Mungu Aliilinda Familia Yetu Wakati wa Maafa
Wang Lan, Beijing
Agosti 6, Mwaka wa 2012
Mnamo Julai 21, mwaka wa 2012, mafuriko makubwa zaidi tangu miaka sitini yalipitia kijijini mwetu kwa nguvu mno. Maafa yalianguka kutoka mbinguni, maji ya mafuriko yalichanganya matope na mawe na kuharibu kijiji chote. Nyumba nyingi ziliharibiwa na maji na maporomoko ya matope.
Baada ya saa kumi na moja alasiri hiyo, mvua ilikuwa ikinyesha kwa nguvu sana. Kulikuwa na maji ya mafuriko na mawe makubwa yaliyoanguka kutoka juu ya nyumba yetu, na maji ya mafuriko yalikuwa makubwa mbele na nyuma ya nyumba yetu. Yalisomba uga wa kuku wa binti yangu na elfu nyingi za kuku, yalisomba mabanda ya nguruwe, na nguruwe pia. Maji yalikuwa karibu kuvamia nyumba yetu. Tulikuwa na mzee wa umri wa miaka 94 na mtoto mchanga mwenye umri wa miezi kumi. Tulikuwa na wasiwasi. Nilipokuwa nikiwabeba yule mzee wa umri wa miaka 94 na yule mtoto mchanga hadi kwa jengo la juu, maji yalikuwa yakianza kuingia katika jengo la chini. Mvua iliendelea kunyesha. Maji yalipanda kuelekea jengo la juu wakati tukiangalia. Nilikuwa na mahangaiko. Nikamwita kwa haraka kada wa kijiji, akasema nilipaswa kukimbilia mlimani, na kwamba pia walikuwa na wakati mgumu kabisa kujitoa nje, ilikuwa kila mtu kujitetea. Katika hofu yangu kubwa, nilifikiria maneno ya Mungu, “Maafa haya yatatekelezwa Nami na ni wazi kwamba Mimi ndiye Niliyeyapanga” (“Unapaswa Kufanya Matendo Mema ya Kutosha Ili Uandae Mwisho Wako wa Safari” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kuamini Mungu kunamaanisha kumtegemea Mungu, huwezi kuwategemea watu, kwa hiyo nilisimama mlangoni nikilia na kumwomba Mungu kwa sauti kubwa: "Ewe Mungu, tuokoe! Ewe Mungu, tuokoe!" Familia yote tulipiga magoti na kuomba: "Ewe Mungu, ikiwa tutakufa katika maafa haya ni kwa haki Yako, kwa sababu tu waasi sana. Tukiokoka maafa haya ni kwa neema Yako. Tutaanza tena, na tutakuwa waangalifu kwa mapenzi Yako, kufanya wajibu wetu na kueneza injili." Kulikuwa na giza na hatukuthubutu kwenda nje. Familia nzima iliketi pamoja kushirikiana na kila mmoja mshiko wa Mungu juu ya jaala ya binadamu wote, jinsi kama Mungu akimfanya mtu afe, hakuna mahali ambapo mtu anaweza kwenda kujificha, hataweza kutoroka kutoka kwa mikono ya Mungu, na hatukuogopa kifo.
Mvua ikanyesha kwa nguvu, kisha ikapungua, na ikaendelea kunyesha usiku kucha.
Alfajiri ilipofika tuliamka na kuona kwamba kulikuwa na rundo kubwa la miamba na mchanga juu ya nyumba yetu, na maji yalikuwa yamezunguka jengo ambamo tulilala usiku; lilikuwa jambo la kushangaza. Niliangalia matope na vifusi mbele na nyuma ya nyumba yetu. Kukiwa na maji mengi na miamba mikubwa juu yetu, jengo ambamo tulijikingia lilikuwa ndilo hatari zaidi, lakini hakuna tone la maji au tope lililoingia, na lile ambalo hatukukaa ndani lilikuwa chini ya maji kabisa, na vitu vingi vilikizolewa kutoka humo. Kwa kweli tuliona upendo na wokovu wa Mungu. Kama haingekuwa Mungu kutuchunga na kutulinda hakuna hata mmoja wetu angeweza kuishi. Familia nzima ilimshukuru Mungu kwa dhati. Ni Mungu aliyetupa fursa hii ya maisha, tunapaswa kuihifadhi kwa upendo, na kufanya liwezekanalo kuanzia sasa kuendelea ili kufanya wajibu wetu na kumridhisha Mungu!
Utukufu wote Uwe kwa Mwenyezi Mungu!
Kutoka Kwa Vita Baina ya Haki na Uovu
Tufuate: Kuhusu Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni