1. Unafaa Kutofautisha Vipi Kati ya Kazi ya Mungu na ya Mwanadamu?
Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Katika Enzi ya Neema, Yesu pia Alinena mengi na kufanya kazi nyingi. Alikuwaje tofauti na Isaya? Alikuwaje tofauti na Danieli? Je, Alikuwa nabii? Ni kwa nini inasemekana kwamba Yeye ni Kristo? Kuna tofauti gani baina yao? Wote walikuwa wanadamu walionena maneno, na maneno yao yalionekana sawa kwa wanadamu. Wote walinena na kufanya kazi. Manabii wa Agano la Kale walitoa unabii, na vivyo hivyo, pia na Yesu. Ni kwa nini iwe hivi? Tofauti hapa inapatikana katika aina ya kazi zao.
Ili kutambua suala hili, huwezi kuangazia asili ya mwili na hufai kuangazia upurukushani wa maneno ya mtu. Daima ni sharti kwanza uangazie kazi ya mtu na athari inazoacha kwa mwanadamu. Unabii uliotolewa na Isaya wakati ule, haukuongeza kitu katika uzima wa mwanadamu, na ujumbe uliopokelewa na watu kama Danieli ulikuwa tu unabii na si njia ya uzima. Ingekuwa si kuonekana kwa moja kwa moja kwa Yehova, hakuna ambaye angelifanya hiyo kazi, kwani haiwezekani kwa wanadamu. Yesu pia Alisema mengi, lakini maneno yake yalikuwa njia ya uzima ambayo kwayo mwanadamu angepata njia ya kutenda. Hii ni kusema kuwa, kwanza, Yeye Angeukimu uzima wa mwanadamu, kwa kuwa Yesu ni uzima; pili, Angeweza kuugeuza upotovu wa mwanadamu; tatu, kazi Yake ingeweza kuifuata ile ya Yehova ili kuendeleza enzi; nne, Angeweza kutambua mahitaji ya mwanadamu kwa ndani na kufahamu anachokosa mwanadamu; tano, Angeweza kuanzisha enzi mpya na kutamatisha enzi ya zamani. Ndiyo maana Anaitwa Mungu na Kristo; Yeye si tofauti na Isaya tu; bali pia na manabii wote. Chukua Isaya kama ulinganisho wa kazi za manabii. Kwanza, asingeweza kuukimu uzima wa mwanadamu; pili, asingeweza kuanzisha enzi mpya. Alikuwa akifanya kazi chini ya uongozi wa Yehova wala si kuanzisha enzi mpya. Tatu, alichokizungumza yeye mwenyewe kilikuwa nje ya ufahamu wake. Alikuwa akipata ufunuo moja kwa moja kutoka kwa Roho wa Mungu, na wengine wasingeelewa hata baada ya kuusikiliza ufunuo huo. Haya machache yanatosha kuthibitisha kuwa kazi yake haikuwa zaidi ya unabii, si zaidi ya kazi iliyofanywa kwa niaba ya Yehova. Hata hivyo asingeweza kumwakilisha Yehova kikamilifu. Alikuwa mtumishi wa Yehova, chombo katika kazi ya Yehova. Aidha alikuwa anafanya kazi katika Enzi ya Sheria tu na katika upeo wa kazi ya Yehova; hakufanya kazi nje ya Enzi ya Sheria. Kwa upande mwingine, kazi ya Yesu ilikuwa tofauti. Alivuka mipaka ya kazi ya Yehova; Alifanya kazi kama Mungu mwenye mwili na kupitia mateso ili amkomboe mwanadamu. Hii ni kusema kuwa Alifanya kazi mpya nje ya ile iliyofanywa na Yehova. Huu ulikuwa mwazo wa enzi mpya. Jambo jingine ni kuwa Aliweza kuyazungumzia mambo ambayo mwanadamu asingeweza kupata. Kazi Yake ilikuwa kazi ndani ya usimamizi wa Mungu na ilijumuisha wanadamu wote. Hakufanya kazi miongoni mwa watu wachache tu, na wala kazi yake haikuwa kuwaongoza watu wachache tu. Kuhusu jinsi Mungu Alivyopata mwili kuwa mwanadamu, jinsi Roho alivyopewa ufunuo wakati ule, na jinsi Roho alivyomshukia mwanadamu kufanya kazi, haya ni mambo ambayo mwanadamu hawezi kuona au kugusa. Haiwezekani kabisa ukweli huu kuwa thibitisho kuwa Yeye ni Mungu mwenye mwili. Kwa sababu hii, tofauti inaweza kupatikana tu kwenye maneno na kazi ya Mungu ambayo ni mambo dhahiri kwa mwanadamu. Hili tu ndilo halisi. Hii ni kwa sababu masuala ya Roho hayaonekani kwako na yanafahamika wazi na Mungu Mwenyewe peke yake, wala hata Mungu kuwa mwili hafahamu yote; unaweza kuthibitisha kama Yeye ni Mungu[a] kutokana na kazi Aliyoifanya tu. Kutokana na kazi Yake, inaweza kuonekana kuwa, kwanza, Anaweza kufungua enzi mpya; pili, Yeye Ana uwezo wa kuyaruzuku maisha ya mwanadamu na kumwonyesha mwanadamu njia ya kufuata. Hii inatosha kuthibitisha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe. Angalau kazi Aifanyayo yaweza kumwakilisha kikamilifu Roho Mtakatifu wa Mungu na kutokana na kazi hiyo inaonekana kuwa Roho wa Mungu yupo ndani yake. Kwa kuwa kazi iliyofanywa na Mungu katika mwili ilikuwa kuanzisha enzi mpya, kuanzisha kazi mpya, na kuanzisha na kufungua mazingira mapya, haya mambo machache tu yanatosha kuthibitisha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe. Hili kwa hivyo linamtofautisha na Isaya, Danieli, na manabii wengine wakuu.
kutoka kwa "Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ya Mungu mwenye mwili huanzisha enzi mpya, na wale wanaoiendeleza kazi Yake ni watu wanaotumiwa Naye. Kazi inayofanywa na mwanadamu yote ipo ndani ya huduma ya Mungu mwenye mwili, na haina uwezo wa kwenda zaidi ya mawanda haya. Ikiwa Mungu mwenye mwili haji kufanya kazi Yake, mwanadamu hana uwezo wa kuhitimisha enzi ya zamani, na hana uwezo wa kuikaribisha enzi mpya. Kazi inayofanywa na mwanadamu ipo tu ndani ya wajibu wake ambao unawezekana kibinadamu, na haiwakilishi kazi ya Mungu. Ni Mungu mwenye mwili pekee ndiye anayeweza kuja na kukamilisha kazi ambayo Anapaswa kuifanya, na mbali na Yeye, hakuna anayeweza kuifanya kazi hii badala Yake. Bila shaka, kile Ninachozungumzia ni kuhusiana na kazi ya kufanyika mwili.
kutoka kwa "Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wengine wanaweza kushangaa, mbona enzi ikaribishwe na Mungu Mwenyewe? Kiumbe kilichoumbwa hakiwezi kusimama kwa niaba Yake? Nyote mnafahamu kuwa Mungu Anakuwa mwili hasa kwa ajili ya kuikaribisha enzi mpya, na, kwa hakika, Anapoikaribisha enzi mpya, Atakuwa Ameikamilisha enzi ya kale wakati uo huo. Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho; ni Yeye Mwenyewe ndiye Anayeanzisha kazi Yake na hivyo lazima iwe ni Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani na huishinda dunia. Kila wakati Yeye Mwenyewe Anapofanya kazi miongoni mwa mwanadamu, ni mwanzo wa mapigano mapya. Bila mwanzo wa kazi mpya, kwa kawaida hakutakuwa na kikomo kwa enzi ya kale. Na bila kikomo kwa enzi ya kale ina maana kuwa vita na Shetani havijafika mwisho. Ni kama tu Mungu Mwenyewe Anakuja miongoni mwa mwanadamu na kutenda kazi mpya ndipo mwanadamu atakapoweza kujitoa kutoka katika umiliki wa Shetani na kupata maisha na mwanzo mpya. Vinginevyo, mwanadamu ataishi milele katika wakati wa kale na milele kuishi katika ushawishi wa kale wa Shetani. Katika kila enzi inayoongozwa na Mungu, sehemu ya mwanadamu huwekwa huru, na hivyo, mwanadamu huendelea na kazi ya Mungu kuelekea enzi mpya. Ushindi wa Mungu ni ushindi kwa wale ambao humfuata Yeye. Kama binadamu wa kuumbwa angepewa usukani wa kutimiza enzi, basi iwe kutoka kwa mtazamo wa mwanadamu ama Shetani, hii ni kama kupinga au kusaliti Mungu, na hivyo kazi ya mwanadamu ingempa Shetani mshikilio. Mwanadamu anapotii na kumfuata Mungu katika enzi iliyokaribishwa na Mungu Mwenyewe tu ndipo Shetani angeshawishiwa kabisa, kwani hiyo ndiyo kazi ya kiumbe aliyeumbwa. Kwa hivyo Nasema kuwa mnafaa tu kufuata na kutii, na hakuna kingine kitakachoulizwa kutoka kwenu. Hiyo ndiyo maana ya kusema kila mmoja kuendeleza kazi na kufanya kazi Yake. Mungu hufanya kazi Yake Mwenyewe na Yeye hahitaji mwanadamu kufanya kazi Yake kwa niaba Yake, na wala hajishughulishi katika kazi ya viumbe. Mwanadamu anafanya kazi yake na haingilii kati kazi ya Mungu, na huo ndio utii wa kweli na ushahidi kuwa Shetani ameshindwa. Baada ya Mungu Mwenyewe kukaribisha enzi mpya, Yeye Mwenyewe hafanyi kazi tena kati ya mwanadamu. Ni wakati huo tu ndipo mwanadamu anaingia rasmi katika enzi mpya kufanya kazi yake na kutekeleza misheni yake kama kiumbe aliyeumbwa. Hivyo ndivyo zilivyo kanuni za kazi zisizowezwa kukiukwa na yeyote. Kufanya kazi katika njia hii pekee ndio yenye busara. Kazi ya Mungu hufanywa na Mungu Mwenyewe. Ni Yeye ndiye Anayeweka kazi katika mwendo, na pia Yeye ndiye Anayemaliza. Ni Yeye ndiye hupanga kazi, na pia Yeye ndiye Anayesimamia, na zaidi ya hayo, ni Yeye ndiye Anayeleta kazi kuzaa matunda. Ni ilivyoandikwa katika Biblia, "Mimi ndiye Mwanzo na Mwisho: Mimi ndiye Mpanzi na Mvunaji." Hayo yote yanahusiana na usimamizi wa kazi Yake yanayofanywa na mkono Wake. Yeye ndiye Mtawala wa mpango wa miaka elfu sita; hakuna anayeweza kufanya kazi Yake kwa niaba Yake ama kuleta kazi Yake hadi mwisho, kwani Yeye ndiye Aliye katika uongozi wa yote. Kwa kuwa Aliumba dunia, Ataongoza ulimwengu mzima kuishi katika nuru Yake, na Atamaliza enzi yote na kuleta mpango Wake wote kwa mafanikio!
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ya Roho Mtakatifu inakamilishwa na kukamilika kupitia watu wa aina nyingi na hali nyingi tofauti tofauti. Ingawa kazi ya Mungu mwenye mwili inaweza kuwakilisha kazi ya enzi zote, na inaweza kuwakilisha uingiaji wa watu katika enzi nzima, kazi kwa watu wengi bado inahitajika kufanywa na watu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu na sio Mungu mwenye mwili. Kwa hivyo, kazi ya Mungu, au huduma ya Mungu mwenyewe, ni kazi ya Mungu mwenye mwili na haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kazi ya Roho Mtakatifu imekamilishwa kupitia watu wa aina mbalimbali na haiwezi kukamilishwa na mtu mahususi mmoja tu, au kufafanuliwa kikamilifu kupitia mtu mmoja mahususi. Wale ambao wanaongoza kanisa pia hawawezi kuiwakilisha kazi ya Roho Mtakatifu kikamilifu; wanaweza kufanya tu kazi fulani ya kuongoza. Kwa njia hii, kazi ya Roho Mtakatifu inaweza kugawanywa katika sehemu tatu: Kazi ya Mungu mwenyewe, kazi ya wanadamu wanaotumiwa, na kazi kwa wale wote walioko katika mkondo wa Roho Mtakatifu. Miongoni mwa hizo tatu, kazi ya Mungu ni kuongoza enzi nzima; kazi ya wanadamu wanatumiwa ni kuwaongoza wafuasi wote wa Mungu kwa kutumwa au kupokea maagizo kwa ajili ya kazi ya Mungu mwenyewe; na wanadamu hawa ndio wanaoshirikiana na kazi ya Mungu; kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu kwa wale waliopo katika mkondo wake ni kudumisha kazi Yake yote, yaani, kudumisha usimamizi wote na kudumisha ushuhuda Wake, na wakati uo huo kuwakamilisha wale wanaoweza kukamilishwa. Sehemu tatu hizi ni kazi kamili ya Roho Mtakatifu, lakini bila kazi ya Mungu Mwenyewe, kazi yote ya usimamizi inaweza kutuama. Kazi ya Mungu Mwenyewe inahusisha kazi ya wanadamu wote, na pia inawakilisha kazi ya enzi nzima. Hii ni kusema kwamba, kazi ya Mungu mwenyewe inawakilisha harakati na mwelekeo wa kazi yote ya Roho Mtakatifu, ilhali kazi ya mitume inafuata kazi ya Mungu na wala haiongozi enzi, na wala haiwakilishi mwelekeo unaofanya kazi wa Roho Mtakatifu katika enzi nzima. Huwa wanafanya tu kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya, ambayo haihusishi kabisa kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu ni mradi ndani ya kazi ya usimamizi. Kazi ya mwanadamu ni wajibu tu wa wanadamu kuweza kutumika na wala haina uhusiano na kazi ya usimamizi. Kwa sababu ya utambulisho na uwakilishaji tofauti wa kazi hii, licha ya ukweli kwamba zote ni kazi za Roho Mtakatifu, kuna tofauti za wazi na bainifu kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Aidha, kiwango cha kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu kwa watu wenye tambulisho tofauti inatofautiana. Hizi ni kanuni na mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi inayotekelezwa na yule anayetumiwa na Mungu ni kwa ajili ya kushirikiana na kazi ya Kristo au Roho Mtakatifu. Mtu huyu anainuliwa na Mungu miongoni mwa wanadamu, yuko pale kuongoza wateule wote wa Mungu, na pia yeye anainuliwa na Mungu ili kufanya kazi ya ushirikiano wa mwanadamu. Na mtu kama huyu, ambaye anaweza kufanya kazi ya ushirikiano wa mwanadamu, matakwa mengi zaidi ya Mungu kwa mwanadamu na kazi ambayo Roho Mtakatifu lazima Afanye miongoni mwa wanadamu inaweza kutimizwa kupitia kwake. Njia nyingine ya kulisema ni hivi: Lengo la Mungu katika kumtumia mtu huyu ni ili wote wanaomfuata Mungu waweze kuelewa bora mapenzi ya Mungu, na waweze kufikia matakwa zaidi ya Mungu. Kwa vile watu hawawezi kuyaelewa maneno ya Mungu na mapenzi ya Mungu moja kwa moja, Mungu amemuinua mtu fulani ambaye anatumiwa kutekeleza kazi kama hiyo. Mtu huyu anayetumiwa na Mungu anaweza kuelezwa kama chombo ambacho Mungu hutumia kuwaongoza watu, kama "mfasiri" anayewasiliana kati ya Mungu na watu. Hivyo, mtu kama huyo hayuko kama yeyote kati ya wale wanaofanya kazi katika nyumba ya Mungu au ambao ni mitume Wake. Kama wao, anaweza kusemekana kuwa mtu anayemhudumia Mungu, lakini katika kiini cha kazi yake na usuli wa kutumiwa kwake na Mungu anatofautiana sana na wafanyakazi wengine na mitume. Kuhusu kiini cha kazi yake na usuli wa kutumiwa kwake, mwanadamu anayetumiwa na Mungu huinuliwa na Yeye, hutayarishwa na Mungu kwa kazi ya Mungu, na yeye hushirikiana katika kazi ya Mungu Mwenyewe. Hakuna mtu anayeweza kushikilia nafasi ya kazi yake, ni ushirikiano wa mwanadamu ndio muhimu katika kazi takatifu. Kazi inayotekelezwa na wafanyakazi wengine au mitume, wakati ule ule, ni uchukuzi na utekelezaji tu wa hali nyingi za matayarisho ya makanisa wakati wa kila kipindi, ama sivyo kazi ya utoaji wa kawaida wa uzima ili kudumisha uzima wa kanisa. Wafanyakazi hawa na mitume hawateuliwi na Mungu, seuze kuweza kuitwa wale wanaotumiwa na Roho Mtakatifu. Wao huchaguliwa kutoka miongoni mwa makanisa na, baada ya kufunzwa na kukuzwa kwa kipindi cha wakati, wale wanaofaa hubaki, huku wale wasiofaa hurudishwa walikotoka. Kwa vile watu hawa huchaguliwa kutoka miongoni mwa makanisa, wengine huonyesha tabia yao halisi baada ya kuwa viongozi, na wengine hata hufanya mambo mengi mabaya na huishia kufutwa. Yule anayetumiwa na Mungu, kwa upande mwingine, ni mtu ambaye ametayarishwa na Mungu, na aliye na ubora fulani wa tabia, na ana ubinadamu. Ametayarishwa na kukamilishwa mapema na Roho Mtakatifu, na anaongozwa kabisa na Roho Mtakatifu, na, inapofikia kazi yake hasa, yeye huongozwa na kuamriwa na Roho Mtakatifu—kutokana na hilo hakuna mkengeuko katika njia ya kuwaongoza wateule wa Mungu, kwani Mungu kwa hakika huwajibikia kazi Yake mwenyewe, na Mungu hufanya kazi Yake nyakati zote.
kutoka kwa "Kuhusu Mungu Kumtumia Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Maneno na kazi za manabii na za wale waliotumiwa na Roho Mtakatifu zote zilikuwa zinafanya wajibu wa mwanadamu, kufanya jukumu lake kama kiumbe na kufanya ambacho mwanadamu anapaswa kufanya. Hata hivyo, maneno na kazi za Mungu mwenye mwili ilikuwa ni kuendeleza huduma Yake. Japo umbile Lake lilikuwa lile la kiumbe, kazi Yake haikuwa kutimiza majukumu Yake bali Huduma Yake. Dhana "wajibu" inarejelea viumbe ilhali "huduma" inarejelea mwili wa Mungu mwenye mwili. Kuna tofauti kubwa kati ya haya mawili, na haya mawili hayabadilishani nafasi. Kazi ya mwanadamu ni kufanya wajibu wake, ilhali kazi ya Mungu ni kusimamia, na kuendeleza huduma Yake. Kwa hivyo, japo mitume wengi walitumiwa na Roho Mtakatifu na manabii wengi wakajazwa Naye, kazi zao na maneno yao yalikuwa tu kutimiza wajibu wao kama viumbe. Japo unabii wao ungeweza kuwa mkubwa kuliko maisha kama yanavyozungumziwa na Mungu mwenye mwili, na hata ubinadamu wao ulikuwa wa hali ya juu kuliko wa Mungu kuwa mwenye mwili, walikuwa bado wanafanya wajibu wao na wala si kutimiza huduma yao. Wajibu wa mwanadamu unarejelea majukumu yake, na ni kitu kinachoweza kupatwa kwa mwanadamu. Hata hivyo, huduma ifanywayo na Mungu mwenye mwili inahusiana na usimamizi Wake, na haiwezi kupatikana kwa mwanadamu. Hata kama Mungu mwenye mwili hunena, kufanya kazi, au kutenda miujiza, Anafanya kazi kubwa katika usimamizi Wake, kazi ambayo haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kazi ya mwanadamu ni kufanya tu wajibu wake kama kiumbe katika hatua fulani ya usimamizi wa Mungu. Bila usimamizi kama huo, yaani, ikiwa huduma ya Mungu kuwa mwili itapotea, pia wajibu wa viumbe utapotea. Kazi ya Mungu kuendeleza huduma Yake ni kumsimamia mwanadamu, ilhali mwanadamu afanyapo wajibu wake ni kutimiza wajibu wake ili kuafikia masharti ya Muumba na haiwezi kwa vyovyote vile kuchukuliwa kwamba ameendeleza huduma ya mtu yeyote. Kwa nafsi asili ya Mungu, yaani, Roho, kazi ya Mungu ni usimamizi wake, bali kwa Mungu kuwa mwili akiwa na umbile la nje la kiumbe, kazi yake ni kuendeleza huduma Yake. Kazi yoyote Aifanyayo Mungu ni ya kuendeleza huduma Yake, na mwanadamu anaweza tu kufanya awezalo ndani ya upeo Wake wa usimamizi na chini ya uongozi Wake.
kutoka kwa "Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Hata mwanadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu hawezi kumwakilisha Mungu Mwenyewe. Na mwanadamu huyu hawezi tu kumwakilisha Mungu bali pia kazi yake haiwezi kumwakilisha Mungu moja kwa moja. Hivyo ni kusema uzoefu wa mwanadamu hauwezi kuwekwa moja kwa moja katika usimamizi wa Mungu, na hauwezi kuwakilisha usimamizi wa Mungu. Kazi yote ambayo Mungu Mwenyewe hufanya ni kazi Anayolenga Kufanya katika mpango Wake wa usimamizi na inahusiana na usimamizi mkuu. Kazi ifanywayo na mwanadamu (mwanadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu) hukidhi uzoefu wake binafsi. Anapata njia mpya ya uzoefu mbali na ile iliyotembelewa na wale waliomtangulia na anawaongoza ndugu zake chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Kinachotolewa na watu hawa ni uzoefu wao ama maandishi ya kiroho ya watu wa kiroho. Ingawa wanatumiwa na Roho Mtakatifu, kazi ya watu kama hao haina uhusiano na kazi ya usimamizi mkuu katika mpango wa miaka elfu sita. Wamesimamishwa na Roho Mtakatifu katika wakati tofauti kuongoza watu katika mkondo wa Roho Mtakatifu hadi wakamilishe kazi yao ama maisha yao yafike mwisho. Kazi wanayofanya ni kutayarisha njia ifaayo kwa ajili ya Mungu Mwenyewe ama kuendeleza kitu kimoja kwa usimamizi wa Mungu Mwenyewe katika dunia. Watu hao hawawezi kufanya kazi kuu katika usimamizi Wake, na hawawezi kufungua njia mpya, ama kumaliza kazi yote ya Mungu kutoka enzi ya kitambo. Kwa hivyo, kazi wafanyayo inawakilisha kiumbe aliyeumbwa pekee akifanya kazi Yake na hawezi kuwakilisha Mungu Mwenyewe Akifanya huduma Yake. Hii ni kwa sababu kazi wanayofanya haifanani na ile inayofanywa na Mungu Mwenyewe. Kazi ya kukaribisha enzi mpya haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba ya Mungu. Haiwezi kufanywa na mwingine ila Mungu Mwenyewe. Kazi yote inayofanywa na mwanadamu ni kufanya wajibu wake kama mmoja wa viumbe na inafanywa akiguswa au kupewa nuru na Roho Mtakatifu. Uongozi ambao watu hao hupeana ni jinsi ya kuzoea katika kila siku ya maisha ya mwanadamu na jinsi mwanadamu anapaswa kutenda kwa maelewano na mapenzi ya Mungu. Kazi ya mwanadamu haihusishi usimamizi wa Mungu ama kuwakilisha kazi ya Roho. Kama mfano, kazi ya Witness Lee na Watchman Nee ilikuwa ni kuongoza njia. Njia iwe mpya au nzee, kazi ilifanywa kwa misingi ya kutozidi kanuni za Biblia. Haijalishi kama makanisa ya mitaa yalirejeshwa yalivyokuwa awali au yalijengwa, kazi yao ilikuwa ni kuanzisha makanisa. Kazi waliyofanya iliendeleza kazi ambayo Yesu Kristo na mitume Wake walikuwa hawajamaliza au kuendeleza zaidi kwenye Enzi ya Neema. Kile walichofanya katika kazi yao kilikuwa ni kurejesha kile ambacho Yesu Kristo Alikuwa Ameomba katika kazi Yake ya vizazi vitakavyokuja baada Yake Yeye, kama vile kuhakikisha kwamba vichwa vyao vimefunikwa, ubatizo, umegaji mkate, au unywaji wa mvinyo. Inaweza kusemekana kwamba kazi yao ilikuwa kubakia tu kwenye Biblia na kutafuta njia zinazotokana tu na Biblia. Hawakupiga hatua yoyote mpya kamwe. Hivyo basi, mtu anaweza kuona tu ugunduzi wa njia mpya ndani ya Biblia, pamoja na mazoea bora zaidi na yenye uhalisia zaidi. Lakini mtu hawezi kupata katika kazi yao mapenzi ya sasa ya Mungu, isitoshe hawezi kupata kazi mpya ambayo Mungu Atafanya kwenye siku za mwisho. Hii ni kwa sababu njia ambayo walitembelea ilikuwa bado ile nzee; hakukuwa na maendeleo yoyote na kitu chochote kipya. Waliendelea kuufuata ukweli wa "kule kusulubishwa kwa Yesu," mazoea ya "kuwaomba watu kutubu na kukiri dhambi zao," msemo kwamba "yule atakayevumilia hata mwisho ataokoka," na msemo kwamba "mwanamume ndiye kichwa cha mwanamke, na mwanamke lazima amtii mume wake." Aidha, waliendeleza dhana ya kitamaduni kwamba "akina dada hawawezi kuhubiri, na wanaweza tu kutii." Ikiwa njia kama hiyo ya uongozi ingeendelea, basi Roho Mtakatifu asingewahi kuweza kutekeleza kazi mpya, kuwaweka binadamu huru dhidi ya falsafa, au kuwaongoza binadamu kwenye himaya ya uhuru na urembo. Hivyo basi, hatua hii ya kazi ya mabadiliko ya enzi lazima ifanywe na kuzungumzwa na Mungu Mwenyewe, la sivyo hakuna mwanadamu anayeweza kufanya hivyo badala Yake. Mpaka hapa, kazi yote ya Roho Mtakatifu iliyo nje ya mfululizo huu imesimama, na wale waliotumiwa na Roho Mtakatifu wamepoteza mwelekeo wao. Kwa hivyo, kwa sababu kazi ya wanadamu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu si sawa na kazi ifanywayo na Mungu Mwenyewe, utambulisho wao na wanayefanya kazi kwa niaba yake ni tofauti. Hii ni kwa sababu kazi ambayo Roho Mtakatifu Analenga Kufanya ni tofauti, na hapo kutoa utambulisho tofauti na hadhi kwa wale wote wafanyao kazi. Wanadamu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu wanaweza kufanya kazi mpya na wanaweza kutoa kazi iliyofanywa katika enzi iliyopita, lakini kazi yao haiwezi kueleza tabia na mapenzi ya Mungu kwa enzi mpya. Wanafanya kazi ili kuondoa kazi ya enzi iliyopita tu, sio kufanya kazi mpya kuwakilisha moja kwa moja tabia ya Mungu Mwenyewe. Hivyo, haijalishi matendo mangapi yaliyopitwa na wakati wanakomesha ama matendo mapya wanaanzisha, bado wanawakilisha mwanadamu na viumbe vilivyoumbwa. Mungu Mwenyewe Akifanya kazi, hata hivyo, Hatangazi wazi kukomeshwa kwa matendo ya enzi ya zamani au kutangaza moja kwa moja kuanzishwa kwa enzi mpya. Yeye hufanya kazi Yake moja kwa moja na kwa njia ya moja kwa. Yeye hufanya kazi Anayolenga kufanya moja kwa moja; hivyo, yeye hueleza moja kwa moja kazi Aliyoleta, Anafanya kazi Yake moja kwa moja Alivyolenga hapo awali, Akieleza uwepo Wake na tabia Yake. Mwanadamu anavyoona, tabia Yake na kazi Yake pia hazifanani na zile ya kitambo. Hata hivyo, kutoka kwa mtazamo wa Mungu Mwenyewe, huu ni uendelezo na ujenzi zaidi wa kazi Yake. Mungu Mwenyewe Akifanya kazi, Anaeleza neno Lake na Analeta kazi mpya moja kwa moja. Tofauti ni, mwanadamu akifanya kazi, ni kwa ukombozi na kusoma, ama ni kwa maendeleo ya maarifa na mpangilio wa mazoezi iliyojengwa juu ya msingi wa kazi za wengine. Hiyo ni kusema, umuhimu wa kazi inayofanywa na mwanadamu ni ya kuweka mkataba na "kutembea njia za kitambo kwa vitu mpya." Hii inamanisha kuwa hata njia ambayo inatembelewa na watu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu imejengwa juu ya yale yalifunguliwa na Mungu Mwenyewe. Kwa hivyo mwanadamu ni baada ya yote mwanadamu, na Mungu ni Mungu.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mnapaswa kujua jinsi ya kutofautisha kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Unaweza kuona nini katika kazi ya mwanadamu? Kuna vitu vingi ambavyo ni uzoefu wa mwanadamu katika kazi ya mwanadamu; kile ambacho mwanadamu anakidhihirisha ndivyo hivyo alivyo. Kazi ya Mungu pia inadhihirisha vile Alivyo, lakini vile Alivyo ni tofauti na mwanadamu alivyo. Kile mwanadamu alicho ni kiwakilishi cha uzoefu na maisha ya mwanadamu (kile ambacho mwanadamu anakipitia au kukabiliana nacho katika maisha yake, au falsafa za maisha alizo nazo), na watu wanaoishi katika mazingira tofauti hudhihirisha utu tofauti. Kama una uzoefu wa kijamii au la na jinsi ambavyo unaishi na kupitia uzoefu katika familia yako inaweza kuonekana katika kile unachokidhihirisha, wakati ambapo huwezi kuona kutoka kwa kazi ya Mungu mwenye mwili kama Ana uzoefu wa maisha ya kijamii au Hana. Anatambua vizuri asili ya mwanadamu, Anaweza kufunua aina ya matendo yote yanayohusiana na kila aina ya watu. Ni mzuri pia katika kufunua tabia ya dhambi ya mwanadamu na tabia yake ya uasi. Haishi miongoni mwa watu wa kidunia, lakini Anatambua asili ya watu wenye mwili wa kufa na upotovu wote wa watu wa duniani. Hivi ndivyo Alivyo. Ingawa Hashughuliki na dunia, Anajua kanuni za kushughulika na dunia, kwa sababu Anaielewa vizuri asili ya mwanadamu. Anajua kuhusu kazi ya Roho ambayo jicho la mwanadamu haliwezi kuiona na kwamba masikio ya mwanadamu hayawezi kusikia, wanadamu wa leo na wanadamu wa enzi zote. Hii inajumuisha hekima ambayo sio falsafa ya maisha na makuu ambayo watu hupata ugumu kuelewa. Hiki ndicho Alicho, kuwa wazi kwa watu na pia kufichika kwa watu. Kile anachokidhihirisha sio kile ambacho mwanadamu asiye wa kawaida alivyo, bali ni tabia za asili na uungu wa Roho. Hasafiri ulimwengu mzima lakini anajua kila kitu kuhusu ulimwengu. Anawasiliana na "sokwe" ambao hawana maarifa au akili, lakini Anadhihirisha maneno ambayo ni ya kiwango cha juu kuliko maarifa na juu ya watu wakubwa duniani. Anaishi miongoni mwa kundi la wanadamu wapumbavu na wasiojali ambao hawana utu na ambao hawaelewi mila na desturi za kibinadamu na maisha, lakini Anaweza kumwambia mwanadamu kuishi maisha ya kawaida, na kwa wakati uo huo kufichua msingi na uduni wa utu wa mwanadamu. Haya yote ndiyo Alivyo, mkuu kuliko vile ambavyo mwanadamu yeyote wa damu na nyama alivyo. Kwake Yeye, si lazima kupitia uzoefu wa masiha ya kijamii magumu na changamani, ili Aweze kufanya kazi Anayotaka kufanya na kwa kina kufichua asili ya mwanadamu aliyepotoka. Maisha duni ya kijamii ambayo ni chafu hayauadilishi mwili Wake. Kazi Yake na maneno Yake hufichua tu kutotii kwa mwanadamu na hayampatii mwanadamu uzoefu na masomo kwa ajili ya kushughulika na ulimwengu. Hahitaji kuipeleleza jamii au familia ya mwanadamu wakati Anapompatia mwanadamu uzima. Kumweka wazi na kumhukumu wanadamu sio udhihirisho wa uzoefu wa mwili Wake; ni kufunua vile mwanadamu asivyokuwa na haki baada ya kufahamu kutotii kwa mwanadamu na kuchukia upotovu wa mwanadamu. Kazi yote Anayoifanya ni kufunua tabia Yake kwa mwanadamu na kudhihirisha asili Yake. Ni Yeye tu ndiye anayeweza kuifanya kazi hii, sio kitu ambacho mtu mwenye mwili na damu anaweza kukipata. Kwa kuangalia kazi Yake, mwanadamu hawezi kuelezea Yeye ni mtu wa aina gani. Mwanadamu hawezi kumwainisha kama mtu aliyeumbwa kwa misingi ya kazi Yake. Kile Alicho pia kinamfanya Asiweze kuainishwa kama mtu aliyeumbwa. Mwanadamu anaweza kumwona tu kama Asiye mwanadamu, lakini hajui amuainishe kwa kundi gani, kwa hivyo mwanadamu analazimika kumuainisha katika kundi la Mungu. Inaleta maana kwa mwanadamu kufanya hivi, kwa sababu Amefanya kazi kubwa miongoni mwa watu, ambayo mwanadamu hawezi kufanya.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ambayo Mungu anafanya haiwakilishi uzoefu wa mwili Wake; kazi ambayo mwanadamu anafanya inawakalisha uzoefu wa mwanadamu. Kila mtu anazungumza juu ya uzoefu wake binafsi. Mungu Anaweza kuonyesha ukweli moja kwa moja, wakati mwanadamu anaweza tu kuonyesha uzoefu unaolingana na huo baada ya kupata uzoefu wa ukweli. Kazi ya Mungu haina masharti na haifungwi na muda au mipaka ya kijiografia. Anaweza kudhihirisha kile Alicho wakati wowote, mahali popote. Anafanya kazi vile Anavyopenda. Kazi ya mwanadamu ina masharti na muktadha; vinginevyo hana uwezo wa kufanya kazi na hawezi kudhihirisha uelewa wake wa Mungu au uzoefu wake wa ukweli. Unatakiwa tu kulinganisha tofauti baina yao ili kuonyesha kama ni kazi ya Mungu mwenyewe au kazi ya mwanadamu.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu hugeuka mwili ili tu Aiongoze enzi na Aanzishe kazi mpya. Lazima muelewe hoja hii. Hii ni tofauti kabisa na kazi ya mwanadamu, na mawili haya hayawezi kuzungumzwa kwa pamoja. Mwanadamu anahitaji muda mrefu wa kukuzwa na kufanywa mkamilifu kabla mwanadamu aweze kutumiwa kutekeleza kazi, na uanadamu wa hali ya juu unahitajika. Mwanadamu hapaswi kudumisha hali yake ya uanadamu wa kawaida tu, bali pia mwanadamu zaidi ya hapo lazima aelewe kanuni nyingi na sheria za tabia kabla ya mengine, na zaidi ya hayo lazima ajifunze zaidi kuhusu hekima na maadili ya mwanadamu. Haya ndiyo mwanadamu lazima kujengwa nayo. Hata hivyo, hivi sivyo ilivo na Mungu mwenye mwili, kwa maana kazi Yake haimwakilishi mwanadamu na wala si ya binadamu; bali ni dhihirisho la moja kwa moja la hali Yake na utekelezi wa moja kwa moja wa kazi Anayopaswa kufanya. (Kwa kawaida, kazi Yake hufanyika wakati inapaswa kufanyika, na sio tu wakati wowote kiholela. Badala Yake, kazi Yake hufanyika wakati ambapo ni wakati wa kukamilisha huduma Yake). Yeye hajihusishi katika maisha ya mwanadamu wala katika kazi ya mwanadamu, hiyo inamaanisha, uanadamu Wake haujengwi na yoyote kati ya haya (lakini hili haliathiri kazi Yake). Anatimiza huduma Yake tu ikiwa wakati umewadia wa kufanya hivyo; haijalishi hali Aliyomo, Yeye huendelea mbele na kazi Anayopaswa kufanya. Haijalishi mwanadamu anajua nini kumhusu, au maoni ya mwanadamu kumhusu, kazi Yake haiathiriki.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi na maonyesho ya Kristo huamua dutu Yake. Yeye Anaweza kukamilisha kwa moyo wa kweli kile Alichoaminiwa kufanya. Anaweza kumwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli, na kwa moyo wa kweli Atafute mapenzi ya Mungu Baba. Yote haya yanaamuliwa na dutu Yake. Na vile vile ufunuo Wake wa asili pia unaamuliwa na dutu Yake; sababu ya ufunuo Wake wa asili kuitwa hivyo ni kwa sababu ya maonyesho Yake siyo maigizo, au matokeo ya elimu na mwanadamu, au matokeo ya miaka mingi ya kukuzwa na mwanadamu. Hakujifunza au kujivika nayo Yeye Mwenyewe; badala yake, ni asili ndani Yake.
kutoka kwa "Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama mwanadamu ndiye ambaye angefanya kazi hii, basi kazi hii ingekuwa kidogo sana. Ingemchukua mwanadamu hadi kiwango fulani, lakini haingekuwa na uwezo wa kumleta mwanadamu katika hatima ya milele. Mwanadamu hana uwezo wa kuamua hatima ya mwanadamu, wala, zaidi ya hayo, hana uwezo wa kuhakikisha matarajio na hatima ya baadaye ya binadamu. Kazi inayofanywa na Mungu, hata hivyo, ni tofauti. Tangu Yeye amuumbe mwanadamu, Yeye anamwongoza; kwa sababu Yeye humwokoa mwanadamu, atamwokoa mwanadamu kwelikweli, na atampata kikamilifu’; kwa kuwa Yeye humwongoza mwanadamu, atamleta kwenye hatima inayofaa; na kwa kuwa Yeye alimuumba mwanadamu na humsimamia mwanadamu, ni sharti Achukue jukumu la hatima ya mwanadamu na matarajio yake. Ni hii ndio kazi ambayo hufanywa na Muumba. Ingawa kazi ya ushindi inatimizwa kwa kutakasa matarajio ya mwanadamu, hatimaye ni lazima mwanadamu aletwe kwenye hatima ifaayo aliyotengenezewa na Mungu kwa ajili yake.
kutoka kwa "Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ya mwanadamu ina mipaka na kadiri inavyoweza kufika. Mtu mmoja anaweza kufanya kazi ya wakati fulani na hawezi kufanya kazi ya enzi nzima—vinginevyo anaweza kuwaongoza watu katika kanuni. Kazi ya mwanadamu inaweza kufaa tu katika kipindi au awamu fulani. Hii ni kwa sababu uzoefu wa mwanadamu una mipaka. Mtu hawezi kulinganisha kazi ya mwanadamu na kazi ya Mungu. Namna mwanadamu anavyofanya mambo na maarifa yake ya ukweli yote yanatumika tu katika mawanda fulani. Huwezi kusema kwamba njia ambayo mwanadamu anaiendea ni matakwa ya Roho Mtakatifu kabisa, kwa sababu mwanadamu anaweza kupewa nuru na Roho Mtakatifu tu na hawezi kujazwa kikamilifu na Roho Mtakatifu. Vitu ambavyo mwanadamu anaweza kuvipitia vyote vipo ndani ya mawanda ya ubinadamu na haviwezi kuzidi mawanda ya fikra katika akili ya kawaida ya mwanadamu. Wale wote wenye udhihirisho halisi wanapitia uzoefu ndani ya mawanda haya. Wanapoupitia ukweli, siku zote ni uzoefu wa maisha ya kawaida ya mwanadamu chini ya nuru ya Roho Mtakatifu, sio kupitia uzoefu kwa namna ambayo inakengeuka kutoka kwa maisha ya kawaida ya mwanadamu. Wanapitia uzoefu wa ukweli ambao unatiwa nuru na Roho Mtakatifu katika msingi wa kuishi maisha yao ya kibinadamu. Aidha, ukweli huu unatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, na kina chake kinahusiana na hali ya mtu huyo. Mtu anaweza kusema kwamba njia wanayoipitia ni maisha ya kawaida ya kibinadamu ya mwanadamu kuutafuta ukweli na kwamba hiyo ndiyo njia ambayo mtu wa kawaida ambaye amepata nuru ya Roho Mtakatifu anaipita. Huwezi kusema kwamba njia wanayoipitia ni njia ambayo imechukuliwa na Roho Mtakatifu. Katika uzoefu wa kawaida wa kibinadamu, kwa sababu watu wanaoutafuta ukweli hawafanani, kazi ya Roho Mtakatifu pia haifanani. Aidha, kwa sababu mazingira wanayoyapitia na kiwango cha uzoefu wao havifanani, kwa sababu ya mchanganyiko wa akili na mawazo yao, uzoefu wao pia umechanganyika kwa kiwango tofauti. Kila mtu anaelewa ukweli kulingana na hali yake tofauti ya kibinafsi. Uelewa wao wa maana halisi ya ukweli hauko kamili, na ni kipengele chake kimoja tu au vichache. Mawanda ambayo ukweli unaeleweka kwa mwanadamu siku zote umejikita katika hali tofauti tofauti za watu, na hivyo hazifanani. Kwa njia hii, maarifa yanayodhihirisha ukweli ule ule na watu tofauti hayafanani. Hii ni sawa na kusema, uzoefu wa mwanadamu siku zote una mipaka, na hauwezi kuwakilisha kikamilifu matakwa ya Roho Mtakatifu, na kazi ya mwanadamu haiwezi kuchukuliwa kama kazi ya Mungu, hata kama kile kinachodhihirishwa na mwanadamu kinafanana kwa karibu sana na mapenzi ya Mungu, hata kama uzoefu wa mwanadamu unakaribiana sana na kazi ya ukamilifu itakayofanywa na Roho Mtakatifu. Mwanadamu anaweza kuwa tu mtumishi wa Mungu, akifanya kazi ambayo Mungu amemkabidhi. Mwanadamu anaweza kudhihirisha maarifa tu chini ya nuru ya Roho Mtakatifu na ukweli alioupata kutokana na uzoefu wake binafsi. Mwanadamu hana sifa na hana vigezo vya kuwa njia ya Roho Mtakatifu. Hana uwezo wa kusema kuwa kazi ya mwanadamu ni kazi ya Mungu. Mwanadamu ana kanuni za kufanya kazi za mwanadamu, na wanadamu wote wana uzoefu tofauti na wana hali zinazotofautiana. Kazi ya mwanadamu inajumuisha uzoefu wake wote chini ya nuru ya Roho Mtakatifu. Uzoefu huu unaweza tu kuwakilisha asili ya mwanadamu na hauwakilishi asili ya Mungu, au mapenzi ya Roho Mtakatifu. Kwa hivyo, njia anayoipita mwanadamu haiwezi kusemwa kuwa njia anayoipita Roho Mtakatifu, kwa sababu kazi ya mwanadamu haiwezi kuwakilisha kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu na uzoefu wa mwanadamu sio matakwa ya Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu ina hatari ya kuangukia katika kanuni, na mbinu za kazi yake zimefinywa katika uelewa wake finyu na hawezi kuwaongoza watu katika njia huru. Wafuasi wengi wanaishi ndani ya mawanda finyu, na uzoefu wao pia unakuwa ni finyu. Uzoefu wa mwanadamu siku zote ni finyu; mbinu ya kazi yake pia ni finyu na haiwezi kulinganishwa na kazi ya Roho Mtakatifu au kazi ya Mungu mwenyewe—hii ni kwa sababu uzoefu wa mwanadamu, hatimaye, ni finyu. Hata hivyo Mungu anafanya kazi Yake, hakuna kanuni kwa kazi yake; vyovyote vile inavyofanywa, haifungwi na njia moja. Hakuna kanuni za aina yoyote ile katika kazi ya Mungu, kazi Yake yote inatolewa kwa uhuru. Haijalishi ni muda kiasi gani mwanadamu anatumia kumfuata Yeye, hawawezi kutengeneza sheria zozote za njia anavyofanya kazi. Ingawaje kazi Yake inaongozwa na kanuni, siku zote inafanywa katika njia mpya na siku zote inakuwa na maendeleo mapya ambayo ni nje ya uwezo wa mwanadamu. Katika kipindi fulani, Mungu anaweza kuwa na njia nyingi tofauti tofauti za kazi na njia tofauti za kuongoza, akiruhusu watu siku zote kuwa na kuingia kupya na mabadiliko mapya. Huwezi kuelewa sheria za kazi Yake kwa sababu siku zote anafanya kazi katika njia mpya. Ni kwa njia hii tu ndiyo wafuasi wa Mungu hawawezi kuanguka katika kanuni. Kazi ya Mungu Mwenyewe siku zote inaepuka mitazamo ya watu na kupinga mitazamo yao. Ni wale tu ambao wanamfuata Yeye kwa moyo wote ndio wanaoweza kubadilishwa tabia zao na wanaweza kuishi kwa uhuru bila kuwa chini ya kanuni zozote au kufungwa na mitazamo yoyote ya kidini. Madai ambayo kazi ya mwanadamu inawawekea watu yamejikita katika uzoefu wake mwenyewe na kile ambacho yeye mwenyewe anaweza kutimiza. Kiwango cha matakwa haya kimejifunga ndani ya mawanda fulani, na mbinu za kutenda pia ni finyu sana. Kwa hivyo wafuasi bila kutambua huishi ndani ya matakwa finyu; kadri muda unavyokwenda, yanakuwa kanuni na taratibu za kidini. … Kazi ambayo Mungu anaifanya haiambatani na mwili wa mwanadamu; haiambatani na mawazo ya mwanadamu bali inapinga mitazamo ya mwanadamu; haijachanganywa na mitazamo ya kidini isiyoeleweka vizuri. Matokeo ya kazi Yake hayawezi kupatikana kwa mwanadamu ambaye hajakamilishwa Naye na yapo nje ya uwezo wa fikira za mwanadamu.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ama maneno yoyote ya Mungu yanayoelekezwa kwa hatima ya binadamu yanahusiana na binadamu ipasavyo kulingana na asili ya kila mtu; hakutakuwa na ajali yoyote, na hakika hakutakuwa na kosa hata kidogo. Mtu anapofanya kazi tu ndipo hisia za binadamu ama maana itachanganywa ndani. Kazi anayofanya Mungu ndiyo inayofaa zaidi; hakika Hataleta madai ya uongo dhidi ya kiumbe yeyote.
kutoka kwa "Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja" katika Neno Laonekana katika Mwili
Tanbihi:
a. Matini asili iliondoa "kama Yeye ni Mungu."
Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni