Nyendo | Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu | Mungu Kuja Duniani na Kuwa Sadaka ya Dhambi
Kuja kwa Bwana Yesu hakumalizi tu enzi nzee iliyofungwa na sheria, na kuwaleta wanadamu kwa enzi mpya, lakini pia kunaboresha uhusiano kati ya mwanadamu na Mungu, na kunaashiria mwanzo mpya, hatua mpya ya kuanzia, kwa kazi ya Mungu ya usimamizi miongoni mwa wanadamu.
Mwenyezi Mungu alisema, "Yesu Anawakilisha kazi yote ya Enzi ya Neema; Alikuwa mwili na kusulubiwa, na Akazindua Enzi ya Neema. Alisulubiwa ili kukamilisha kazi ya ukombozi, ili kumaliza Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema, na hivyo Yeye Aliitwa "Kamanda Mkuu", "Sadaka ya Dhambi," "Mkombozi." Kwa hiyo kazi ya Yesu ilitofautiana katika maudhui kutokana na kazi ya Yehova, ingawa zilikuwa sawa katika kanuni. Yehova Alianzisha Enzi ya Sheria, Akajenga msingi imara wa nyumbani, mahali pa kuzaliwa pa kazi Yake hapa duniani, na Alitoa amri; haya yalikuwa mafanikio Yake mawili, yanayowakilisha Enzi ya Sheria. Kazi ya Yesu haikuwa kutoa amri, bali kutimiza amri, na hivyo kutangaza Enzi ya Neema na kuhitimisha Enzi ya Sheria ambayo ilidumu kwa miaka elfu mbili. Alikuwa mwanzilishi, kuikaribisha Enzi ya Neema, ilhali ukombozi ulibakia msingi wa kazi Yake. Na hivyo mafanikio Yake Yalikuwa pia mara mbili: kufungua enzi mpya, na kukamilisha kazi ya ukombozi kupitia kusulubiwa Kwake. Kisha Akaondoka. Katika hatua hiyo, Enzi ya Sheria ilifikia mwisho wake na mwanadamu aliingia katika Enzi ya Neema."
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni