Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima
Tamko la Kumi na Tisa
Mwenyezi Mungu alisema, Ni shughuli sahihi ya mwanadamu kuchukua maneno Yangu kama msingi wa maisha yake. Mwanadamu lazima aanzishe fungu lake binafsi katika kila sehemu ya maneno Yangu; kutofanya hivyo kutakuwa kuuliza matata, kutafuta maangamizo yake mwenyewe. Binadamu haunijui, na kwa sababu ya hili, badala ya kuleta maisha yake Kwangu badala, anachofanya ni kujipanga tu mbele Yangu na takataka mikononi mwake, na hivyo kujaribu kuniridhisha.
Lakini, mbali na kuridhishwa na mambo yalivyo, Naendelea kutoa matakwa kwa binadamu. Napenda sifa za mwanadamu, lakini Nachukia wizi wake. Wanadamu wote wana mioyo iliyojaa ulafi; ni kama moyo wa binadamu unadhibitiwa na Shetani, na mwanadamu hawezi kuponyoka na kutoa moyo wake Kwangu. Ninapozungumza, mwanadamu husikiza sauti Yangu kwa makini; lakini Ninapokoma kuzungumza, anaanza tena “biashara” yake na kusitisha kabisa kuyajali maneno Yangu, ni kama maneno Yangu ni duni kwa biashara yake. Sijawahi kuwa mzembe kwa binadamu, na bado Nimekuwa pia mvumilivu na mkarimu kwa binadamu. Na hivyo, kwa sababu ya huruma Yangu, binadamu wote wamekuwa wenye kiburi, wasio na maarifa na tafakari ya binafsi, na wanatumia vibaya uvumilivu Wangu ili kunidanganya. Hakuna mmoja kati yao anayenijali kwa dhati, na hakuna mmoja kweli ananithamini kama kitu apendacho moyoni mwake; ni wakati tu walipo na wakati wa ziada ndipo wanaponitambua kwa kiwango duni. Juhudi ambazo Nimetumia kwa mwanadamu tayari ni zaidi ya kipimo. Ninamfanyia mwanadamu aina ya pekee ya kazi, na mbali na haya, Nimempaa mzigo wa ziada, ili, ndani ya kile Ninacho na kile Nilicho, mwanadamu anaweza kupata maarifa na kupitia mabadiliko. Simtaki mwanadamu awe “mtumiaji” tu, lakini Namtaka awe “mzalishaji” anayeweza kumshinda Shetani. Ingawa Sidai chochote kutoka kwa mwanadamu, hata hivyo Nina viwango vya matakwa Ninayoyatoa, kwani kuna madhumuni kwa yale Ninayoyafanya, na pia Ninatenda kulingana na kanuni: Sichezi kiholela, anavyodhani mwanadamu, wala Siundi mbingu na dunia na mambo mengi ya uumbaji kwa ghafla na bila mpango. Kwa kazi Zangu, mwanadamu anapaswa kuwa na uwezo wa kuona kitu, kupata kitu. Hapaswi kutumia vibaya uchangamfu wa ujana wake, ama kutunza maisha yake kama vazi ambalo linakusanya vumbi; badala yake, anapaswa kujilinda vikali, kuchukua kutoka kwa fadhila Yangu kwa ajili ya starehe yake mwenyewe, hadi, kwa sababu Yangu, hawezi kumrudia Shetani, na kwa sababu Yangu anamshambulia Shetani. Si Ninachomwulizia mwanadamu ni rahisi hivi?
Mwangaza hafifu unapoanza kuonekana Mashariki, watu wote ulimwenguni kwa sababu hii wanaupa kipaumbele mwangaza ulio Mashariki. Bila kujawa na usingizi, wanadamu huenda kuchunguza chanzo cha mwangaza wa mashariki, lakini kwa sababu ya vikwazo vya uwezo wa binadamu, hakuna anayeweza kuona mahali unapotokea mwangaza. Wakati yote yaliyo ulimwenguni yameangaziwa kabisa, mwanadamu atazinduka kutoka usingizi na ndoto, na hapo tu ndipo atakapotambua kwamba siku Yangu inawadia polepole duniani. Binadamu wote wanasherehekea kwa sababu ya ujio wa mwangaza, na kwa sababu ya haya hawalali tena, na si wapumbavu tena. Chini ya mng’aro wa mwangaza Wangu, binadamu wote wanakuwa na uwazi wa akili na mtazamo, na ghafla wanakuwa na furaha ya maisha. Chini ya kifuniko cha ukungu, Nawalinda wanadamu. Wanyama wote wako katika mapumziko; kwa sababu ya ujio wa mwangaza hafifu, kila kitu katika uumbaji kinafahamu kwamba maisha mapya yanakaribia. Kwa sababu hii, wanyama pia wanatoka nje ya mapango yao, kutafuta chakula. Mimea, bila shaka, si tofauti, na kwa mng’aro wa mwangaza majani yao ya kijani yanang’aa, yakisubiri kutakasa sehemu yao binafsi Kwangu wakati Niko duniani. Wanadamu wote wanataka ujio wa mwangaza, lakini bado wanahofia ujio wake, na wasiwasi kwamba ubaya wao hutafichika tena, kwani mwanadamu yu uchi kabisa, na hajafunikwa. Watu wangapi wanahofia, kwa sababu ya ujio wa mwangaza, na kwa sababu mwangaza umetokea, wako katika hali ya mshtuko? Watu wangapi, baada ya kuuona mwangaza, wamejawa majuto yasiyo na mipaka, wakichukia uchafu wao, lakini, bila uwezo wa kubadilisha ukweli uliotimia, wanaweza tu kunisubiri kutamka hukumu. Watu wangapi, wakisafishwa na mateso gizani, wanapoona mwangaza wanapigwa ghafla na umuhimu wake mkubwa, na hatimaye kukumbatia mwangaza karibu na vifua vyao, wakiogopa kuupoteza tena? Watu wangapi, badala ya kutupwa nje ya uzingo na kutoka kwa ghafla kwa mwanga, wanaendelea tu na kazi ya kila siku, kwa sababu wamekuwa vipofu kwa miaka mingi, na hivyo hawana habari kwamba mwangaza umekuja, wala hawaridhishwi nao. Katika mioyo ya wanadamu, Mimi siko juu, wala chini. Wanadamu hawajali iwapo Nipo au la, kama kwamba maisha ya mwanadamu hayawezi kuwa na upweke zaidi iwapo Sipo, na iwapo Nipo, hayatafaidika na furaha. Kwa sababu wanadamu hawanithamini, raha Ninayowapa ni chache. Lakini punde tu binadamu unaponiabudu kidogo, basi pia Nitafanya mabadiliko kwa mtazamo Wangu kwa binadamu. Kwa sababu hii, wakati tu binadamu unapofahamu sheria hii, ndipo tu wanadamu watakapokuwa na bahati ya kujitolea Kwangu na kudai vitu vilivyo mikononi Mwangu. Hakika pendo la mwanadamu Kwangu halifungwi tu na maslahi yake mwenyewe? Hakika imani yake Kwangu haifungwi tu kwa mambo Ninayompa? Inaweza kuwa kwamba, isipokuwa tu yeye kuona mwangaza Wangu, mwanadamu hawezi kunipenda kwa dhati kwa njia ya imani yake? Hakika nguvu za mwanadamu na afya hazizuiliwi na hali ya leo? Inaweza kuwa kwamba mwanadamu anahitaji ujasiri ili anipende?
Kutegemea kuwepo Kwangu, mambo mengi ya uumbaji yanakubali kwa utiifu mahali yanamoishi, na katu, bila ya nidhamu Yangu, hayajihusishi na uasherati bila kujali. Kwa hivyo, milima inakuwa mipaka kati ya mataifa ulimwenguni, maji yanakuwa vikwazo vya kuwatenga watu kati ya nchi, na hewa inapuliza kutoka kwa mwanadamu mmoja hadi mwingine katika uwanda wa dunia. Binadamu tu huwezi kweli kutii matakwa ya mapenzi Yangu; hii ndiyo maana Nasema kwamba, kwa viumbe vyote, mwanadamu pekee ni ndiye wa kundi la wasiotii. Mwanadamu hajawahi kweli kunitii, na kwa sababu hii wakati wote Nimemweka chini ya nidhamu kali. Iwapo katikati ya binadamu, itakuja kuwa kwamba utukufu Wangu umetandaa ulimwengu nzima, basi hakika Nitachukua utukufu Wangu wote na kuufanya uwe wazi mbele ya mwanadamu. Kwa sababu katika uchafu wake mwanadamu hafai kutazama utukufu Wangu, kwa maelfu ya miaka Sijawahi kujitokeza hadharani, lakini Nimebakia mafichoni; kwa sababu hii utukufu Wangu hujawahi kuwa wazi mbele ya mwanadamu, na mwanadamu daima amezama kwa shimo la kina la dhambi. Nimeusamehe udhalimu wa binadamu, lakini wanadamu hawajui jinsi ya kujihifadhi, na badala yake daima wanajiweka wazi kwa dhambi, kuruhusu dhambi kuwajeruhi. Huu si ukosefu wa mwanadamu wa kujiheshimu na kujipenda? Katikati ya binadamu, kuna kweli yeyote anayeweza kupenda? Ibada ya mwanadamu inaweza kuwa na uzito wa wakia ngapi? Hakuna bidhaa safi zilizochanganywa na kinachoitwa uhalisi wake? Si ibada yake imeungana kabisa na mkanganyiko? Ninachohitaji ni upendo wa mwanadamu usiogawanyika. Mwanadamu hanijui, na ingawa anaweza kupata kunijua, hatanipa moyo wake wa ukweli na dhati. Kwa mwanadamu, Sidai kile asichotaka kupeana. Akinipa ibada yake, Nitaikubali bila pingamizi; lakini asiponiamini, na kukataa kujitoa hata kidogo Kwangu, badala ya kukasirika juu ya hayo, Nitamwondoa tu kwa njia ingine na kumtuma kwa nyumba inayomfaa. Radi, inayovingirika angani, inamwangusha chini mwanadamu, milima ya juu, inapoanguka, inamzika; wanyama pori kwa njaa yao wanamla kwa ulafi; na bahari, zinapobingirika, zinazingira kichwa chake. Binadamu wanapojishughulisha na migogoro ya mauaji ya jamii, wanadamu wote watatafuta maangamizo yao katika majanga yatokayo katikati ya binadamu.
Ufalme unapanuka miongoni mwa binadamu, unachipua miongoni mwa binadamu, unasimama miongoni mwa binadamu; hakuna nguvu inayoweza kuharibu ufalme Wangu. Kwa watu Wangu walio katika ufalme wa leo, nani kati yenu si mwanadamu miongoni mwa wanadamu? Nani kati yenu yu nje ya hali ya ubinadamu? Wakati hatua Yangu ya kwanza mpya itatangazwa kwa wengi; binadamu utaguswa vipi? Mmeona na macho yenu hali ya mwanadamu; hakika bado hamna matumaini ya kudumu milele kwa dunia hii? Sasa Natembea ng’ambo katikati ya watu Wangu, Naishi katikati ya watu Wangu. Leo, walio na pendo la kweli Kwangu, watu kama hawa wamebarikiwa; wamebarikiwa wanaonitii, hakika watabaki katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonijua, hakika watakuwa na mamlaka katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonitafuta, hakika watatoroka vifungo vya Shetani na kufurahia baraka ndani Yangu; wamebarikiwa wanaoweza kujiacha, hakika wataingia katika milki Yangu, na kurithi fadhila ya ufalme Wangu. Wanaokimbia kimbia kwa ajili Yangu Nitawaadhimisha, wanaopata gharama kwa ajili Yangu Nitawakumbatia kwa furaha, wanaonitolea sadaka Nitawapa starehe. Wanaopata raha ndani ya maneno Yangu, Nitawabariki; hakika watakuwa nguzo zinazoshikilia mwamba kwa ufalme Wangu, hakika watakuwa na fadhila isiyo na kifani kwa nyumba Yangu, na hakuna anayeweza kulinganishwa nao. Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kutatufa ahadi mlizopewa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza, katikati ya giza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtakuwa shujaa na imara katika nchi ya Sinimu. Kupitia mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaangaza ndani ya ulimwengu wote kwa utukufu Wangu.
Machi 19, 1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni