Jumamosi, 20 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (2)

Katika wakati ambapo Yesu Alifanya kazi Uyahudi, Aliifanya wazi, lakini sasa, Nazungumza na Kufanya kazi kati yenu kwa siri. Wasioamini hawana ufahamu wowote. Kazi Yangu kati yenu imetengwa kutoka kwa nyingine. Maneno haya, kuadibu huku na hukumu hii, vinajulikana tu kwako na sio mwingine. Kazi hii yote inatendeka kati yenu na kuonekana tu kwenu; hakuna yeyote asiyeamini anayefahamu haya, kwani muda haujafika. Wanadamu hao wako karibu kufanywa wakamilifu baada ya kuvumilia adibu, lakini wale walio nje hawajui lolote juu yake. Kazi hii imefichwa sana! Kwao, Mungu mwenye mwili ni siri, lakini kwa wale walio katika mkondo, Anaweza kuchukuliwa kuwa wazi.

Ijumaa, 19 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (7)

Ubinadamu wenu ni wenye upungufu mno, hali yenu ya maisha ni ya chini na kushusha hadhi mno, hamna ubinadamu, na hamna utambuzi. Hiyo ndiyo maana mnahitaji kujiandaa na mambo ya ubinadamu. Kuwa na dhamiri , urazini, na utambuzi, kujua jinsi ya kuzungumza na kutazama vitu, kuwa makini kwa usafi, kutenda kama binadamu wa kawaida—vyote hivi ni ufundi ustadi wa ubinadamu wa kawaida. Mnapofanya hivi vizuri, ubinadamu wenu ni wa kiwango kinachohitajika. Kipengele kingine ni kujihami kwa ajili ya maisha yenu ya kiroho. Lazima mjue kazi yote ya Mungu duniani na muwe na uzoefu wa maneno Yake.

Alhamisi, 18 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Ni Lazima Muielewe Kazi; Msifuate kwa Rabsha!

Kwa sasa kuna watu wengi ambao huamini kwa njia ya rabsha. Udadisi wenu ni mkubwa mno, tamaa yenu ya kufuatilia baraka ni kubwa mno, na hamu yenu ya kufuatilia maisha ni ndogo mno. Waumini katika Yesu siku hizi wamejaa shauku. Yesu atawakaribisha katika nyumba ya mbinguni–je, wao hawawezi kuamini? Watu wengine ni waumini katika maisha yao yote, wameamini kwa miaka arobaini au hamsini, na hawachoki kamwe kusoma Biblia. Hii ni kwa sababu bila kujali kinachotokea, mradi wao wanaamini, wataingia mbinguni. Mmemfuata Mungu kwa njia hii kwa miaka michache tu, lakini tayari mnajitahidi sana na hamna uvumilivu tena.

Jumatano, 17 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya

Siku hizi watu wengi hawatilii maanani mafunzo yapi yanayopaswa kusomwa wakati wa upatano na wengine. Nimegundua kuwa wengi wenu hawawezi kujifunza mafunzo hata kidogo wakati wa ushirikiano na wengine. Wengi wenu mnashikilia maoni yenu mwenyewe, na wakati mnafanya kazi kanisani, unatoa maoni yako na yeye anatoa yake, moja uhusiano na mingine, bila kushirikiana kabisa. Mnajihusisha tu katika kutoa umaizi wenu wenyewe wa ndani, unaingia tu katika kuachilia huru “mizigo” ndani yenu, si kutafuta uzima hata kidogo.

Jumanne, 16 Julai 2019

Kanisa la Mwenyezi Mungu - Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu

Kadiri unavyozingatia mapenzi ya Mungu, ndivyo unavyokuwa na mzigo zaidi; kadiri unavyokuwa na mzigo, ndivyo uzoefu wako utakuwa mwingi zaidi. Unapokuwa mzingatifu wa mapenzi ya Mungu, Mungu atakupa mzigo huu, na Mungu atakupa nuru ya mambo ambayo amekuaminia. Baada ya Mungu kukupa mzigo huu, utaangalia ukweli wa kipengele hiki unapokula na kunywa maneno ya Mungu. Kama una mzigo unaohusiana na hali ya maisha ya ndugu, huu ni mzigo ulioaminiwa kwako na Mungu, na sala zako za kila siku daima zitaubeba mzigo huu. Kile ambacho Mungu hufanya kimeaminiwa kwako, uko radhi kutekeleza kile ambacho Mungu anataka kufanya, na hivi ndivyo inavyomaanisha kuuchukua mzigo wa Mungu kama wako.

Alhamisi, 11 Julai 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Saba"

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Saba

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Msiwe na Wasiwasi Wowote Kuhusu Majaribio ya Mungu
Wale Wanaomcha Mungu na Kujiepusha Na Maovu Wanatazamiwa kwa Utunzwaji na Mungu, Huku Wale Walio Wajinga Wanaonekana kuwa Duni na Mungu

Jumapili, 7 Julai 2019

Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa

Katika siku za mwisho, Mungu alipata mwili ili kufanya kazi Aliyopaswa kufanya na kutekeleza huduma Yake ya maneno. Alikuja yeye mwenyewe ili kufanya kazi kati ya wanadamu kwa lengo la kuwakamilisha wale watu ambao wanaipendeza nafsi Yake. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo Yeye hufanya tu hiyo kazi wakati wa siku za mwisho. Ni wakati wa siku za mwisho tu ambapo Mungu alipata mwili ili kufanya kazi kwa kiwango kikubwa. Ingawa Yeye huvumilia shida ambazo watu wanaweza kupata ugumu kuvumilia, ingawa Yeye kama Mungu mkuu ana unyenyekevu wa kuwa mtu wa kawaida, hakuna kipengele cha kazi Yake kimecheleweshwa, na mpango Wake haujatupwa katika mchafuko hata kidogo.

Jumamosi, 6 Julai 2019

Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje

Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawaida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu.