Jumamosi, 20 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II” Sehemi ya Tatu

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemi ya Tatu

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. 
Maudhui ya video hii: 
Uhuru: Awamu ya Tatu 
1. Baada ya Kuwa Huru, Mtu Huanza Kupitia Ukuu wa Muumba
2. Kuwaacha Wazazi wa Mtu na Kuanza kwa Bidii Kuendeleza Wajibu Wako Kwenye Ukumbi wa Sanaa wa Maisha 
Ndoa: Awamu ya Nne 
1. Mtu Hana Chaguo Kuhusu Ndoa
2. Ndoa Inazaliwa Kutokana na Hatima ya Wandani Wawili

Mwenyezi Mungu anasema, Kama kuzaliwa kwa mtu na kulelewa kwake ni “kipindi cha matayarisho” katika safari ya mtu maishani, kuweka lile jiwe la msingi katika hatima ya mtu, basi uhuru wa mtu ndio mazungumzo nafsi ya kufungua hatima ya maisha ya mtu. Kama kuzaliwa na kukua kwa mtu ni utajiri ambao wameweza kulimbikiza kwa minajili ya hatima yao maishani, basi uhuru wa mtu huyo unaanza wakati ule wanaanza kutumia au kuongeza utajiri huo. Wakati mtu anawaacha wazazi na kuwa huru, masharti ya kijamii ambayo anakabiliana nayo, na aina ya kazi na ajira inayopatikana kwa mtu, vyote vinaamriwa na hatima na havina uhusiano wowote na wazazi wa mtu. Baadhi ya watu huchagua kozi nzuri katika chuo na huishia kupata kazi ya kutosheleza baada ya kuhitimu, na hivyo basi kupiga hatua ya kwanza ya mafanikio katika safari yao ya maisha. Baadhi ya watu hujifunza na kumiliki mbinu nyingi tofauti na ilhali hawapati kazi katu ambayo inawafaa au hawapati cheo chao, bila kutaja kwamba hawana ajira yoyote; wakati wa safari ya maisha yao wanajipata wakiwa wamekwazwa katika kila kona, wameandamwa na matatizo, matumaini yao madogo na maisha yao hayana uhakika. Baadhi ya watu wanatia bidii katika masomo yao, ilhali wanakosa kwa karibu sana fursa zao zote za kupokea elimu ya juu zaidi, na wanaonekana kuwa na hatima ya kutotimiza fanisi, matamanio yao ya kwanza kabisa katika safari yao ya maisha yanatowekea tu hewani. Bila kujua[d]kama barabara iliyo mbele ni laini au yenye miamba, wanahisi kwa mara ya kwanza namna ambavyo hatima ya binadamu imejaa vitu vya kubadilikabadilika, na wanachukulia maisha kwa tumaini na hofu. Baadhi ya watu, licha ya kutokuwa na elimu nzuri sana, huandika vitabu na kutimiza kiwango cha umaarufu; baadhi, ingawaje hawajui kusoma na kuandika sana, huunda pesa katika biashara na hivyo basi wanaweza kujikidhi…. Kazi anayochagua mtu, namna mtu anavyozumbua riziki: je, watu wanao udhibiti wowote kuhusu, kama wanaweza kufanya uchaguzi mzuri au uchaguzi mbaya? Je, yanapatana na matamanio na uamuzi wao? Watu wengi zaidi hutamani wangeweza kufanya kazi kidogo na kupata mapato mengi zaidi, wasitie bidii sana katika jua na mvua, wavalie vyema, wametemete na kung’aa wakiwa kila pahali, kuwapita sana wengine kwa uwezo, na kuleta heshima kwa mababu wao. Matamanio ya watu ni timilifu kweli, lakini watu wanapochukua hatua zao za kwanza katika safari ya maisha yao, wanaanza kwa utaratibu kutambua namna ambavyo hatima ya binadamu ilivyo na hali ya kutokuwa timilifu, na kwa mara ya kwanza wanang’amua kwa kweli hoja hii kwamba, ingawaje mtu anaweza kufanya mipango thabiti kwa minajili ya mustakabali wake, ingawaje mtu anaweza kuhodhi mawazoni ndoto shupavu, hakuna yule aliye na uwezo au nguvu za kutambua ndoto zake mwenyewe, hakuna yule aliye katika hali ya kudhibiti mustakabali wake. Siku zote kutakuwepo na kitalifa fulani kati ya ndoto za mtu na uhalisia ambao lazima mtu akabiliane nao; mambo siku zote hayawi vile ambavyo mtu angetaka yawe, na watu wanapokumbwa na uhalisi kama huu hawawezi kutimiza hali ya kutosheka au kuridhika. Baadhi ya watu wataenda hadi kiwango chochote cha kufikirika, wataweza kutia bidii za kipekee na kujitolea pakubwa kwa minajili ya riziki na mustakabali wao, katika kujaribu kubadilisha hatima yao wenyewe. Lakini hatimaye, hata kama wataweza kutambua ndoto na matamanio yao kupitia kwa njia ya bidii yao wenyewe, hawawezi kubadilisha hatima zao, na haijalishi watajaribu vipi kwa njia ya ukaidi hawatawahi kuzidi kile ambacho hatima yao imewapangia. Licha ya tofauti katika uwezo, kiwango cha akili, na hiari ya kutenda, watu wote ni sawa mbele ya hatima, jambo ambalo halileti utofauti kati ya wakubwa na wadogo, wale wa kiwango kile cha juu na cha chini, wanaotukuzwa na wakatili. Ile kazi ambayo mtu anafuatilia, kile anachofanya mtu ili kuzumbua riziki, na kiwango kipi cha utajiri ambacho mtu amelimbikiza katika maisha yake vyote haviamuliwi na wazazi wa mtu, vipaji vya mtu, jitihada za mtu au malengo ya mtu, vyote vinaamuliwa kabla na Muumba.


Tufuate: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni