwa uaguzi na uganga? Wanapata uradhi wa aina gani kutoka kwa hayo? (Udadisi.) Ni udadisi tu? Haiwezi kuwa udadisi. Ni nini lengo la ubashiri? Mbona ufanyiwe? Si kwa ajili ya kuona siku za baadaye? Watu wengine wanasomwa nyuso zao ili kutabiri siku za baadaye, wengine wanafanya hivyo ili kuona iwapo watakuwa na bahati nzuri au la. Wengine wanafanya hivyo ili kuona vipi ndoa zao zitakuwa, na bado wengine wanafanya hivyo kuona bahati itakayoletwa na mwaka ulio mbele. Watu wengine wanasomwa nyuso zao kuona matarajio ya wana na binti zao yatakuwa vipi na kuona vipengele vyote vya vitu hivi, na wanabiashara wengine wanafanya hivyo kuona watatengeneza pesa ngapi ili waweze kupata mwongozo kwa kile wanachopaswa kufanya. Watu wengine wanataka tu kujua bahati yao itakuwaje na siku za baadaye zitaleta nini. Je, ni kuridhisha udadisi tu? (La.) Wakati watu wanasomwa nyuso zao ama kufanya vitu vya aina hii, ni kwa faida ya siku zao za baadaye binafsi na wanaamini kwamba haya yote yanahusiana kwa karibu na hatima zao. Je, kuna yoyote katika mambo haya yaliyo ya manufaa? (La.) Mbona si ya manufaa? Si kitu kizuri kujua kidogo kuhusu siku za badaye? Hii inakusaidia kujua wakati shida inaweza kutokea, ili uweze kuiepuka kama ulikuwa unajua kuihusu awali, siyo? Kupigiwa ramli kunaweza kukuruhusu kuongozwa kuhusiana nako, ili mwaka ulio mbele uweze kuwa mzuri na unaweza kuwa tajiri ukifanya biashara. Si hii ni ya manufaa? (La.) Iwapo ina manufaa haituhusu, hatutaishiriki leo; mjadala wetu hauhusishi maudhui na mada hii. Shetani anatumiaje ushirikina kumpotosha mwanadamu? Kile ambacho watu wanajua kuhusu vitu kama ubashiri, kusoma uso, na uaguzi ni ili waweza kujua bahati zao zitakuwa vipi katika siku za baadaye na vile njia iliyo mbele inakaa, lakini mwishowe, ni mikono ya nani inadhibiti vitu hivi? (Mikono ya Mungu.) Viko katika mikono ya Mungu. Kuhusiana na Shetani, kwa kutumia mbinu hizi, anataka watu wajue nini? Shetani anataka kutumia kusoma uso na uaguzi ili kuwaambia watu kwamba anajua bahati zao mbeleni, na Shetani anataka kuwaambia watu kwamba anajua vitu hivi na anavidhibiti. Shetani anataka kutumia fursa hii na kutumia mbinu hizi kudhibiti watu, ili kwamba watu wanamwekea imani isiyoweza kutambua na kutii kila neno lake. Kwa mfano, ukisomwa uso, mwaguzi akifunga macho yake na kukwambia kila kitu ambacho kimekufanyikia katika miongo michache iliyopita kwa uwazi kamili, ungehisi vipi ndani yako? Ghafla ungehisi, “Nimependezwa sana na huyu mwaguzi, yuko sahihi sana! Sijawahi mwambia yeyote maisha yangu ya nyuma, alijuaje kuyahusu?” Haitakuwa vigumu sana kwa Shetani kujua maisha yako ya nyuma, siyo? Mungu amekuongoza hadi leo, na Shetani pia amewapotosha watu wakati huo wote na amekufuata. Shetani ni roho ovu; kupita kwa miongo kwako si chochote kwa Shetani na si vigumu kwake kujua vitu hivi. Wakati unajua kwamba alichosema Shetani ni sahihi, si unampa moyo wako? Siku zako za baadaye na bahati yako, si unategemea udhibiti wake? Papo hapo, moyo wako utahisi heshima ama ustahi kwake, na kwa watu wengine, nafsi zao pengine tayari zimenyakuliwa naye. Na utamwuliza mwaguzi mara moja: “Napaswa kufanya nini baada ya hapa? Napaswa kuepukana na nini mwaka ujao? Ni vitu gani ambavyo sipaswi kufanya? Na kisha atasema: “Hupaswi kwenda pale, hupaswi kufanya hili, usivae nguo za rangi fulani, hupaswi kwenda pahali kama hapo na hapo mara nyingi, na unapaswa kufanya mambo fulani zaidi…” Si utatia vyote anavyosema moyoni mara moja? (Ndiyo.) Ungevikariri haraka kuliko neno la Mungu. Mbona ungevikariri haraka hivyo? (Vina faida kwangu.) Kwa sababu ungetaka kumtegemea Shetani kwa sababu ya bahati njema, si hapa ndipo anaunyakua moyo wako? Unapofanya kile anachosema na maneno yake sasa yanakuwa ukweli kama alivyotabiri, hungetaka kurudi nyuma kwake na kujua ni bahati gani mwaka unaokuja utaleta? (Ndiyo.) Utafanya chochote Shetani anakwambia ufanye na utaepukana na vitu anakwambia uepukane navyo, si unatii vyote anasema? Utaletwa chini ya bawa lake haraka sana, kupotoshwa, na kuwekwa chini ya udhibiti wake. Hii inafanyika kwa sababu unaamini anachosema ni ukweli na kwa sababu unaamini kwamba anajua kuhusu maisha yako ya nyuma, maisha yako ya sasa, na vitu ambavyo siku za badaye zitaleta; hii ni mbinu Shetani anatumia kudhibiti watu. Lakini kwa kweli, ni nani aliye katika udhibiti? Ni Mungu Mwenyewe, si Shetani. Shetani anatumia tu hila zake hapa kudanganya watu wajinga, kuwadanganya watu wanaoona tu ulimwengu wa maumbile kumwamini na kumtegemea. Kisha, wataanguka katika mshiko wa Shetani na kutii kila neno lake. Lakini Shetani wakati wowote hupunguza jitihada watu wanapotaka kumwamini na kumfuata Mungu? Shetani hapunguzi jitihada. Katika hali hii, watu kweli wanaanguka katika mshiko wa Shetani? (Ndiyo.) Tunaweza kusema kwamba tabia ya Shetani hapa haina haya hata kidogo? (Ndiyo.) Mbona tungesema hivyo? (Shetani anatumia hila.) Hmm, kwa sababu hila za Shetani ni za ulaghai na zinadanganya. Shetani hana haya na anawadanganya watu kufikiria kwamba anadhibiti kila kitu chao na kuwadanganya watu kufikiria kwamba anadhibiti hatima zao. Hii inawafanya watu wajinga kuja kumtii kabisa na anawadanganya na sentensi moja ama mbili tu na katika kuchanganyika kwao, watu wanasujudu mbele yake. Si hii ni sahihi? (Ndiyo.) Hivyo, Shetani anatumia mbinu za aina gani, anasema nini kukufanya umwamini? Kwa mfano, pengine hujamwambia Shetani idadi ya watu katika familia yako, lakini anaweza kusema kwamba kuna watatu katika familia yako, akiwemo binti ambaye ana miaka 7, na pia umri wa wazazi wako. Iwapo ulikuwa na tuhuma na shaka zako mwanzoni, hutahisi kwamba anaaminika zaidi kidogo baada ya kusikia hayo? (Ndiyo.) Na kisha Shetani anaweza kusema, “Kazi imekuwa ngumu kwako leo, wakubwa wako hawakupi utambuzi unaostahili na daima wanafanya kazi dhidi yako.” Baada ya kuyasikia hayo, ungefikiri, “Hiyo ni sahihi kabisa! Mambo hayajakuwa yakienda vizuri kazini.” Hivyo ungemwamini Shetani zaidi kidogo. Kisha angesema kitu kingine kukudanganya, kukufanya umwamini hata zaidi, na kidogo kidogo, utajipata huwezi kupinga ama kuwa na tuhuma kwake tena. Shetani anatumia tu hila chache zisizo na maana, hata ndogo zisizojalisha, kukufadhaisha. Unapofadhaishwa, hutaweza kupata njia zako, hutajua kile cha kufanya, na utaanza kufuata kile Shetani anasema. Hii ni mbinu ya “ah nzuri sana” anayotumia Shetani kumpotosha mwanadamu pahali unapoingia katika mtego wake bila kusudi na unashawishiwa naye. Unaona, Shetani anakwambia mambo machache ambayo watu wanafikiria kuwa mambo mazuri, na kisha anakwambia kile cha kufanya na kile cha kuepuka na hivyo ndivyo unaanza kufuata njia hiyo bila kusudi. Punde unapoanza kufuata njia hiyo, haitakuwa chochote ila shida kwako; daima utakuwa ukifikiria kile alichosema Shetani na kile alichokwambia ufanye, na bila kujua utamilikiwa naye. Mbona hivi? Ni kwa sababu wanadamu hawana ukweli na hivyo hawawezi kusimama dhidi ya majaribu na ushawishi wa Shetani. Wanapokabiliwa na uovu, ujanja, usaliti, na kijicho cha Shetani, wanadamu ni wajinga sana, wasiojua na wanyonge, siyo? Si hii ni mojawapo ya njia ambayo Shetani anampotosha mwanadamu? (Ndiyo.) Mwanadamu anadanganywa na kulaghaiwa bila kusudi, kidogo kidogo, kupitia mbinu mbalimbali za Shetani, kwa sababu hawana uwezo wa kutofautisha kati ya mema na hasi. Hawana kimo hiki, na uwezo wa kumshinda Shetani.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni