Neno la Mungu "Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?"(Official Video)
Mwenyezi Mungu anasema, "Unapaswa kuona kuwa mapenzi Yake na kazi Yake si rahisi kama ilivyokuwa katika kuumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Kwa sababu kazi ya leo ni kubadilisha wale waliopotoshwa, wale waliokufa ganzi, na kutakasa walioumbwa kisha kushughulikiwa na Shetani, si kuumba Adamu na Hawa, ama hata kuumba mwanga, ama aina yote ya mimea na wanyama. Kazi Yake sasa ni kutakasa wote waliopotoshwa na Shetani ili kwamba wamrejelee, wawe miliki Yake na wawe utukufu wake.
Kazi kama ile si rahisi jinsi mwanadamu anavyofikiria kuhusu kuumbwa kwa mbingu na nchi na vilivyomo, wala si sawa na kumkemea Shetani aende katika shimo lisilo na mwisho, kama anayvodhania mwanadamu. Bali, ni kumbadilisha mtu, kubadili kilicho hasi kuwa chanya na kufanya kuwa miliki Yake ambacho si chake. Huu ndio undani wa hadithi ya hatua hii ya kazi ya Mungu. Lazima ufahamu wala usirahisishe mambo. Kazi ya Mungu ni tofauti na kazi nyingine. Uzuri wake hauwezi kutambuliwa na akili za mwanadamu wala hekima Yake kupatikana vile. Mungu Haumbi kila kitu wala kuharibu kila kitu. Bali, Anabadilisha viumbe vyote na kutakasa vyote vilivyonajisiwa na Shetani. Kwa hiyo, Mungu Ataanzisha kazi kuu, na huu ndio umuhimu wa kazi ya Mungu. Baada ya kusoma maandishi haya, je, unaamini kuwa kazi ya Mungu ni rahisi vile?"
Soma Zaidi: Maneno ya Mungu "Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?"
Tufuate: Kuhusu Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni