Jumapili, 11 Novemba 2018

Sura ya 5 Lazima Uujue Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili | 3. Ni Nini Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu Mwenye Mwili na Kazi ya Roho?

3. Ni Nini Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu Mwenye Mwili na Kazi ya Roho?

Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Ingawa kazi ya Mungu mwenye mwili inahusisha shida nyingi zisizofikirika, matokeo ambayo yanapatikana mwishowe yanazidi kwa mbali sana kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu moja kwa moja. Kazi ya mwili inahusisha ugumu mwingi sana, na mwili hauwezi kuwa na utambulisho mkubwa kama wa Roho, hauwezi kufanya matendo ya kimiujiza kama Roho, achilia mbali kuwa na mamlaka kama ya Roho. Lakini kiini cha kazi inayofanywa na mwili huu usiokuwa wa kawaida ni kuu zaidi kulinganisha na kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho, na Mwili huu ndio jibu kwa mahitaji yote ya mwanadamu. Kwa wale wanaotaka kuokolewa, thamani ya Roho ipo chini zaidi kulinganisha na ile ya mwili. Kazi ya Roho inaweza kuufikia ulimwengu wote, katika milima yote, mito, maziwa, na bahari, lakini kazi ya mwili kwa ufanisi zaidi inahusiana na kila mtu anayekutana Naye. Aidha, mwili wa Mungu katika umbo la kushikika unaweza kueleweka vizuri na kuaminiwa na mwanadamu, na unaweza kuimarisha maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu, na anaweza kumwachia mwanadamu mvuto wa kina wa matendo halisi ya Mungu. Kazi ya Roho imefungwa sirini, ni vigumu kwa viumbe wenye mwili wa kufa kuelewa, na vigumu zaidi kwao kuona, na hivyo wanaweza kutegemea tu vitu vya kufikirika. Hata hivyo, kazi ya mwili ni ya kawaida, na imejikita katika uhalisia, na ina hekima kubwa sana, na ni ukweli unaoweza kuonekana kwa macho ya mwanadamu; mwanadamu anaweza kupitia uzoefu wa hekima ya Mungu, na hana haja ya kuwa na mitazamo yake mikubwa. Huu ndio usahihi na thamani halisi ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Roho anaweza tu kufanya vitu ambavyo havionekani kwa mwanadamu na vigumu kwake kufikiria, kwa mfano nuru ya Roho, mzunguko wa Roho na uongozi wa Roho, lakini kwa mwanadamu mwenye akili, hivi havitoi maana inayoeleweka. Vinatoa maana ya kusonga, au ya jumla tu, na havitoi maelekezo kwa maneno. Hata hivyo, kazi ya Mungu mwenye mwili, ni tofauti sana: Ina mwongozo sahihi wa maneno, ina nia ya dhati, ina malengo yanayoeleweka vizuri. Na hivyo mwanadamu hahitaji kupapasa, au kutumia fikra zake, au kufanya makisio. Huu ndio uwazi wa kazi katika mwili, na tofauti yake kubwa na kazi ya Roho. Kazi ya Roho inafaa tu kwa mawanda finyu, na haiwezi kuchukua kazi ya mwili. Kazi ya mwili inampatia mwanadamu malengo halisi zaidi na yanayohitajika na maarifa yaliyo halisi zaidi na yenye thamani kuliko kazi ya Roho Mtakatifu. Kazi ambayo ina thamani kubwa kwa mwanadamu aliyepaotoka ambayo inatoa maneno sahihi, malengo wazi ya kufuata, na ambayo inaweza kuonekana na kuguswa. Ni kazi halisia tu, na uongozi wa wakati ndio unaofaa kwa ladha ya mwanadamu, na kazi halisi ndiyo inayoweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika silika yake iliyoharibika. Hii inaweza kufanywa na Mungu mwenye mwili tu; ni Mungu mwenye mwili peke yake Ndiye anayeweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika hali yake ya zamani ya kupotoka. Ingawa Roho ni dutu ya asili wa Mungu, kazi kama hii inaweza tu kufanywa na mwili Wake. Ikiwa Roho angefanya kazi peke Yake, basi haingewezekana kwa kazi Yake kuwa ya ufanisi—huu ni ukweli rahisi kabisa. Ingawa watu wengi wamekuwa maadui wa Mungu kwa sababu ya mwili huu, anapokamilisha kazi Yake, wale ambao wapo kinyume Chake hawataacha tu kuwa maadui Zake, bali kinyume Chake watakuwa mashahidi Wake. Watakuwa mashahidi watakaokuwa wameshindwa Naye, mashahidi ambao wana ulinganifu na Yeye na ambao hawatenganishwi Naye. Atamsababisha mwanadamu kujua umuhimu wa kazi Yake katika mwili kwa mwanadamu, na mwanadamu atajua umuhimu wa mwili huu katika maana ya uwepo wa mwanadamu, atajua thamani Yake halisi katika ukuaji wa maisha ya mwanadamu, aidha, atajua mwili huu utakuwa chemchemi ya uhai ambayo kwayo mwanadamu hataachana nayo. Ingawa Mungu mwenye mwili anatofautiana sana na utambulisho na nafasi ya Mungu, na anaonekana kwa mwanadamu kuwa hana ulinganifu na hadhi yake halisi, mwili huu, ambao hauna sura halisi ya Mungu, au utambulisho halisi wa Mungu, unaweza kufanya kazi ambayo Roho wa Mungu hawezi kuifanya moja kwa moja. Hiyo ndiyo maana ya kweli na thamani ya Mungu mwenye mwili, na ni umuhimu huu na thamani ambayo mwanadamu hawezi kuithamini na kuikubali. Ingawa wanadamu wote wanamtazamia Roho wa Mungu na wanamdharau Mungu mwenye mwili, bila kujali vile wanavyoona au kufikiri, maana na thamani halisi ya mwili inapita kwa mbali ile ya Roho. Bila shaka, hii ni kwa mujibu wa mwanadamu aliyepotoka. Kwa kila mtu anayetafuta ukweli na anatamani kumwona Mungu, Kazi ya Roho inaweza kutoa tu ufunuo, na hisia ya kuona maajabu ambayo hayaelezeki na kufikirika, na hisia ambayo ni kuu, ya juu sana kuliko uwezo wa mwanadamu, na inayotamanika, lakini ambayo pia haifikiwi na haipatikani kwa wote. Mwanadamu na Roho wa Mungu wanaweza tu kutazamana kwa mbali, kana kwamba kuna umbali mrefu baina yao, na hawawezi kufanana kamwe, kana kwamba wametengenishwa na kitu kisichoonekana. Kwa hakika, hizi ni fikra za uongo ambazo Roho amempatia mwanadamu, kitu ambacho ni kwa sababu Roho na mwanadamu sio wa aina moja, na Roho na mwanadamu hawawezi kuishi pamoja katika ulimwengu mmoja, na kwa sababu Roho hana kitu chochote cha mwanadamu. Kwa hivyo mwanadamu hana haja ya Roho Mtakatifu, maana Roho hawezi kufanya kazi inayohitajika sana na mwanadamu moja kwa moja. Kazi ya mwili inampatia mwanadamu malengo halisi ya kufuata, maneno halisi, na hisia kwamba Yeye ni halisi na wa kawaida, kwamba ni mnyenyekevu na wa kawaida. Ingawa mwanadamu anaweza kumwogopa, kwa watu wengi Yeye ni rahisi kuhusiana Naye: Mwanadamu anaweza kuuona uso wake, na kusikia sauti yake, na hahitaji kumwangalia kwa kutokea mbali. Mwanadamu anahisi kuwa ni rahisi kuufikia mwili huu, sio wa mbali au usioeleweka, bali unaoonekana na kushikika, maana mwili huu upo katika ulimwengu mmoja na mwanadamu.
kutoka kwa "Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu haufanywi moja kwa moja kupitia njia ya Roho ama kama Roho, kwani Roho Wake hawezi kuguzwa ama kuonekana na mwanadamu, na hawezi kukaribiwa na mwanadamu. Kama Angejaribu kumwokoa mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya Roho, mwanadamu hangeweza kupokea wokovu Wake. Na kama sio Mungu kuvalia umbo la nje la mwanadamu aliyeumbwa, mwanadamu hawangeweza kupokea wokovu huu. Kwani mwanadamu hawezi kumkaribia kwa njia yoyote ile, zaidi kama jinsi hakuna anayeweza kukaribia wingu la Yehova. Ni kwa kuwa mwanadamu wa kuumbwa tu, hivyo ni kusema, kuliweka neno Lake katika mwili Atakaogeukana kuwa, ndio ataweza kulifanya neno yeye Mwenyewe ndani ya wale wote wanaomfuata. hapo ndipo mwanadamu ataskia mwenyewe neno Lake, kuona neno Lake, na kupokea neno Lake, kisha kupitia hili aokolewe kamili. Kama Mungu hangegeuka na kupata mwili, hakuna mwanadamu mwenye mwili ambaye angepokea wokovu huo mkuu, wala hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye angeokolewa. Kama Roho wa Mungu angefanya kazi moja kwa moja kati ya mwadamu, mwanadamu angepigwa ama kubebwa kabisa kama mfungwa na Shetani kwani mwanadamu hawezi kushirikiana na Mungu. Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama Roho wa Mungu angemwongelesha mwanadamu moja kwa moja, wote wangejiwasilisha kwa sauti hiyo, na kuanguka chini bila maneno ya ufunuo, vile Paulo alivyoanguka chini kukiwa na nuru alipokuwa akisafiri kwenda Damasko. Mungu angeendelea kufanya kazi kwa njia hii, mwanadamu hangeweza kutambua upotovu wake kupitia kwa hukumu katika neno na kupata wokovu. Ni kwa kupata mwili pekee ndiyo Ataweza kuwasilisha maneno Yake Mwenyewe kwa masikio ya wale wote ambao wana masikio waweze kuyasikia maneno Yake na kupokea kazi Yake ya hukumu kupitia kwa neno. Hayo tu ndio matokeo yanayopokewa na neno Lake, badala ya kutokea kwa Roho ikimtisha mwanadamu kuwasilisha. Ni kupitia tu kwa kazi ya vitendo na ya ajabu ndio tabia ya mwanadamu, iliyofichika ndani zaidi kwa enzi nyingi, ifichuliwe kabisa ili mwanadamu aitambue na kuibadilisha. Hili ndiyo kazi ya vitendo ya Mungu mwenye mwili wa Mungu; Ananena na kutekeleza hukumu juu ya mwanadamu kupitia kwa neno. Haya ndiyo mamlaka ya Mungu mwenye mwili na umuhimu wa Mungu kupata mwili. Inafanyika kuonyesha mamlaka ya Mungu mwenye mwili, matokeo yanayopatikana na kazi ya neno, na kwamba Roho Amekuja kwa mwili; Anaonyesha mamlaka Yake kupitia hukumu juu ya mwanadamu kwa neno. Ingawa mwili Wake ni hali ya nje ya mwanadamu wa kawaida, ni matokeo ambayo neno Lake linapokea ndiyo yanamwonyesha mwanadamu kuwa Amejaa mamlaka, kwama ni Mungu Mwenyewe na kwamba maneno Yake ni uelezo wa Mungu Mwenyewe. Hii inaonyesha wanadamu wote kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe, Mungu Mwenyewe Aliyekuwa mwili, na kwamba Hawezi kukosewa na yeyote. Hakuna anayeweza kuepuka hukumu Yake kupitia kwa neno, na hakuna nguvu ya giza inayoweza kutamalaki juu ya mamlaka Yake. Mwanadamu anamtii Yeye kabisa kwa sababu Yeye ni Neno aliyepata mwili, mamlaka Yake, na hukumu Yake kwa neno. Kazi iliyoletwa na mwili Wake uliokuwa mwili ni mamlaka ambayo Anamiliki.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa sababu yule anayehukumiwa ni mwanadamu, mwanadamu ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa, na sio roho ya Shetani ambayo inahukumiwa moja kwa moja, kazi ya hukumu haifanywi katika ulimwengu wa roho, bali miongoni mwa wanadamu. Hakuna anayefaa zaidi na mwenye vigezo, kuliko Mungu mwenye mwili kwa ajili ya kuhukumu upotovu wa mwili wa mwanadamu. Ikiwa hukumu ingefanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu, basi isingekuwa inajumuisha wote. Aidha, kazi kama hiyo itakuwa vigumu kwa mwanadamu kuikubali, maana Roho hawezi kukutana uso kwa uso na mwanadamu, na kwa sababu hii, matokeo hayawezi kuwa ya haraka, wala mwanadamu hataweza kuona kwa uwazi kabisa silika ya Mungu isiyokuwa na mawaa. Shetani anaweza tu kushindwa kabisa ikiwa Mungu mwenye mwili anahukumu upotovu wa mwanadamu. Kuwa sawa na mwanadamu akiwa na ubinadamu wa kawaida, Mungu mwenye mwili anaweza kumhukumu mwanadamu asiye na haki; hii ni ishara ya utakatifu Wake wa ndani na hali yake ya kutokuwa wa kawaida. Ni Mungu pekee ndiye aliyehitimu, na aliye katika nafasi ya kumhukumu mwanadamu, maana ana ukweli, na mwenye haki na kwa hivyo Ana uwezo wa kumhukumu mwanadamu. Wale ambao hawana ukweli na haki hawafai kuwahukumu wengine. Ikiwa kazi hii ingefanywa na Roho wa Mungu, basi usingekuwa ushidi dhidi ya Shetani. Roho kiasili huwa ameinuliwa sana kuliko viumbe wenye mwili wa kufa, na Roho wa Mungu ni mtakatifu kwa asili, na anaushinda mwili. Ikiwa Roho alifanya kazi hii moja kwa moja, asingeweza kuhukumu kutotii kote kwa mwanadamu, na asingeweza kufichua hali nzima ya mwanadamu ya kutokuwa na haki. Kwa maana kazi ya hukumu pia inafanywa kwa mitazamo ya mwanadamu juu ya Mungu, na mwanadamu hajawahi kuwa na dhana yoyote juu ya Roho, na hivyo Roho hana uwezo wa kufunua hali ya mwanadamu ya kutokuwa na haki, wala kuweza kuweka wazi kabisa hali hiyo ya kutokuwa na haki. Mungu mwenye mwili ni adui wa wale wote wasiomjua. Kupitia kuhukumu dhana za mwanadamu na kumpinga Yeye, Anafunua hali yote ya kutotii ya mwanadamu. Matokeo ya kazi Yake katika mwili yapo dhahiri zaidi kuliko yale ya kazi ya Roho. Na hivyo, hukumu ya wanadamu wote haifanywi moja kwa moja na Roho, bali ni kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu mwenye mwili anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu, na Mungu mwenye mwili anaweza kumshinda kabisa mwanadamu. Katika uhusiano wake na Mungu mwenye mwili, mwanadamu huwa anapiga hatua kutoka katika upinzani na kuwa mtii, kutoka katika mateso na kukubaliwa, kutoka katika mitazamo na kuwa na maarifa, na kutoka kukataliwa hadi upendo. Haya ni matokeo ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anaokolewa tu kwa kukubali hukumu Yake, bali hatua kwa hatua tu atamwelewa taratibu kupitia neno la mdomo Wake, ametwaliwa Naye wakati wa upinzani wake Kwake, na anapata uzima kutoka Kwake wakati wa kukubali kuadibu Kwake. Hii yote ni kazi ya Mungu mwenye mwili, na sio kazi ya Mungu katika utambulisho Wake kama Roho. Kazi iliyofanywa na Mungu mwenye mwili ni kazi kubwa sana, na ni kazi ya kina sana, na sehemu muhimu ya hatua tatu za kazi ya Mungu ni hatua mbili za kazi ya kufanyika mwili.
kutoka kwa "Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama kazi hii ingefanywa na Roho—kama Mungu hangepata mwili, na badala yake Roho angenena moja kwa moja kupitia radi ili mwanadamu hangekuwa na njia ya kuwasiliana na Yeye, je, mwanadamu angejua tabia yake? Kama Roho tu Angefanya kazi, basi mtu hangekuwa na njia yoyote ya kujua tabia Yake. Watu wanaweza tu kuona tabia ya Mungu kwa macho yao wenyewe wakati Anapopata mwili, wakati ambapo Neno laonekana katika mwili, na Anaonyesha tabia Yake yote kupitia mwili. Mungu kweli huishi kati ya wanadamu. Anaonekana; mwanadamu anaweza kweli kujihusisha na tabia Yake na kile Anacho na Alicho; ni kwa njia hii tu ndiyo mwanadamu anaweza kumjua kweli.
kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kitu kizuri kuhusu kazi Yake katika mwili ni kwamba anaweza kuacha maneno sahihi na ya kusihi, na mapenzi Yake kwa mwanadamu kwa wale wanaomfuata, ili kwamba hapo baadaye wafuasi wake waweze kueneza kazi Yake yote katika mwili kwa usahihi zaidi na kwa udhabiti na mapenzi Yake kwa wanadamu wote kwa wanaoikubali njia hii. Ni kazi ya Mungu mwenye mwili pekee miongoni mwa wanadamu ndiyo inayokamilisha ukweli wa Mungu kuwa na kuishi pamoja na mwanadamu. Ni kazi hii pekee ndiyo inayotimiza shauku ya mwanadamu kuutazama uso wa Mungu, kushuhudia kazi ya Mungu, na kusikia neno la Mungu. Mungu mwenye mwili anahitimisha enzi ambayo Yehova alionekana mgongo tu, na pia anahitimisha enzi ya mwanadamu kuamini katika Mungu asiye dhahiri. Kwa umahususi, kazi ya Mungu mwenye mwili wa mwisho inawaleta wanadamu wote katika enzi ambayo ni halisi zaidi, ya matendo zaidi na nzuri zaidi. Hahitimishi tu enzi ya sheria na mafundisho ya kidini; la umuhimu zaidi, anamfunulia mwamadamu Mungu ambaye ni halisia na wa kawaida ambaye ni mwenye haki na mtakatifu, ambaye anafungua kazi ya mpango wa usimamizi na kuonesha siri za hatma ya mwanadamu, ambaye alimuumba mwanadamu na kuhitimisha kazi ya usimamizi, na ambaye amebakia sirini kwa maelfu ya miaka. Anaihitimisha enzi ya Mungu asiye yakini, anaihitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanatamani kuutafuta uso wa Mungu lakini wanashindwa, anahitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanamtumikia Shetani, na anawaongoza wanadamu wote katika enzi mpya kabisa. Haya yote ni matokeo ya Mungu mwenye mwili badala ya Roho wa Mungu.Wakati Mungu anapofanya kazi katika mwili wake, wale wanaofuata wanakuwa hawatafuti tena vitu hivyo visivyo yakini, na wanaacha kukisia mapenzi ya Munguasiye yakini. Mungu anapoeneza kazi Yake katika mwili, wale wanaomfuata wataieneza kazi ambayo Ameifanya katika mwili kwa vikundi na madhehebu yote, na watazungumza maneno Yake yote katika masikio ya wanadamu wote. Yote yale yanayosikizwa na wale wanaoipokea injili Yake yatakuwa ni ukweli wa kazi Yake, yatakuwa mambo ambayo mwanadamu ameyashuhudia na kuyaona, na utakuwa ukweli na sio uvumi. Ukweli huu ni ushahidi ambao anauenezea kazi na pia ni zana ambazo Anazitumia katika kueneza kazi. Bila uwepo wa ukweli, Injili yake isingeweza kuenea katika nchi zote na maeneo yote; bila ukweli bali kwa fikra tu za mwanadamu, Asingweza kufanya kazi ya kuushinda ulimwengu wote. Mwanadamu hawezi kumgusa Roho, na wala hawezi kumwona, na kazi ya Roho haiwezi kuacha ushahidi au ukweli wowote zaidi wa kazi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu kamwe hataweza kuuona uso halisi wa Mungu, na siku zote ataamini katika Mungu asiye yakini ambaye hayupo. Mwanadamu hataweza kuutazama uso wa Mungu, hataweza kusikia maneno yaliyozungumzwa na Mungu moja kwa moja. Hata hivyo picha anazozijenga mwanadamu kumhusu Mungu, sio halisi na haziwezi kuchukua nafasi ya uso halisi wa Mungu; silika ya asili ya Mungu, na kazi ya Mungu Mwenyewe haiwezi kuigizwa na mwanadamu. Mungu wa mbinguni asiyeonekena na kazi Yake inaweza kuletwa tu duniani na Mungu mwenye mwili ambaye Yeye binafsi anafanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Hii ndiyo njia halisi ambayo Mungu anaonekana kwa mwanadamu, ambayo kwayo mwanadamu anamwangalia Mungu na kuujua uso wa kweli wa Mungu, na haiwezi kufanikishwa na Mungu asiyekuwa katika mwili. Baada ya Mungu kufanya kazi yake hadi hatua hii, kazi yeke tayari imeshafanikiwa kuwa na matokeo mazuri, na imekuwa ni mafanikio kamili. Kazi binafsi ya Mungu mwenye mwili tayari imekwishakamilisha asilimia tisini ya kazi yote ya usimamizi wa Mungu. Mwili umetoa mwanzo mzuri katika kazi Yake yote, na muhtasari kwa ajili ya kazi Yake yote, na ametangaza kazi Yake yote na Ameifanya ya mwisho kupitia ujazaji tena wa kazi hii yote. Kuanzia sasa, hakutakuwepo na Mungu mwingine katika mwili kwa ajili ya kufanya hatua ya nne ya kazi ya Mungu, na hakutakuwa na kazi ya miujiza zaidi ya Mungu mwenye mwili wa tatu.
kutoka kwa "Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni